Yericko Nyerere's banner
Yericko Nyerere's profile picture

Yericko Nyerere

@YerickoNyerereT255,983 subscribers

9 Awards-Winning Back to Back Best AUTHOR of the Year AFRICA 2023/2024/2025/2026 | Intelligence and Security Analyst |MNA CHAUMMA Party| CEO YECCO GROUP LTD

Shorts

Naishukuru Kamati Kuu ya chama changu CHAUMMA Tanzania kwakuniteua kuwa Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kigamboni. Niko tayari kupeperusha Bendera ya Chama kwa Mapambano ya kuwakomboa Wanakigamboni!

Naishukuru Kamati Kuu ya chama changu CHAUMMA Tanzania kwakuniteua kuwa Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kigamboni. Niko tayari kupeperusha Bendera ya Chama kwa Mapambano ya kuwakomboa Wanakigamboni!

52,016 Aufrufe

Wamejificha weeee hatimaye wamejitokeza hadharani! Halafu mwanachama halisi anainuka anasema Lissu anafaa kuwa mwenyekiti bila kujua nyuma yake kuna agenda gani? Wajumbe wa Mkutano Mkuu msifanye makosa yatakayokigharimu Chama chetu! Dola na CCM yake wanaingilia uchaguzi wanamtaka Lissu kwa nguvu kubwa wametoa pesa na wanafanya kampeni za Wazi kabisa, Malengo yao ni kuwa Lissu ni mropokaji tu asiyeweza kuongoza taasisi ya Kisiasa inayohitaji hekima, busara na USIRI mkubwa, Kwamba Lissu hana uwezo wa kutafuta pesa ya kuendeshea chama, Kwamba Lissu akiwa Mwenyekiti hakuna Taasisi wala Watu wa Heshima nchini na nje ya Nchi watakaoshirikiana na Chadema kwakuwa Mwenyekiti wake Lissu HANA SIRI, ni Mropokaji kwa chochote watakachoshirikiana nae! Na hivyo Chama kitamfia ndani ya miezi michache tu baada ya kuchaguliwa na CCM itabaki salama dhidi ya Chadema ya Lissu. CCM inaamini akina Lema ni wahuni tu wasioweza hata kujitafutia pesa ya kulisha familia zao badala yake wao na Familia zao wanalishwa na Serikali za Canada na Ubelgiji kama wakimbizi wa Kisiasa. Kwavyovyote vile, hawawezi kuongoza chama cha siasa Tanzania ambacho kukiongoza unatakiwa kuwa na Maarifa, misuli ya uchumi, busara na hekima. Wajumbe epukeni mihemko, Lindeni Chama chenu, Mchagueni Mh Freeman Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti. Freeman Mbowe ana hekima, ana busara, msikivu, ana uthubutu na anaeleweka kwa kila mtu! Na Yericko Nyerere

Wamejificha weeee hatimaye wamejitokeza hadharani! Halafu mwanachama halisi anainuka anasema Lissu anafaa kuwa mwenyekiti bila kujua nyuma yake kuna agenda gani? Wajumbe wa Mkutano Mkuu msifanye makosa yatakayokigharimu Chama chetu! Dola na CCM yake wanaingilia uchaguzi wanamtaka Lissu kwa nguvu kubwa wametoa pesa na wanafanya kampeni za Wazi kabisa, Malengo yao ni kuwa Lissu ni mropokaji tu asiyeweza kuongoza taasisi ya Kisiasa inayohitaji hekima, busara na USIRI mkubwa, Kwamba Lissu hana uwezo wa kutafuta pesa ya kuendeshea chama, Kwamba Lissu akiwa Mwenyekiti hakuna Taasisi wala Watu wa Heshima nchini na nje ya Nchi watakaoshirikiana na Chadema kwakuwa Mwenyekiti wake Lissu HANA SIRI, ni Mropokaji kwa chochote watakachoshirikiana nae! Na hivyo Chama kitamfia ndani ya miezi michache tu baada ya kuchaguliwa na CCM itabaki salama dhidi ya Chadema ya Lissu. CCM inaamini akina Lema ni wahuni tu wasioweza hata kujitafutia pesa ya kulisha familia zao badala yake wao na Familia zao wanalishwa na Serikali za Canada na Ubelgiji kama wakimbizi wa Kisiasa. Kwavyovyote vile, hawawezi kuongoza chama cha siasa Tanzania ambacho kukiongoza unatakiwa kuwa na Maarifa, misuli ya uchumi, busara na hekima. Wajumbe epukeni mihemko, Lindeni Chama chenu, Mchagueni Mh Freeman Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti. Freeman Mbowe ana hekima, ana busara, msikivu, ana uthubutu na anaeleweka kwa kila mtu! Na Yericko Nyerere

