
MwanzoTvPlus
@MwanzoTvPlus • 124,828 subscribers
Independent Online Media serving East Africa with premier news - Uncensored and Undaunted
Videos

#TANZANIA: BILA KATIBA MPYA HATUTASHIRIKI UCHAGUZI - CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesema hakitoshiriki kwenye uchaguzi wowote hadi pale serikali itakapokubali mchako wa Katiba mpya itakayosaidia kuwa a uchaguzi huru na haki. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Serengeti, Naibu Katibu Mkuu bara, Aman Golugwa amesema serikali bado ina muda mrefu wa kujiandaa na kufanikisha suala hilo la Katiba mpya huku Makamu Mwenyekiti bara, John Heche akiitaka serikali kuja na mikakati ya kujenga viwanda vitakavyosaidia ajira kwa vijana.
MwanzoTvPlus49,498 görüntüleme • 18 gün önce

#TANZANIA: WANANCHI WAMEFICHUA WAHARIFU NA TUMEWEZA KUWANYAKUWA - KATAMBI Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi hii leo Julai 07, 2026 akizungumza na Wanahabari maeneo ya Ubungo maji jijini Dar Es Salaam alipokuwa akiangalia hali ilivyo baada ya uwepo wa tishio la maandamano nchini hapo amesema hali ni shwari kote nchini na kwamba Wananchi walitoa taarifa ya waharifu na wakafanikiwa kuwanyakuwa mapema sana, "wananchi wamefichua waharifu na tumeweza kuwanyakuwa ili waweze kufika kwenye vyombo vya sheria" Zaidi:
MwanzoTvPlus57,240 görüntüleme • 3 ay önce

#TANZANIA: CHADEMA KUANZISHA KAMPENI NZITO KUSHINIKIZA LISSU KUACHIWA HURU, "TUTAANDAA MAANDAMANO MAKUBWA, HATUTAPIGA MAGOTI" Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara, John Heche leo Aprili 09, 2026 wakati wa mjadala maalum ulioendeshwa kwa njia ya mtandao ambapo Tundu Antiphas Lissu anatimiza mwaka mmoja (siku 365) akiwa gerezani ametoa wito kwa Watanzania walio ndani na nje ya nchi hususani Vijana kuanzisha kampeni maalum ya kuzishinikiza Mamlaka kumuachia huru Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu akisema Lissu hajatenda kosa bali amebambikiwa kesi. “Jambo langu kwako wewe Kijana unayetuona, unayedai kwamba unatuunga mkono sio kusemea chinichini, tunapaswa kuanzisha kampeni kubwa wamuachie Tundu Lissu kwasababu Lissu amekamatwa kwa ajili yetu, kwasababu wote tunajua na wote tunaamini Lissu hana kosa, ni Mtu mwema anayetupigania, ili asikate tamaa ili asiwe na baridi kule aliko anafikiri kwamba nimekamatwa na Watu niliokuwa nawapigania wamerudi nyuma, tunapaswa kuanzisha kuanzia leo kampeni kubwa kwenye kila platform Instagram, Facebook, TikTok, Twitter ya kumdai Tundu Lissu” - Heche “Watu wetu wa Diaspora mfanye kama waliofanya Watu wa Diaspora waliokuwepo wa Afrika Kusini wakati ule , Vijana wetu mlioko ndani ya nchi tuandike vipeperushi visambae kwenye masoko, kwenye nguzo za umeme zikiwa na picha ya Lissu na ujumbe wa kutaka Lissu aachiwe” - John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara. Zaidi:
MwanzoTvPlus39,837 görüntüleme • 6 ay önce

#BREAKING: NCHIMBI AFUKUZWA UANACHAMA WA CCM KUANZIA LEO AGOSTI 26, 2026 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Balozi Dkt. Asha Rose Migiro ametangaza uamuzi wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kuwa wamemfukuza uanachama Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi uanachama wa chama hicho kutokana na utovu wa nidhamu. Zaidi:
MwanzoTvPlus11,174 görüntüleme • 1 ay önce

#BREAKING: PIGO KUBWA KWA TANZANIA BAADA YA BUNGE LA ULAYA KUPITISHA HOJA YA KUVUNJA MSAADA WA MAENDELEO Kamati za Mambo ya Nje na Maendeleo za Umoja wa Ulaya zimepitisha hoja itakayolazimisha Bunge la Ulaya kupitia Kamati ya Maendeleo kuondoa Mpango wa Kila Mwaka wa Maendeleo kwa Tanzania, hatua inayotafsiriwa kama hasara kubwa kwa taifa. Tazama ZAIDI:
MwanzoTvPlus20,072 görüntüleme • 4 ay önce

