
Martin Maranja Masese
@IAMartin_ • 610,617 subscribers
MMM | Sperm That Won The Race | Cogito, ergo Sum | Patria o Muerte, Venceremos |
Shorts
Videos

Kubaaaaabake. Masela wamekataa porojo. Zimeletwa stori za awamu ya sita, watu wamezomeaa balaa. Watu wapo kwenye burudani unawaletea habari za awamu ya sita. Tunajenga arenaaa. Tunajenga arenaaaa. Tuna, tuna, tuna miaka nenda rudi. Masela wamekataa porojo. 😁
Martin Maranja Masese101,992 görüntüleme • 14 gün önce

GIRISHONI amefanya niipakue hii makala, tusikilize wote. Wote sasa tukatazame makala ya BBC AFRICA EYE ya mwaka 2026 inaangazia mapambano ya kisiasa ya Tundu Lissu na jaribio la mauaji dhidi yake la mwaka 2017, ikionyesha juhudi zake zinazoendelea za kudai mageuzi ya mfumo wa uchaguzi nchini Tanzania licha ya kukabiliwa na mashtaka ya uhaini aliyopewa mwaka 2025. Halafu baadae tutapata muda wa kujadili kipeperushi cha Serikali katili ya CCM kilichotolewa na GIRISHONI.
Martin Maranja Masese55,836 görüntüleme • 10 gün önce

Kitila Mkumbo amenikumbusha kitabu cha Chinua Achebe (A Man of the People) wakati Waziri wa Utamaduni, Chief the Honourable M.A. Nanga, M.P. anasema “Teaching is a very noble profession”. Chief Nanga anatamka maneno hayo akifahamu ukweli ni kinyume chake. Anaisifu taaluma ya ualimu kwa misingi ya heshima lakini yeye ameacha ualimu na kuingia katika siasa na kuwa fisadi mkubwa. KITILA, kama UALIMU ungelikuwa unalipa kuliko SIASA usingeacha ualimu ili utafute UBUNGE na baadae WAZIRI. Ualimu ungelikuwa unalipa kuliko siasa usingeondoka UDSM. Kiinua mgongo kwa mbunge mmoja wa Bunge la Tanzania ni Sh380 Milioni baada ya kipindi cha miaka 5. Mwalimu gani analipwa mafao hayo akistaafu na miaka 55 au 60? Mwalimu gani anapata mshahara wa Sh22 Milioni kwa mwezi kama mbunge? Kitila Mkumbo (PhD), profesa kuwa muongo hata haipendezi. We are experiencing a cultural and intellectual decline.
Martin Maranja Masese37,046 görüntüleme • 12 gün önce

CHADEMA sasa hivi si chama cha siasa tu, ni imani iliyozama mioyoni mwa watu! Baada ya kushiba nondo za maana kutoka kwa viongozi, wananchi wenyewe wamemwaga upendo kwa kuchangia kiasi cha TZS 5,992,255 kidogo kidogo (Tone kwa Tone), kisha burudani ya ngoma za ukombozi ikafuata. CCM ili ipate vibe kama hili, ni lazima imwage mabilioni kusomba wasanii ili kuvuta watu. #PeoplesPower #KatibaMpya #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese94,713 görüntüleme • 2 ay önce

CHADEMA iko imara zaidi sasa! Msiyumbishwe. Adui yetu mkuu anajulikana. Ni dola dhalimu na katili ya CCM inayofanya kila njia kutudhoofisha. Kuwa kiongozi au mwanachama wa CHADEMA ni msimamo wa kijasiri na utayari wa kupambana kulinda ustawi wa chama chetu. Kusimama imara ndiyo silaha yetu. #PeoplesPower
Martin Maranja Masese21,303 görüntüleme • 14 gün önce