65,316 Aufrufe

Dunia imebadilika sana, usiishi kwenye mawazo ya ulimwengu wa giza kwamba Israel ndio taifa teule lenye nguvu ya kijeshi na kijasusi, Dunia ya leo nchi zote zina nguvu ya kijeshi na kijasusi. Leo kuamkia jumapili Israel miji yake mikuu kama Tel Aviv, Jerusalem, Bethelehem na Haifa inanyeshewa mvua ya makombora na Iran hadi dunia inashangaa Iran imepata wapi uwezo huu mkubwa wa kumiliki makombora ambayo hayawezi kuzuilika na mifumo ya ulinzi ya Israel?. Israel yenyewe jana siku nzima iliishambulia Iran kwa kulenga maeneo muhimu na kuua viongozi na wataalumu wa nyuklia tu, Wakati huo Iran inashambulia maeneo yote ya Kiraia, kijeshi na vituo vya utafiti, Kimsingi hasara za uhai zinalingana ambapo taarifa ya Israel leo inasema vifo 35 vimetokea, ijapo miji mingi zaidi ya Israel inawaka moto, na Iran imesema watu 71 wamefariki tangu uvamizi wa Israel uanze majuzi. Mifumo ya Ulinzi imeshindwa kabisa kuzuia makombora ya Iran yenye teknolojia ya Kirusi. Jana Israel iliangamiza ghala la mafuta la Irain, Lakini Iran imetoa jibu kali zaidi kwa makombora zaidi ya 30 kwenye miji mingi hasa Tel Aviv, Jerusalem, Bethelehem na Haifa, Nini tutarajie baada ya usiku wa kuamkia leo Miji ya muhimu ya Tel Aviv na Haifa kuangamizwa vikali na Iran? Ukitaka kujua undani wa mgogoro wa Mashariki ya Kati, Soma Kitabu cha Moscow Opareshen Ukraine. Nimeeleza kwa kirefu sana sana! Kurasa 1400 za kitabu kipya cha MOSCOW: Oparesheni Ukraine zitakufunulia undani zaidi kwa mgogoro huu! Kitabu kina Kurasa 1,400 Sura 1-14, Marejeo 389 Bei ya soko 150,000/= (Kitabu kwaajili ya wote). Nunua kwa: LIPA NAMBA TIGO 7489022 LIPA NAMBA VODA 5352627 TIGOPESA kawaida 0715865544 CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE). Kwa Dar ni free delivery Nje ya Dar nauli 8,000/=

Dunia imebadilika sana, usiishi kwenye mawazo ya ulimwengu wa giza kwamba Israel ndio taifa teule lenye nguvu ya kijeshi na kijasusi, Dunia ya leo nchi zote zina nguvu ya kijeshi na kijasusi. Leo kuamkia jumapili Israel miji yake mikuu kama Tel Aviv, Jerusalem, Bethelehem na Haifa inanyeshewa mvua ya makombora na Iran hadi dunia inashangaa Iran imepata wapi uwezo huu mkubwa wa kumiliki makombora ambayo hayawezi kuzuilika na mifumo ya ulinzi ya Israel?. Israel yenyewe jana siku nzima iliishambulia Iran kwa kulenga maeneo muhimu na kuua viongozi na wataalumu wa nyuklia tu, Wakati huo Iran inashambulia maeneo yote ya Kiraia, kijeshi na vituo vya utafiti, Kimsingi hasara za uhai zinalingana ambapo taarifa ya Israel leo inasema vifo 35 vimetokea, ijapo miji mingi zaidi ya Israel inawaka moto, na Iran imesema watu 71 wamefariki tangu uvamizi wa Israel uanze majuzi. Mifumo ya Ulinzi imeshindwa kabisa kuzuia makombora ya Iran yenye teknolojia ya Kirusi. Jana Israel iliangamiza ghala la mafuta la Irain, Lakini Iran imetoa jibu kali zaidi kwa makombora zaidi ya 30 kwenye miji mingi hasa Tel Aviv, Jerusalem, Bethelehem na Haifa, Nini tutarajie baada ya usiku wa kuamkia leo Miji ya muhimu ya Tel Aviv na Haifa kuangamizwa vikali na Iran? Ukitaka kujua undani wa mgogoro wa Mashariki ya Kati, Soma Kitabu cha Moscow Opareshen Ukraine. Nimeeleza kwa kirefu sana sana! Kurasa 1400 za kitabu kipya cha MOSCOW: Oparesheni Ukraine zitakufunulia undani zaidi kwa mgogoro huu! Kitabu kina Kurasa 1,400 Sura 1-14, Marejeo 389 Bei ya soko 150,000/= (Kitabu kwaajili ya wote). Nunua kwa: LIPA NAMBA TIGO 7489022 LIPA NAMBA VODA 5352627 TIGOPESA kawaida 0715865544 CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE). Kwa Dar ni free delivery Nje ya Dar nauli 8,000/=

