
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania • 879,673 subscribers
Chama Cha Mapinduzi (CCM) - #Tanzania's governing party, founded on 5th February 1977. Membership: 15 million | https://t.co/KzE7LiVgt9
Videos

🎥𝐁𝐀𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐋𝐈𝐎 𝐍𝐉𝐄 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐋𝐈𝐎𝐊𝐀𝐍𝐀 𝐔𝐑𝐀𝐈𝐀 𝐖𝐀 𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐘𝐄𝐓𝐔 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐂𝐇𝐎𝐂𝐇𝐄𝐀 𝐕𝐔𝐑𝐔𝐆𝐔 𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐈𝐒𝐈𝐓𝐀𝐖𝐀𝐋𝐈𝐊𝐄: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amesema kuwa zipo taarifa zinazodai kuwepo kwa watu wanaojaribu kuchochea migawanyiko na vurugu zinazoweza kuhatarisha amani na utulivu wa Taifa. Ndugu Kihongosi ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kusimama imara kulinda uhuru, umoja na mshikamano wa nchi yetu, huku akisisitiza umuhimu wa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuimarisha umoja wa kitaifa, amani na maendeleo ya Watanzania wote. Amesema Tanzania itaendelea kuwa imara pale wananchi watakapoweka mbele maslahi ya Taifa, kudumisha upendo na kushirikiana kujenga nchi yenye mshikamano na ustawi kwa wote. Tembelea: ______ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #MtumishiWaWote
Chama Cha Mapinduzi89,888 görüntüleme • 4 ay önce

CHAMA CHAO KIMEKOSA DIRA, CHAMA CHAO KIMEKOSA MWELEKEO-KENANI
Chama Cha Mapinduzi15,549 görüntüleme • 1 ay önce

#CCM yamjibu #NAPE hoja ya Ushindi katika chaguzi. Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla kimemjibu Mbunge wa Mtama Ndg. Nape Nnauye kuhusu imani yake juu ya ushindi katika chaguzi mbalimbali nchini. Ndg. Makalla amesisitiza kuwa CCM haihitaji mbeleko na itashinda kutokana na rekodi nzuri ya kuwaletea wananchi maendeleo. Aidha, amesisitiza kuwa kauli iliyotolewa na kiongozi huyo haikihusu Chama Cha Mapinduzi na ni mawazo yake yeye mwenyewe. CCM itaendelea kuheshimu demokrasia na maamuzi yeyote ya wananchi kupitia sanduku la kura kama ilivyo siku zote. #CCMimaraSerikaliImara #SamiaNiWetuSote
Chama Cha Mapinduzi179,431 görüntüleme • 2 yıl önce

📌📌 MWENEZI MAKONDA ATATUA HADI KERO ZA WAZUNGU Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda kwa kuzingatia imani ya Chama Cha Mapinduzi ya kwamba Binadamu wote ni sawa, ameithibitisha imani hiyo kwa kusikiliza changamoto ya Mwanamama mzungu aliposimama na kusalimiana na Wananchi wa Kwasadala Wilayani Hai alipokuwa njiani kuelekea Mkoani Arusha. Mwanamama huyo wa kizungu aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sekila ambaye alieleza mgogoro wake na Benki ya ABSA na kuomba msaada katika utatuzi wa mgogoro huo ambapo Mwenezi Makonda ameagizia haki kutendeka kwa Mwanamama huyo. Chama Cha Mapinduzi kikiongozwa na Mwenyekiti wake Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kinaamini binadamu wote na sawa katika kupata haki sawa pasipo kujali dini, ukabila, rangi wala utaifa ukiwa ndani ya Taifa letu. 🗓️ 23 Januari, 2024 #CCMKazini #VitendoVinaSauti #KaziIendelee
Chama Cha Mapinduzi111,171 görüntüleme • 2 yıl önce

*Wasira: ACT, CHADEMA wasitafute mchawi viongozi wao kuzuiwa Angola.* Na MWANDISHI WETU KUTOKANA na hatua ya kuzuiwa kwa baadhi ya viongozi wa upinzani wa Tanzania kuingia nchini Angola, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amewataka viongozi hao wasiinyooshee kidole serikali. Wasira alitoa kauli hiyo jana, siku moja baada ya Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar na Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kuzuiliwa na mamlaka za Angola kuingia nchini humo juzi. Makamu Mwenyekiti Wasira alieleza hayo alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM katika ukumbi wa Kanisani, Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe ambako anaendelea na ziara ya kikazi. "Leo nimesoma viongozi walikuwa wanaenda Angola lakini wamenyang'anywa paspoti huko ni Angola sio hapa, hapa hatuja wanyang'anya paspoti na hata ikimaliza muda wake tunawapa, ili waende wanakotaka halafu warudi salama," nakuongeza "Wamelalamika kwa nini serikali imekaa kimya kwani sisi tunasimamia Airpoti ya Angola? Airpoti ya Angola inasimamiwa na watu wa Angola, na pia huenda walikuwa na jambo lao ambalo lilitiliwa shaka. Wangeuawa tungesema kwa nini wamewaonea watu wasiokuwa na hatia," alisema. Aliongeza kuwa "Sasa kuwaambia tu msiingie kuna tatizo gani simrudi tu nyumbani," Mbali na Othman na Lissu wengine waliozuiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quatro de Fevereiro jijini Luanda viongozi wengine marais wastaafu kutoka Botswana na Colombia, Waziri Mkuu Mstaafu wa Lesotho, na baadhi ya wakuu wa vyama vya siasa kutoka baadhi ya za Afrika. Viongozi hao, walikwenda Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD) yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation yakiwa na lengo la kuwakutanisha baadhi ya wadau kutoka Afrika kwa madai ya kujadili demokrasia na kubadilishana uzoefu. Baada ya kuzuiliwa viongozi, ACT-Wazalendo ilitoa taarifa ya kushangazwa na ukimya wa serikali kushindwa kutoa kauli na kutaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ifafanue na kutoa msimamo wa serikali kuhusu suala hilo. #KaziNaUtu #TunasongaMbele
Chama Cha Mapinduzi31,830 görüntüleme • 1 yıl önce

