
MwanzoTvPlus
@MwanzoTvPlus • 124,244 subscribers
Independent Online Media serving East Africa with premier news - Uncensored and Undaunted
Videos

#TANZANIA: WANANCHI WAMEFICHUA WAHARIFU NA TUMEWEZA KUWANYAKUWA - KATAMBI Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi hii leo Julai 07, 2026 akizungumza na Wanahabari maeneo ya Ubungo maji jijini Dar Es Salaam alipokuwa akiangalia hali ilivyo baada ya uwepo wa tishio la maandamano nchini hapo amesema hali ni shwari kote nchini na kwamba Wananchi walitoa taarifa ya waharifu na wakafanikiwa kuwanyakuwa mapema sana, "wananchi wamefichua waharifu na tumeweza kuwanyakuwa ili waweze kufika kwenye vyombo vya sheria" Zaidi:
MwanzoTvPlus56,906 просмотров • 15 дней назад

#TANZANIA: CHADEMA KUANZISHA KAMPENI NZITO KUSHINIKIZA LISSU KUACHIWA HURU, "TUTAANDAA MAANDAMANO MAKUBWA, HATUTAPIGA MAGOTI" Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara, John Heche leo Aprili 09, 2026 wakati wa mjadala maalum ulioendeshwa kwa njia ya mtandao ambapo Tundu Antiphas Lissu anatimiza mwaka mmoja (siku 365) akiwa gerezani ametoa wito kwa Watanzania walio ndani na nje ya nchi hususani Vijana kuanzisha kampeni maalum ya kuzishinikiza Mamlaka kumuachia huru Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu akisema Lissu hajatenda kosa bali amebambikiwa kesi. “Jambo langu kwako wewe Kijana unayetuona, unayedai kwamba unatuunga mkono sio kusemea chinichini, tunapaswa kuanzisha kampeni kubwa wamuachie Tundu Lissu kwasababu Lissu amekamatwa kwa ajili yetu, kwasababu wote tunajua na wote tunaamini Lissu hana kosa, ni Mtu mwema anayetupigania, ili asikate tamaa ili asiwe na baridi kule aliko anafikiri kwamba nimekamatwa na Watu niliokuwa nawapigania wamerudi nyuma, tunapaswa kuanzisha kuanzia leo kampeni kubwa kwenye kila platform Instagram, Facebook, TikTok, Twitter ya kumdai Tundu Lissu” - Heche “Watu wetu wa Diaspora mfanye kama waliofanya Watu wa Diaspora waliokuwepo wa Afrika Kusini wakati ule , Vijana wetu mlioko ndani ya nchi tuandike vipeperushi visambae kwenye masoko, kwenye nguzo za umeme zikiwa na picha ya Lissu na ujumbe wa kutaka Lissu aachiwe” - John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara. Zaidi:
MwanzoTvPlus39,542 просмотров • 3 месяцев назад

#BREAKING: PIGO KUBWA KWA TANZANIA BAADA YA BUNGE LA ULAYA KUPITISHA HOJA YA KUVUNJA MSAADA WA MAENDELEO Kamati za Mambo ya Nje na Maendeleo za Umoja wa Ulaya zimepitisha hoja itakayolazimisha Bunge la Ulaya kupitia Kamati ya Maendeleo kuondoa Mpango wa Kila Mwaka wa Maendeleo kwa Tanzania, hatua inayotafsiriwa kama hasara kubwa kwa taifa. Tazama ZAIDI:
MwanzoTvPlus20,035 просмотров • 1 месяц назад

#TANZANIA: TAHARUKI CHUONI: MWENYEKITI WA CHASO AKABWA NA KESI YA MKOPO KINYUME CHA SHERIA Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mwanafunzi wa sheria mwaka wa nne katika chuo kikuu cha cha Mt. Agustino Sauti ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chadema vyuoni (CHASO) mkazi wa Mtaa wa Nyamalango kata ya Luchelele wilayani Nyamagana kwa tuhuma za kukopesha fedha kinyume cha sheria. ZAIDI:
MwanzoTvPlus16,144 просмотров • 1 месяц назад

#TANZANIA: JAJI MSTAAFU AMVAA KAMANDA MULIRO KWA KUZUIA MAANDAMANO YA CHADEMA NA KUTISHA WATU KILA KONA Jaji mstaafu Makaramba amvaa Kamanda Muliro kwa kuzuia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kile alichodai kuwa kuna viashiria vya uvunjifu wa amani, ampa darasa la kisheria, Jaji adai Jeshi la Polisi lilitanda kila kona na magari ya washa washa ili ila anayetaka kuandamana aogope. Zaidi:
MwanzoTvPlus83,945 просмотров • 1 год назад