25,970 Aufrufe

Videos

YerickoNyerereT's profile picture

Leo nimesikiliza hotuba ya Rais yenye Mamlaka kamili, Hotuba ya Rais wa Nchi Huru, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama. Pamoja na mapungufu kwenye maeneo kadhaa hasa mfano kushambulia kwa nguvu kubwa wale wanatajwa ni wachochezi wa ndani, badala yake kwa maoni yangu ilitakiwa wahubiriwe kwa lugha ya Mfariji Mkuu (Comforter in Chief), lugha ambayo Yesu na Mtume Mohamed waliitumia dhidi ya watu wema na wahalifu wa enzi hizo waliopinga kazi yao dunia, nimemuona rais kachukia sana, yes lazima achukie mbele ya washenzi wa taifa letu, ndivyo inavyotakiwa kwa taifa lenye nguvu ya kulinda uhuru wake! Lakini kwa kiasi kikubwa imekuwa hotuba thabit ya mkuu wa nchi halisi, Binafsi kwa miaka mingi nilikuwa sijaliona taifa langu likitetea ukuu wake kwamtindo wa hotuba ya Mkuu wa Nchi yenye ladha njema kama leo. Imenikumbusha hotuba ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 23 Januari 1967. Akizionya Ureno, Uingereza na Marekani. Pia imenikumbusha Rais Nyerere alipovunja uhusiano wake na Uingereza kwakumfukuza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania. Imenikubusha Rais Nyerere alipopinga ubaguzi wa Raingi kwasusia shughuli zote za kimataifa zilizoihusisha Afrika Kusini ya Makaburu hadi kufika kuzuia timu zetu za taifa kutoshiriki michuano ya Olimpiki. Na mwisho imenikumbusha hotuba ya Rais Mkapa mwaka 2001 alipopinga kwa nguvu zote shinikizo la mabeberu waliotaka kuingilia mgogoro wa ndani uliotokana na mauaji ya zanzibar na mwembechai yaliyotokana na CUF kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2000. Rais Samia amegusa vitu vingi muhimu sana ambavyo nimekuwa nikivisema tangu mwanzo, Na vingine tulivisema huko nyuma kabisa ndani ya vyama vya siasa, ikatafsirika kuwa ni propaganda. Vitu hivyo ni: 1. Amesema kuwa tukio la 29 oktoba lilikuwa jaribio la mapinduzi. Hili nilishalisema tangu siku moja baada ya jaribio lile na ndio msimamo wangu leo na kesho na historia itaandikwa hivyo! Hakukuwa na maandamano! 2. Amesema waandaaji wa uhalifu huu ni mabeberu wanaopigana vita vya kiuchumi kuzisaka raslimali zetu na ustawi wetu. Hili nilishalisema tangu siku moja baada ya jaribio lile na ndio msimamo wangu leo na kesho na historia itaandikwa hivyo! 3. Amesema vijana wengi walilipwa kuhamasisha na kufanya uhalifu huu. Hili nilishasema na kuweka ushahidi wa taasisi zilizowalipa ikiwemo taasisi ya Ford Foundation ya Marekani ambayo imemlipa Maria Sarungi kupitia taasisi yake inayoitwa Change Tanzania iliyopokea zaidi ya bilioni 10 katika kipindi kifupi cha miezi 10 tu hivi, Zingatia taasi ya Maria imesajiliwa Tanzania inatakiwa kufanya kazi zake Tanzania, lakini kwa miaka zaidi ya mitano Maria hayupo Tanzania, na taasisi haifanyi kazi zake lakini inapokea mabilioni, nakuwalipa vijana makumi kwa mamia nchini na wengine amewatoroshea Nairobi huko sasahivi. 4. Rais ameweka ukweli rasmi na kufuta propaganda ya muda mrefu iliyoenezwa na Tundu Lissu kipindi cha uchaguzi wa Chademw kwamba Mbowe amelambishwa asali. Rais amesema kuwa Lissu ndie alimpatia pesa alipokwenda kumuona Ubelgiji tena Rais alitoa pesa yake ya safari, Rais hajaishia hapo, amesema Lissu na Wenzake waliporudi Tanzania kwaamana ya Gobless Lema nk aliwapa pesa ya kujikimu. Na mwisho wakaanza kumtukana Rais huyuhuyu! Si mimi nasema, bali Rais Samia kasema yeye kwa kinywa chake! Hili jambo la Lissu kulambishwa asali mimi binafsi nilisema kipindi cha kampeni kwamba ninazo taarifa sahihi Lissu amepewa pesa, na kama nimsafi kweli mbona hajatangaza hadharani hiyo pesa aliyopewa pale Ubelgiji? Bahati mbaya tayari wanaharakati uchwara walikuwa washavamia na kuteka chama hivyo hawakusikia wala kuelewa sauti yoyote nje ya Lissu ambae alijimilikisha usafi wa moyo na mwili na akajimilikisha ukweli na haki ya nchi hii. Lakini sisi tunaomjua kuwa ni muongo na mlamba asali mkubwa, wala hatukuwashangaa, tuliacha ungo upande lifti, na sasa tunafurahi kuona ukweli umefika kwa njia ya ngazi. Rais wa nchi kafunga mjadala wa Uzushi ulioenezwa na Lissu na

