
The Chanzo
@TheChanzo • 79,457 subscribers
We Are Bilingual Multimedia Storytellers Looking At The World From Ground Up. Una habari? WhatsApp/Telegram 0753815105
Videos

'Mkipata nafasi msaidieni mke wangu',Mhadhiri UDOM anayeshitakiwa kesi ya ugaidi
The Chanzo62,271 Aufrufe • vor 13 Tagen

Kamwaga: ACT Wazalendo Ichukue Uongozi Kututoa Kwenye Mkwamo wa Kisiasa Dar es Salaam. Mwandishi wa habari mkongwe nchini Ezekiel Kamwaga ametoa wito kwa chama cha ACT Wazalendo kuchukua uongozi kuelekea kukwamua mkwamo wa kisiasa nchini kwani chama hiko kina wanasiasa wenye uzoefu na masuala hayo. Akizungumza kwenye mkutano wa kitaifa ulioandaliwa na chama cha ACT Wazalendo juu ya mkwamo wa kijamii na kisiasa uliopo Tanzania kufuatia matukio ya Oktoba 29, Kamwaga amesema kwa sasa ni kama kila upande upo kifungoni hivyo unahitajika utayari wa kisiasa kutoka mahali ambapo Tanzania imefikia sasa.
The Chanzo97,326 Aufrufe • vor 3 Monaten

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Afrika Kusini EFF Julius Malema amevishukia vyama tawala barani Afrika vilivyohusika na vuguvugu la uhuru ikiwemo CCM, ZANU-PF, SWAPO, FRELIMO na ANC kuwa kitakachowamaliza ni kifo cha asili ambacho hakikwepeki kwani havitaweza kujivua gamba ili kuendeleza ajenda ya ukombozi.
The Chanzo28,622 Aufrufe • vor 28 Tagen

Pro. Chachage alikerwa vyuo vikuu kushushwa hadhi kuwa kama shule za sekondari, anasema Dkt. Kamata Ameyasema haya kwenye mhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Agosti 14, 2026 katika kumbukizi ya miaka 20 tangu kifo cha mwanazuoni nguli wa Tanzania Prof, Chachage S. Chachage.
The Chanzo13,161 Aufrufe • vor 12 Tagen

Utata Kiongozi wa Dini Aliyetangaza Kikosi Chake. Serikali Yaonya Juu ya Magenge Gumzo kubwa limeendelea mtandaoni kufuatia Katibu wa Baraza la Habari la Waislamu nchini Tanzania (BAHAKITA), Sheikh Said Mwaipopo kueleza kuwa ana kikosi kwa jina la Mbwa Mwitu, ambapo ameeleza kuwa kikosi hicho kimejipanga kupambana na waandamanaji, ikiwemo kuwatambua na kuwafuata majumbani kwao vinara wanaohamasisha maandamano.
The Chanzo53,648 Aufrufe • vor 2 Monaten

Kada wa CCM aliyeripoti kutekwa na kuteswa azungumza- 'Walinilazimisha nimtukane Makamu wa Rais' Kada wa CCM, Kazungu Bakari Kazungu ameeleza kuwa watekaji waliomchukua maeneo anapokaa huko mkoani Tanga, mnamo Agosti 04, 2026, walimhoji juu ya video zake huku wakimshurutisha kumtukana Makamu wa Rais. Kazungu pia ameeleza watu hao walimtaka atoe list, wakimhusisha na kuhusika kupanga maandamano. Jambo ambalo Kazungu ameeleza hakua analifahamu. Kazungu amekuwa ni moja ya wanachama wa CCM, waliojizolea umaarufu mtandaoni kwa video zao za uchambuzi wa masuala ya kisiasa, kwa mrengo wa chama chake. Video zinazomuonesha Kazungu akiwa ameumia vikali zilisambaa mtandaoni mnamo Agosti 07, 2026, pamoja na taarifa ya yeye kutekwa, jambo liloibua mjadala mkali. Polisi wameeleza kuwa wanachunguza tukio hilo.
The Chanzo16,961 Aufrufe • vor 19 Tagen

