
Brenda Rupia Jonas
@BrendaRupia • 20,230 subscribers
Director of Publicity and Communications CHADEMA|Secretary General of the Women wing in Kinondoni Region|Mom|Citizen of my Nation.
Shorts
Videos

Kesi imeanza na Mwenyekiti Lissu akasema analo neno la kusema kabla ya kuanza kesi. “ Lengo pekee la DPP (Mkurugenzi wa mashtaka)la kufungua mashauri haya ni ili kupoteza muda tu ili niendelee kukaa Mahabusu . Leo ni siku ya 166 tangu tarehe 24 Februari tangu Mawakili wa serikali waende mahakama ya Rufaa na huko nikawashinda na sasa tumerudi Mahakama kuu lakini tumerudi baada ya siku 166,tuendelee lakini ipo siku tutazungumza kuhusu haya yote yalioendelea na kuhusu huyo anaewatuma na itambidi awajibike” anasema Mwenyekiti. “Someone will have to pay for all of this someday” says Honerable Tundu Antiphas Lissu
Brenda Rupia Jonas27,264 views • 4 days ago

In Tarime, polling stations remain deserted as residents have boycotted the election.
Brenda Rupia Jonas137,277 views • 9 months ago

Kesi imeahirishwa hadi kesho saa 3:00 asubuhi. Mwenyekiti Tundu Lissu ameomba usikilizwaji wa kesi uanze mapema tofauti na ilivyokuwa leo, kutokana na utaratibu wa kumuweka katika chumba cha mahabusu (lock up) hadi muda wa kuanza kesi unapofika. Katika hatua hiyo, Mheshimiwa Jaji ametoa amri kwamba Mwenyekiti Lissu asipelekwe lock up, kwa kuwa yeye si mshtakiwa katika kesi hii. Tunawaalika wanachama, wapenda demokrasia na watetezi wa haki wote kufika mahakamani kushuhudia mwenendo wa kesi hii muhimu, ambapo kwa mara ya kwanza kiongozi wa upinzani atamhoji Mkuu wa Magereza kuhusu utaratibu wa Gereza la Ukonga kuzuia au kuweka vikwazo kwa mawakili kukutana na mteja wao. Tunaendelea kusimamia misingi ya haki, uwazi na utawala wa sheria.
Brenda Rupia Jonas17,103 views • 25 days ago

CHADEMA tumekuwa tukisisitiza jambo hili kwa muda mrefu; Katiba Mpya imekuwa wimbo wetu na ndiyo ajenda yetu kuu. Hongera kwako Bwana Nchimbi kwa kuunga mkono hoja hii, hata kama imekuja kwa kuchelewa. Lakini ukweli uliowaambia Watanzania ni jambo ambalo tumesema kwa muda mrefu: Taifa letu linahitaji mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali, na Katiba Mpya ndiyo msingi wa kuleta mabadiliko hayo. Hata hivyo, kauli hizi zimekuja kwa kuchelewa sana kutoka upande wenu. Sasa Watanzania wanataka kufahamu msimamo wa Ndugu Samia Suluhu Hassan kuhusu suala hili. Mchakato wa Katiba Mpya utaanza lini? Bwana Nchimbi,una nafasi ya kusaidia kuondoa vikwazo vilivyopo kwa sababu Chama Cha Mapinduzi ndio yenye hofu ya kutoka madarakani. Wananchi tayari wameshaeleza msimamo wao: wanataka Katiba Mpya na wanataka Mwenyekiti Tundu Lissu awe huru bila masharti yoyote. Wakati umefika wa kusikiliza sauti ya wananchi na kuchukua hatua. Tumebakiza Tsh. Laki tano pekee kufikisha Tsh. Milioni 200 katika Marathon ya kuchangia Tsh. milioni 334 ya kuwezesha kikao cha Baraza Kuu la Umma. CHANGIA M-Pesa Namba: 0744446969 Jina: CHADEMA HQ NMB Bank Namba: 22606600140 Jina: Chama cha Demokrasia na Maendeleo #KatibaMpyaFreeTunduLissu
Brenda Rupia Jonas13,416 views • 21 days ago

TAFAKURI KWA KAULI YAKO KOMBO "Kama mauaji yaliyotokea Oct 29 na siku zilizofuatia ni polisi walikuwa wanatekeleza katiba!, Sasa kwa nini mnaongelea kuliponya taifa kama polisi walikuwa wanatekeleza katiba?Kwa nini hamuoni kama katiba waliyoitekeleza inaumwa na inahitaji itibiwe ipone ili iliponye taifa?'"🤷♂️. Katiba mpya inahitajika sasa. #KatibaMpyaFreeTunduLissu
Brenda Rupia Jonas16,868 views • 2 months ago

