
Mwananchi Newspapers
@MwananchiNews • 1,088,993 subscribers
Shorts
Videos

Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi ametoa wito maalum kwa baadhi ya wasanii maarufu nchini kufika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kesho Jumatano, Septemba 2, 2026. Miongoni mwa wasanii hao ni Q Chief, Dudu Baya, Chid Mbezi, Mwijaku na Martha wa Jese.
Mwananchi Newspapers73,490 просмотров • 2 месяцев назад

Nyota wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Rio Ferdinand amesema hajafika Tanzania kufanya siasa bali kusaidia kuhamasisha vijana kupitia mchezo wa soka. Ferdinand ametoa kauli hiyo leo Mei 22,2026 baada ya kuwepo kwa mijadala mbalimbali kuhusu ziara yake nchini, akisema hawezi kuzuiwa kuitembelea Afrika wala kuambiwa nini afanye. “Mimi si mwanasiasa na sijaja kuzungumzia siasa. Nimekuja kuhamasisha vijana kupitia soka,” alisema Ferdinand
Mwananchi Newspapers99,775 просмотров • 5 месяцев назад

Wadhifa wa Makamu wa Rais kwa Dk Emmanuel Nchimbi, ulikoma rasmi Agosti 26, 2026 baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutangaza kumfukuza uanachama, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Hamza Johari amelieleza Bunge. #mwananchiupdates #tunawezeshataifa
Mwananchi Newspapers37,828 просмотров • 2 месяцев назад

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu imeshindwa kusikilizwa leo Ijumaa, Agosti 14, 2026, baada ya shahidi wa 18 wa upande wa mashtaka kudaiwa amepata dharura ya kiafya na kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi wake. Upande wa Jamhuri umeiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi siku nyingine, ukidai kuwa shahidi huyo amepata changamoto ya kiafya na kwenda hospitalini. Hata hivyo, Lissu amepinga ombi hilo akisema tayari Mahakama ilitoa amri kwa upande wa mashtaka kuleta mashahidi wasiopungua wawili kila siku kesi inapokuwa inasikilizwa. Hivyo, aliiomba Mahakama isikubali ombi la Jamhuri. Lissu almesisitiza kuwa yupo tayari kuendelea na kesi hiyo siku ya leo na kutaka upande wa mashtaka ulete mashahidi wen gine mahakamani. Amesema iwapo Jamhuri imeshindwa kuendelea na ushahidi, basi ifunge ushahidi na kesi iende kwenye hatua nyingine, akidai upande huo "umekata pumzi." Hata hivyo, Jopo la majaji watatu linalosikiliza kesi hiyo, likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiana na James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, limekubali ombi la upande wa Jamhuri na kuahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026. #mwananchiupdates #tunawezeshataifa
Mwananchi Newspapers44,116 просмотров • 2 месяцев назад

Happyness Alphonce hakuwahi kufikiria kwamba siku moja kazi yake ya kuendesha mabasi yaendayo haraka, maarufu kama ‘mwendokasi’, ya kampuni ya Mofat yanayohudumia njia ya Mbagala jijini Dar es Salaam, ingemweka katika nafasi ya kumwendesha abiria wa aina ya pekee, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Lakini Agosti 7, 2026, imegeuka kuwa siku ya kipekee katika maisha yake, baada ya kupewa nafasi ya kumwendesha Rais, tukio lililomwachia kumbukumbu ambayo, kwa hakika, hataisahau. Akizungumza na Mwananchi wiki hii katika mahojiano maalumu, Happyness anasema alikuwa miongoni mwa madereva watano waliochaguliwa kuendesha mabasi yaliyombeba Rais Samia kutoka kituo cha Water Front, katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hadi Mtoni kwa Aziz Ally, Wilaya ya Temeke, alikokwenda kuzindua mradi wa mabasi yaendayo haraka wa awamu ya pili (BRT II). Soma zaidi kwenye tovuti ya Mwananchi... #mwananchiupdates #tunawezeshataifa
Mwananchi Newspapers43,127 просмотров • 2 месяцев назад

Ukiacha nguvu, fursa, heshima na wingi wa marafiki unaokuwa nao ukiwa na cheo, waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla, amesema mambo huwa kinyume chake mamlaka yanapokutoka, akisimulia hata uliowaona wa karibu wamepotea. Katika simulizi yake aliyoihusianisha na maisha yake ya sasa akiwa si waziri wala mbunge, amesema hata huduma ambazo awali alizipata kwa rahisi na haraka, kwa sasa zinahusisha milolongo na nyingine wahusika hawapokei simu wala kujibu baruapepe. #mwananchiupdates #tunawezeshataifa
Mwananchi Newspapers77,439 просмотров • 6 месяцев назад

Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismael Jusa, amesema si lazima mazungumzo ya kisiasa ya yasimamiwe na msuluhishi wa nje ili yawe na tija, akieleza kuwa uzoefu wa Zanzibar mwaka 2001 unaonyesha kuwa pande zinazohusika zinaweza kufikia mwafaka zenyewe.
Mwananchi Newspapers26,451 просмотров • 1 месяц назад

Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati, January Makamba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwapo kwa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115, ni hatua muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Mwananchi Newspapers32,157 просмотров • 2 месяцев назад

