
Habari Digital
@HabariDigital_ • 246,165 subscribers
Kwa Habari, Burudani na Matukio, Kitaifa na Kimataifa, Saa Ishirini na Nne, Siku Saba za Wiki.
Shorts
Videos

Jemedari Said ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram 👇 Wachezaji wetu huwa wanachomwa sindano wakati gani? Kabla ya mechi, wakati wa half time, baada ya mechi? Naona mabomba ya sindano kwenye hii video kutoka kwenye chumba cha wachezaji baada ya mchezo. Huwa ni sindano za maumivu au za jambo gani? Kama za maumivu, kweli bado wachezaji wanachukua risk ya kuchoma sindano na kuingia kiwanjani? Au ni baada ya mchezo? Mbona CCTV Camera imezibwa pia? Kwenye hiki chumba kulikuwa na nini cha siri hivyo? Kama sio sahihi kuwa na cameras kwenye dressing rooms kwanini ziliwekwa? Kama sahihi kwanini zizibwe namna hii? Nini ambacho hakikupaswa kujulikana? Anahoji Jemedari Said
Habari Digital132,313 次观看 • 1 年前

Papa Leo XIV ameonekana kupuuza na kuikwepa bendera inayowakilisha jumuiya za watu wenye mwelekeo tofauti wa kijinsia wakiwemo wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja. Papa Leo XIV ameonyesha dalili za kukataa jumuiya hizo wakati akisalimiana na kubariki hadhara iliyojitoleza wakati akizungumza na wataaluma wa habari siku ya Jumatatu Mei 12, 2025, kwenye Ukumbi wa Paul VI mjini Vatican. Hata hivyo baadhi wa watu wanatoa maoni juu ya video hiyo na kueleza kuwa Papa Leo hakupuuza bendera hiyo bali hakuwa na uwezo wa kusalimia pande zote mbili (kushoto na kulia) wakati akikatiza katikati hadhara hiyo, hivyo alilazimika kusalimia kila upande kwa zamu huku akisonga mbele, na alipofika eneo lenye bendera ilikuwa ni zamu ya upande wa kulia huku bendera ikiwa upande wa kushoto. Wanaharakati na taasisi mbalimbali zinazounga mkono jumuiya hizo, tayari wameanza kumtuhumu na kumkosoa Papa Leo XIV kwa kupuuza bendera hiyo. Nini maoni yako.....
Habari Digital83,956 次观看 • 1 年前

VIDEO: Kufuatia matukio ya utekaji na mauaji yanayoripotiwa kutokea nchini., Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amezitaka mamlaka kualika wataalamu kutoka nje ya Tanzania kwaajili ya kuvichunguza vyombo vya ulinzi na usalama. Lissu ameyasema hayo leo Septemba 11, 2024 alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam akitokea nchini Ubelgiji.
Habari Digital106,486 次观看 • 1 年前

VIDEO: Aliyekuwa Naibu Rais Kenya, Rigathi Gachagua amelazimika kutoka mbio kunusuru usalama wake, baada ya kundi la vijana kuzua vurugu hivyo kulazimu ibada ya mazishi kukatishwa, Tukio hilo limetokea katika eneo la Limuru, kaunti ya Kiambu ambapo magari ya msafara wa Gachagua yameharibiwa huku baadhi wa wasaidizi wake wakijeruhiwa. Wasaidizi wa Gachagua wanaituhumu serikali kuhusika na mpango huo, wakidai njama hiyo ilipangwa na Mbunge wa Limuru ambaye naye amekana kuhusika na vurugu hizo. #HabariDigital 🎥KTN
Habari Digital97,047 次观看 • 1 年前

VIDEO: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema [ Godbless E.J. Lema ] ametoa utabiri wake baada ya kufutwa usajili wa kanisa la ufufuo na uzima linaloongozwa na askofu Josephat Gwajima. Aidha Lema amekosoa hatua zilizochukuliwa na mamlaka akieleza kuwa aliyetakiwa kuchukuliwa hatua ni askofu Gwajima na si kuifungia taasisi yote.
Habari Digital61,252 次观看 • 1 年前

VIDEO: Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema atakwenda mahakamani kuishitaki serikali ya Tanzania. Lissu amesisitiza kuwa atashinda kesi hiyo hivyo serikali ya Tanzania itatakiwa kumlipa fidia na wasipofanya hivyo basi ataanza kuzikamata ndege za Tanzania zinazofanya safari zake nje ya nchi
Habari Digital81,735 次观看 • 1 年前

Aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni mwanamke wa kipekee mwenye akili na maono makubwa, kiasi kwamba hajawahi kumuona mwanamke mwingine mwenye uwezo kama wake. Akizungumza leo Juni 24, 2025, kwenye Jukwaa la Wanawake lililofanyika jijini Arusha, Makinda amewataka wanawake na Watanzania kwa ujumla kumheshimu na kumuunga mkono Rais Samia, huku akisisitiza kuwa baadhi ya mijadala inayoibuka dhidi yake ni kwa sababu ya wivu kutoka mataifa jirani. "Nawaombeni mkapige kura kwa Mama. Tujiulize tu, wanawake tuna kitu kingine zaidi ya Mama Samia? Hakuna mwanamke mwenye akili ajabu kama Mama Samia, sijawahi kuona. Hawa wenzetu majirani wanatuonea wivu," amesema Makinda. Aliongeza "Haya maneno na mijadala unayoyaona ni wivu tu... Sasa sisi tumfunike, tumpe heshima. Hao wengine hata mkiwapigia kura mbona hawatashinda... kwanini mpige kura ya kupoteza?"
Habari Digital47,133 次观看 • 1 年前