
Martin Maranja Masese
@IAMartin_ • 612,199 subscribers
MMM | Sperm That Won The Race | Cogito, ergo Sum | Patria o Muerte, Venceremos |
Shorts
Videos

Mwenyekiti Tundu Lissu amesema hataki upumbavu wa kutembelewa usiku gerezani. Hataki vikao vya gizani. Yupo tayari kuishi gerezani hadi haki ipatikane, kwa kuwa anapigania haki, yupo tayari gharama. Kama unampenda sana, njoo mahakamani. #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese32,776 просмотров • 5 дней назад

“The truth is an offense, but not a sin” Mwenyekiti Tundu A.M Lissu amenukuu maneno ya Bob Marley & The Wailers kutoka katika wimbo wa ‘Jah Live’ ambao ulitoka mwaka 1975 kufuatia kifo cha aliyekuwa Mfalme wa Ethiopia, Haile Selassie I (kifo chake kilitangazwa 27 Agosti 1975).
Martin Maranja Masese17,331 просмотров • 4 дней назад

Tundu Lissu amehitimisha kutoa ushahidi wake wa msingi (examination-in-chief) katika kesi ya uhaini inayomkabili. Upande wa Jamhuri (mashtaka) umeanza na unaendelea kumhoji/kumfanyia dodoso (cross-examination). Jaji Dunstan Nduguru ameahirisha shauri hadi kesho, Jumatano, 27 Agosti 2026, saa 3:00 asubuhi.
Martin Maranja Masese29,458 просмотров • 12 дней назад

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. Tupo tayari kuendelea na usikilizaji wa utetezi wa Mwenyekiti wetu, Tundu A.M. Lissu. Baada ya kukamilisha msingi wa ushahidi wa tabia yake njema (good character), Tundu Lissu ataelekeza hoja zake kwenye hati ya mashtaka ili kuonyesha kutokuwepo kwa kosa lolote la jinai linalokidhi vigezo vya uhaini. #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese26,525 просмотров • 13 дней назад

Kubaaaaabake. Masela wamekataa porojo. Zimeletwa stori za awamu ya sita, watu wamezomeaa balaa. Watu wapo kwenye burudani unawaletea habari za awamu ya sita. Tunajenga arenaaa. Tunajenga arenaaaa. Tuna, tuna, tuna miaka nenda rudi. Masela wamekataa porojo. 😁
Martin Maranja Masese103,791 просмотров • 1 месяц назад

Kesi ya uhaini wa uongo na kubumba tu inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A.M Lissu imehairishwa saa tano asubuni leo baada ya upande wa mashtaka kusema hawana shahidi mwingine kwa leo baada ya shahidi wa 16 wa Jamhuri, ACP Amin Mahamba kumaliza kutoa ushahidi wake. TAL ameeleza Mahakama hilo halitakiwi kutokea tena na kuanzia kesho Jamhuri wabebe mashahidi wa kutosha kwa siku moja #FreeTunduLissu #TunduLissuSioMhaini
Martin Maranja Masese39,427 просмотров • 27 дней назад

Jaji Dunstan Nduguru amehairisha shauri hadi jumatatu 23 August 2026 saa tatu asubuhi ambapo Tundu Lissu ataendelea na utetezi wake katika kesi ya uhaini inayomkabili. TAL ameanza kujitetea mwenyewe akiwa ni shahidi wa kwanza uoande wa utetezi. WE SHALL OVERCOME. #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese25,812 просмотров • 17 дней назад

MaCCM wamefilisika kisiasa; wamebaki kutegemea nguvu za dola na Mahakama, ambako bado tunawashinda kwa hoja. Sasa wanajaribu kuzuia CHADEMA kuzungumza na waandishi wa habari nje ya viunga vya Mahakama. Hii ni baada ya kesi ya kikatiba inayohusu haki za Tundu A.M Lissu gerezani ikiwa ni pamoja na haki ya faragha kwa mawakili wake. Polisi wanadai hii ni amri kutoka kwa Msajili wa Mahakama. Nafikiri, tutaihoji amri hii Mahakamani na kuhakikisha sheria inatunzwa, inalindwa na kuheshimiwa! #FreeTunduLissu #TunduLissuSioMhaini #FreeTunduLissu #TunduLissuSioMhaini
Martin Maranja Masese52,529 просмотров • 1 месяц назад