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema Tanzania inathamini mchango wa washirika wa maendeleo katika kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali, lakini ameeleza kuwa ushirikiano huo unapaswa kujengwa katika misingi ya heshima, nidhamu na kuthamini uhuru wa Taifa. Nape amezungumza hayo Jumanne Mei 26, 2026 bungeni Dodoma wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Aidha, amesema Tanzania imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na marafiki zake wa kimataifa, hivyo changamoto za muda mfupi haziwezi kuwa msingi wa kupima mahusiano hayo.
Mwananchi Newspapers60,104 просмотров • 5 месяцев назад

Hakuna ajuaye kesho yake. Huu ndio msemo unaoweza kuutumia katika safari ya Elizabeth Peter, mama aliyelazwa katika Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) kwa siku 339 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya tumaini kupatikana. Mama huyo wa watoto wawili alijikuta akiingia katika chumba hicho baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Juni 20, 2025, akitokea nchini India alikokwenda kupatiwa matibabu. Akizungumza na Mwananchi kuhusu safari ya ugonjwa wa Elizabeth, Anna Bariki, mtoto wa mwisho wa mama huyo, anasema mama yake alianza kuugua kwa muda mrefu akiwa mkoani Mbeya. "Alianza kuugua miaka kadhaa iliyopita akisumbuliwa na presha. Lakini kwa muda mrefu hatukufanikiwa kufahamu chanzo halisi cha changamoto yake. Kwa kuwa alikuwa anaishi mkoani, tulimleta Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi," anasimulia Anna. Soma zaidi kwenye tovuti ya Mwananchi… #mwananchiupdates #tunawezeshataifa
Mwananchi Newspapers37,276 просмотров • 3 месяцев назад

Familia ya kijana Elvis Pemba ambaye kifo chake kina utata, imedai kuna ofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe amehusika kutokana na wivu wa mapenzi. Mwili wa Elvis (19) umezikwa leo Februari 14, 2025 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Soma kwa undani katika Tovuti ya Mwananchi. #mwananchiupdates #tunaliwezeshataifa
Mwananchi Newspapers167,195 просмотров • 1 год назад

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Benson Kigaila, Salum Mwalimu na makada wengine wakiwasili katika ukumbi Golden Tulip, panakofanyika mkutano mkuu wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) leo Mei 19, 2025. #mwananchiupdates #tunaliwezeshataifa
Mwananchi Newspapers135,110 просмотров • 1 год назад

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania badala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji, ni vema wakajiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi. Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumatatu Septemba 16, 2024 katika Baraza la Maulid lililofanyika kitaifa mkoani Geita. Majaliwa amesema tangu awamu ya tatu, nne, tano na sasa awamu ya sita, matukio ya aina hiyo yamekuwa yakitokea hususan kipindi cha kukaribia uchaguzi na kwamba jamii inapaswa kujitafakari na kujiuliza kwanini matukio hayo hutokea kwenye kipindi kama hicho. “Rais alitoa karipio juu ya yanayotokea, matukio haya yanatokea kila kipindi fulani, lazima tujiulize kwanini yanajitokeza hasa inapokaribia uchaguzi. Nani anafanya, ni rahisi kusema polisi, ni muhimu tukatafakari kwanini wakati huu na nani anafanya” amesema Majaliwa. Majaliwa amesema Jeshi la Polisi pekee haliwezi kulilinda Taifa, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda usalama wa nchi na kusema Serikali itaendelea kuhamasisha wanachi kulilinda Taifa na kuifanya nchi kuwa imara kwa kutambua viashiria vya matukio yanayovunja amani na utulivu. Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi (Imeandikwa na Rehema Matowo) #mwananchiupdates #tunaliwezeshataifa
Mwananchi Newspapers182,430 просмотров • 2 лет назад

Mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, Victoria Mkwizu amejifungua pacha watano ambapo wa kiume ni watatu na wawili wa kike. Victoria amejifungua watoto hao Jumamosi ya Juni 13, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam. Taarifa ya MNH imesema jopo la madaktari bingwa wamefanikisha kujifungua salama kwa Victoria. "Watoto hao, watatu wa kiume na wawili wa kike, wamezaliwa wakiwa katika hali nzuri na wanaendelea kupatiwa uangalizi wa karibu, huku Muhimbili ikiendelea kusimamia huduma bora kwa mama na watoto hao," imeeleza taarifa ya MNH. #mwananchiupdates #tunawezeshataifa
Mwananchi Newspapers45,095 просмотров • 4 месяцев назад

Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu akikumbatiana na kada wa chama hicho na Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa mara baada ya kesi iliyofunguliwa na mawakili wawili kuahirishwa kwa muda, leo Julai 22,2026. Lissu amekutana na Msigwa katika Mahakama Kuu Dar es Sa-laam kwa mara ya kwanza, tangu mchungaji huyo arejee Chadema akitoka Chama cha Mapinduzi (CCM). Mchungaji Msigwa aliyewahi kwua Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa alihamia Chama cha Mapinduzi (CCM), Juni 2024 na takribani mwaka mmoja kupita, mwanasiasa huyo amerejea tena Chadema Mei 23, 2026.
Mwananchi Newspapers32,946 просмотров • 3 месяцев назад

Kada wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, ni miongoni mwa watu waliojitokeza kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambayo leo imeanza tena baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi mitano. Mbali na Mpina, wapo pia viongozi wa juu wa Chadema, akiwemo Makamu Mwenyekiti, John Heche, Katibu Mkuu, John Mnyika pamoja na wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Chadema. Kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, inatarajiwa kuendelea mfululizo kuanzia leo baada ya kusimama tangu Februari 24, 2026.
Mwananchi Newspapers24,752 просмотров • 2 месяцев назад