Yericko Nyerere

64,224 Aufrufe • vor 7 Monaten

YerickoNyerereT's profile picture

Jela sio sehemu salama, hakuna aliyekaa jela akabaki na msimamo wake uleule, Nampongeza Lissu kwakubadili msimamo wake na kuomba sasa maridhiano ya mezani, Ukikomaa utafia jela ndugu….. Waulize wapinzani wengine Afrika kilichowakuta. Yuko mtu kwasababu ya uelewa mdogo anaamini kuwa Marekani na Ulaya watakuja kumtoa Lissu pale Ukonga au watakuja kuitoa CCM madarakani na Lissu awe Rais. Hizo ni ndoto za chizi na kuota ndoto kwa kiumbe cha Mwenyezi Mungu sio dhambi…. Ulaya na Marekani wanaangalia maslahi yao, Vyovyote ccm na samia watakachowafanyia watz ilimradi maslahi ya Ulaya na Marekani hayaguswi basi sahauni ndoto zenu, mtaishia kupokea barua za matamko ya kulaani na kusisitiza amani na demokrasia tu. Nakujueni mnavichwa vigumu mtakomaza mafuvu yenu kubisha… Tulishauri tangu mwanzo kwamba tufanye siasa za maridhiano, tukawaambia kuwa hii ni kesi ya kisiasa, Siasa ndio imemweka jela Lissu, na Siasa ndio itamtoa jela Lissu, kwa lugha rahisi ni kwamba Lissu lindie kafanya Lissu aende jela, na Lissu ndie atafanya Lissu atoke jela. Kwakibri na jeuri ya umamuma wetu mlitutusi mkatuita wasaliti. Bahati nzuri Lissu akili imemjia kalitambua hili japo kwakuchelewa sana, Tumpongeze na tumtie moyo… karibuni kwenye siasa za kistaarabu za maridhiano kwa maslahi ya Tanzania yetu. Ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba Mahakama iachwe ifanye kazi yake na haki ipatikane, Lissu atatukuta mbele tukiendelea na vikao vya maridhiano au atakuta nchi ilisharidhiana inaendelea vizuri na atafaidi matunda ya maridhiano. Na Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

