
Martin Maranja Masese
@IAMartin_ • 613,152 subscribers
MMM | Sperm That Won The Race | Cogito, ergo Sum | Patria o Muerte, Venceremos |
Shorts
Videos

Kubaaaaabake. Masela wamekataa porojo. Zimeletwa stori za awamu ya sita, watu wamezomeaa balaa. Watu wapo kwenye burudani unawaletea habari za awamu ya sita. Tunajenga arenaaa. Tunajenga arenaaaa. Tuna, tuna, tuna miaka nenda rudi. Masela wamekataa porojo. 😁
Martin Maranja Masese104,363 Aufrufe • vor 3 Monaten

Tumepiga stori mbili tatu na Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu. Mahakama imesema hukumu itatoka Novemba 06, 2026. Tumemhakikishia kwamba Christmas tutakuwa pamoja na tutafungua shampeni kuisheherekea. TAL ametuasa tusibweteke kwani mbele kuna mzigo mzito—sisi CHADEMA tukiyeyusha tu, nchi imeshakwenda na maji. Sisi ndiyo tutaikomboa nchi hii kutoka kwa wateka nyara. Cheameni, amesisitiza kimasta kabisa “mimi nitatoka, nikitoka ni kazi.”
Martin Maranja Masese23,218 Aufrufe • vor 24 Tagen

Leo baada ya kesi kuhairishwa, nimemuomba Mwenyekiti Tundu Antiphas Lissu atupe ujumbe wa siku. Kwa kuzingatia leo ni siku ya demokrasia, Tundu Lissu ametoa wito kwa Watanzania – “Demokrasia haidondoki kutoka mbinguni; inapiganiwa na ina gharama zake. Ukitaka demokrasia, lazima uwe tayari kulipa bei inayotakiwa na historia.” #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese34,180 Aufrufe • vor 1 Monat

Tundu Lissu. The man, the myth, the legend. Mwenyekiti Tundu Antiphas Lissu amemaliza kutoa hoja zake za mwisho (final submission) katika kesi ya uhaini inayomkabili. Ujumbe wake ni kwamba TUSIOGOPE. Nimemfikishia ule ujumbe wa kiduanzi wa MaCCM kwamba “vyombo vyote vya ulinzi na usalama ni mali ya CCM” na TAL amesema angalau wamethibitisha na wajibu wetu sasa ni kupambana kuvunja mfumo huu wa chama kimoja. #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese22,582 Aufrufe • vor 26 Tagen

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akiwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini ya uongo dhidi ya Serikali ya CCM, ametoa wito kwa wananchi kutonyamaza pindi haki za wengine zinapokiukwa. Kwa siku ya pili mfululizo, Tundu Lissu ameendelea kuhoji alipo aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM na Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, huku akiwataka viongozi wa dini, hasa maaskofu wa Kanisa Katoliki, kukemea vitendo visivyo vya haki vinavyoendelea nchini.
Martin Maranja Masese24,411 Aufrufe • vor 29 Tagen