Mchawi binadamu, paka anatumwa tu. MPEMBA ametumwa kumshambulia NAMBA MBILI wao na amembatiza jina la YUDA. Kosa lake ni kusema alipendwa sana na JIWE. Wamekasirika sana. Jamaa anasema JIWE alimtupa Brazil. Wanasema ametengwa hadi na familia ya ‘WHITE HAIR’. Eti ni kweli, wazee wa ‘Safari ya Matumaini’ mmemtenga 'Mzee wa Mustachi'? Sisi wengine tunafurahi. Kazi yetu moja tu, kuchochea kunu. Ushirika wa 'wanyonya damu' hauwezi kudumu. NB; kama wapo wengi, kwanini hakuna makofi? SIJAPENDA.
Martin Maranja Masese58,438 görüntüleme • 1 ay önce

Kuporwa kwa uwanja wa michezo wa Sahara uliopo kata ya Mabibo, Ubungo—ambalo ni eneo la wazi la umma—ni uthibitisho tosha la jinsi wananchi wanavyokosa watetezi wa haki zao pale CHADEMA wanapokuwa nje ya vyombo vya maamuzi. Wananchi wa eneo hili sasa wapo hatarini kupoteza kabisa ardhi hii ya wazi ambayo wameitumia kwa miaka mingi kwa ajili ya michezo na shughuli za kijamii.
Martin Maranja Masese47,364 görüntüleme • 1 ay önce

KATAMBI, acha kutufokea. Tupatie uthibitisho wa kisheria. Tuonyeshe ni ibara gani ya Katiba au sheria gani inayokupa mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Kama katazo lenu ni halali, thibitisheni hilo kwa kutaja vifungu vya sheria. Taifa hili linatakiwa kuongozwa kwa misingi ya sheria na Katiba, na si kwa mabavu au utawala wa kiimla.
Martin Maranja Masese24,864 görüntüleme • 25 gün önce

Jana niliandika ujumbe nikikosoa kitendo cha Mzee MBOWE kumuombea msamaha SABAYA. Nimepata maoni mengi; wengine wakisema sikuwa sawa. Ipo hivi. Kuna mambo katika siasa hayawezi kufutwa na maneno laini na mepesi ya “msamaha,” hususani msamaha usiotoka kwa mtenda dhambi mwenyewe. Utawala wa SABAYA katika wilaya ya Hai haukuwa wa kisiasa tu; ulikuwa ni utawala wa chuma na ukatili uliopitiliza. Hata Mzee MBOWE anafahamu hilo. Makosa ya uhujumu uchumi na unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery) yaliyomfunga gerezani wakati ule, ni tone dogo sana katika bahari ya unyama wake. Wapo watu walitekwa, kuteswa, na kuachwa na vilema vya kudumu. Kusema mtu huyu anastahili msamaha bila toba ya dhati kwa wahanga, si tu ni kosa, ni dhihaka. Miongoni mwa wahanga wa genge la SABAYA ni ndugu yetu Simon MNYAMPANDA, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai. Ndugu yetu aliteswa. Simon Mnyampanda aliteswa kwa umeme. Ameeleza wazi kwamba, alihojiwa kuhusu mahusiano yake na Mzee MBOWE. Mwisho, alipigwa misumari ya miguu. Huyu ni mtu aliyepata mateso hayo akimlinda Mzee MBOWE na CHADEMA. Leo Mzee MBOWE anajigeuza kadinali na kumuombea msamaha mtesaji SABAYA? Genge hilo halikuishia hapo. Genge hilo lilikuwa kama MAHARAMIA. Walivamia nyumbani kwa mgombea udiwani wa kata ya Narumu katika jimbo la Hai. Baada ya kumkosa, walitoa adhabu ya kinyama kwa watu waliokuwepo nyumbami kwa kuwakata masikio na sehemu nyingine. Nyumba nzima ilitapakaa damu. Hawa ni binadamu, si takwimu za kisiasa. Hawa watu waliotendewa mambo hayo wapo. Baadhi ya ushahidi wa masuala hayo nimeambatanisha katika makala hii. Inasikitisha kuona Mzee Mbowe anatumia mateso ya wafuasi wake kama mtaji wa kisiasa (political capital). Binafsi nimejiuliza maswali mengi tangu hiyo jana. Je, wahanga wameombwa msamaha na kufidiwa? Je, mateso yao yamekuwa ngazi ya makubaliano ya kisiasa? Hii si dharau kwa wale walioteswa wakikupigania? Sabaya anapaswa kuomba msamaha kwa waathirika, si kuombewa. Vinginevyo, hii ni michezo ya kumtengenezea mazingira ya kupata uteuzi katika Serikali ya CCM. Watu wa Hai hawajasahau. Damu na machozi ya wahanga bado vinadai haki. Msamaha bila toba ni baraka kwa ukatili mwingine ujao. Haki kwanza, msamaha baadaye. Binafsi, nilimheshimu Mzee Mbowe kiasi cha kumpa mwanangu wa tatu jina la “Freeman”. Leo hii, nahisi usaliti mkubwa moyoni mwangu kwa mambo hayo. Kunyamaza mbele ya usaliti huu si busara, bali ni upumbavu ambao kesho utatunyong’onyesha. Nimeandika ili kulinda hadhi ya jina la mwanangu. Siku mtoto wangu akiniuliza, nitamjibu kwa utimamu kabisa. “Nilitetea maana halisi ya ‘Freeman’ wakati jina hilo lilipotaka kuchafuliwa na siasa za kimaslahi.”
Martin Maranja Masese71,455 görüntüleme • 3 ay önce

