
Privaldinho
@privaldinho • 982,346 subscribers
YANGA SC DIGITAL MANAGER…… Author || Lawyer || Sports Pundit ||
Shorts
Videos

Katika Quran, kuna sura inajulikana kama Surat Mariam. Nafikiri ndio sura pekee ambayo imepewa jina la mwanamke. Suratu Mariam ni sura ya 19 katika sura 114 za Quran, ikiwa ipo juzu la 16 katika majuzu 30 ya Qur’an. Sura hii imebebwa na aya 98 katika aya 6666 za Quran Tukufu (Mtaniwia radhi na kunisahihisha kama nitakuwa nimekosea hapo) Sura hii imegusia baadhi ya manabii wakubwa wakubwa kama vile Nabii Zakaria, Yaquub, Idriss, Yahya, Ibrahim, Is-haq, na Ismail Sura hii inamtaja mwanamke/Binti (Mariam mama yake Yesu Kristo maarufu kama Nabii Issah) ambaye alikuwa msafi sana, aliyeish maisha yake yote katika hali ya kiimani kuanzia utoto wake hadi katika ujana wake. Nafikiri ukirejea hata kwenye biblia, usafi wake umetajwa Injili ya Luka 1:42, “Akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na yeye utakayemzaa amebarikiwa”. Quran inasema Malaika walimwambia, ‘Ewe Maryam, hakika Mwenyezi MUNGU amekuchagua wewe na akakutakasa, na akakuteua kuliko wanawake wa ulimwengu wote. Sura hii inarudisha nyuma kidogo inatukumbusha kuhusu agano la kale Ukirejea agano la kale kupitia kitabu cha Nabi Isaya 7:14 “Tazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi” Maana yake mwanamke ametumika katika kuukomboa ulimwengu. Je Binti wa leo umejiandaa vipi katika ukombozi? Sio lazima ukomboe ulimwengu, je umejiandaa hata kujikomboa mwenyewe katika usafi wa kimwili na kiroho? Basi mwezi huu mtukufu wa Maria tuutumie kuyatafakari maisha yetu ya kiroho. Ni muda mzuri wa kusali rozari kwa wale wakristo wakatoliki katika kuuenzi utakatifu wa Maria. Lakini tuna mengi ya kujiuliza, Je yupo Nabii ambaye amekutabira mema kama Nabii Issaya alivyofanya kwa Mariam? Au mtaani wanakusema kwa ubaya? Je ndugu yangu mwanaume wewe ni Nabii Isaya kwa mwanamke yoyote? Huenda utabiri wako ni kusaidia mama zetu, dada zetu, wake zetu (simaanishi kuhonga kwa ajili ya zinaa au uasherati) naamanisha maisha ya kiroho na kimwili katika hali ya usafi. Usiogope, ama kwa hakika kwa kuwa bado upo hai basi ni wakati sasa. Salaam Maria..
Privaldinho19,602 Aufrufe • vor 2 Jahren
Keine weiteren Inhalte verfügbar