The Chanzo's banner
The Chanzo's profile picture

The Chanzo

@TheChanzo79,017 subscribers

We Are Bilingual Multimedia Storytellers Looking At The World From Ground Up. Una habari? WhatsApp/Telegram 0753815105

Videos

TheChanzo's profile picture

Sheikh Mwaipopo Anakingiwa Kifua na Wenye Mamlaka? Gumzo kubwa linaendelea mtandaoni kufuatia Katibu wa Baraza la Habari la Waislamu nchini Tanzania (BAHAKITA) Sheikh Said Mwaipopo kuendelea kutangaza vikosi vyake akivipa majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama. Wengi wameonesha kushtushwa zaidi baada ya Julai 04, 2026, Mwaipopo kujitokeza pamoja na vijana waliovalia kininja, akisisitiza ni watu wenye mafunzo ya kutoa mateso, mapambano na ulinzi na kushambulia. 'Kwa mujibu wa ibara ya 147 ya Katiba yetu inaanzisha Majeshi: Jeshi la Polisi Jeshi la Wananchi, pamoja na jeshi la magereza. Ukisoma pia sheria ya Jeshi la Polisi pamoja na huduma saidizi ni dhahiri shahiri kwamba jukumu la ulinzi, la usalama wa raia na mali zao litakuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi," anaeleza Wakili Maduhu William akizungumza na The Chanzo. "Sasa kama tumeanza kuruhusu watu binafsi kuwa na majukumu ya kiulinzi ambayo kwa uwazi ni ya Jeshi la Polisi, nafikiri hiyo haijakaa sawa. Kwa sababu kila mtu akiamua nchi hii sasa atoke hadharani aseme nina kikundi cha mbwa koko, nina kikundi cha nyuki, au cha chui mimi nafikiri kama taifa hatuwezi kufika," anafafanua zaidi Wakili Maduhu. Wengi wameonesha hofu wakilinganisha kikundi cha Mwaipopo na vikundi vya kigaidi kama Boko Haram, ambavyo msingi wa kuanzishwa hudai ni kutetea wananchi. "Kumbukumbu zangu zinaniambia ni mara ya pili inaweza ikawa mara ya tatu [anajitokeza] inazua mashaka zaidi inaonyesha kwamba huyu mtu ana baraka za mamlaka kwa sababu, mamlaka ambazo zinahusika na hicho anachokisema kazi anayotaka kuifanya zipo," anaeleza Dk. Muhidini Shangwe, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu. Shangwe ambaye ni mtafiti na mtaalamu wa mifumo ya uongozi anaeleza kuwa hofu kubwa ya jambo kama la Mwaipopo ni kujenga msingi wa kutokuwa na utawala wa sheria. "Nadhani mara ya kwanza viongozi Waandamizi wa polisi namkumbuka Kamanda Muliro alisema kwamba naye amepata hizo taarifa lakini anafanya uchunguzi. Kwa hiyo wakati bado anafanya uchunguzi, huyu bwana ameibuka tena mara ya pili,sasa utakuwa uchunguzi juu ya uchunguzi. Lakini hii ni kiashiria kwamba,sijui nitaiweka vipi kuonesha kwamba hana baraka za mamlaka," aliongeza. Mwaipopo amedai kuwa kikundi chake pia kinafanya majukumu ya kufuatilia na kuchunguza maeneo mbalimbali, majukumu ambayo yanaingiliana na majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama. "Hao anaowaita Mbwakoko hawajasajiliwa kama kampuni ya ulinzi ambayo sheria zetu za nchi zinataka kampuni za ulinzi zisajiliwe kwa ajili ya kutoa huduma za kiusalama. Inashangaza kwa nini mpaka leo Jeshi la Polisi halijamchukulia hatua," anaeleza Wakili Maduhu. The Chanzo ilimuandikia Waziri wa Mambo ya Ndani juu ya suala hili, bado haijapokea majibu.

The Chanzo

10,393 Aufrufe • vor 2 Tagen