21,805 Aufrufe • vor 2 Monaten

YerickoNyerereT's profile picture

Kwamara ya kwanza kwenye jukwaa la kimataifa, Nimeiona ladha ya sauti ya ki-nchi ambayo kwahakika niliona mwaka kati ya 1994-95 ikitoka kwa Hayati Mwalimu Nyerere wakati wa Mandela akitwaa madaraka. Leo nimemuona na kumsikia tulia.ackson Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Tanzania. Yes nimefurahishwa na majibu yake, amejibu kwa kutulia na kwa tone ya mamlaka mbele ya Wahafidhina wa Magharibi ambao bado akili zao zinaamini Afrika ni Koloni lao. Kauli hii ya Dkt. Tulia Ackson, ameitoa akifungua Mkutano Mkuu wa 149 wa IPU uliofanyika Geneva, Uswisi ambapo amewasisitiza Wajumbe wa Bunge hilo kumuamini na kumpa nafasi afanye kazi yake na waache kufikiria dhana ya Ukoloni kwa wanaofikiria hivyo ikiwemo kupinga kila kitu kwakuwa anatokea Tanzania au Afrika. Dkt. Tulia ameyasema hayo baada ya baadhi ya Wajumbe kukosoa uamuzi wake wa kufanya ziara Nchini Urusi na kukutana na Rais Vladimir Putin kuhusu vita ya Ukraine badala ya kwenda Gaza, Lakini ukifatilia Wajumbe waliokosoa wengi wanaonekana wako nje ya dunia mpya hata hawajui taarifa na ratiba za IPU kwani ni wazi Dkt. Tulia alipochaguliwa tu November mwaka jana 2023 alienda Israel na Palestine na kuonana na Viongozi wa pande zote, Wajumbe wa IPU kwa sehemu kubwa wamejazwa propaganda za ubaya wa Urusi wameshindwa hata kujua ratiba za viongozi wao. Katika maelezo ya majibu ya Tulia amesema hajachagua upande kwenye migogoro yote na kwamba IPU inapambana kurejesha amani kwenye migogoro hiyo. Wajumbe wa mkutano huu ni 1,500 wakiwemo Maspika, Naibu Maspika, Wakuu wa Misafara na Wabunge. Nafikiri sasa mmejua kwanini niliamua kuupinga Ushoga na Usagaji na kuamua kuunga mkono Urusi katika oparesheni yake Ukraine nikiamini ilikuwa imechokozwa vya kutosha na Magharibi wakiongozwa na Marekani, Chaguo kuu lilikuwa ni oparesheni hiyo ambayo sasa imerejesha heshima ya mrengo wa kushoto na kulia Duniani. Dunia pamekuwa na Adabu sio kama zamani rimonti kukaa Washington. Katika tafakuri, Kuna funzo na hoja kuu mbili zinaibuka hapa, (1)Kwanza Tulia ameona kwa macho demokrasia ya kupingwa na kujibu hoja ambapo aina hii ya maongozi yeye hajaizoea, kwakuwa ni muumini wa udikteta aliyezaliwa katika mikono ya kidikteta. (2)Pili hoja ya leo kule Ulaya kwa namna ilivyojibiwa, inaibua mjadala mpya kwamba mfumo wa chama cha Mapinduzi ambacho kimantiki mimi huwa nakataa kwakusema hiki sio chama cha siasa bali ni umoja wa vyombo vya dola yaani TISS, JWTZ, Polisi, Magereza, Uhamiaji Takukuru na TRA, Kwamba mjadala muhimu ni kuwa mfumo huu ni kandamizi na hatari sana, hauruhusu watu kutumia akili yao yote isipokuwa akili kidogo sana sawa na ile ya kutenganishia mboga na ugali tu, kipimo ni Tulia leo na kisha rejea nyuma umuone tulia wa Lumumba. Na Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

92,802 Aufrufe • vor 1 Jahr

YerickoNyerereT's profile picture

Kama bado kuna mwanachama au kiongozi wa chadema hajastuka hii hali na kuchukua hatua kunusuru basi huyo mwanachama/kiongozi ndie tatizo kwenye chama chetu…. Naendelea kushauri viongozi wa chama taifa wachukue hatua mwenendo huu si sawa! Msilewe kwa kuona mikutano inajaa watu, Watanzania ndivyo walivyo hata Mwamposa huwa anajaza watu, Hata Gwajima huwa anajaza watu, Hata Diamond huwa anajaza watu, Hata simba na yanga huwa zinajaza watu, Chama ni mtandao wa Uongozi. Mtandao ukifa ni vigumu kuwa na chama. Hata leo Lipumba au Mbatia ukiwapa pesa ya mkutano na maandalizi yote watajaza watu hadi wakanyagane. Watanzania sio wachoyo linapokuja suala la mtu anayeisema ccm au anayefanya miujiza ya kiroho au anayewaburudisha kwa muziki au kwa soka! Sekretarieti yote iliyokuwepo kwenye uongozi uliopita imeondoka Chadema isipo kuwa watu wawili tu Mnyika na Pambalu. Viongozi wa Kanda 8 zote za Tanzania Bara wamejiondoa Uongozi Mzima wa Mkoa Kilimanjaro kuanzia matawi, Kata, Majimbo, Wilaya na Mkoa umejiondoa, Uongozi wote wa Mkoa wa Temeke wamejiondoa. Leo uongozi wa Mkoa Tabora umeondoka. Hatustuki? Bado tunafanya propaganda kwamba hao wanaoondoka kwakuwa wamekosa vyeo ndani ya chama? Tuache uongo na kukomaza mafuvu, kuna tatizo! Hebu tukubaliane na ukweli kuwa sisi ni chama cha kidemokrasia tumekoseana turudi mezani tuyajenge. Enyi viongozi wangu, nani amewewafanya kuwa na mioyo migumu kama farao? Mimi naona mbele kuna giza!!! OFA YA PAPA MPYA INAISHA LEO. Pata Kitabu cha UJASUSI kwa 25,000 tu badala ya bei halisi ya 80,000/=. Lipia kwa: Lipa Tigo 7489022 Lipa Voda 5352627 M-Pesa. 0755865544 TIGOPESA 0715865544 CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE). Kwa Dar ni free delivery Nje ya Dar nauli 8,000/=

