
Brenda Rupia Jonas
@BrendaRupia • 19,603 subscribers
Director of Publicity and Communications CHADEMA|Secretary General of the Women wing in Kinondoni Region|Mom|Citizen of my Nation.
Shorts
Videos

TAFAKURI KWA KAULI YAKO KOMBO "Kama mauaji yaliyotokea Oct 29 na siku zilizofuatia ni polisi walikuwa wanatekeleza katiba!, Sasa kwa nini mnaongelea kuliponya taifa kama polisi walikuwa wanatekeleza katiba?Kwa nini hamuoni kama katiba waliyoitekeleza inaumwa na inahitaji itibiwe ipone ili iliponye taifa?'"🤷♂️. Katiba mpya inahitajika sasa. #KatibaMpyaFreeTunduLissu
Brenda Rupia Jonas16,721 görüntüleme • 13 gün önce

In Tarime, polling stations remain deserted as residents have boycotted the election.
Brenda Rupia Jonas137,166 görüntüleme • 7 ay önce

Daima tutasimamia haki na usawa.Pongezi kwenu wanawake wote na hongereni kwa kufika Musoma.
Brenda Rupia Jonas16,902 görüntüleme • 3 ay önce

Kaka Kabendera umezungumza ukweli usiopingika. Wanatupeleka mahakamani kila siku kwa kesi za mchongo. Kesi hii sio ya Jamhuri, bali ni kesi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Antiphas Lissu. Niwaambie tu Chama Cha Mapinduzi na serikali yenu haram: ukweli haujawahi kufichika. Mnaweza kutuchelewesha, lakini hamuwezi kutuzuia kufika tunapopaswa kufika. Tulipo leo si tulipoanzia na safari ya mabadiliko haiwezi kuzimwa kwa vitisho wala kesi za kubambikiza. Nchi yetu ina changamoto nyingi kila kona: gharama za maisha, ajira kwa vijana, huduma za afya, elimu, na uchumi wa wananchi wa kawaida. Kwa nini hamuelekezi nguvu zenu huko? Kwa kuendelea kutumia vyombo vya dola dhidi ya wapinzani wa kisiasa, mnajichimbia shimo ambalo litakuwa gumu kulifukia. Zile ahadi za bima ya afya kwa wananchi wote ziko wapi? Je, bado tuendelee kusubiri utekelezaji usio na tarehe? Muachieni Tundu Lissu. Acheni chama chetu kifanye siasa zake kwa uhuru kama Katiba inavyoruhusu. Waachieni wananchi wapime sera, hoja na maono ya vyama tofauti, kisha waamue kwa hiari yao. Demokrasia haiwezi kustawi kwa kubana sauti za wanao wapinga. #FreeLissu #TunaWatuTutashinda
Brenda Rupia Jonas17,040 görüntüleme • 3 ay önce

Nkasi: CHADEMA yazuiwa na vyombo vya dola kupanda miti 1,500 kwa “maelekezo kutoka juu”. Rais haram huyo huyo anawahimiza Watanzania wapande miti. Huu sio utawala wa sheria, ni utawala wa upendeleo wa kisiasa. Kama kupanda miti ni uzalendo, basi kwanini uzalendo wa CHADEMA unahesabika kosa? Au Watanzania sasa wanapimwa kwa kadi ya chama?
Brenda Rupia Jonas14,940 görüntüleme • 4 ay önce

Bw. Makala, naona unajitekenya na kucheka mwenyewe. Lakini tambua hili: Chadema Tanzania si chama cha jana wala cha kuzimwa kwa kejeli – ni mpango wa Mungu. Kimevuka majaribu, kimesimama leo, na kitaendelea kusimama kesho kwa mkono wake Mwenyezi Mungu. Unakumbuka ndugu yako Mwigulu Nchemba, PhD alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama chenu? Alishirikiana na wengine kumtengenezea Mh. Lwakatare (aliyekuwa Mkurugenzi wa Ulinzi wa CHADEMA) kesi ya ugaidi – na kwa majigambo, akatangaza Bungeni kuwa Chadema imefungwa duniani na mbinguni. Lakini tazama, Mungu ni mwaminifu – Lwakatare alishinda kesi, na mwaka 2015 akaingia Bungeni kwa tiketi ya Chadema. Huo ndio mkono wa Mungu, si maigizo ya kisiasa ya jukwaami na propaganda. Rejesha kumbukumbu zako: babu yangu, SM Wasira, akiwa waziri kipenzi enzi za Mzee Kikwete, aliwahi pia kutamka kwa majigambo bungeni kuwa Chadema itakufa kabla ya 2015. Lakini Mungu akaonyesha ukuu wake – mwaka huo ukawa wa historia. Bila “goli la mkono” tungekuwa tumeandika historia tofauti. Leo nawe unarudia mtindo ule ule wa kauli zisizo na maana – jifunze kutoka kwa waliokutangulia. Badala ya laana zenu, historia huandikwa kwa vitendo na kwa ridhaa ya Mungu. Mwaka 2025 Jiandaeni kwa makubwa zaidi – mark this tweet. Na kwa kuwa unaufuatilia sana mambo ya CHADEMA basi free Tundu Antiphas Lissu – na utuambie yuko wapi Mdude Nyagali ! Usisahau, changia pia kupitia 0744 446 969 kwa jina CHADEMA HQ – maana najua moyoni mwako unaichukulia CHADEMA kuwa ngome ya matumaini ya watanzania.
Brenda Rupia Jonas28,644 görüntüleme • 1 yıl önce

