
Samia Suluhu
@SuluhuSamia • 1,828,834 subscribers
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. President of the United Republic of Tanzania
Shorts
Videos

Leo imekuwa siku ya kihistoria kwa nchi yetu ambapo nimezindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la Mwaka 2024). Hatua hii ni utekelezaji wa maelekezo niliyotoa bungeni Aprili 2021, ambapo maboresho haya yamelenga kuiwezesha nchi yetu kuendana na mabadiliko makubwa yaliyotokea kwa miongo miwili ndani na nje ya nchi. Ninawapongeza wote mlioshiriki kuandaa sera hii, hasa wananchi mliotoa maoni, kwani mmeshiriki katika kujenga hatma ya nchi yenu na mmeweka alama isiyofutika. Aidha, nimeielekeza Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukuwa hatua za haraka, ikiwemo kutoa ufafanuzi, pindi kauli au matamko yanapotolewa kuhusu nchi yetu ili kudhibiti upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu. Nchi yetu itaendelea kubaki salama, yenye amani, umoja na utulivu, na hakuna mtu yeyote atakayetuondolea nguzo hizi muhimu.
Samia Suluhu599,341 次观看 • 1 年前

Leo alasiri nimetangaza uteuzi wa Baraza la Mawaziri pamoja na Naibu Mawaziri. Kwa pamoja, tutafanya kazi ya kutekeleza jukumu la msingi la kuwatumikia wananchi. Dhamana hii ni wajibu na pia deni ambalo tunapaswa kuwalipa wananchi kwa kuwatumikia kwa ari, bidii na uaminifu mkubwa. Ninawatakia kila la kheri. Mwenyezi Mungu awasimamie na kuwaongoza.
Samia Suluhu207,683 次观看 • 7 个月前

Sambamba na mambo mengine, katika hotuba yangu ya kulifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nimevielekeza vyombo vya sheria hasa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwafutia makosa vijana na watoto wetu ambao kwa kutokujua, walifanya makosa kwa kufuata mkumbo Oktoba 29 mwaka huu. Nikiwa Mama na Mlezi, ninawasihi vijana wote kuendelea kulinda amani na mshikamano wa nchi yetu, na hata siku moja msikubali kushawishiwa kuichoma nchi yenu wenyewe.
Samia Suluhu102,129 次观看 • 7 个月前

Sehemu ya kazi siku ya leo nilipokutana na kufanya mazungumzo na mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, Ikulu, Dar es Salaam. Tumekuwa na mjadala mzuri kuhusu kushirikiana katika masuala ya uhifadhi pamoja na utafiti. Sambamba na hayo, nimesikiliza dhamira ya Sir Jim Ratcliffe kuitumia Klabu ya Manchester United kutangaza utalii wa nchi yetu, ambapo pia nimemkaribisha kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Michezo (Sports Academy) hapa nchini. Nimepokea na kumshukuru kwa salamu za kheri toka kwa Kocha Ruben Amorim kwa niaba ya wachezaji wa Klabu ya Manchester United, na za Kocha Mstaafu, Sir Alex Ferguson.
Samia Suluhu160,336 次观看 • 1 年前

Hotuba yangu mapema leo Ikulu, Dodoma nilipozindua Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025. Nina imani na uwezo na weledi wa tume hii. Taarifa yao juu ya kiini cha tatizo itatuongoza kujielekeza kwenye hatua sahihi za kiutendaji na mazungumzo ya kuleta maelewano, kuimarisha usalama, amani na umoja wetu. Mwenyezi Mungu Mtukufu awasimamie na kuwaongoza.
Samia Suluhu84,637 次观看 • 7 个月前

Dar es Salaam 08.02.2025 My Welcome and Opening remarks at the Joint Southern African Development Community (SADC) and the East African Community (EAC) Heads of State and Government Summit on the prevailing security situation in the Eastern Democratic Republic of Congo (DRC). As regional leaders, history will judge us harshly if we remain still and watch the situation worsen day by day. In line with the principle of African solutions for Africa’s problems, our countries have a collective responsibility to ensure we urgently address the existing security challenges that have heavily impacted the well-being of innocent civilians. This joint summit meeting in Dar es Salaam presents an opportunity to recommit our collective efforts in addressing the conflicts, and reaffirm our sustainable peace and stability in the entire EAC and SADC regions. It is crucial that we find a durable solution that upholds sovereignty, promotes inclusivity and ensures that the people of DRC can enjoy the durable peace and security that they have been yearning for, for decades. As a steadfast advocate for peace in Africa, Tanzania is deeply concerned about the persistent insecurity in Eastern DRC. The ongoing conflict not only destabilizes our brotherly nation, but also puts serious dents on our consistent efforts to enhance regional integration. My country remains committed to supporting ongoing diplomatic initiatives to end this conflict, and so we call on all parties involved to positively engage in negotiations, prioritize the well-being of the people, and commit to a peaceful co-existence.
Samia Suluhu162,834 次观看 • 1 年前