Yericko Nyerere

55,202 Aufrufe • vor 1 Jahr

YerickoNyerereT's profile picture

Jasusi hatari nyuma ya NGO nchini Burkina Faso. Jasusi Joe Bassey kutoka Perrot Island nchini Cana ameachia nyaraka za siri zinazofichua kwamba Bi Claire Dubois, mwanamke Mfaransa katika miaka 30 iliyopita aliwasili Burkina Faso akijifanya kama mkurugenzi wa NGO ya Magharibi iitwayo Hope Forward, ambayo shughuli zake kuu ilikuwa ni kusaidia elimu ya wasichana na afya ya wanawake. Bi Claire alijionyesha kama mwanamisaada ya kiutu aliyelenga kusaidia wanawake wa Kiafrika, akitembelea vijiji, shule, na masoko, na kutumia muda mwingi kusifu uongozi wa Burkina Faso kwenye televisheni ya serikali. Walakini, nyuma ya shuguuli hii ya kibinadamu, Bi Dubois alikuwa akijishughulisha na ujasusi. Alikuwa akikusanya taarifa za kijasusi kwenye tovuti za kijeshi, ikiwa ni pamoja na vituo vya mafunzo ya kijeshi, vituo vya mafuta, na vituo vya uongozaji wa ndege zisizo na rubani, akitumia kivuli cha kazi ya kibinadamu. Katika kazi zake zilizoonekana ni za kiraia lakini alibeba simu mbili-moja ya kiraia na ya pili ni simu maalumu kwa mawasiliano kijasusu na aliitumia kutuma barua pepe zilizowekwa katika mfumo wa ulinzi imara ambazo ni ramani zilizochakatwa vizuri na picha za setilaiti za maeneo nyeti ya kijeshi, kwenda kwa watu wa NATO na majasusi wemgine wa kigeni. Shirika la ujasusi la Burkina Faso kwa msaada wa Shirika la Ujasusi la Urusi FSB tayari lilikuwa limetilia shaka shughuli Mama huyu na kufuatilia mawasiliano yake kwa ukaribu sana hasa kuingilia mawasiliano ya simu yake ambayo ilikuwa ikitumia Setelaiti. Baads ya kujiridhisha kwamba Bi Claire anafanya shughuli za kijasusi kweli, Walifanikiwa kuzuia nyaraka hizo zisiwe zinawafikia Nato na washirika kwakuwa tayari mawasiliano hayo ya Bi Claire walikuwa wameyaingilia kila akituma email zilikuwa zinaingia Moscow sio Brusels tena. Rais Ibrahim Traoré aliwaamuru majasusi wake wamwache aendelee kukusanya nyaraka za misheni yake ili wamkamate akiwa na ushahidi halisi. Na baada ya miezi kadhaa, Hatimaye, alikamatwa na kuwekwa hadharani katika Kongamano la Kitaifa la Mamlaka ya Afrika, ambapo rais aliwasilisha nyaraka zake za siri na barua pepe zote moja kwa moja jukwaani, akifichua shughuli zake za kijasusi kwa ulimwengu. Na baadaye akazuiliwa kimya kimya na serikali licha ya shinikizo la nchi za magharibi kwakutumia mgongo wa azimio la kidiplomasia, Rais Traoré alisisitiza juu ya uwazi na haki, akisisitiza usaliti wa kuaminika ni adui wa Bukinafaso. Swali la kujiuliza, ni mashirika mangapi ya kigeni yako nchini na yanafanya shughuli wazosema watafanya bila kuwa na agenda nyingine? Wanafuatliwa kwa kiwango gani? Jibu lipo Lumumba! Na Yericko Nyerere PATA OFA YA PAPA MPYA WA ROMA Pata Kitabu cha UJASUSI kwa 25,000 tu badala ya bei halisi ya 80,000/=. Lipia kwa: Lipa Tigo 7489022 Lipa Voda 5352627 M-Pesa. 0755865544 TIGOPESA 0715865544 CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE). Kwa Dar ni free delivery Nje ya Dar nauli 8,000/=