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwenye shahada ya uzamivu katika sayansi ya siasa, amewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, na sasa MaCCM yamekabidhiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwake. Fikiria, ni mshauri wa Rais eneo hilo. Daktari wa falsafa (Ph.D) hawezi kueleza mpango wa Serikali katika kuongeza thamani mazao ya uvuvi ili kuongeza kipato cha wavuvi. Battery Low. Hakika, CCM ni kansa. Catastrophe..
Martin Maranja Masese34,576 görüntüleme • 1 ay önce

Ndugu Madenge katika jambo hili umenisikitisha sana. Sikutegemea unaweza kuwa sehemu ya kejeli hizi. Hao wengine ni wapumbavu tu ukijumlisha na huyo Masanja (hawakunishangaza) Siyo kwamba mnachekesha, mmeonesha ujinga wenu. Mmeonesha jinsi mlivyo machawa wa watawala. Na mmejitenga na jamii kubwa ya watanzania. Mmechagua kuwa maadui wa umma. Twitter (X) mnalalamika kuhusu umeme kila siku, watu tunakwenda barabarani na mabango ya umeme mnakwenda kutukejeli? Kweli nimeamini sasa, kuwa “paid slave” ni dhambi. Unatumikishwa tu. Masanja hajaenda shule. Hakuna ubongo kichwani, anawezaje kuwapa maudhui (content) za kipunbavu hivi na mkazitumia? Au ninyi pia mmekubali kuwa wapumbavu kama yeye? Mbaya zaidi ni kwamba wote katika kundi hilo hakuna hata ambaye ana diploma au degree ya uandishi wa habari na utangazaji. Wameokotwa kijanja-kijanja na leo wanakejeli watanzania. Kama mmeshindwa kuandamana na hamtaki, maiwadhihaki wananchi hao wachache ambao wamekubali kuandamana kwa gharama zao wenyewe. Mnapata faida gani wakiacha kuandamana? Naelewa, watangazaji wa EFM hapo mnalipwa vizuri. Maumivu makubwa ya ugumu wa maisha na kupanda kwa bidhaa sokoni hakuwagusi. Labda ndiyo maana mnakejeli haya maandamano. Mnakosea sana. Mtaani kuna maumivu makali. Wananchi hawana maji wala umeme. Sukari bei juu na mtaani haipo. Miundombinu ni duni na serikali inakusanya kodi. Jukwaa pekee kueleza hayo ni katika maandamano. Biashara za watu mtaani zinakufa. Mitaji yao imepotea. Media ambayo ingelitumika kufikisha ujumbe kwa serikali ndiyo inakejeli maandamano ambayo yanatumika kupaza sauti za watu mtaani. Maandamano yale yanatumika kufikisha ujumbe kwa watawala. Ukisoma mabango wananchi wameandika na kubeba kero zao, wanatembea kwa zaidi ya kilometa 20, kuziwasilisha, mnawakejeli? Mnatumika na DOLA kwa nia ovu. Mnafifisha morali ya umma kujitokeza katika maandamano ya amani ambayo yanasaidia kubeba sauti kubwa ya umma kwenda kwa watawala. Mnakosea sana. Hili ni tatizo kubwa. Kwa kuwa mmiliki wa EFM ni mwana CCM kindakindaki anatumia chombo chake cha habari kukejeli shughuli za kisiasa na maandamano ya kiraia. Huu