GIRISHONI amefanya niipakue hii makala, tusikilize wote. Wote sasa tukatazame makala ya BBC AFRICA EYE ya mwaka 2026 inaangazia mapambano ya kisiasa ya Tundu Lissu na jaribio la mauaji dhidi yake la mwaka 2017, ikionyesha juhudi zake zinazoendelea za kudai mageuzi ya mfumo wa uchaguzi nchini Tanzania licha ya kukabiliwa na mashtaka ya uhaini aliyopewa mwaka 2025. Halafu baadae tutapata muda wa kujadili kipeperushi cha Serikali katili ya CCM kilichotolewa na GIRISHONI.
Martin Maranja Masese58,236 просмотров • 1 месяц назад

CHADEMA sasa hivi si chama cha siasa tu, ni imani iliyozama mioyoni mwa watu! Baada ya kushiba nondo za maana kutoka kwa viongozi, wananchi wenyewe wamemwaga upendo kwa kuchangia kiasi cha TZS 5,992,255 kidogo kidogo (Tone kwa Tone), kisha burudani ya ngoma za ukombozi ikafuata. CCM ili ipate vibe kama hili, ni lazima imwage mabilioni kusomba wasanii ili kuvuta watu. #PeoplesPower #KatibaMpya #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese95,484 просмотров • 3 месяцев назад

Ndugu Madenge katika jambo hili umenisikitisha sana. Sikutegemea unaweza kuwa sehemu ya kejeli hizi. Hao wengine ni wapumbavu tu ukijumlisha na huyo Masanja (hawakunishangaza) Siyo kwamba mnachekesha, mmeonesha ujinga wenu. Mmeonesha jinsi mlivyo machawa wa watawala. Na mmejitenga na jamii kubwa ya watanzania. Mmechagua kuwa maadui wa umma. Twitter (X) mnalalamika kuhusu umeme kila siku, watu tunakwenda barabarani na mabango ya umeme mnakwenda kutukejeli? Kweli nimeamini sasa, kuwa “paid slave” ni dhambi. Unatumikishwa tu. Masanja hajaenda shule. Hakuna ubongo kichwani, anawezaje kuwapa maudhui (content) za kipunbavu hivi na mkazitumia? Au ninyi pia mmekubali kuwa wapumbavu kama yeye? Mbaya zaidi ni kwamba wote katika kundi hilo hakuna hata ambaye ana diploma au degree ya uandishi wa habari na utangazaji. Wameokotwa kijanja-kijanja na leo wanakejeli watanzania. Kama mmeshindwa kuandamana na hamtaki, maiwadhihaki wananchi hao wachache ambao wamekubali kuandamana kwa gharama zao wenyewe. Mnapata faida gani wakiacha kuandamana? Naelewa, watangazaji wa EFM hapo mnalipwa vizuri. Maumivu makubwa ya ugumu wa maisha na kupanda kwa bidhaa sokoni hakuwagusi. Labda ndiyo maana mnakejeli haya maandamano. Mnakosea sana. Mtaani kuna maumivu makali. Wananchi hawana maji wala umeme. Sukari bei juu na mtaani haipo. Miundombinu ni duni na serikali inakusanya kodi. Jukwaa pekee kueleza hayo ni katika maandamano. Biashara za watu mtaani zinakufa. Mitaji yao imepotea. Media ambayo ingelitumika kufikisha ujumbe kwa serikali ndiyo inakejeli maandamano ambayo yanatumika kupaza sauti za watu mtaani. Maandamano yale yanatumika kufikisha ujumbe kwa watawala. Ukisoma mabango wananchi wameandika na kubeba kero zao, wanatembea kwa zaidi ya kilometa 20, kuziwasilisha, mnawakejeli? Mnatumika na DOLA kwa nia ovu. Mnafifisha morali ya umma kujitokeza katika maandamano ya amani ambayo yanasaidia kubeba sauti kubwa ya umma kwenda kwa watawala. Mnakosea sana. Hili ni tatizo kubwa. Kwa kuwa mmiliki wa EFM ni mwana CCM kindakindaki anatumia chombo chake cha habari kukejeli shughuli za kisiasa na maandamano ya kiraia. Huu ni UPUMBAVU. Kazi ambazo mnazifanya hapo leo EFM/ETV, Malcom X alizieleza vizuri sana mwaka 1963. “house Negro” na “field Negro.” Ninyi watangazaji wa EFM ni ‘house negro’ kwa matendo na tabia zenu hizi. House negro aliishi katika nyumba ya bwana wake - ghorofa au dari - lakini bado aliishi katika nyumba ya bwana, alivaa mabaki ya nguo za bwana wake. Alikula chakula bwana wake alikiacha mezani. House negro alijatanabaisha kila mara kwa maana ileile ambayo bwana wake alijitambulisha. House negro alijiweka katika daraja sawa na bwana wake, wakati huo ni myumwa na kijakazi. Bwana wake aliposema, “Tuna chakula kizuri,” alisema, “Ndiyo, sisi tuna chakula kingi kizuri.” Bwana wake aliposema “tuna nyumba nzuri hapa,” alisema, “Ndiyo, tuna nyumba nzuri hapa.” Bwana wake akiugua, house negro angemuuliza “Kuna nini bosi, sisi wagonjwa?”. Maumivu ya bwana wake yalikuwa maumivu yake mara mbili. Aliumia kuliko hata watoto wa bwana wake. House negro ilimuuma zaidi bwana wake kuwa mgonjwa kuliko yeye mwenyewe kuwa mgonjwa. Hawa sasa ndiyo wafanyakazi wa EFM/ETV. Hizi ni tabia zao za kitumwa, house negro. But I know, nothing you can if you’re just a paid slave. 🙏🏽 Brigedia Mtikila, MMM.
Martin Maranja Masese457,031 просмотров • 2 лет назад

