
Johari Mshana
@joharimshana • 2,609 subscribers
Am here to stay!! 
Shorts
Videos

Uhanarakati umeshakufa Tanzania na wamehuaribu wao wenyewe, imagine mtu yuko serious kabisa anasema uongo kwa kuchezea na kuyatumia maisha ya mwenzao yuko jela. Samia wakati yuko kigoma, jioni Kagame anakutana na Bill gates kwahiyo Kagame alichomoka ikulu na bodaboda akakimbilia boda ya kigoma kukutana na Rais! Huruma kwa wananchi. Tafuteni namna ya kusema na donors wenu kuhusu Lissu lakini kutunga stori kuhusu mtu ambaye anateseka jela sio vizuri. Kule hakuna hakuna maisha ambayo nyie mnaishi ba ndugu. Ila ndugu zake Lissu nao nahisi wanapenda haya maisha ya ndugu yao kutumiwa hivi. Kwahiyo stori ya Urgent ndio hii ndio maana wengine hawajaijali,.
Johari Mshana20,455 Aufrufe • vor 7 Tagen

Kumekuchaa, Dada wa watu kafanikiwa kupata mtoto wa kiume!! Hongera kwake.
Johari Mshana94,532 Aufrufe • vor 1 Monat

Sisi tuko busy na Ufisadi na Heche na Matajiri wa katoro 😂 mengine tupumzike kwanza. Jaman nimetumiwa video ya mzigo wa Makamu semeni SUUUUUUUUUUU 😂 Haya bwanaharusi huyu hapa, na yeye sio mnyonge… nisaidieni basi kama mnawajua nipate card ya harusi niende kahama nasikia ndoa ni kahama! Dada yenu nafaa mimi kwa matumizi ya wasukuma. Ila mbona kama WACHAGA kwasasa ni kama wanapumulia michine tuu 😂 niambie harusi zipi zina hela WASUKUMA au WACHAGA?
Johari Mshana22,038 Aufrufe • vor 20 Tagen

Watoto wa Tanzania wanakula raha, kwahiyo huyu alitakiwa awe Mbunge?
Johari Mshana50,391 Aufrufe • vor 2 Monaten

Niitieni John Heche, kuna ujumbe wake kutoka kwa vijana wake wakimwambia huku mtaani ndani ntiti na nje ntiti. Siasa ukichanganya na harakati madhara yake haya unataka kila siku usikike wakati muda umeisha wa jukwaa. Unakuta kazi ya kufanya Maria anafanya Heche, uzuri kizazi hiki hakina shida unakumbushw tu KIKUBWA kama hivi. Umeshindwa kutusikia wazee wenzio haya Heche kula chuma hiko kutoka kwa vijana - tukutane 2030.
Johari Mshana23,934 Aufrufe • vor 1 Monat

Wambea wenzangu muwe mnanizingatia sana, hapa mimi umbea ni wowote tu! Haya sasa nawaza za ndaniii ya familia ya kigogo!! Ooh sijawaambia kigogo ni nani, akhuu niliwaambia ni Mhe. Abdallah Ulega 😆! Sasa bwana, Mama Ulega ( Mbunge wa viti maalum) anamtafuta mke wa kaka yenu mji mzimaa huu toka weekend imeanza! Mjitahidi kumficha dada yetu huko Najma, mke wa ulega kashaandaa kikosi cha kina da china na siwa 😂. Narudia, oa ukiwa una kipato hata kama ni 100! Na zingatieni hata nyumba mara ya mwisho kaka yenu alikuwa anakaa kodi alilipa mwanamke alitoa wapii sijuiii 🏃 🏃
Johari Mshana44,943 Aufrufe • vor 4 Monaten

Tulishawahi kuwa na kipengele cha kusema kuwa tunahitaji wanaharakati wapya hawa tuliokuwa nao, washatupiga sana na matukio. Haya wiki iliyopita tulianza kushuhudia wanaharakati wakitunishiana misuli akiongozwa na Mange na Rachel tukajua vita imeisha lol kumbe inaanza. Betina ni Mange usije ukajiuliza 😂 Haya Rachel anatoa warning kwa wanaharakati wenzake kutokuperekeshwa na Mange kwa kila anachokisema 😂! Ila kawasahau tu CHADEMA hapo hasa MNYIKA na yeye huwa anaingiaga sana kichwa kichwa. Haya hao ndio watu mliowaamini kwasasa kazi yao kusuuzana na kabla ya December watavuana nguo tupo hapa.
Johari Mshana12,070 Aufrufe • vor 28 Tagen