Mapema leo nchi yetu ilipoandika historia kwa uzinduzi wa Treni ya Kisasa ya Umeme (SGR) ambapo pia nimeitumia kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma. Baada ya kukamilika kwa kazi hii njema, sasa tumeanza kazi ya vipande vipya vya Tabora kwenda Isaka, Isaka hadi Mwanza, pamoja na kile cha kutoka Tabora hadi Kigoma, na kisha kuunganisha na nchi majirani zetu ili kufungua milango zaidi ya fursa za kiuchumi kwa wananchi wetu.
Samia Suluhu205,467 次观看 • 1 年前

Excellencies and distinguished guests, delegates, partners and friends, welcome to Tanzania for the Mission 300 Africa Energy Summit to be held in Dar es Salaam on the 27th and 28th of January 2025. This summit marks a historic moment in our collective efforts to accelerate energy access across Africa, and to take bold actions to power our continents's future. Karibuni sana.
Samia Suluhu153,604 次观看 • 1 年前

Mapema leo katika Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro niliposhiriki Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa Mwaka 2024 na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jeshi letu limepiga hatua kubwa katika kipindi cha miaka 60. Nimeendelea kusisitiza kwamba huduma bora za kipolisi kwa umma wa Watanzania zitatokana na kubadilika kifikra, usimamizi wa sheria na matumizi ya TEHAMA. Serikali itaendelea na kazi ya kulijengea uwezo kimiongozo na kibajeti. Kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao ikiwemo haki ya uhai ambayo inalindwa na Katiba yetu. Kote duniani kupokwa kwa haki ya uhai hukemewa na Serikali na kuhakikisha vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinafanya uchunguzi na kupata majawabu, kama ambavyo nchi yetu pia inafanya. Maisha ya mwanadamu yeyote yule yana thamani isiyomithilika. Katika hali yoyote ile uhai wa mwanadamu ni jambo adhimu sana. Uhai wa kila Mtanzania unalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama inavyoeleza katika Ibara ya 14. Hatuhitaji kuelekezwa na mtu yeyote jinsi ya kutekeleza jukumu hili kwani Katiba yetu tayari ina maelekezo ya kutosha. Kama Amiri Jeshi Mkuu nimeapa kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndani yake ipo haki ya kuishi, na kwamba nitafanya kila linalowezekana kuimarisha ulinzi na uhai wa kila Mtanzania. Katika hili sina muhali. Falsafa yetu ya 4R inalenga kutuleta pamoja zaidi kama Watanzania na si mwanya wa kuvunja sheria zetu na kuifarakanisha nchi yetu. Huku Serikali na vyombo ya ulinzi na usalama vikiendelea kutekeleza jukumu lake la kulinda haki hii ya uhai, kama jamii kwa sauti moja tuendelee kukemea na kujali damu ya kila Mtanzania kwa uzito ule ule bila kujali ni nani, anatoka wapi, ama kundi gani. Uhai ni uhai. Tukemee pia uovu wa aina zote katika jamii yetu ikiwemo wale wanaopanga kuvuruga amani ya nchi yetu.
Samia Suluhu123,803 次观看 • 1 年前

Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dodoma, Mei 30, 2025 Siku ya pili ya mkutano wetu jijini Dodoma ambapo kwa pamoja tumezindua Ilani ya CCM 2025-2030. Ilani hii imeandaliwa kwa weledi mkubwa kwa manufaa ya Taifa letu, ikilenga zaidi katika kuchochea mapinduzi ya kiuchumi, kuzalisha ajira na kuboresha maisha ya wananchi. Vipaumbele vingine ni kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, kukuza matumizi ya sayansi na teknolojia, kudumisha amani, utulivu na usalama, kudumisha utamaduni, na kukuza sanaa na michezo na kuongeza kasi ya maendeleo vijijini. Aidha, tukielekea kwenye uchaguzi mkuu, nimezielekeza kamati za kuteua wagombea kutenda haki ili tupate viongozi watakaotekeleza ilani kikamilifu. Pia, nimewaasa wanachama wa CCM kuimarisha umoja na mshikamano, tuingie kwenye uchaguzi tukiwa wamoja, ili chama chetu kipate ushindi mkubwa na turudi kuendeleza kazi ya kuwatumikia wananchi wote.
Samia Suluhu70,016 次观看 • 1 年前

Kijiji cha Chamwino, Dodoma, 17 Mei 2025 Nilipoungana na wanakijiji wenzangu waliojitokeza kwa wingi kujiandikisha na wengine kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Mpigakura. Nimewakumbusha kuwa Uchaguzi ni sauti yetu wananchi, hivyo sote tujiandae kushiriki kikamilifu.
Samia Suluhu67,320 次观看 • 1 年前