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es salaam Kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu A.M Lissu. Upande wa Jamhuri leo umeleta shahidi wake mwingine ambaye ni afisa wa jeshi la polisi kuendelea kutoa ushahidi wake katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti Tundu A.M Lissu.
Martin Maranja Masese22,302 просмотров • 28 дней назад

Kitila Mkumbo amenikumbusha kitabu cha Chinua Achebe (A Man of the People) wakati Waziri wa Utamaduni, Chief the Honourable M.A. Nanga, M.P. anasema “Teaching is a very noble profession”. Chief Nanga anatamka maneno hayo akifahamu ukweli ni kinyume chake. Anaisifu taaluma ya ualimu kwa misingi ya heshima lakini yeye ameacha ualimu na kuingia katika siasa na kuwa fisadi mkubwa. KITILA, kama UALIMU ungelikuwa unalipa kuliko SIASA usingeacha ualimu ili utafute UBUNGE na baadae WAZIRI. Ualimu ungelikuwa unalipa kuliko siasa usingeondoka UDSM. Kiinua mgongo kwa mbunge mmoja wa Bunge la Tanzania ni Sh380 Milioni baada ya kipindi cha miaka 5. Mwalimu gani analipwa mafao hayo akistaafu na miaka 55 au 60? Mwalimu gani anapata mshahara wa Sh22 Milioni kwa mwezi kama mbunge? Kitila Mkumbo (PhD), profesa kuwa muongo hata haipendezi. We are experiencing a cultural and intellectual decline.
Martin Maranja Masese37,679 просмотров • 1 месяц назад

Mchawi binadamu, paka anatumwa tu. MPEMBA ametumwa kumshambulia NAMBA MBILI wao na amembatiza jina la YUDA. Kosa lake ni kusema alipendwa sana na JIWE. Wamekasirika sana. Jamaa anasema JIWE alimtupa Brazil. Wanasema ametengwa hadi na familia ya ‘WHITE HAIR’. Eti ni kweli, wazee wa ‘Safari ya Matumaini’ mmemtenga 'Mzee wa Mustachi'? Sisi wengine tunafurahi. Kazi yetu moja tu, kuchochea kunu. Ushirika wa 'wanyonya damu' hauwezi kudumu. NB; kama wapo wengi, kwanini hakuna makofi? SIJAPENDA.
Martin Maranja Masese58,748 просмотров • 3 месяцев назад