ni UPUMBAVU. Kazi ambazo mnazifanya hapo leo EFM/ETV, Malcom X alizieleza vizuri sana mwaka 1963. “house Negro” na “field Negro.” Ninyi watangazaji wa EFM ni ‘house negro’ kwa matendo na tabia zenu hizi. House negro aliishi katika nyumba ya bwana wake - ghorofa au dari - lakini bado aliishi katika nyumba ya bwana, alivaa mabaki ya nguo za bwana wake. Alikula chakula bwana wake alikiacha mezani. House negro alijatanabaisha kila mara kwa maana ileile ambayo bwana wake alijitambulisha. House negro alijiweka katika daraja sawa na bwana wake, wakati huo ni myumwa na kijakazi. Bwana wake aliposema, “Tuna chakula kizuri,” alisema, “Ndiyo, sisi tuna chakula kingi kizuri.” Bwana wake aliposema “tuna nyumba nzuri hapa,” alisema, “Ndiyo, tuna nyumba nzuri hapa.” Bwana wake akiugua, house negro angemuuliza “Kuna nini bosi, sisi wagonjwa?”. Maumivu ya bwana wake yalikuwa maumivu yake mara mbili. Aliumia kuliko hata watoto wa bwana wake. House negro ilimuuma zaidi bwana wake kuwa mgonjwa kuliko yeye mwenyewe kuwa mgonjwa. Hawa sasa ndiyo wafanyakazi wa EFM/ETV. Hizi ni tabia zao za kitumwa, house negro. But I know, nothing you can if you’re just a paid slave. 🙏🏽 Brigedia Mtikila, MMM.
Martin Maranja Masese456,972 görüntüleme • 2 yıl önce

Hii tuliifahamu, mbogamboga lazima muogope. Hatimaye mmekimbia magetoni baada ya kupigwa paipu mfululu. Tumewatandika spakoo za kutosha sana. Pumzi ndogo, hamuwezi kufanya siasa za kujibu hoja, mmeomba msaada wa bunduki. Mbogamboga mnachokishuhudia sasa sivyo mlivyotarajia. Kila CHADEMA inapokanyaga ni mtiti, mafuriko. Wananchi wanapambana kwa nguvu kuchangia harakati za chama kupitia TONE TONE. Tunajua ile inawauma sana. MaCCM, mlifikiri kwa kupora uchaguzi, kujitangazia ushindi wa 98% na kujipachikia kura milioni 32, mngetawala bila upinzani na kuizika CHADEMA kisiasa? Uhalali haujengwi kwa kupora uchaguzi, unatokana na ridhaa ya wananchi. Mkaenda kufadhili mashoga zenu (ACT na CHAUMMA) ili washiriki uigizaji wenu wa demokrasia bandia. Baada ya kupora uchaguzi wameshindwa kufanya mikutano ya hadhara. Mbogamboga, hamtaweza kuwanyamazisha watu wote. Sisi siyo mazombi. #KatibaMpya #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese20,830 görüntüleme • 28 gün önce
0:45
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Fungua kwa tahadhari; ⚠️ Picha za kutekwa na kuuawa kwa Joshua Mollel (21), mwanafunzi wa kilimo kutoka Tanzania. Serikali ya Tanzania ilitangaza kwamba, Joshua Mollel aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la HAMAS mnamo tarehe 7 Oktoba 2023. Pumzika kwa amani Joshua 🙏🏽
Martin Maranja Masese368,205 görüntüleme • 2 yıl önce