Ijumaa kuu leo, jana nimemsikia Mhe. Gwajima waziri Dr. Dorothy Gwajima akisema ameunda kamati ya kuangalia maswala ya kina Anko T, Mama Naomba nikuongezee kitu! Hawa wawili ni wapenzi na sauti unayosikia ni ya Mmiliki wa tamthilia ya kombolela, akimlilia mwanaume mwenzake ambaye ni msanii mwenzake anaitwa Chollo! Unaona jinsi kizazi kinapenyezewa tabia ovu za kishetani ambazo nchi yetu hatutaki!! Sikiliza sauti!! Kwa mwenendo huu, inatakiwa na wizara yako iwe inatupa report kila mwaka aibu hizi! Bila aibu wameshona mpaka sare, ni kama wanaishi wotee hawa!!
Johari Mshana35,647 Aufrufe • vor 4 Monaten

STEVE NYERERE MUAGUE IDRIS SULTAN INATOSHA, MGANGA WAKO HATARI Wazee wamenipa mapya eeh Johari, unajua Idris ule ugonjwa ni karogwa na Steve Nyerere, walipishana soon tu baada ya kutoka Korea. Sasa mpe ujumbe amuague mwenzie inatoshaaa! 😂 Jaman mfikishieni ujumbe Steve Nyerere!!
Johari Mshana32,411 Aufrufe • vor 3 Monaten

Naomba nitume salaam zangu za dhati kwa wanaharakati, kwasababu Chadema waliielewa sana hii speech na wanatambua kuwa wako chini ya sheria za serikali ila wanaharakati bado. Hata ukienda kwenye muswada wa Marekani hauwezi kukuta masharti yasitekelezeka na same tu EU, ambao wanaelewa kwamba hii ni nchi huru inayofuata katiba. Sasa Njoo kwa Nchi ya Mange na Maria - wanawapa vijana vitu vya kuwaambia serikali ifanye ambavyo haviwezekani ni tahira tu ndio anaweza fanya hivyo. Post inayokuja nitakuwekea Masharti ya Maria na Mange kisha ya USA na EU, uone Lengo la kila mmoja kwa Tanzania 🇹🇿. Na inavyochekesha kutoka kwa wanaharakati na Chadema nimesahau!! Haya kula Chuma hichooooo….
Johari Mshana13,281 Aufrufe • vor 1 Monat

Wanaharakati kwenye makazi yao Nairobi huko, sasa hapo anasubiri content kutoka kwa Maria ili aje mitandaoni aseme bado anaomboleza 29 October hana raha na anaumia dah! Wakati yuko kwenye starehe zake anabadilisha wanawake kila siku anapiga mpaka threesome!! Drama sana. Huyu ndio anakuambia tukaandamane kwa hela za Maria na amnesty!! Hivi tumefikia wapi kuhusu kupata wanaharakati wengine?
Johari Mshana16,944 Aufrufe • vor 2 Monaten

Nimekubali kuwa mnaenda kushangilia, sasa ndio muende wote watu wazima jaman? Yaan nikiangalia hiyo ndege Naona watu wazima wazima tu, na wale ni U 17 si mngeweka hata kundi flani la age zinazoendana mbona kuna wachambuzi wapya wapya- kuna content creators wa michezo vijana wapo tele tu, na nyie muwe mnabadilika badilisheni watu, wapeni watu fursa! Sasa hapo U 17 mtaenda, ya U 23 mtaenda nyie nyie na ya wakubwa mtaenda nyie nyie- nendeni na wakati bwana, tunataka sura mpya kwenye vitu tumezichoka hizoooo!! Vipi mmekunywa chai? Maana naona leo siku nzito nimeanza na watu wazima, 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 anasema mdomo wangu huwa unaniponza 😂
Johari Mshana13,891 Aufrufe • vor 2 Monaten

Tupate Tangazo kwa wadhamini kwanza, haya wale wa ulaya hawatutaki sikieni na oneni hii leo. Brussels Airlines imeanza safari zake za moja kwa moja kati ya Brussels (Ubelgiji) na Kilimanjaro kuanzia tarehe 3 Juni 2026. Ndege hizi zitakuwa zikifanya safari mara mbili kwa wiki mwanzoni. kutoka Ulaya kuingia moja kwa moja Kaskazini mwa Tanzania. Itafungua mtandao mpana wa Ulaya. Alafu kuna wa Ulaya ya Maria na misaada alafu kuna hii ya biashara na uwekezaji Tanzania- ndio kwanza kumekuchaa!!
Johari Mshana13,484 Aufrufe • vor 2 Monaten
Keine weiteren Inhalte verfügbar