#TANZANIA: YALIYOTOKEA NCHINI KWETU, YAMETUTIA DOA, HUENDA YAKATUPUNGUZIA SIFA YA KUPATA MIKOPO - RAIS SAMIA "Mara nyingi tunategemea kupata kutoka nje, mikopo kutoka kwenye taasisi mbali mbali za kimataifa, Mabenki ya Kimataifa, lakini yaliyotokea nchini kwetu (wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025) yametutia doa kidogo kwa hiyo huenda yakatupunguzia sifa ya kupata hiyo mikopo kwa urahisi kama tulivyopata muhula wa kwanza wa awamu hii..., lakini doa tulilojitia huenda likaturudisha nyuma, kwa maana hiyo tuna kazi ya kutafuta fedha humu ndani" - Rais Samia Rais Samia Suluhu ameyazungumza hayo leo Novemba 18, 2025 mara baada ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri Ikulu Chamwino jijini Dodoma Zaidi:
MwanzoTvPlus39,280 просмотров • 8 месяцев назад

#TANZANIA: MWABUKUSI ATEMA CHECHE KALI! 'HUU ULIKUWA UCHAGUZI WA GIZA' Chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS kimesema kinaendelea kuandaa mazingira ya kufungua mashauri mbalimbali nchini kutokana na matukio ya vifo vilivyotokea siku ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania. ZAIDI:
MwanzoTvPlus33,674 просмотров • 8 месяцев назад

#TANZANIA: TUNAAMBIWA VIJANA WALIOINGIA BARABARANI WALILIPWA, NGOs ZICHUNGUZWE - RAIS SAMIA Rais wa Tanzania, Samia Suluhu hii leo Novemba 20, 2025 Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma amesema uundwaji wa Tume Huru ya Kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2025 umezingatia matakwa ya Sheria ambayo inampa mamlaka ya kuunda tume maalum kuchunguza masuala nyeti ya kitaifa. Rais Samia ameitaka tume hiyo kuchunguza kwa kina mchango wa vyama vya siasa, asasi za kiraia (NGOs) za ndani na nje pamoja na tuhuma za vijana kulipwa fedha kabla ya kuingia kwenye maandamano. Aidha, Rais Samia amesisitiza kuwa hata kama kulikuwa na changamoto za kisiasa kati ya vyama, Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama au Serikali, haipaswi kufikia hatua ya vurugu, uharibifu na vifo. Zaidi:
MwanzoTvPlus30,577 просмотров • 8 месяцев назад

#TANZANIA:MTU ALIYEMLETA ABDUL NYUMBANI KWANGU KUJA KUNIHONGA, ANAGOMBEA UMAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA NA ANAMUUNGA MKONO MBOWE - LISSU "Mtu aliyemleta Abdul (Mtoto wa Rais Samia Suluhu) nyumbani kwangu kuja kunihonga, anagombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa chama (CHADEMA) na amesema anamuunga Mwenyekiti (Mbowe) mkono" - Tundu Antiphas Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na mgombea Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Zaidi:
MwanzoTvPlus56,911 просмотров • 1 год назад

“RAIA WANATEKWA, SERIKALI INATAZAMA!” – MCHUNGAJI KIGAVA AVUNJA UKIMYA Sikiliza:
MwanzoTvPlus26,879 просмотров • 7 месяцев назад

#TANZANIA: MZEE SARUNGI NDIYE ALIYEKUWA MTU WA KWANZA KUTEOA WAZO LA KUJENGWA TAASISI YA MOI - DKT MPOKI Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI, Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema Prof. Philemon Sarungi maisha yake yalikuwa mtu wa sekta ya afya hata Taasisi ya MOI yeye ndiye aliyeandika wazo la kujengwa Taasisi hiyo ndipo wengine wakafuata. Zaidi:
MwanzoTvPlus47,288 просмотров • 1 год назад

#TANZANIA: KIKEKE AHOJI NANI ALIYETOA ODA YA WATU KUUAWA WAKATI WA MAANDAMANO OKTOBA 29, 2025 Mwandishi Mkongwe nchini Tanzania, Salim Kikeke hii leo Novemba 25, 2025 wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo amehoji kuwa nani alitoa oda ya kuua baada ya kutokea kwa maandamano wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwak huu wa 2025?
MwanzoTvPlus24,942 просмотров • 7 месяцев назад

#TANZANIA: FATHER KITIMA AMUONGOZA RAIS SAMIA KUAGA MWILI WA KARDINALI PENGO Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Padre Charles Kitima hii leo Februari 27, 2026 katika Misa ya kumuaga aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar Es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amemuongoza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kuaga mwili wa Askofu huyo. Zaidi:
MwanzoTvPlus14,406 просмотров • 4 месяцев назад

#TANZANIA: NIMEKUWA MUHANGA WA SERIKALI NILIYOISAIDIA KUSHINDA - KADA WA CCM Mtoto wa Deo Filikunjombe mwana Chama Cha Mapinduzi kindaki ndaki aelezea matatizo ya Serikali ya chama chake na mapungufu ya Jeshi la Polisi mbele ya Freeman Mbowe "Nimekuwa muhanga wa Serikali niliyoisaidia ishinde, hii sio Serikali ambayo sisi tuliipigania" - Mtoto wa Deo Filikunjombe Kada wa Chama Cha Mapinduzi mbele ya mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo Agosti 22, 2024 Mikocheni Dar Es Salaam.
MwanzoTvPlus42,674 просмотров • 1 год назад