
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2 • 37,671 subscribers
The main Opposition Political Party in Tanzania ✌️
Shorts
Videos

"Kamati Kuu imeelekeza kwamba viongozi waelekeze nguvu zao zote za kumsaidia mwenyekiti kama mashahidi wake. Katika muktadha huu Kamati Kuu imeazimia kusogeza mbele tarehe ya mkutano wa Baraza Kuu kutoka tarehe 15/9/2026 mpaka tarehe nyingine itakayoazimiwa." Mhe. Amani Golugwa
Chadema Tanzania81,754 次观看 • 17 天前

MILIONI 100 ZIMETIMIA! 🔥 Watanzania mmeandika historia! Sasa wananchi wamemjibu SIR TIVA kwa vitendo. Ahadi yake ilikuwa wazi; Watanzania wakifikisha TSh. Milioni 100, naye atachangia TSh. Milioni 2. Lengo la TSh. Milioni 100 tumelitimiza. Sasa Watanzania wanamkaribisha Sativa kutimiza ahadi yake ya kuchangia TSh. Milioni 2 kwa ajili ya Baraza Kuu la Umma. TUENDELEE KUCHANGIA, MARATHON BADO INAENDELEA. M-Pesa Namba: 0744446969 Jina: CHADEMA HQ NMB Bank Namba ya Akaunti: 22606600140 Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Tanzania72,193 次观看 • 2 个月前

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasikitika kuwatangazia kifo Suez Dani Maradufu ambaye ni dereva wa Makamu wa Mwenyekiti Bara, Mheshimiwa John Heche. Suez amekutwa amefariki leo asubuhi Jumatano, Julai 01, 2026 chumbani kwenye nyumba ya wageni aliyofikia, mjini Kigoma. Mwili umechukuliwa na Polisi kuupeleka hospitali ya mkoa wa Kigoma kwa ajili ya taratibu nyingine za uchunguzi. Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama, ndugu jamaa na marafiki kwenye msiba huu mzito. Taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa. Bwana alitoa. Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
Chadema Tanzania34,713 次观看 • 2 个月前

Jeshi la Polisi limezuia mkutano wa hadhara uliokuwa umepangwa kufanyika leo, tarehe 27 Juni 2026, katika eneo la Rambo, Mkoa wa Tabora. Tangu asubuhi, askari walizingira uwanja wa Mwananchi Square na kuwazuia wananchi kusogelea eneo hilo. Kutokana na hali hiyo, msafara wa Makamu Mwenyekiti wa Chama, Mhe. John Heche, ulilazimika kuondoka kuelekea Kigoma kwa ajili ya kuendelea na ratiba ya vikao vya chama. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia msafara huo tangu ulipoanza safari yake kutoka Tabora Mjini.
Chadema Tanzania30,627 次观看 • 2 个月前

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, pamoja na viongozi wengine wa Chama, wakiwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu, inayotarajiwa kuendelea kusikilizwa leo, Jumatatu, Agosti 10, 2026.
Chadema Tanzania14,833 次观看 • 1 个月前

ASANTENI WATANZANIA! TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 50 ✌️ Ndani ya saa 96 sawa na siku 4. Asanteni kwa mwitikio wenu mkubwa. Mpaka sasa, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 50 katika Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334 kwa ajili ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma. Huu ni ushahidi kwamba Watanzania wanaweza. Safari inaendelea. Kila mchango una thamani. Tuendelee kuchangia hadi tufikie lengo letu la TSh. Milioni 334. ✌️ SIR TIVA
Chadema Tanzania20,688 次观看 • 2 个月前

"Zimeshaingia kwenye akaunti ya chama shilingi milioni mia moja (100), Jana usiku niliongea na diaspora, pale pale walichanga milioni 20, Wataziweka kwenye akaunti ya chama. Nina kila sababu ya kuwashukuru Watanzania, nguvu ipo kwenye namba." Mhe. John Heche, Makamu Mwenyekiti Bara TUENDELEE KUCHANGIA KUFANIKISHA BARAZA KUU LA UMMA. M-Pesa Namba: 0744446969 Jina: CHADEMA HQ NMB Bank Namba ya Akaunti: 22606600140 Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Tanzania15,990 次观看 • 2 个月前

Takwimu za kikanda za mwezi Aprili 2026; Kenya Petrol: Tsh 3,700 Diesel: Tsh 3,680 Kodi: 28% Uganda Petrol: TSh 3,600 Diesel: TSh 3,550 Kodi: 27% Rwanda Petrol: TSh 3,750 Diesel: TSh 3,720 Kodi: 30% Zambia Petrol: TSh 3,800 Diesel: TSh 3,770 Kodi: 30% Mhe. John Heche
Chadema Tanzania30,141 次观看 • 5 个月前