Samia Suluhu's banner
Samia Suluhu's profile picture

Samia Suluhu

@SuluhuSamia1,828,834 subscribers

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. President of the United Republic of Tanzania

Shorts

Hongereni Yanga kwa ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii. #KariakooDerby Huku Taifa likiendelea kuchapa kazi, tunatarajia burudani safi ya msimu mpya wa Ligi Kuu toka kwenu Watani wa Jadi pamoja na Azam, Coastal Union, Dodoma Jiji, Fountain Gate, JKT, KMC, Kagera Sugar, KenGold, Mashujaa, Namungo, Pamba Jiji, Singida Black Stars, Tabora United na Tanzania Prisons. Kila la kheri.

Hongereni Yanga kwa ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii. #KariakooDerby Huku Taifa likiendelea kuchapa kazi, tunatarajia burudani safi ya msimu mpya wa Ligi Kuu toka kwenu Watani wa Jadi pamoja na Azam, Coastal Union, Dodoma Jiji, Fountain Gate, JKT, KMC, Kagera Sugar, KenGold, Mashujaa, Namungo, Pamba Jiji, Singida Black Stars, Tabora United na Tanzania Prisons. Kila la kheri.

153,704 views

Videos

SuluhuSamia's profile picture

Dar es Salaam 08.02.2025 My Welcome and Opening remarks at the Joint Southern African Development Community (SADC) and the East African Community (EAC) Heads of State and Government Summit on the prevailing security situation in the Eastern Democratic Republic of Congo (DRC). As regional leaders, history will judge us harshly if we remain still and watch the situation worsen day by day. In line with the principle of African solutions for Africa’s problems, our countries have a collective responsibility to ensure we urgently address the existing security challenges that have heavily impacted the well-being of innocent civilians. This joint summit meeting in Dar es Salaam presents an opportunity to recommit our collective efforts in addressing the conflicts, and reaffirm our sustainable peace and stability in the entire EAC and SADC regions. It is crucial that we find a durable solution that upholds sovereignty, promotes inclusivity and ensures that the people of DRC can enjoy the durable peace and security that they have been yearning for, for decades. As a steadfast advocate for peace in Africa, Tanzania is deeply concerned about the persistent insecurity in Eastern DRC. The ongoing conflict not only destabilizes our brotherly nation, but also puts serious dents on our consistent efforts to enhance regional integration. My country remains committed to supporting ongoing diplomatic initiatives to end this conflict, and so we call on all parties involved to positively engage in negotiations, prioritize the well-being of the people, and commit to a peaceful co-existence.

Samia Suluhu

162,834 views • 1 year ago

SuluhuSamia's profile picture

Mapema leo katika Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro niliposhiriki Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa Mwaka 2024 na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jeshi letu limepiga hatua kubwa katika kipindi cha miaka 60. Nimeendelea kusisitiza kwamba huduma bora za kipolisi kwa umma wa Watanzania zitatokana na kubadilika kifikra, usimamizi wa sheria na matumizi ya TEHAMA. Serikali itaendelea na kazi ya kulijengea uwezo kimiongozo na kibajeti. Kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao ikiwemo haki ya uhai ambayo inalindwa na Katiba yetu. Kote duniani kupokwa kwa haki ya uhai hukemewa na Serikali na kuhakikisha vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinafanya uchunguzi na kupata majawabu, kama ambavyo nchi yetu pia inafanya. Maisha ya mwanadamu yeyote yule yana thamani isiyomithilika. Katika hali yoyote ile uhai wa mwanadamu ni jambo adhimu sana. Uhai wa kila Mtanzania unalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama inavyoeleza katika Ibara ya 14. Hatuhitaji kuelekezwa na mtu yeyote jinsi ya kutekeleza jukumu hili kwani Katiba yetu tayari ina maelekezo ya kutosha. Kama Amiri Jeshi Mkuu nimeapa kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndani yake ipo haki ya kuishi, na kwamba nitafanya kila linalowezekana kuimarisha ulinzi na uhai wa kila Mtanzania. Katika hili sina muhali. Falsafa yetu ya 4R inalenga kutuleta pamoja zaidi kama Watanzania na si mwanya wa kuvunja sheria zetu na kuifarakanisha nchi yetu. Huku Serikali na vyombo ya ulinzi na usalama vikiendelea kutekeleza jukumu lake la kulinda haki hii ya uhai, kama jamii kwa sauti moja tuendelee kukemea na kujali damu ya kila Mtanzania kwa uzito ule ule bila kujali ni nani, anatoka wapi, ama kundi gani. Uhai ni uhai. Tukemee pia uovu wa aina zote katika jamii yetu ikiwemo wale wanaopanga kuvuruga amani ya nchi yetu.

Samia Suluhu

123,803 views • 1 year ago