
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2 • 37,206 subscribers
The main Opposition Political Party in Tanzania ✌️
Shorts
Videos

MILIONI 100 ZIMETIMIA! 🔥 Watanzania mmeandika historia! Sasa wananchi wamemjibu SIR TIVA kwa vitendo. Ahadi yake ilikuwa wazi; Watanzania wakifikisha TSh. Milioni 100, naye atachangia TSh. Milioni 2. Lengo la TSh. Milioni 100 tumelitimiza. Sasa Watanzania wanamkaribisha Sativa kutimiza ahadi yake ya kuchangia TSh. Milioni 2 kwa ajili ya Baraza Kuu la Umma. TUENDELEE KUCHANGIA, MARATHON BADO INAENDELEA. M-Pesa Namba: 0744446969 Jina: CHADEMA HQ NMB Bank Namba ya Akaunti: 22606600140 Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Tanzania71,848 Aufrufe • vor 8 Tagen

ASANTENI WATANZANIA! TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 50 ✌️ Ndani ya saa 96 sawa na siku 4. Asanteni kwa mwitikio wenu mkubwa. Mpaka sasa, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 50 katika Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334 kwa ajili ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma. Huu ni ushahidi kwamba Watanzania wanaweza. Safari inaendelea. Kila mchango una thamani. Tuendelee kuchangia hadi tufikie lengo letu la TSh. Milioni 334. ✌️ SIR TIVA
Chadema Tanzania20,528 Aufrufe • vor 10 Tagen

"Zimeshaingia kwenye akaunti ya chama shilingi milioni mia moja (100), Jana usiku niliongea na diaspora, pale pale walichanga milioni 20, Wataziweka kwenye akaunti ya chama. Nina kila sababu ya kuwashukuru Watanzania, nguvu ipo kwenye namba." Mhe. John Heche, Makamu Mwenyekiti Bara TUENDELEE KUCHANGIA KUFANIKISHA BARAZA KUU LA UMMA. M-Pesa Namba: 0744446969 Jina: CHADEMA HQ NMB Bank Namba ya Akaunti: 22606600140 Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Tanzania15,833 Aufrufe • vor 8 Tagen

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasikitika kuwatangazia kifo Suez Dani Maradufu ambaye ni dereva wa Makamu wa Mwenyekiti Bara, Mheshimiwa John Heche. Suez amekutwa amefariki leo asubuhi Jumatano, Julai 01, 2026 chumbani kwenye nyumba ya wageni aliyofikia, mjini Kigoma. Mwili umechukuliwa na Polisi kuupeleka hospitali ya mkoa wa Kigoma kwa ajili ya taratibu nyingine za uchunguzi. Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama, ndugu jamaa na marafiki kwenye msiba huu mzito. Taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa. Bwana alitoa. Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
Chadema Tanzania34,375 Aufrufe • vor 24 Tagen

Jeshi la Polisi limezuia mkutano wa hadhara uliokuwa umepangwa kufanyika leo, tarehe 27 Juni 2026, katika eneo la Rambo, Mkoa wa Tabora. Tangu asubuhi, askari walizingira uwanja wa Mwananchi Square na kuwazuia wananchi kusogelea eneo hilo. Kutokana na hali hiyo, msafara wa Makamu Mwenyekiti wa Chama, Mhe. John Heche, ulilazimika kuondoka kuelekea Kigoma kwa ajili ya kuendelea na ratiba ya vikao vya chama. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia msafara huo tangu ulipoanza safari yake kutoka Tabora Mjini.
Chadema Tanzania30,627 Aufrufe • vor 28 Tagen

Mhe. Tundu Antiphas Lissu akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. "#NoReformsNoElection"
Chadema Tanzania234,170 Aufrufe • vor 1 Jahr

Takwimu za kikanda za mwezi Aprili 2026; Kenya Petrol: Tsh 3,700 Diesel: Tsh 3,680 Kodi: 28% Uganda Petrol: TSh 3,600 Diesel: TSh 3,550 Kodi: 27% Rwanda Petrol: TSh 3,750 Diesel: TSh 3,720 Kodi: 30% Zambia Petrol: TSh 3,800 Diesel: TSh 3,770 Kodi: 30% Mhe. John Heche
Chadema Tanzania30,141 Aufrufe • vor 3 Monaten

Leo tarehe 19 Mei 2026, katika eneo la Isaka, Jimbo la Msalala mkoani Shinyanga, Jeshi la Polisi wamezuia msafara uliokuwa ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Mzee Said, uliokuwa ukielekea kwenye uzinduzi wa vizimba vya Chama, pamoja na upandishaji wa bendera.
Chadema Tanzania18,413 Aufrufe • vor 2 Monaten

Tanzania: Ushahidi mpya juu ya mauaji ya Oktoba 29, 2025. 🎥 DW News
Chadema Tanzania41,140 Aufrufe • vor 6 Monaten

"Pamoja na zuio haramu dhidi ya Chadema kuondolewa bado ofisi ya Msajili inatafuta njia za kufanya shughuli za Chadema zisimamishwe. Baada ya kikao cha Kamati Kuu tulichokaa tarehe 28 na 29 Aprili 2026 na matamko ya Kamati Kuu tuliyotoa tarehe 2 na 5 Mei 2026 kwa umma juu ya masuala mbalimbali, tumeandikiwa barua na Ofisi ya Msajili ya kutakiwa kujieleza." Mhe. MNYIKA John John
Chadema Tanzania15,460 Aufrufe • vor 2 Monaten

Sisi tunasema hatutapiga magoti kwa mtu yeyote anayeteka, anayeuwa na kupoteza watu, kama umekubali kuwa kiongozi wa umma lazima ukubali kukosolewa. Huyu anayefunga makanisa yanapomwambia acha kuteka watu kwanini tumuonee aibu na kumwogopa, mimi Heche sitamwogopa na tutasonga mbele. Albert Oltereu tangulia, sisi tunakwambia, wenzako tutavaa viatu vyako tutapambana na kusonga mbele, Mungu atubariki." Mhe.John Heche
Chadema Tanzania52,119 Aufrufe • vor 1 Jahr