📌📌 #TunaendeleaNaMama🇹🇿 : SALAMU KWA MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Samia Suluhu Kuelekea Mwisho wa Mwaka 2023 , Kijana Mzalendo Komrade Nyanda Kabundi amepata Fursa ya Kuelezea Makubwa Yanayofanywa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan Jinsi anavyoongoza Nchi na Kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Tuendelee kumpa pongezi na salaam za mwisho wa mwaka Mama yetu na Mwenyekiti wa CCM kwa namna na kipaji ulichonacho kupitia Whatsapp NUMBER 0734 398 129 Samia Suluhu #VitendoVinaSauti #TunaendeleaNaMama🇹🇿 #CCMImara
Chama Cha Mapinduzi39,821 görüntüleme • 2 yıl önce

"...ningemuomba Mhe. Mutungi (Msajili wa Vyama Vya Siasa) afuatilie jinsi hivi vyombo vya upinzani vinavyotaka kuleta vurugu katika nchi, vinavyoendesha mambo yao ndani ya vyama vyao, Katiba ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo haifuatwi kabisa, nasema kwa ujasiri mkubwa..." - Ndg. Peter Msigwa Mchungaji Peter Msigwa amesema hayo akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Kawe Viwanja vya Panga Kinondoni. 🗓 16 Julai 2024. Ziara ya Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo Ndugu Amos Makalla. #VitendoVinaSauti #TunaendeleaNaSamia #KaziIendelee
Chama Cha Mapinduzi31,267 görüntüleme • 2 yıl önce

🔰CCM NAMBA MOJA Wajumbe Karibuni Dodoma, Tukamshuhudie Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa Tarehe 29-30 Mei 2025 Katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre 🔰KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE
Chama Cha Mapinduzi21,415 görüntüleme • 1 yıl önce

WANACHAMA MILIONI 13 - NI NGUVU, NI SAUTI, NI USHINDI! Kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za nchi yetu, chama kimoja, chama chetu – CCM – kimesajili wanachama zaidi ya milioni 13 kwa mfumo wa kidijitali. Hii si idadi tu. Huu ni muungano wa dhamira na silaha ya ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu. Katika mchakato wa kuchukua fomu, tumeona ari. Tumeshuhudia maelfu wakijitokeza kwa heshima na uzalendo. Leo, tunasema kwa fahari: CCM ni zaidi ya chama cha siasa, CCM ni muungano wa watu wenye dhamira ya kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo ya Taifa letu. Chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tumeandika historia pamoja, wanachama milioni 13 ni nguvu, ni sauti, ni ushindi. Kwa sauti moja, tunasema; OKTOBA... TUNATIKI! #IlaniYaUshindi2025 #OktobaTunatiki
Chama Cha Mapinduzi19,755 görüntüleme • 1 yıl önce

RAIS SAMIA: HATUTARUHUSU MTU YOYOTE KUVURUGA AMANI YA NCHI YETU KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE✅
Chama Cha Mapinduzi14,110 görüntüleme • 1 yıl önce

Pokea shukrani raia namba 1 wa Nchi hii, Rais wangu na Mwenyekiti wa Chama changu (CCM) Komredi Samia Suluhu Hassan #SamiaWaWatanzania🇹🇿 Samia Suluhu kazi unayoifanya ni kubwa na watanzania tunaiona. Asante kwa kuimarisha demokrasia, wanasiasa wanakushukuru ndani ya mioyo yao.
Chama Cha Mapinduzi22,757 görüntüleme • 3 yıl önce

CCM NDIO CHAMA KIKUBWA NA CHENYE USHAWISHI ZAIDI BARANI AFRIKA UBAO UNASOMA 13,000,670 Kufikia tarehe 29 Mei 2025, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa kimesajili jumla ya wanachama 13,000,670 kupitia mfumo wa kielektroniki, na hivyo kuendelea kuwa miongoni mwa vyama vya siasa vyenye wanachama wengi zaidi barani Afrika. #chamalawana #Kazinaututunasongambele
Chama Cha Mapinduzi13,173 görüntüleme • 1 yıl önce

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Akiongoza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa kwa Njia ya Mtandao unaofanyikia katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, leo tarehe 26 Julai, 2025
Chama Cha Mapinduzi11,841 görüntüleme • 1 yıl önce