Huyu kiumbe amesema ukweli, jinsi MaCCM wanavitumia vyombo vya dola kwa maslahi yao binafsi. Ni uthibitisho ambao waliuficha gizani. Wameamua kufunguka na kusema ukweli. Watanzani wenzangu, lazima upuuzi huu tujibu kwa kiwango cha kutosha. Tusipuuze. MaCCM wanajaribu kutumia uelewa hafifu wa wananchi katika masuala ya katiba, kupotosha. 1.Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kwamba Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Mamlaka ya chama (CCM), Sheria ya 1984 Na.15, ilitungwa wakati wa chama kimoja, (Ibara ya 10 imefutwa na Sheria Na.4 1992). CCM ni chama cha siasa, siyo dola. CCM siyo mamlaka ya nchi. 2.Ibara ya 4 ya Katiba ya JMT inataja vyombo vinavyotekeleza mamlaka ya nchi: Serikali, Mahakama, Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa maeneo yake ya mamlaka. CCM haijawekwa katika Ibara hiyo kama chombo cha mamlaka ya nchi. Hili ni jambo la msingi: chama cha siasa si chombo cha dola kwa sababu tu kinaongoza Serikali. Hii ieleweke vizuri. 3.Ibara ya 8(1) ya katiba ya Tanzania ndiyo inatoa jibu la moja kwa moja zaidi. Katiba inaeleza kwamba: Mamlaka yote kuhusu nchi hutoka kwa wananchi. Na inaendelea kueleza kwamba; Serikali inapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano, lengo kuu la Serikali ni ustawi wa wananchi, na Serikali inawajibika kwa wananchi. 4.Ibara ya 147(2) inasema Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndiyo inaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka majeshi kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania. Katiba ya Tanzania haijasema kwa ajili ya CCM. Hapo ndipo kauli hii ya kipumbavu inapogongana moja kwa moja na Katiba. Katiba ya JMT inataja nchi na wananchi; haisemi chama tawala. 5.Ibara ya 147(3) inakataza askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kujiunga na chama cha siasa, isipokuwa haki yake ya kupiga kura. Ibara hiyo inawahusu JWTZ, Polisi, Magereza na JKT. Kama vyombo hivyo vingekuwa mali halali ya CCM, kwa nini Katiba inakataza askari kujiunga na chama cha siasa? Hili ni hitaji la kutenganisha taasisi za usalama na ushindani wa vyama. 6.Ibara ya 148 inamtambua Rais akiwa Amiri Jeshi Mkuu, si Mwenyekiti wa CCM wala Katibu wa CCM. Mamlaka hayo yanatokana na nafasi ya kikatiba ya Rais, si uanachama wake katika chama. CCM ni chama cha siasa siyo dola. Serikali ni chombo cha dola. Vyombo vya ulinzi na usalama ni taasisi za kikatiba/kisheria za dola. Rais ana mamlaka ya kikatiba kama Amiri Jeshi Mkuu 7.Ibara ya 20(1) inampa kila mtu uhuru wa kujiunga na chama na Ibara ya 21(1) inampa kila raia haki ya kushiriki katika utawala wa nchi moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa. Leo chama A kinaongoza serikali, kesho chama B kinaweza kushinda uchaguzi. JWTZ, Polisi, Magereza na taasisi nyingine za dola haziwezi kubadilika kuwa mali ya chama cha siasa. 8. Katiba haielezi vyombo vya ulinzi na usalama ni mali ya CCM. CCM ni chama cha siasa tu; JWTZ, JKT, Polisi, Magereza ni taasisi za dola. MaCCM acheni kuchanganya chama na Serikali Ibara ya 147(2) inaeleza wazi Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaweza kuunda na kudumisha majeshi kwa madhumuni ya “ulinzi na usalama wa eneo na wananchi wa Tanzania.” Hakuna CCM hapo 9.Ibara ya 148 ya Katiba inampa Rais mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu — si kwa kuwa ni mwanachama wa CCM. Kugeuza taasisi za dola kuwa ‘mali ya CCM’ ni kuchanganya chama na dola Kuyaita ‘mali ya CCM’ mamlaka ya Kikatiba ya RAIS ni kupotoka. CCM inaweza kuongoza Serikali; Katiba ya JMT haibadiliki kuwa mali ya CCM, taasisi za dola hazibadiliki kuwa mali za CCM 10.Katika mfumo wa kikatiba wa vyama vingi, uaminifu wa askari unatakiwa kuwa kwa Katiba na nchi, si kwa chama cha siasa. Hilo ndilo linalofanya Ibara ya 147(3) kuwa na maana zaidi hapa Vyombo hivi vimeanzishwa kwa mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya nchi na wananchi, ndani ya mfumo wa Katiba si mali ya chama cha siasa. Katiba Mpya is a must MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Martin Maranja Masese22,157 Aufrufe • vor 27 Tagen

CHADEMA sasa hivi si chama cha siasa tu, ni imani iliyozama mioyoni mwa watu! Baada ya kushiba nondo za maana kutoka kwa viongozi, wananchi wenyewe wamemwaga upendo kwa kuchangia kiasi cha TZS 5,992,255 kidogo kidogo (Tone kwa Tone), kisha burudani ya ngoma za ukombozi ikafuata. CCM ili ipate vibe kama hili, ni lazima imwage mabilioni kusomba wasanii ili kuvuta watu. #PeoplesPower #KatibaMpya #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese95,873 Aufrufe • vor 5 Monaten

