
Gilly Bonny Tv
@GillyBonnyTv • 126,486 subscribers
Independent Media I WhatsApp +255655832712
Videos
0:29
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma, amemtolea uvivu mwanasiasa wa CHADEMA, John Heche, akimshutumu kwa kutoa kauli za kejeli na dharau dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan. Msukuma amesema haikubaliki kwa mwanasiasa kama Heche kuendelea kumsema Rais kwa namna ya kubeza juhudi zake, huku akisisitiza kuwa viongozi wa upinzani wanapaswa kuwa na nidhamu ya maneno wanapojadili masuala ya kitaifa.
Gilly Bonny Tv68,340 views • 1 year ago

Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, ameeleza kuwa kifo cha ghafla cha aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Suez Dani Maradufu, kimeacha maumivu makubwa ndani ya familia ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na mchango, uaminifu na utu aliokuwa nao marehemu wakati wa uhai wake. Matiko amebainisha hayo leo Jumapili, Julai 5, 2026, wilayani Tarime mkoani Mara, akitoa salamu za faraja mbele ya umati wa wanachama, viongozi na waombolezaji waliofurika kumsindikiza marehemu Suez katika nyumba yake ya milele. Mwanasiasa huyo ameeleza kuwa ukaribu wa kikazi wa zaidi ya miaka 15 aliokuwa nao na marehemu unamfanya ashuhudie pengo kubwa lililoachwa ndani ya chama, kwani Suez alikuwa ni mtu aliyetawaliwa na hekima na busara za kipekee katika majukumu yake. "Nimesimama hapa kwa masikitiko makubwa sana ikizingatia nimeshaishi kwenye familia ya CHADEMA kwa zaidi ya miaka 10, 15... Kifo ni jambo ambalo linaumiza sana, lakini kifo hiki kinaumiza zaidi pale ambapo kinamchukua nguzo ya familia, mtu ambaye anategemewa na marafiki, ndugu lakini zaidi na taifa, na kifo cha ghafla," amesema Matiko. Matiko ametoa pole za dhati kwa John Heche, akimtaka kupokea msiba huo kwa ustahimilivu kwani anatambua wazi kuwa marehemu Suez hakuwa dereva tu wa kawaida, bali alikuwa ni nguzo na sehemu ya familia yake ya karibu. Pia amewapa pole mjane na watoto kwa kuondokewa na mhimili wao. Ametamatisha kwa kuwakumbusha wote waliokusanyika msibani hapo kuwa maisha ya duniani ni mapito na kila mmoja anapaswa kutenda mema yanayompendeza Mungu, huku akiwatia moyo wana-CHADEMA kuendelea kuwa wamoja na kushikamana katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Gilly Bonny Tv11,375 views • 1 month ago

KOCHA WA SIMBA SC, FADRU DEVIS AKIWA UWANJANI ENZI ZAKE AKISAKATA KABUMBU
Gilly Bonny Tv58,588 views • 1 year ago

"Diamond Platnumz badilika hakuna wa kukulia bilioni mbili katika harusi" Dudu baya
Gilly Bonny Tv60,377 views • 1 year ago