Video yükleniyor...

Video Yüklenemedi

Ana Sayfaya Dön

10,372 görüntüleme • 3 ay önce •via X (Twitter)

0 Yorum

Yorum bulunmuyor

Orijinal gönderinin yorumları burada görünecek

Benzer Videolar

Mkurugenzi wa Babuu Cancer Foundation ambaye pia ni Mtangazaji wa Clouds Media Group, Cedou Mandingo maarufu Babu wa Kitaa amesema Watu wengi wamepona Saratani Tanzania akiwemo yeye kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa kwenye sekta ya afya. Babuu amesema hayo mbele ya Waziri wa Afya Jenista Mhagama jana Aprili 19, 2025 alipotembelea kambi maalum ya uchunguzi wa magonjwa ya saratani ikiwemo saratani ya matiti na tezi dume katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph Peramiho Mkoani Ruvuma iliyoendelea hadi leo April 20, 2025 ikiwa jana ni siku ya tano . “Mimi ni Shujaa wa saratani niliyeugua saratani nikiwa hapa nchini, nimetibiwa hapa nchini na nimepona hapa nchini, lengo la Mimi kuja kwenye kambi hii ni kuwaaminisha kwamba unaweza kupata saratani na ukapona, sio Mimi tu niliyepona saratani Tanzania wapo wengi wamepona kutokana na mageuzi makubwa aliyofanya Rais Samia kwenye sekta ya afya” Wananchi zaidi ya 900 wamepatiwa huduma za uchunguzi na matibabu ya ugonjwa wa saratani bila malipo katika Hospitali ya MT. Joseph Peramiho, huduma ambazo kutolewa na Madaktari bingwa wa magonjwa ya saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa muda wa siku nne huku "Watu 18 wamegundulika kuwa na viashiria vya ugonjwa huo ambapo 12 ni Wanawake ambao tayari wameshapatiwa matibabu na sita ni Wanaume ambao wamepewa rufaa ya kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi, tuna kila sababu ya kumshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya haya yote kwasababu ya kujali uhai wa maisha ya Watanzania” #MillardAyoUPDATES

millardayo

23,296 görüntüleme • 1 yıl önce

Vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kacheuka maarufu Babuu (22) wamefariki dunia huku vifo vyao vikigubikwa na utata kwakuwa mara ya mwisho December 27,2023 walichukuliwa kwa nguvu nyumbani kwao Vingunguti Jijini Dar es salaam na Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari na kisha kupelekwa kusikojulikana na baada ya Familia kuwatafuta bila mafanikio hatimaye December 28,2023 asubuhi miili yao ikafikishwa Amana Hospital na Watu waliojitambulisha ni Askari wakidai miili hiyo wameiokota. Mzee Swalehe Kacheuka ambaye ni Baba Mzazi wa Shomari ameiambia AyoTV kuwa “Babuu alikuwa anafanya kazi Kariakoo kampuni ya kuuza pikipiki, aliporudi kazini wakaja Wat waliojitambulisha ni Askari ila hawajavaa sare wakamsimamisha kwamba upo chini ya ulinzi akawauliza nimefanyaje wakawa wanabishana wakampiga risasi ya mguu, Kaka yake katoka wakamnyooshea bastola, akaja Rafiki yake Ismail wakati wanamkunja akasogea wakampiga risasi ya mguuni na wakawachukua wote wakaondoka nao, Ismail walimpakia kwenye IST, Bakari wakampakia kwenye Defender” Kwa upande wake Mzazi wa Shemeji wa Bakari Ismail amesema “Tulipopata taarifa asubuhi December 28,2023 tukaamkia Polisi Buguruni tukaambiwa hawajaletwa, tukazunguka vituo vya polisi karibu sita hatukufanikiwa, tukazunguka Hospitali tukaambiwa hawajaletwa, mida ya saa 8 mchana tukaambiwa kuna miili Amana ambayo imepelekwa na Polisi wakisema wameowakota Vingunguti” Familia hizo mbili zimesema miili ya Vijana hao imekutwa na matundu ya risasi na macho yao yametobelewa, Ayo TV imefanya jitihada za kulitafuta Jeshi la Polis Kanda Maalum ya Dar es salaam ili kupata taarifa zaidi kuhusu tukio hilo lakini hatujafanikiwa ingawa bado tunaendelea na jitihada za kuwatafuta

millardayo

362,684 görüntüleme • 2 yıl önce