Ndugu Madenge katika jambo hili umenisikitisha sana. Sikutegemea unaweza kuwa sehemu ya kejeli hizi. Hao wengine ni wapumbavu tu ukijumlisha na huyo Masanja (hawakunishangaza) Siyo kwamba mnachekesha, mmeonesha ujinga wenu. Mmeonesha jinsi mlivyo machawa wa watawala. Na mmejitenga na jamii kubwa ya watanzania. Mmechagua kuwa maadui wa umma. Twitter (X) mnalalamika kuhusu umeme kila siku, watu tunakwenda barabarani na mabango ya umeme mnakwenda kutukejeli? Kweli nimeamini sasa, kuwa “paid slave” ni dhambi. Unatumikishwa tu. Masanja hajaenda shule. Hakuna ubongo kichwani, anawezaje kuwapa maudhui (content) za kipunbavu hivi na mkazitumia? Au ninyi pia mmekubali kuwa wapumbavu kama yeye? Mbaya zaidi ni kwamba wote katika kundi hilo hakuna hata ambaye ana diploma au degree ya uandishi wa habari na utangazaji. Wameokotwa kijanja-kijanja na leo wanakejeli watanzania. Kama mmeshindwa kuandamana na hamtaki, maiwadhihaki wananchi hao wachache ambao wamekubali kuandamana kwa gharama zao wenyewe. Mnapata faida gani wakiacha kuandamana? Naelewa, watangazaji wa EFM hapo mnalipwa vizuri. Maumivu makubwa ya ugumu wa maisha na kupanda kwa bidhaa sokoni hakuwagusi. Labda ndiyo maana mnakejeli haya maandamano. Mnakosea sana. Mtaani kuna maumivu makali. Wananchi hawana maji wala umeme. Sukari bei juu na mtaani haipo. Miundombinu ni duni na serikali inakusanya kodi. Jukwaa pekee kueleza hayo ni katika maandamano. Biashara za watu mtaani zinakufa. Mitaji yao imepotea. Media ambayo ingelitumika kufikisha ujumbe kwa serikali ndiyo inakejeli maandamano ambayo yanatumika kupaza sauti za watu mtaani. Maandamano yale yanatumika kufikisha ujumbe kwa watawala. Ukisoma mabango wananchi wameandika na kubeba kero zao, wanatembea kwa zaidi ya kilometa 20, kuziwasilisha, mnawakejeli? Mnatumika na DOLA kwa nia ovu. Mnafifisha morali ya umma kujitokeza katika maandamano ya amani ambayo yanasaidia kubeba sauti kubwa ya umma kwenda kwa watawala. Mnakosea sana. Hili ni tatizo kubwa. Kwa kuwa mmiliki wa EFM ni mwana CCM kindakindaki anatumia chombo chake cha habari kukejeli shughuli za kisiasa na maandamano ya kiraia. Huu ni UPUMBAVU. Kazi ambazo mnazifanya hapo leo EFM/ETV, Malcom X alizieleza vizuri sana mwaka 1963. “house Negro” na “field Negro.” Ninyi watangazaji wa EFM ni ‘house negro’ kwa matendo na tabia zenu hizi. House negro aliishi katika nyumba ya bwana wake - ghorofa au dari - lakini bado aliishi katika nyumba ya bwana, alivaa mabaki ya nguo za bwana wake. Alikula chakula bwana wake alikiacha mezani. House negro alijatanabaisha kila mara kwa maana ileile ambayo bwana wake alijitambulisha. House negro alijiweka katika daraja sawa na bwana wake, wakati huo ni myumwa na kijakazi. Bwana wake aliposema, “Tuna chakula kizuri,” alisema, “Ndiyo, sisi tuna chakula kingi kizuri.” Bwana wake aliposema “tuna nyumba nzuri hapa,” alisema, “Ndiyo, tuna nyumba nzuri hapa.” Bwana wake akiugua, house negro angemuuliza “Kuna nini bosi, sisi wagonjwa?”. Maumivu ya bwana wake yalikuwa maumivu yake mara mbili. Aliumia kuliko hata watoto wa bwana wake. House negro ilimuuma zaidi bwana wake kuwa mgonjwa kuliko yeye mwenyewe kuwa mgonjwa. Hawa sasa ndiyo wafanyakazi wa EFM/ETV. Hizi ni tabia zao za kitumwa, house negro. But I know, nothing you can if you’re just a paid slave. 🙏🏽 Brigedia Mtikila, MMM.
Martin Maranja Masese457,037 Aufrufe • vor 2 Jahren

Mwenyekiti Tundu Lissu amesema hataki upumbavu wa kutembelewa usiku gerezani. Hataki vikao vya gizani. Yupo tayari kuishi gerezani hadi haki ipatikane, kwa kuwa anapigania haki, yupo tayari gharama. Kama unampenda sana, njoo mahakamani. #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese35,345 Aufrufe • vor 1 Monat