Kaka Kabendera umezungumza ukweli usiopingika. Wanatupeleka mahakamani kila siku kwa kesi za mchongo. Kesi hii sio ya Jamhuri, bali ni kesi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Antiphas Lissu. Niwaambie tu Chama Cha Mapinduzi na serikali yenu haram: ukweli haujawahi kufichika. Mnaweza kutuchelewesha, lakini hamuwezi kutuzuia kufika tunapopaswa kufika. Tulipo leo si tulipoanzia na safari ya mabadiliko haiwezi kuzimwa kwa vitisho wala kesi za kubambikiza. Nchi yetu ina changamoto nyingi kila kona: gharama za maisha, ajira kwa vijana, huduma za afya, elimu, na uchumi wa wananchi wa kawaida. Kwa nini hamuelekezi nguvu zenu huko? Kwa kuendelea kutumia vyombo vya dola dhidi ya wapinzani wa kisiasa, mnajichimbia shimo ambalo litakuwa gumu kulifukia. Zile ahadi za bima ya afya kwa wananchi wote ziko wapi? Je, bado tuendelee kusubiri utekelezaji usio na tarehe? Muachieni Tundu Lissu. Acheni chama chetu kifanye siasa zake kwa uhuru kama Katiba inavyoruhusu. Waachieni wananchi wapime sera, hoja na maono ya vyama tofauti, kisha waamue kwa hiari yao. Demokrasia haiwezi kustawi kwa kubana sauti za wanao wapinga. #FreeLissu #TunaWatuTutashinda
Brenda Rupia Jonas17,057 views • 5 months ago

Bw. Makala, naona unajitekenya na kucheka mwenyewe. Lakini tambua hili: Chadema Tanzania si chama cha jana wala cha kuzimwa kwa kejeli – ni mpango wa Mungu. Kimevuka majaribu, kimesimama leo, na kitaendelea kusimama kesho kwa mkono wake Mwenyezi Mungu. Unakumbuka ndugu yako Mwigulu Nchemba, PhD alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama chenu? Alishirikiana na wengine kumtengenezea Mh. Lwakatare (aliyekuwa Mkurugenzi wa Ulinzi wa CHADEMA) kesi ya ugaidi – na kwa majigambo, akatangaza Bungeni kuwa Chadema imefungwa duniani na mbinguni. Lakini tazama, Mungu ni mwaminifu – Lwakatare alishinda kesi, na mwaka 2015 akaingia Bungeni kwa tiketi ya Chadema. Huo ndio mkono wa Mungu, si maigizo ya kisiasa ya jukwaami na propaganda. Rejesha kumbukumbu zako: babu yangu, SM Wasira, akiwa waziri kipenzi enzi za Mzee Kikwete, aliwahi pia kutamka kwa majigambo bungeni kuwa Chadema itakufa kabla ya 2015. Lakini Mungu akaonyesha ukuu wake – mwaka huo ukawa wa historia. Bila “goli la mkono” tungekuwa tumeandika historia tofauti. Leo nawe unarudia mtindo ule ule wa kauli zisizo na maana – jifunze kutoka kwa waliokutangulia. Badala ya laana zenu, historia huandikwa kwa vitendo na kwa ridhaa ya Mungu. Mwaka 2025 Jiandaeni kwa makubwa zaidi – mark this tweet. Na kwa kuwa unaufuatilia sana mambo ya CHADEMA basi free Tundu Antiphas Lissu – na utuambie yuko wapi Mdude Nyagali ! Usisahau, changia pia kupitia 0744 446 969 kwa jina CHADEMA HQ – maana najua moyoni mwako unaichukulia CHADEMA kuwa ngome ya matumaini ya watanzania.
Brenda Rupia Jonas28,644 views • 1 year ago

Nkasi: CHADEMA yazuiwa na vyombo vya dola kupanda miti 1,500 kwa “maelekezo kutoka juu”. Rais haram huyo huyo anawahimiza Watanzania wapande miti. Huu sio utawala wa sheria, ni utawala wa upendeleo wa kisiasa. Kama kupanda miti ni uzalendo, basi kwanini uzalendo wa CHADEMA unahesabika kosa? Au Watanzania sasa wanapimwa kwa kadi ya chama?
Brenda Rupia Jonas14,940 views • 6 months ago

Kuongozwa na mtu kama Gerson Msigwa ni fedheha kwa Taifa. Fikiria serikali kupitia kwake inasema mtu akitekwa, kama hajapatikana wao wafanye nini ,ivi kweli? Sasa kwani, serikali kazi yake ni nini kama si kulinda usalama wa wananchi wake? Kauli kama hizi zinaonesha ni kwa nini tunasema #NoReformsNoElection. Kwa mawazo ya aina hii, mtu kama wewe, Msigwa, hustahili kabisa kuendelea kushikilia wadhifa wa uwajibikaji wa umma. Ni aibu kwa Taifa na fedheha kwa wananchi unaodai kuwatumikia.
Brenda Rupia Jonas16,081 views • 10 months ago

We don’t want CCM Hatutaki CCM GenZ wapo barabarani. No Reforms No Election
Brenda Rupia Jonas11,688 views • 9 months ago

“Kufunga funga makanisa si jambo zuri.Mnafunga makanisa ili watoto wakasali wapi sunday school? Wamekosa nini?” amesema mzee wa upako. Kufunga makanisa kwa sababu tu Gwajima anamuombea Tundu Antiphas Lissu ni ushahidi wa serikali inayoogopa maombi na hoja kuliko kitu kingine chochote. Huu si uvunjaji tu wa uhuru wa ibada, bali ni hofu ya kisiasa iliyovaa joho la madaraka. Mnaanzaje kupambana na imani ya watu halafu mdai kuwa mnaongoza kwa haki? Mchezo huu mchafu utawatokea puani. Mungu hahusiki na dhulma.
Brenda Rupia Jonas14,373 views • 1 year ago

“Chaguzi zetu haziendi sawasawa” amesema Askofu wa KKT mkoani Tabora.
Brenda Rupia Jonas10,665 views • 1 year ago
No more content to load