Jana niliandika ujumbe nikikosoa kitendo cha Mzee MBOWE kumuombea msamaha SABAYA. Nimepata maoni mengi; wengine wakisema sikuwa sawa. Ipo hivi. Kuna mambo katika siasa hayawezi kufutwa na maneno laini na mepesi ya “msamaha,” hususani msamaha usiotoka kwa mtenda dhambi mwenyewe. Utawala wa SABAYA katika wilaya ya Hai haukuwa wa kisiasa tu; ulikuwa ni utawala wa chuma na ukatili uliopitiliza. Hata Mzee MBOWE anafahamu hilo. Makosa ya uhujumu uchumi na unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery) yaliyomfunga gerezani wakati ule, ni tone dogo sana katika bahari ya unyama wake. Wapo watu walitekwa, kuteswa, na kuachwa na vilema vya kudumu. Kusema mtu huyu anastahili msamaha bila toba ya dhati kwa wahanga, si tu ni kosa, ni dhihaka. Miongoni mwa wahanga wa genge la SABAYA ni ndugu yetu Simon MNYAMPANDA, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai. Ndugu yetu aliteswa. Simon Mnyampanda aliteswa kwa umeme. Ameeleza wazi kwamba, alihojiwa kuhusu mahusiano yake na Mzee MBOWE. Mwisho, alipigwa misumari ya miguu. Huyu ni mtu aliyepata mateso hayo akimlinda Mzee MBOWE na CHADEMA. Leo Mzee MBOWE anajigeuza kadinali na kumuombea msamaha mtesaji SABAYA? Genge hilo halikuishia hapo. Genge hilo lilikuwa kama MAHARAMIA. Walivamia nyumbani kwa mgombea udiwani wa kata ya Narumu katika jimbo la Hai. Baada ya kumkosa, walitoa adhabu ya kinyama kwa watu waliokuwepo nyumbami kwa kuwakata masikio na sehemu nyingine. Nyumba nzima ilitapakaa damu. Hawa ni binadamu, si takwimu za kisiasa. Hawa watu waliotendewa mambo hayo wapo. Baadhi ya ushahidi wa masuala hayo nimeambatanisha katika makala hii. Inasikitisha kuona Mzee Mbowe anatumia mateso ya wafuasi wake kama mtaji wa kisiasa (political capital). Binafsi nimejiuliza maswali mengi tangu hiyo jana. Je, wahanga wameombwa msamaha na kufidiwa? Je, mateso yao yamekuwa ngazi ya makubaliano ya kisiasa? Hii si dharau kwa wale walioteswa wakikupigania? Sabaya anapaswa kuomba msamaha kwa waathirika, si kuombewa. Vinginevyo, hii ni michezo ya kumtengenezea mazingira ya kupata uteuzi katika Serikali ya CCM. Watu wa Hai hawajasahau. Damu na machozi ya wahanga bado vinadai haki. Msamaha bila toba ni baraka kwa ukatili mwingine ujao. Haki kwanza, msamaha baadaye. Binafsi, nilimheshimu Mzee Mbowe kiasi cha kumpa mwanangu wa tatu jina la “Freeman”. Leo hii, nahisi usaliti mkubwa moyoni mwangu kwa mambo hayo. Kunyamaza mbele ya usaliti huu si busara, bali ni upumbavu ambao kesho utatunyong’onyesha. Nimeandika ili kulinda hadhi ya jina la mwanangu. Siku mtoto wangu akiniuliza, nitamjibu kwa utimamu kabisa. “Nilitetea maana halisi ya ‘Freeman’ wakati jina hilo lilipotaka kuchafuliwa na siasa za kimaslahi.”
Martin Maranja Masese71,675 просмотров • 4 месяцев назад
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Fungua kwa tahadhari; ⚠️ Picha za kutekwa na kuuawa kwa Joshua Mollel (21), mwanafunzi wa kilimo kutoka Tanzania. Serikali ya Tanzania ilitangaza kwamba, Joshua Mollel aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la HAMAS mnamo tarehe 7 Oktoba 2023. Pumzika kwa amani Joshua 🙏🏽
Martin Maranja Masese368,257 просмотров • 2 лет назад

Ndugu yetu Edgar Mwakabela, SIR TIVA amepatikana katika hifadhi ya Katavi. Ameteswa na ameumizwa sana. Tunaomba watu wa Katavi mtusaidie haraka sana apate msaada wa matibabu. Rais Samia Suluhu umefika huku? Tulisema hatuwezi kurudi katika zama hizi za kuwatesa wakosoaji wako.
Martin Maranja Masese290,158 просмотров • 2 лет назад

Kuporwa kwa uwanja wa michezo wa Sahara uliopo kata ya Mabibo, Ubungo—ambalo ni eneo la wazi la umma—ni uthibitisho tosha la jinsi wananchi wanavyokosa watetezi wa haki zao pale CHADEMA wanapokuwa nje ya vyombo vya maamuzi. Wananchi wa eneo hili sasa wapo hatarini kupoteza kabisa ardhi hii ya wazi ambayo wameitumia kwa miaka mingi kwa ajili ya michezo na shughuli za kijamii.
Martin Maranja Masese47,520 просмотров • 3 месяцев назад