
Gilly Bonny Tv
@GillyBonnyTv • 126,522 subscribers
Independent Media I WhatsApp +255655832712
Videos

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita, Manisha, amepatikana akiwa hai kaskazini mwa nchi ya Nepal katika eneo la Timure, wilayani Rasuwa, baada ya kukaa chini ya udongo na vifusi kwa saa 60 kufuatia mafuriko makubwa yaliyokumba eneo hilo. Mtoto huyo aliokolewa Ijumaa jioni, Agosti 28, 2026, na timu ya uokoaji ya Jeshi la Polisi la Kulinda Mipaka (APF) la Nepal, baada ya waokoaji kusikia sauti ya mtoto akilia kutoka chini ya udongo wakati wakiendesha msako. Mamlaka za uokoaji zimeeleza kuwa Manisha alinusurika kifo kufuatia muundo wa mbao uliomwangukia na kumkinga usoni, hatua iliyozuia udongo kumfunika kabisa kichwa chake na kumwezesha kuendelea kupata hewa chini ya vifusi hivyo. Baada ya kuchimbiwa na kutolewa akiwa amepoteza fahamu, alipewa huduma ya kwanza kituoni hapo na kisha kusafirishwa kwa helikopta ya Jeshi siku iliyofuata, Jumamosi, Agosti 29, 2026, kuelekea Mji Mkuu wa Nepal, Kathmandu, kwa matibabu zaidi. Msemaji wa APF, DIG Netra Bahadur Karki, amethibitisha kuwa wazazi wa mtoto huyo nao walinusurika kwenye mafuriko hayo nchini Nepal na sasa wameunganishwa na binti yao katika hospitali hiyo jijini Kathmandu wakiendelea kupokea matibabu
Gilly Bonny Tv14,064 görüntüleme • 26 gün önce

VIDEO : Msikilize Dk. Sulle kuhusu athari zinazotokana na ulaji sana wa nyama ya Ngurue. 🎥Mbengo Tv
Gilly Bonny Tv152,626 görüntüleme • 1 yıl önce

Hospitali ya Mafunzo ya Chuo Kikuu cha Jimbo la Benue (BSUTH) nchini Nigeria, imefanya uzikaji wa pamoja wa miili 12 iliyokaa kwa muda mrefu mochwari bila kudaiwa wala kutambuliwa na ndugu. Zoezi hilo lifanyika Jumamosi, Agosti 29, 2026, likisimamiwa na Wakala wa Usafi wa Mazingira wa Jimbo la Benue (BENSESA) kwa lengo la kulinda afya ya jamii na kuzingatia sheria za mazingira. Mkurugenzi Mtendaji wa BSUTH, Dkt. Stephen Hwande, ameeleza kuwa uamuzi huo ulikuwa wa dharura ili kuzuia mrundikano wa miili iliyoanza kuharibika, hatua inayoweza kuzalisha virusi na kusababisha milipuko ya magonjwa kwa wafanyakazi na wananchi. Ili kuboresha huduma za hifadhi ya miili na kuzuia changamoto kama hizo, hospitali hiyo imefunga mitambo mipya ya kisasa ya umeme ya kuhifadhia maiti (electric embalming machines) na kukarabati vyumba vyote vya baridi. Pia, uongozi umetangaza kuanza kwa mafunzo rasmi ya wataalamu wa radiology kuanzia Septemba 1, 2026, ili kuongeza ufanisi wa vifaa vipya vya vipimo vilivyowekwa hospitalini hapo.
Gilly Bonny Tv12,013 görüntüleme • 26 gün önce
0:29
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Raia mmoja wa mwafrika ambae haijafahamika anatokea nchi gani alijikuta akitupa lawama na kuondoka kwenye mazishi bila ya kumuaga papa Francis , hii ni baada ya kunyimwa ruhusu ya kuingia kwenda kumuaga kwa mara ya mwisho papa Francis aliyefariki wiki hii.
Gilly Bonny Tv81,433 görüntüleme • 1 yıl önce

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma, amemtolea uvivu mwanasiasa wa CHADEMA, John Heche, akimshutumu kwa kutoa kauli za kejeli na dharau dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan. Msukuma amesema haikubaliki kwa mwanasiasa kama Heche kuendelea kumsema Rais kwa namna ya kubeza juhudi zake, huku akisisitiza kuwa viongozi wa upinzani wanapaswa kuwa na nidhamu ya maneno wanapojadili masuala ya kitaifa.
Gilly Bonny Tv68,341 görüntüleme • 1 yıl önce

KOCHA WA SIMBA SC, FADRU DEVIS AKIWA UWANJANI ENZI ZAKE AKISAKATA KABUMBU
Gilly Bonny Tv58,588 görüntüleme • 1 yıl önce

"Diamond Platnumz badilika hakuna wa kukulia bilioni mbili katika harusi" Dudu baya
Gilly Bonny Tv60,377 görüntüleme • 1 yıl önce