#BREAKING: RAIS SAMIA ATANGAZA KUANZA KWA MARIDHIANO NA KATIBA MPYA Rais Samia Suluhu leo Julai 30, 2026 atangaza rasmi kuanza kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya na kuanza kwa maridhiano nchini humo. Rais Samia ameyasema hayo leo alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu jijini Dar Es Salaam. Zaidi:
MwanzoTvPlus12,371 görüntüleme • 2 ay önce

#TANZANIA:MTU ALIYEMLETA ABDUL NYUMBANI KWANGU KUJA KUNIHONGA, ANAGOMBEA UMAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA NA ANAMUUNGA MKONO MBOWE - LISSU "Mtu aliyemleta Abdul (Mtoto wa Rais Samia Suluhu) nyumbani kwangu kuja kunihonga, anagombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa chama (CHADEMA) na amesema anamuunga Mwenyekiti (Mbowe) mkono" - Tundu Antiphas Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na mgombea Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Zaidi:
MwanzoTvPlus56,925 görüntüleme • 1 yıl önce

#TANZANIA: TAHARUKI CHUONI: MWENYEKITI WA CHASO AKABWA NA KESI YA MKOPO KINYUME CHA SHERIA Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mwanafunzi wa sheria mwaka wa nne katika chuo kikuu cha cha Mt. Agustino Sauti ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chadema vyuoni (CHASO) mkazi wa Mtaa wa Nyamalango kata ya Luchelele wilayani Nyamagana kwa tuhuma za kukopesha fedha kinyume cha sheria. ZAIDI:
MwanzoTvPlus16,168 görüntüleme • 4 ay önce

#TANZANIA: MZEE SARUNGI NDIYE ALIYEKUWA MTU WA KWANZA KUTEOA WAZO LA KUJENGWA TAASISI YA MOI - DKT MPOKI Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI, Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema Prof. Philemon Sarungi maisha yake yalikuwa mtu wa sekta ya afya hata Taasisi ya MOI yeye ndiye aliyeandika wazo la kujengwa Taasisi hiyo ndipo wengine wakafuata. Zaidi:
MwanzoTvPlus47,288 görüntüleme • 1 yıl önce

#TANZANIA: TUNAAMBIWA VIJANA WALIOINGIA BARABARANI WALILIPWA, NGOs ZICHUNGUZWE - RAIS SAMIA Rais wa Tanzania, Samia Suluhu hii leo Novemba 20, 2025 Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma amesema uundwaji wa Tume Huru ya Kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2025 umezingatia matakwa ya Sheria ambayo inampa mamlaka ya kuunda tume maalum kuchunguza masuala nyeti ya kitaifa. Rais Samia ameitaka tume hiyo kuchunguza kwa kina mchango wa vyama vya siasa, asasi za kiraia (NGOs) za ndani na nje pamoja na tuhuma za vijana kulipwa fedha kabla ya kuingia kwenye maandamano. Aidha, Rais Samia amesisitiza kuwa hata kama kulikuwa na changamoto za kisiasa kati ya vyama, Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama au Serikali, haipaswi kufikia hatua ya vurugu, uharibifu na vifo. Zaidi:
MwanzoTvPlus30,589 görüntüleme • 11 ay önce

#TANZANIA: WATOTO NA VIJANA WANAKAMATWA NA KUWASINGIZIA, TUNALIPELEKA WAPI HILI TAIFA?, WAAMBIENI UKWELI - MWABUKUSI Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi amewasihi viongozi wa dini kusema ukweli hasa pale wanapokutana na viongozi wa serikali juu ya kamata kamata ya watoto na vijana na kuwasingizia kisa kuwakosoa watawala, "tunawaona, mko nao, waambieni ukweli, waache kuwakamata watoto na vijana kwa kuwasingizia, tunalipeleka wapi hili taifa, kwanini tunakosa hekima katika usimamizi na utekelezaji wa sheria?" Zaidi:
MwanzoTvPlus11,542 görüntüleme • 3 ay önce

#TANZANIA: ALIYEWAKEJELI VIJANA WA GEN Z ATAKIWA KUOMBA RADHI "Nakutaka utuombe radhi kwamba hatujui tunachokitaka, sisi Young generation (Gen Z) tunajuwa tunachokitaka, ndio maana hawa wanaofanya wanayoyafanya wanajuwa kwamba hawawezi kutupa tunachokitaka kama vijana wa Gen Z" - Rukaya Zaidi:
MwanzoTvPlus12,429 görüntüleme • 3 ay önce