Yericko Nyerere

52,293 Aufrufe • vor 1 Jahr

YerickoNyerereT's profile picture

Nilipoeleza katika Makala kuu kwamba Lissu hana sifa za kuwa Mwemyekiti wa Chadema Taifa kwasababu ni MUONGO, wengi mlipinga na natusi juu, Niliorodhesha uongo wake mwingi ikiwemo Uzushi wake juu ya kinachoitwa Mabilioni ya Abdul…. Sasa Jana akiwa Maria Space alimtuhumu na kumzuishia Mwenyekiti wa @chadematzofficial Mh Freeman Mbowe kwamba ajiamulia yeye binafsi kumwalika Mh Rais Samia kwenye kongamano la BAWACHA na kutoa tuzo! Sasa ushahidi mwingine wa UONGO wa Lissu ni katika Video Sauti akisikika akimsifu Rais na uamuzi wa chama kumwalika katika kongamano hilo! Hii ikithibitisha kuwa Lissu alishiriki kumwalika Rais kwenye Kongamano hilo Kwa namna Lissu alivyokidhalilisha chama huko nyuma na jana akikituhumu chama na viongozi wake kwa mambo mbalimbali, akitoa siri za kamati kuu na kukibagaza chama vilivyo, Nadiriki kusema, Lissu anakosa sifa hata ya kuwa mwanachama tu wa Chadema, Kama kamati ya uchaguzi itafuata kanuni za uchaguzi, Basi Lissu anatakiwa kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hiki kwakuwa amevunja maadili na kanuni za uchaguzi! Kamati kuu ya chama ina kiapo cha Wajumbe kuhakikisha wanalinda siri za chama na haitatokea mjumbe wa aina yoyote kutoa au kuzungumza mambo yaliyojadiliwa katika kamati kuu. Lakini jana Lissu kayamwaga yote hadharani jambo ambalo sio utaratibu wa vyama vyote vya siasa duniani! Inashangaza kuona leo Lissu anakanusha hata yale ambayo alishiriki kuyaamua na kuyasifia kama mambo mema. Huyu ni muongo, mnafiki, mzandiki na mtu asiye na heshimu kwa wengine. Anawatungia uzushi wenzake kwa mambo ambayo nae ni sehemu ya maamuzi, bila kujali anakiumiza chama Kwa kiasi gani, ilimradi yeye aonekane wa tofauti. Kiongozi asiye mkweli, asiye heshimu wenzake katika nia moja anapoteza sifa za kuaminika kukabidhiwa Taasisi kubwa na nyeti kama CHADEMA. Kwanamna yoyote Lissu Hafai kuwa Mwenyekiti wa Chama chetu na hafai kuwa Mwanachadema! Nasisiti kushauri Kamati kuu ikutane kumjadili na kumwajibisha kiongozi huyu aliyekosa maadili ya kichama! Na Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

