
Tundu Antiphas Lissu
@TunduALissu • 841,522 subscribers
National Chairman @chademaTZ2 🇹🇿 | Former President of the Tanganyika Law Society | Activist
Shorts
Videos

Breaking: Hon. Tundu Lissu has been arrested a little while ago in Mbinga, Songea. Mr. Lissu was arrested after addressing a public rally. Officer Commanding District (OCD) led the operation. Until now, it is unknown under what grounds Mr. Lissu has been arrested. Admin.
Tundu Antiphas Lissu198,838 просмотров • 1 год назад

Ezekia Wenje amekiri mwenyewe kwamba kuna video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake. Ni kweli. Walirekodi kikao hicho chote kwa video. Ili kuondoa ubishi wa suala hili ninawashauri watoe video recording yote ya kikao hicho. Wasikate vipande vipande wala wasihariri chochote. Watoe video nzima ya mjadala huo ili wanachama na Watanzania wajue ni akina nani walituhumiwa kwa kupokea pesa ya Abduli na mama yake, ushahidi niliouwasilisha dhidi yao na wao wenyewe walijiteteaje!!!
Tundu Antiphas Lissu197,846 просмотров • 1 год назад

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa BAWACHA. Kama unataka na wewe, au mwanamke mwenzako anayefaa nae apate fursa za uongozi bungeni au kwenye udiwani miaka ijayo, nakushauri upige kura ya mabadiliko kwenye Uchaguzi wa BAWACHA kesho na Uchaguzi Mkuu wa chama tarehe 21 Januari. Ni kura ya mabadiliko pekee itakayoondoa umalkia katika ubunge na udiwani wa viti maalum katika chama chetu. Ni kura ya mabadiliko pekee itakayohakikisha wanawake wengine nao wanapata fursa za kuwa wabunge na madiwani wa viti maalum. Celestine Malley-Simba ameweka msimamo wake wazi kwamba atapiga kura ya mabadiliko tarehe 21 Januari. Na mimi namuunga mkono; lakini mimi sio mpiga kura kesho, na wala viti maalum havinifaidishi mimi binafsi. Wewe uliye mpiga kura wa BAWACHA kesho na viti maalum vya ubunge na udiwani vinakuhusu, nenda kaunge mkono mabadiliko ndani ya chama chetu. Piga kura yako kwa Celestine Malley-Simba kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA.
Tundu Antiphas Lissu135,548 просмотров • 1 год назад

Kwa vijana wote mlioko & mnaoelekea Mbeya: Na Mimi niko njiani kuja Mbeya kuungana nanyi. Kama ni kuzuiliwa au kukamatwa, & mimi wanizuie au kunikamata. Huu sio wakati kukaa kimya, kuogopa au kuuma uma maneno. Ni wakati wa kusimama & kuhesabiwa. Tupaze sauti kwa nguvu zetu zote!
Tundu Antiphas Lissu129,330 просмотров • 2 лет назад

Wamaasai wa Ngorongoro wanapinga kuondolewa kwa nguvu kutoka Ngorongoro. Serikali ya Samia imewanyang'anya elimu, afya, maji & chakula. Imewafuta kwa maelfu kwenye Daftari la Wapiga Kura. Licha ya ukatili huu, wananchi hawa wamekataa kuondoka kwenye eneo lao. Mimi nawaunga mkono!
Tundu Antiphas Lissu117,470 просмотров • 2 лет назад

Samia alisema Wamaasai wa Ngorongoro waondoke kwao kwa hiari. Baadae akawafutia elimu, afya & maji. Halafu Tume ya Uchaguzi ikawafutia haki za kupiga kura. Sasa mkwe wake amefuta vijiji & kata zao. Samia amevunja Sheria & Katiba. Tupinge azma yake haramu dhidi ya wanaNgorongoro!
Tundu Antiphas Lissu93,434 просмотров • 2 лет назад
2:13
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Day 14 Mchango Update: katika wiki mbili hizi tumeshapokea jumla ya sh. 46,660,279. Kwa sababu tuko barabarani kuanzia tarehe 30 May hadi 22 Juni, tutakuwa tunatoa jumla ya michango tu. Hatutaweza kutoa mchanganuo wa idadi ya wachangiaji, wastani kwa siku na wa kila mchangiaji.
Tundu Antiphas Lissu80,412 просмотров • 2 лет назад

An impromptu roadside stop in Morogoro!!! Ikungi and The Village here we come!!!
Tundu Antiphas Lissu99,868 просмотров • 3 лет назад

The Ngorongoro Maasai in open protests to demand restoration of their ancestral lands & residency rights; & restoration of the social service programs illegally diverted as part of the starve-them-out-of-Ngorongoro strategy of the Samia regime. I STAND WITH THE NGORONGORO MAASAI!
Tundu Antiphas Lissu77,683 просмотров • 3 лет назад

Leo ni mwanzo mpya wa mwaka 2026. Tunafungua ukurasa wa kwanza wa kitabu kipya chenye kurasa 365 tupu, kinachotualika kutafakari yaliyopita jana, kuishi kikamilifu leo, na kuwa na matumaini thabiti kwa ajili ya kesho. Hata hivyo, Siku hii ya Mwaka Mpya inawasili katika ukimya unaotia wasiwasi. Tundu Lissu yupo jela kwa zaidi ya siku 268 na amezuiwa kuzungumza na Taifa leo. Tundu anaendelea kusimama imara bila kuyumba wala kufanya maridhiano hadaa, na imani yake katika haki ya lengo alilolitumikia maisha yake yote bado haijatetereka hata kidogo. Kwa hiyo, karibuni tena kusikiliza kwa makini na kwa tafakari maneno aliyoyasema mwaka moja uliopita, katika hotuba yake ya “Salamu za Mwaka Mpya 2025.” Maneno haya, aliyo yasema wakati ule, sasa yana uzito mpya na uhalisia mkubwa zaidi. #HakunaMaridhianoBilaUkweliNaUwajibikaji #HakunaAmaniBilaHaki #NoReformsNoElections #FreeTunduLissu — Admin
Tundu Antiphas Lissu27,599 просмотров • 9 месяцев назад
Больше нет контента для загрузки