Hofu yatanda kwa wafanyabiashara wa Coco Beach: Wadai kupewa mwezi mmoja kuondoka kumpisha mwekezaji Wakizungumza na The Chanzo leo, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kwenye fukwe za Coco wamesema baadhi ya viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni waliwaita na kuwapa taarifa ya kutakiwa kuondoka ndani ya siku 30 kupisha uwekezaji. Katika malalamiko ya wafanyabiashara hao, wameeleza pia kusikitishwa na kauli za watendaji hao kwa mfanyabiashara wa kike, kauli zenye viashiria ya kutaka rushwa ya ngono. Kufuatia malalamiko haya ya wafanyabiashara wadogo, The Chanzo inaendelea na jitihada za kuwapata halmashauri ya Manispaa ya kinondoni kutoa ufafanuzi juu ya madai ya wafanyabiashara hawa.
The Chanzo83,998 Aufrufe • vor 5 Monaten

Mama asimulia jinsi alivyoshuhudia kijana wake Damour Nyakairo akichukuliwa na watu saba waliofika nyumbani kwao na Landcruiser Nyeupe. Akizungumza na The Chanzo leo Mei 02, 2026, Lilian Swai ambaye ni mama mzazi wa Damour Nyakairo, ameeleza kuwa kijana wake amechukuliwa asubuhi ya leo na watu waliokataa kujitambulisha, na kumpeleka kusikofahamika. “Wameondoka naye hatujui kapelekwa wapi. Wametoka huko watu saba wakaja,mimi nashangaa watu wanakimbia mvua au wanakimbia nini? Moja kwa moja wanamfuata Damur na mimi nimekuwa hapa. Wakamshika, wawili wanamshika na mmoja akatoa pingu mfukoni akamfunga. Nikauliza kuna nini [wakasema] tutajua huko huko, nyie nani? Wakasema tutajuana huko huko,” anaeleza Lilian Swai mama wa Damour. “Kwa hiyo wakambeba watu watatu wakamshika, wakambeba wakamburuza mpaka kwenye gari. Mimi nikawa nataka kuingia na yeye huko, wananivuta wakanitoa nje.”
The Chanzo61,975 Aufrufe • vor 3 Monaten

Mbunge Asenga apendekeza TBC waandae taarifa ya habari ya taifa, vyombo vyote virushe.
The Chanzo204,512 Aufrufe • vor 1 Jahr

Serikali ya Mtaa Iyunga Mbeya Yafyeka Mahindi Ya Wananchi Kuzuia Yasifiche Vibaka
The Chanzo404,652 Aufrufe • vor 3 Jahren

Mbunge Matiko apendekeza Gen-Z wa Kenya Wakamatwe "Udhalilishaji mtandaoni unafanywa na hao watu wa nje tunasema, lakini zinasambazwa na kwenye mitandao ya Kitanzania, tuko wapi? Kwa nini tunaruhusu hii? Ni udhalilishaji na unaweza kuona kwamba ni udhalilishaji kwa sababu Mama, yaani Rais wetu ni mwanamke," alieleza Mbunge Esther Matiko. "Lazima tukatae, tukiendelea kujua kwamba sisi sote ni Watoto wa mama Afrika Mashariki, mamlaka za nchi ya Tanzania na mamlaka za nchi jirani, ambapo nimeona, sijaona nchi jirani mamlaka zake zikikemea hili. Mshirikiane, mambo ya ndani ya hapa idara ya mawasiliano na kule Kenya, tuwakamate hawa Gen-Z wa kule
The Chanzo158,341 Aufrufe • vor 1 Jahr

Asimulia Wananchi Walivyowafukuza Waliomchukua Msaidizi wa Lissu: 'Walifyatua Risasi Nyingi Sana'
The Chanzo41,041 Aufrufe • vor 3 Monaten

Former President Kikwete in 2012 explaining the origin of the M23 rebels in the Democratic Republic of Congo (DRC). This took place during a press conference after the meeting of the heads of state of the Great Lakes countries, held in Kampala, Uganda, on August 8, 2012, regarding peace talks in the DRC.
The Chanzo164,700 Aufrufe • vor 1 Jahr

Mbowe na Lissu wakifurahia katika mkutano mkuu wa wanawake CHADEMA
The Chanzo159,186 Aufrufe • vor 1 Jahr