GIRISHONI amefanya niipakue hii makala, tusikilize wote. Wote sasa tukatazame makala ya BBC AFRICA EYE ya mwaka 2026 inaangazia mapambano ya kisiasa ya Tundu Lissu na jaribio la mauaji dhidi yake la mwaka 2017, ikionyesha juhudi zake zinazoendelea za kudai mageuzi ya mfumo wa uchaguzi nchini Tanzania licha ya kukabiliwa na mashtaka ya uhaini aliyopewa mwaka 2025. Halafu baadae tutapata muda wa kujadili kipeperushi cha Serikali katili ya CCM kilichotolewa na GIRISHONI.
Martin Maranja Masese58,825 Aufrufe • vor 3 Monaten

MaCCM wamefilisika kisiasa; wamebaki kutegemea nguvu za dola na Mahakama, ambako bado tunawashinda kwa hoja. Sasa wanajaribu kuzuia CHADEMA kuzungumza na waandishi wa habari nje ya viunga vya Mahakama. Hii ni baada ya kesi ya kikatiba inayohusu haki za Tundu A.M Lissu gerezani ikiwa ni pamoja na haki ya faragha kwa mawakili wake. Polisi wanadai hii ni amri kutoka kwa Msajili wa Mahakama. Nafikiri, tutaihoji amri hii Mahakamani na kuhakikisha sheria inatunzwa, inalindwa na kuheshimiwa! #FreeTunduLissu #TunduLissuSioMhaini #FreeTunduLissu #TunduLissuSioMhaini
Martin Maranja Masese52,645 Aufrufe • vor 3 Monaten

Kesi ya uhaini wa uongo na kubumba tu inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A.M Lissu imehairishwa saa tano asubuni leo baada ya upande wa mashtaka kusema hawana shahidi mwingine kwa leo baada ya shahidi wa 16 wa Jamhuri, ACP Amin Mahamba kumaliza kutoa ushahidi wake. TAL ameeleza Mahakama hilo halitakiwi kutokea tena na kuanzia kesho Jamhuri wabebe mashahidi wa kutosha kwa siku moja #FreeTunduLissu #TunduLissuSioMhaini
Martin Maranja Masese39,948 Aufrufe • vor 2 Monaten
0:45
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Fungua kwa tahadhari; ⚠️ Picha za kutekwa na kuuawa kwa Joshua Mollel (21), mwanafunzi wa kilimo kutoka Tanzania. Serikali ya Tanzania ilitangaza kwamba, Joshua Mollel aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la HAMAS mnamo tarehe 7 Oktoba 2023. Pumzika kwa amani Joshua 🙏🏽
Martin Maranja Masese368,285 Aufrufe • vor 2 Jahren

Ndugu yetu Edgar Mwakabela, SIR TIVA amepatikana katika hifadhi ya Katavi. Ameteswa na ameumizwa sana. Tunaomba watu wa Katavi mtusaidie haraka sana apate msaada wa matibabu. Rais Samia Suluhu umefika huku? Tulisema hatuwezi kurudi katika zama hizi za kuwatesa wakosoaji wako.
Martin Maranja Masese290,198 Aufrufe • vor 2 Jahren

Tundu Lissu amehitimisha kutoa ushahidi wake wa msingi (examination-in-chief) katika kesi ya uhaini inayomkabili. Upande wa Jamhuri (mashtaka) umeanza na unaendelea kumhoji/kumfanyia dodoso (cross-examination). Jaji Dunstan Nduguru ameahirisha shauri hadi kesho, Jumatano, 27 Agosti 2026, saa 3:00 asubuhi.
Martin Maranja Masese29,458 Aufrufe • vor 1 Monat

Back in the High Court (Dar es Salaam) today as Vice-Chairman John Heche faces cross-examination by State lawyers. We remain steadfast in our support for Chairman Tundu Antiphas Lissu as he confronts these treason charges. To stand by him throughout this trial is not merely an act of solidarity; it is a historic duty, and one we undertake with profound pride. #FreeTunduLissu #StandWithLissu
Martin Maranja Masese20,680 Aufrufe • vor 1 Monat