63,981 Aufrufe • vor 1 Jahr

YerickoNyerereT's profile picture

Kuna vita kubwa sana ya Ujasusi wa Kiuchumi inaendelea kati ya Dodoma na Nairobi kwa miaka kama sita hivi sasa ambayo picha ya wazi inaonyesha mwenendo mwema sana kwa Dodoma ukilinganisha na historia ya kiuchumi tulikotoka. Leo Nairobi imeelekeza nguvu zake kupambana Dom katika eneo la michezo ambako kwa miaka kama 15 hivi Dodoma imekuwa kiongozi kwa eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla wake. Vita ya uwanja bora wa michezo kuelekea Afcon inatafsiri wazi namna mamlaka za Nairobi walivyopania. Eneo hilo la michezo kwa Dodoma sio geni na wala sio kipaumbele cha ujasusi wa kiuchumi kwani tayari ilishakuwa na uwanja mkubwa wenye sifa ya Kidunia, pamoja na upekee wa uwanja wa Talanta ambao Kenya inaubeba kama agenda kuu. Na ukiondoa hilo Tayari Tanzania ina viwanja vyenye sifa ya kimataifa vinavyotumika kwa mechi za usiku kama vile Benjamini Mkapa, Amani, Azam, KMC, Mkwawani, Gwambina, Twalipo, Dodoma nk. Viwanja hivyo kutumika kwa michezo ya ligi kuu usiku ni hatua itakayowachukua Nairobi miaka kufikia ukiondoa kampeni hizi za ujenzi wa viwanja zilizowaamsha usingizini. Kwa miaka zaidi ya 25 hivi Kenya alikuwa ameshikilia sekta ya anga hadi anga ya Tz alikuwa anaimiliki yeye kipindi kile tz ikiwa haina ndege kabisa, Kuingia kwa Hayati Magufuli madarakani 2015 kuliamsha vita ya anga na Kenya iliyopiganwa kwa jasho na damu, Tanzania ilianza na hatua ya kurejesha haki ya anga lake, kisha kutoka kuwa haina ndege hata moja, ikanunua ndege 2 ambazo zilianza kufanya safari za maziwa makuu na kusini mwa Afrika, Huku ushindani ukiendelea, Tanzania ikaongeza idadi ya ndege na kufika hadi sasa Air Tanzania ina miliki zaidi ya 43% ya ndege zote nchini Tanzania. Kwamjibu wa mtandao wa Planespotter unaojihusisha na utoaji wa tafiti mbalimbali katika sekta ya anga duniani, umelitaja shirika la ndege la Air Tanzania kuwa na jumla ya ndege 16, ikiwa ni siku kadhaa kupita baada ya kutoa tafiti zilizoonyesha idadi kamili ya ndege zote zinazofanya kazi nchini Tanzania ambazo ni jumla ya ndege 37. Idadi kamili ya ndege katika shirika hilo inalifanya kuwa shirika lenye ndege nyingi zaidi nchini Tanzania, kwa zaidi ya 43% huku 67% zikisalia katika mashirika mengine 17 yaliyopo nchini Tanzania. Ndege zote 16 zinazomilikiwa na Air Tanzania zimetoka katika makampuni manne tofauti ya uundaji wa ndege ambayo ni kampuni ya Airbus, Boeing, Bombardier na De Havilland. Hivyo ni sawa na kusema kuwa Air Tanzania, inamiliki ndege moja aina ya Dash 8-Q300,ndege tano aina ya Dash 8-Q400 , ndege nne aina ya Airbus A220-300, ndege mbili za Boeing 737 Max 9, ndege tatu za Boeing 787- 8 Dreamliner na ndege moja ya mizigo aina ya Boeing 767-300F. Hadi muda huu Tanzania imefanikiwa kuiondoa Kenya katika udhibiti wa ruti za Kutoka Tanzania kwenda Zambia, Zimbabwe, Malawi, kwa 95%, Afrika Kusini kwa 42%, Nigeria % 41%, China na India 81%, Rwanda 34%, Congo DRC 91% nk. Hii ni hatua kubwa sana katika vita vya kibiashara katika sekta ya anga. Ndege za Tanzania ndizo zinapendwa zaidi na Wasafiri wengi Afrika kwakuwa ni mpya na za kisasa zaidi ukilinganisha na ndege za Kenya. Huduma za ndani ya Ndege kwa Tanzania ni nzuri zaidi kuliko Kenya. Mwaka 2021 katikati wakati Serikali ya Rais Samia imeingia, Binafsi nilishauri katika moja ya makala yangu kwamba yafanyike mabadiliko makubwa ya sera ya anga ili kukabili ushindani wa kidunia na mapigo ya jirani, nilitoa ushauri huo baada ya mwekezaji mzawa Bwana Laurance Masha kushindwa kuendesha shirika lake la Ndege la Fast Jet katika nazingira yaliyohuzunisha sana, Kwa sera za wakati huo ilikuwa ni ngumu na hatari sana ukitaka kuwekeza katika eneo hilo la anga, Moja ya mambo machache niliyoshauri yarekebishwe ambayo niliona ni kikwazo kikubwa kwa wawekezaji binafsi sekta hii ya anga ilikuwa ni gharama za moja kwa moja unazowajibika wewe mwenye ndege kuzikabili mbele ya mamlaka, ambapo nawe mwekezaji kimsingi utashusha kwa mlaji ambae ni abiria. (direct cost anazokutana nazo abiria apandae ndege)

Yericko Nyerere

18,357 Aufrufe • vor 5 Monaten