Ndugu yetu Edgar Mwakabela, SIR TIVA amepatikana katika hifadhi ya Katavi. Ameteswa na ameumizwa sana. Tunaomba watu wa Katavi mtusaidie haraka sana apate msaada wa matibabu. Rais Samia Suluhu umefika huku? Tulisema hatuwezi kurudi katika zama hizi za kuwatesa wakosoaji wako.
Martin Maranja Masese290,100 görüntüleme • 2 yıl önce

Milio ya risasi za moto imesikika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo, Dar es Salaam. Watu hao waliokwenda kumkamata Askofu Josephat Gwajima wamepambana kuvamia chumba chake lakini waumini wameendelea kuzuia asichukuliwe. Waumini hao wamekwenda kufunga barabara ya Morogoro.
Martin Maranja Masese154,364 görüntüleme • 1 yıl önce

Kirando, Nkasi Kaskazini, Rukwa. Hii ni leo. Hakuna kiongozi wa kitaifa yeyote. Hapa alikuwepo AIDA KENANI na watu wake tu. Mnaweza kuwatoa roho wafuasi wote wa CHADEMA lakini hamuwezi kuondoa imani kwa watu. Kwa sasa, CHADEMA ni imani ya watu. CHADEMA kwetu ni lifestyle yetu.
Martin Maranja Masese40,008 görüntüleme • 2 ay önce

Hatuweki huu upumbavu hapa kwamba tunataka huruma ya MSAJILI, hapana. Tunaweka huu UPUMBAVU hapa kuonyesha mbogamboga walivyo WAPUMBAVU. Mwenyekiti wa wanawake wa mbogamboga wote ndiyo huyu? MSAJILI atajikausha kama anaaga maiti. Huyu maza ubongo wake ameacha mochwari? Sasa angetufanya nini? Angetuua wote? Sisi tukisema haya maneno, watavumilia? Je, ana uhakika bila bunduki za DOLA hawa mbogamboga wanatuweza? Maza kama huyu, anamuweza nani? Anyways, MAVAMPAYA yanataka damu. YAMEPAGAWA.
Martin Maranja Masese29,765 görüntüleme • 2 ay önce

Jana usiku saa nane, nimepata taarifa kutoka kwa watu walikuwepo Boardrom Bar, Sinza Mapambano, Dar es Salaam askari wa jeshi la polisi wamevamia na kuanza kukamata wanawake wanaojiuza Katika ubishani na walinzi wa Boardroom Bar, polisi wakafyatua risasi ambayo ilimpiga kichwani mlinzi mmoja wa Boardroom na kumuua. Hadi sasa hatujasikia taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi Katika video hizo, unamuona askari mmoja ameingia hadi ndani ya Boardroom ameshika bunduki akilenga wateja. Ni jambo la kusikitisha sana kuona jeshi la polisi likihangaika na nyege za watanzania NB; yeyote ambaye anazo taarifa kamili kuhusu tukio hili, atujulishe. Inawezekana kabisa wamiliki wa Boardroom wakataka jambo limalizike kimya kimya, lakini LAZIMA haki za huyo mlinzi zipatikane.
Martin Maranja Masese268,854 görüntüleme • 2 yıl önce