Jana niliandika ujumbe nikikosoa kitendo cha Mzee MBOWE kumuombea msamaha SABAYA. Nimepata maoni mengi; wengine wakisema sikuwa sawa. Ipo hivi. Kuna mambo katika siasa hayawezi kufutwa na maneno laini na mepesi ya “msamaha,” hususani msamaha usiotoka kwa mtenda dhambi mwenyewe. Utawala wa SABAYA katika wilaya ya Hai haukuwa wa kisiasa tu; ulikuwa ni utawala wa chuma na ukatili uliopitiliza. Hata Mzee MBOWE anafahamu hilo. Makosa ya uhujumu uchumi na unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery) yaliyomfunga gerezani wakati ule, ni tone dogo sana katika bahari ya unyama wake. Wapo watu walitekwa, kuteswa, na kuachwa na vilema vya kudumu. Kusema mtu huyu anastahili msamaha bila toba ya dhati kwa wahanga, si tu ni kosa, ni dhihaka. Miongoni mwa wahanga wa genge la SABAYA ni ndugu yetu Simon MNYAMPANDA, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai. Ndugu yetu aliteswa. Simon Mnyampanda aliteswa kwa umeme. Ameeleza wazi kwamba, alihojiwa kuhusu mahusiano yake na Mzee MBOWE. Mwisho, alipigwa misumari ya miguu. Huyu ni mtu aliyepata mateso hayo akimlinda Mzee MBOWE na CHADEMA. Leo Mzee MBOWE anajigeuza kadinali na kumuombea msamaha mtesaji SABAYA? Genge hilo halikuishia hapo. Genge hilo lilikuwa kama MAHARAMIA. Walivamia nyumbani kwa mgombea udiwani wa kata ya Narumu katika jimbo la Hai. Baada ya kumkosa, walitoa adhabu ya kinyama kwa watu waliokuwepo nyumbami kwa kuwakata masikio na sehemu nyingine. Nyumba nzima ilitapakaa damu. Hawa ni binadamu, si takwimu za kisiasa. Hawa watu waliotendewa mambo hayo wapo. Baadhi ya ushahidi wa masuala hayo nimeambatanisha katika makala hii. Inasikitisha kuona Mzee Mbowe anatumia mateso ya wafuasi wake kama mtaji wa kisiasa (political capital). Binafsi nimejiuliza maswali mengi tangu hiyo jana. Je, wahanga wameombwa msamaha na kufidiwa? Je, mateso yao yamekuwa ngazi ya makubaliano ya kisiasa? Hii si dharau kwa wale walioteswa wakikupigania? Sabaya anapaswa kuomba msamaha kwa waathirika, si kuombewa. Vinginevyo, hii ni michezo ya kumtengenezea mazingira ya kupata uteuzi katika Serikali ya CCM. Watu wa Hai hawajasahau. Damu na machozi ya wahanga bado vinadai haki. Msamaha bila toba ni baraka kwa ukatili mwingine ujao. Haki kwanza, msamaha baadaye. Binafsi, nilimheshimu Mzee Mbowe kiasi cha kumpa mwanangu wa tatu jina la “Freeman”. Leo hii, nahisi usaliti mkubwa moyoni mwangu kwa mambo hayo. Kunyamaza mbele ya usaliti huu si busara, bali ni upumbavu ambao kesho utatunyong’onyesha. Nimeandika ili kulinda hadhi ya jina la mwanangu. Siku mtoto wangu akiniuliza, nitamjibu kwa utimamu kabisa. “Nilitetea maana halisi ya ‘Freeman’ wakati jina hilo lilipotaka kuchafuliwa na siasa za kimaslahi.”
Martin Maranja Masese71,838 Aufrufe • vor 6 Monaten

Mchawi binadamu, paka anatumwa tu. MPEMBA ametumwa kumshambulia NAMBA MBILI wao na amembatiza jina la YUDA. Kosa lake ni kusema alipendwa sana na JIWE. Wamekasirika sana. Jamaa anasema JIWE alimtupa Brazil. Wanasema ametengwa hadi na familia ya ‘WHITE HAIR’. Eti ni kweli, wazee wa ‘Safari ya Matumaini’ mmemtenga 'Mzee wa Mustachi'? Sisi wengine tunafurahi. Kazi yetu moja tu, kuchochea kunu. Ushirika wa 'wanyonya damu' hauwezi kudumu. NB; kama wapo wengi, kwanini hakuna makofi? SIJAPENDA.
Martin Maranja Masese58,913 Aufrufe • vor 4 Monaten

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. Tupo tayari kuendelea na usikilizaji wa utetezi wa Mwenyekiti wetu, Tundu A.M. Lissu. Baada ya kukamilisha msingi wa ushahidi wa tabia yake njema (good character), Tundu Lissu ataelekeza hoja zake kwenye hati ya mashtaka ili kuonyesha kutokuwepo kwa kosa lolote la jinai linalokidhi vigezo vya uhaini. #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese27,577 Aufrufe • vor 1 Monat

Appearing as his own legal counsel, Tundu Antiphas Lissu delivers his closing argument today, September 28, 2026, in a high-stakes treason trial before three High Court judges in Dar es Salaam. The crowded courtroom burst into repeated applause as he stepped into the dock and greeted the crowd. #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese13,690 Aufrufe • vor 26 Tagen