
Clouds Media
@CloudsMediaLive • 1,935,778 subscribers
A multi-national company that is one of East & Central Africa’s most respected media houses and has been recognized as one of the country's premier.
Videos

Ungepata nafasi ya kuwa Rais kwa siku moja tu kitu gani cha kwanza ungefanya? Team #PB
Clouds Media152,698 Aufrufe • vor 9 Monaten

Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma limethibitisha kumpata Padre Camillius Nikata wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, ambaye alikuwa ameripotiwa kupotea tangu Oktoba 9, 2025. Padre Nikata, ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), amepatikana akiwa salama katika mashamba ya kijiji cha Mawa, kilichopo kata ya Hanga, wilayani Namtumbo. #CloudsDigitalUpdates
Clouds Media102,442 Aufrufe • vor 9 Monaten

Jumatatu ya Novemba 3,2025 Uongozi na wafanyakazi wa CLOUDS MEDIA GROUP pamoja na Familia ya Mtopa tulishirikiana na Ndugu ,Jamaa na Marafiki wa Master Tindwa Mtopa katika kukamilisha safari ya mwisho ya mpendwa wetu #MasterWaMchezo ambayo ni kumsindikiza katika makazi yake ya milele Makaburi ya Kwa Mama Kibonge Buza , Dar es Salaam. Master Tindwa Mtopa #MasterWaMchezo alifariki kwa kupigwa risasi siku ya Oktoba 30, 2025 akiwa nyumbani kwake Yombo Dovya Dar es Salaam. Clouds Media inawashukuru wote walioungana na familia katika kumsindikiza na kumhifadhi katika makazi yake ya milele. Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Master Tindwa mahali pema peponi. Ungana na Sports Xtra leo saa tatu usiku kwa kipindi maalum kuhusu #MasterWaMchezo ambapo tutajadili mengi yaliyomhusu kipindi cha uhai wake.
Clouds Media62,633 Aufrufe • vor 9 Monaten

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amesema kamwe hatoacha kuwawajibisha wazembe, wavivu na watendaji wote wa Mkoa wa Arusha wasiotimiza majukumu yao kikamilifu licha ya kuongezeka kwa kelele na ukosoaji unaoelekezwa kwake kutokana na mtindo wake wa Uongozi. Mhe. Paul Christian Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Mei 27, 2024 wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli ikiwa ni siku yake ya tatu ya ziara za kutembelea wilaya zote za Mkoa wa Arusha ili kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kauli ya Mhe. Mkuu wa Mkoa imekuja kufuatia baadhi ya watu kunukuliwa na vyombo vya habari wakimtaja Mhe.Makonda kama mdhalilishaji wa watumishi wa Umma ndani ya Mkoa wa Arusha, suala ambalo Mkuu wa Mkoa amelitaja kutombabaisha ama kumpunguzia kasi katika kusimamia watendaji wavivu na wazembe wanaoshindwa kutimiza majukumu yao katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha. #CloudsDigitalUpdates
Clouds Media127,998 Aufrufe • vor 2 Jahren

"Nilipotoka pale hatua ya kwanza nilikwenda BRELA kuhakikisha kama ni kweli hawa watu wamesajiliwa. Nilipofika BRELA wakaniambia imesajiliwa na wakaniambia ilipo ambapo ni sahihi kabisa wakanipatia na registration namba, kuhakikisha kwamba wale watu wamesajiliwa na taasisi ya Serikali hiyo ikanishinikiza zaidi kumbe na serikali inajua juu ya hiki? Lakini baada ya hapo nikaanza kusikia pia anasema Mh. Bashe (Waziri wa Kilimo) amemtembelea na kuona jinsi kilimo cha Vanilla kimekua vizuri na amemuahidi kumpatia eneo kubwa la kujenga kiwanda cha kuchakata Vanilla ili iuzwe hapa nchini"-Rebeca Eliazar Kyaka muathirika wa utapeli wa Mr. Manguruwe. #PBCloudsFM #Tumekuverify
Clouds Media86,731 Aufrufe • vor 1 Jahr

Hili ndio neno la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kuhusiana na Sakata la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezifungia Bar mbalimbali kutokana na kukiuka taratibu na sheria za Usimamizi wa Mazingira na upigaji kelele za Muziki. #SentroyaCloudsTv
Clouds Media109,587 Aufrufe • vor 3 Jahren

Big Joe Joseph Kusaga - Mkurugenzi Mtendaji Clouds Media Group amesema kuwa anaamini elimu ambayo Watanzania wataendelea kuipata kupitia Clouds na Mchongo Tv itasaidia wengi kuingia kwenye kilimo na kukuza uchumi na itafika wakati ambao dola 1 tutainunua kwa Tsh. 100. #AsanteKwaTafu #GenC4Life
Clouds Media50,029 Aufrufe • vor 1 Jahr

“Kwenye vyama vya siasa vya upinzani kuwapata wagombea, kuwapata viongozi, kuwapata watu wenye maono sio kazi nyepesi kwa sababu watu wengi wanakimbia wajibu huu. Tuna maono tunayapigania, hatujayafikia na bado tuna kazi kubwa mbele - Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA #KikaoNaMwenyekiti #AsanteKwaTafuu
Clouds Media47,029 Aufrufe • vor 1 Jahr