James Mbowe's banner
James Mbowe's profile picture

James Mbowe

@JamesMbowe444,849 subscribers

Videos

JamesMbowe4's profile picture

Nimemsikiliza Mbunge wa Hai, (viti maalum) video aliyojirekodi akitoa tuhuma mbalimbali kumuhusu Mh Freeman Mbowe amezungumza Mengi katika hali ya kuutweza Utu wa Mh Freeman Mbowe akitoa tuhuma kadhaa kwenye video yake akiwa Dodoma . 1. Anasema Mh Mbowe ametangaza vita hali ya hatari akiwa Narumu Lakini hajasema ilikuwa tarehe ngapi. Na hiyo vita inaanza lini na akasahau mtu pekee kwa mujibu wa Katiba ya Nchi anayeweza kutangaza hali ya Hatari ni Rais pekee. Hii inaonyesha jinsi huyu bwana mdogo alivyo kishoia 2 Amesema Mbowe ametoka magereza akajenga ghorofa. 3 Anasema Mbowe hajawahi kutafuta hela, hela alizonazo alirithi kutoka kwa Baba yake yaani Mzee Aikaeli. 4 Amesema Mbowe ni tapeli wa kisiasa kwamba amewatapeli watu wa Hai kwa muda mrefu 5 Amesema Mbowe alikuwa anashawishi watu kwa pombe ya kiroba, Gongo sasa hivi amebadili mbinu anatumia Sukari kuwarubuni watu. 6 Hapa akaenda mbali zaidi na kusema historia ya Mzee Aikaeli na mwanae Freeman Mbowe ni watu wa Damu za watu hii ni tuhuma nzito sana 7 Akasema Mbowe amewatumia watu wa Hai kama condom na kis hha kuwatupa 8 Anasema Hata Mke wa Mbowe hataki kukaa naye 9 Akasema siku Mbowe akimchokoza atasema yote. Ushauri wangu kwa Mh Freeman Mbowe tuhuma hizi alizotoa huyu dogo ni nzito sana, Nashauri haraka iwezekanavyo jambo hili lipelekwe mahakamani ili huyu dogo akathibitishie mahakama juu ya haya aliyoyasema. Katika historia ya Hai hatujawahi kuwa na Mbunge kilaza kama huyu dogo, Mh Rais @samia_suluhu_hassan Mh Katibu Mkuu wa CCM Emmanuel Nchimbi matokeo ya kuuwa mfumo wa Demokrasia wa kupata viongozi wanaotokana na kura za wananchi ndio tunapata sampuli hizi za viongozi ambao hawastahili Hata kuongoza kundi la mbuzi. Huyu dogo ameingia Madarakani kwa gharama za watu wa Hai kupigiliwa misumari miguuni, kukatwa Masikio, kuingizia watu chupa sehemu zao za siri, kupiga watu shoti, kukata watu ndevu kwa sime asifikiri tumesahau. Hiki kiburi Najua umekipata zaidi baada ya kuona Nia ovu ya kuharibu Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kuengua wagombea wetu pasipo na sababu ukaona sasa unaweza kufungua mdomo wako na kuutweza Utu wa Freeman Mbowe hapana sitakubali Ujinga huu kwa gharama yoyote ile.

James Mbowe

46,725 views • 1 year ago

No more content to load