Kuongozwa na mtu kama Gerson Msigwa ni fedheha kwa Taifa. Fikiria serikali kupitia kwake inasema mtu akitekwa, kama hajapatikana wao wafanye nini ,ivi kweli? Sasa kwani, serikali kazi yake ni nini kama si kulinda usalama wa wananchi wake? Kauli kama hizi zinaonesha ni kwa nini tunasema #NoReformsNoElection. Kwa mawazo ya aina hii, mtu kama wewe, Msigwa, hustahili kabisa kuendelea kushikilia wadhifa wa uwajibikaji wa umma. Ni aibu kwa Taifa na fedheha kwa wananchi unaodai kuwatumikia.
Brenda Rupia Jonas16,073 görüntüleme • 7 ay önce

We don’t want CCM Hatutaki CCM GenZ wapo barabarani. No Reforms No Election
Brenda Rupia Jonas11,682 görüntüleme • 7 ay önce

“Kufunga funga makanisa si jambo zuri.Mnafunga makanisa ili watoto wakasali wapi sunday school? Wamekosa nini?” amesema mzee wa upako. Kufunga makanisa kwa sababu tu Gwajima anamuombea Tundu Antiphas Lissu ni ushahidi wa serikali inayoogopa maombi na hoja kuliko kitu kingine chochote. Huu si uvunjaji tu wa uhuru wa ibada, bali ni hofu ya kisiasa iliyovaa joho la madaraka. Mnaanzaje kupambana na imani ya watu halafu mdai kuwa mnaongoza kwa haki? Mchezo huu mchafu utawatokea puani. Mungu hahusiki na dhulma.
Brenda Rupia Jonas14,373 görüntüleme • 1 yıl önce

Nimesikiliza Bunge la leo kwa mshangao na masikitiko makubwa.Aibu naona mimi. Na jiuliza, wabunge wa CCM hawana utu kabisa? Wamelogwa? Au sisi Watanzania tumezoea kupuuzwa na kudharauliwa kiasi hiki? Inaingia akilini kweli kwa Spika kuruhusu mijadala ya kipuuzi kama ile? Cha kuhuzunisha zaidi ni kuona wanawake wakishangilia vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji na ubakaji dhidi ya Agatha Atuhaire na wenzake—vilivyotekelezwa na vyombo vya dola! Hatukubali, hatunyamazi. Hii ni nchi yetu sote. Leo, yeyote anayemkosoa “Mama” au mfumo wa kiimla wa Iddi Amin Mama, anapotezwa. Jeshi, polisi, TISS—vyote vinatumika kama silaha ya kisiasa dhidi ya wananchi. Chama Cha Mapinduzi mjue haiwezekani kutunyamazisha wala kutupoteza wote. Kidogo kidogo, mafuta na maji vinaanza kutengana—hata miongoni mwenu. Wenye dola wanamuogopa anayesema ukweli kwa sauti yake tu! Leo tutawasukia WaKenya. Dunia inashudia.Msitusingizie Chadema Tanzania Msimamo wetu uko pale pale: #NoReformsNoElection. Changia kuendeleza movement kupitia namba: 0744 446 969 Jina: CHADEMA HQ. ✌️✌️
Brenda Rupia Jonas13,426 görüntüleme • 1 yıl önce

Taarifa ya leo ya Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania, Mh. MNYIKA John John, ikiambatana na ushahidi wa video, inafichua ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu—wanachama na viongozi wa CHADEMA walikamatwa na kuteswa walipokuwa wakielekea kufuatilia kesi ya Tundu Antiphas Lissu Mahakama ya Kisutu April 24, 2025. Tunaitaka Serikali kuwajibika. Waziri wa Mambo ya Ndani na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM Bw. Muliro lazima wawajibishwe. Dunia inapaswa kufahamu: ukandamizaji wa kisiasa haukubaliki Tanzania ya sasa!
Brenda Rupia Jonas12,141 görüntüleme • 1 yıl önce

“Chaguzi zetu haziendi sawasawa” amesema Askofu wa KKT mkoani Tabora.
Brenda Rupia Jonas10,664 görüntüleme • 11 ay önce
Daha fazla içerik yok.