
MeaMswahili
@meamswahili • 22,718 subscribers
GOD First 🙏... East Africa Kid, From Tanzania 🇹🇿 Entertainment || Sports || Trending news & Life style. #WeAreStillInTheRace.
Shorts
Videos

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, Amejibu Kuhusu Chapisho la John Heche, ambapo Aliposti picha na taarifa kwenye Instagram yake akionyesha wakazi wa Kijiji cha Iponda, Kata ya Ilembula, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe, wakifukua mchanga kwenye mto uliokauka kutafuta maji ya kuoga na kupikia. #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili58,366 Aufrufe • vor 10 Tagen
2:51
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Latita ameripotiwa kufariki dunia katıka mazingira ya kutatanisha ndani ya Lodge ya Dolphın, eneo la Kaloleni jijini Arusha, usiku wa kuamkia Oktoba 18, 2026. Kwa mujibu wa mashuhuda, marehemu alikuwa amepanga chumba namba nne kwa Shilingi 30,000 tangu mchana, kabla ya kuingia ndani ya chumba hicho akiwa na mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa mteja wake. Baadaye, marafiki zake walipoona hajatoka kwa muda mrefu, waliamua kwenda kuangalia hali yake. Inadaiwa kuwa walimkuta akiwa amefungwa mikono, mdomo umezibwa na mtandio ukiwa shingoni mwake. Mara baada ya kumkuta katika hali hiyo, marafiki zake walimpeleka katika Hospitali ya Mount Meru, lakini walibaini kuwa tayari amefariki dunia. Taarifa za mashuhuda pia zinadai kuwa mwanaume aliyekuwa naye chumbani aliondoka na fedha pamoja na Simu ya marehemu, ingawa utambulisho wake bado haujafahamika. Hadi sasa, chanzo rasmi cha kifo hicho hakijathibitishwa. Uchunguzi wa mamlaka husika unahitajika kubaini mazingira ya tukio hilo na ukweli wa madai yanayohusishwa nalo. 🎥: AyoTV👊 #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili26,712 Aufrufe • vor 15 Tagen

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 Video fupi iliyorekodiwa katika Kanisa Kuu la Metz, Ufaransa, imezua mjadala mkubwa mitandaoni. Papa Leo XIV anaonekana akisalimiana na maaskofu na mapadre weupe, kisha kupita karibu na padri/askofu mweusi bila kusalimiana waziwazi, kabla ya kuendelea kumsalimia Rais Emmanuel Macron na wageni wengine. Baadhi ya Watu wanasema Papa “alimpuuza” kiongozi mweusi kutoka Afrika na Akaendelea Kusalimia Wengine. #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili51,906 Aufrufe • vor 1 Monat

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 Rais wa Mongolia 🇲🇳 Ukhnaagiin Khurelsukh (miaka 58), ametamba sana mitandaoni baada ya kuonekana akiinua uzito wa pauni 220 (takriban kilo 100) mara 20 kwenye bench press. Tukio hilo lilitokea alipotembelea kituo cha jeshi. Alivua koti la suti, akafanya marudio hayo mbele ya wanajeshi, kisha akasalimiana nao. #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili45,448 Aufrufe • vor 1 Monat

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 Jana, Oktoba 17, 2026, huko Guayaquil, Ecuador (Kanisa la Our Lady of Perpetual Help), Padre Patricio Sánchez alifariki dunia ghafla baada ya msalaba mkubwa wa mbao uliokuwa ukutani altareni kuanguka na kumpiga kichwani alipokuwa anaadhimisha Misa iliyokuwa ikirushwa mubashara. Tukio hilo limeleta simanzi kubwa kwa waumini wa parokia hiyo na Kanisa Katoliki kwa ujumla. Padre alifariki akiwa katikati ya huduma yake ya kitume. Jimbo Kuu la Guayaquil pamoja na Kardinali Luis Gerardo Cabrera Herrera walitoa taarifa rasmi wakituma rambirambi kwa familia, ndugu na marafiki wa Padre Patricio Sánchez Molinari. #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili11,311 Aufrufe • vor 14 Tagen

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 Producer Master J ambaye pia ni Jaji wa BSS amechukizwa kwa maamuzi ya Majaji wenzake kumtupa nafasi ya nne Freya mshiriki kutoka Congo. Baadhi ya taarifa zilisambaa kuwą Masterj Jana hakuwepo kwenye fainali ya BSS kwasababu zilizotajwa kuwa na mgogoro na Wenzake lakini ukimsikiliza Vizuri MasterJ utagundua alikuwa nje ya nchi. #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili32,215 Aufrufe • vor 3 Monaten

🚨𝐓𝐑𝐄𝐍𝐃𝐈𝐍𝐆 Maneno ya Mkurugenzi wa CloudsFM Kusaga Kuhusiana na Ubaya wa Vita..!! #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili49,241 Aufrufe • vor 7 Monaten

⛔️𝐓𝐑𝐄𝐍𝐃𝐈𝐍𝐆...! Huyu Afande Ataweza Kulinda Raia na Mali Zake Zote Kweli…?!😅😅 #VisitMOSHI🇹🇿
MeaMswahili99,048 Aufrufe • vor 1 Jahr

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 Basi la shule lililokuwa likibeba wanafunzi wa King David Junior School Ndejje (Wilaya ya Wakiso) Limepata ajali mbaya mjini Kapchorwa, na kusababisha vifo vya Wanafunzi zaidi ya 20 Usiku wa Kuamkia Leo. Basi hilo, lenye namba ya usajili UA 108BQ, lilikuwa likirudi Kampala kutoka katika ziara ya kielimu ya Sipi Falls. Ripoti zinaeleza kwamba basi lilitatizwa na matatizo ya kiufundi wakati wa safari. Wanafunzi na wafanyakazi wengine waliojeruhiwa walipelekwa katika Hospitali ya Kapchorwa kwa matibabu. #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili22,437 Aufrufe • vor 3 Monaten

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 Mwenyekiti Wa Taasisi Ya Mama Ongea Na Mwanao Steve Nyerere Awavaa Wanasiasa Wanaosema Wasanii Wanatumika Kisiasa Kupitia Tamasha La Miaka 30 Ya Bongo Flava. Steve Amesema Jukwaa Hilo Lina Mchango Mkubwa Kwa Vijana Wapo Wasanii Walipotea Na Kuingia Kwenye Matumizi Ya Dawa Za Kulevya lakini Tamasha Hilo limekuja kuwaokoa Na kuwaheshimisha. #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili15,472 Aufrufe • vor 2 Monaten

🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 “Huwezi Ukaiangusha Iran 🇮🇷 Mimi Nakuhakikishia Leo” - Prophet IPM. #MeaMswahiliUPDATES
MeaMswahili35,109 Aufrufe • vor 8 Monaten