
Rose Mayemba
@rose_mayemba • 47,709 subscribers
Chadema Central Committee member, Pharmaceutical Technician,Business woman& Child of God...
Shorts
Videos

Huu ndo ukweli mchungu kuhusu Mafuta. Leo TPDC ukiwauliza Vitol walipatikaje?, alishindanishwa na nani?, mikataba yao iko wapi? Hawana majibu Ukiwauliza mahusiano ya Vitol na Namaro( kampuni iliyosajiliwa Dubai na mmiliki anayeishi Tanzania) yakoje? Watakaa kimya. Ukiwauliza zile taarifa za Mafuta zaidi ya Lita Milioni 300 ambazo zinaingia na kuuzwa bila kurekodiwa popote watakuita mchochezi. Kumbuka! Kuna taarifa za Abdul na Namaro kuiba sh 544 kwenye kila lita moja ya mafuta na taarifa za ndani kabisa zinasema pesa hizi zimetumika kununulia silaha za kuwapa kikosi maalumu cha Abdul na Samia cha utekaji,na hakuna mhusika hata mmoja anayeweza kutoka na kuitolea maelezo ya kina. Sasa wewe mtanzania mwenzangu hebu tujiulize hivi ni kweli hawajui kwamba ukipandisha gharama za mafuta umepandisha bei ya kila kitu nchini kuanzia Sukari, Mafuta, Chumvi etc... Wanafanya yote haya kumkomoa nani? TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
Rose Mayemba20,756 次观看 • 11 天前

UKIZOEA VYA KUNYONGA HAYA NDO MADHARA YAKE. Naambiwa NDUGU BASHITE huko kwenye Uchaguzi wa Kamati ya OLYMPIC Tanzania kapindua Matokeo ya URAIS hadharani. Katuma watu wake kuhakikisha Mshindi hatangazwi. Uchaguzi wenye wapiga kura 36 umezingirwa na Maaskari zaidi ya 10 wenye mitutu ya Bunduki. Imagine kati ya wagombea watatu aliyepewa ushindi ni yule aliyepata kura Moja. Naambiwa mwangalizi wa kimataifa ambaye ametokea UGANDA alibaki ametoa macho, anashangaa kila kitu, mwisho akawaambia "aibu kabisa hii" akaondoka. Sasa jifikirie kama wanaweza uhuni huu mbele ya macho ya wageni, wakiwa peke yao si ndo hatari zaidi? Tukiwaambia nchi imeoza na inahitaji overwhole mnaona kama ni chuki za wapinzani. Hebu ona nchi inavyofedheheshwa kwa mambo madogo kama haya. Tuliwaambia mkishamalizana na upinzani mtaanza kulana wenyewe kwa wenyewe. Haya, sie ya kwetu macho, tunajiandaa na 77 ya kesho. Matokeo halisi ni haya hapa. 1. ANTHONY MTAKA KURA 29 2. HENRI TANDAU KURA 6 3. LEONARD THADEO KURA 1 MSHINDI WETU KWA MUJIBU WA VIBARAKA WA BASHITE NI NDUGU LEONARD THADEO.
Rose Mayemba33,660 次观看 • 25 天前

Mtu yeyote mwenye sensible mind hawezi kuzungumza haya anayozungumza huyu mwanamke hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa liko katikati ya majonzi... Ujasiri huu unawezekana tu kwa 1. Mtu aliyechanganyikiwa, 2.Aliyebeba kichwa bila ubongo waswahili wanaiita hiyo kichwa "debe tupu"...
Rose Mayemba20,223 次观看 • 2 个月前

Mimi nina roho ndogo sana, Hii video nimeitazama jana nikashindwa kuimaliza, nimerudia leo asubuhi, mchana leo nikapata ujasiri nikasikiliza yote. Huyu ni mwanamke kama mimi, amejaliwa mtoto mmoja wa kipekee kama ilivyo kwangu. Lakini mwenzangu mtoto wake hajawahi kurudi nyumbani yeye wala mwili wake tangu October 29. Mama anamuomba Samia awaonyeshe Makaburi angalau wawe wanaenda kuwaangalia watoto wao. Anakumbuka vile alimsomesha kwa kuuza uji mpaka anakua, kwamba mapito yote aliyopitia kumlea alikuwa akimlea ili Samia aje kumuua. Huyu ni mmoja tu, niambie ni akina mama wangapi wanapitia haya anayopitia huyu mama aliyebebeshwa mateso ya kudumu kwa kutokuanua matanga ya mwanae mpaka siku ya kufa kwake. Ila Samia, iko siku yako.😭
Rose Mayemba11,595 次观看 • 1 个月前

Usiku wa kuamkia leo vijana wetu wamekesha kulinda Jukwaa na vizimba, baadhi ya vizimba wamefanikiwa kuvivunja hivyo tulilazimika kuvijenga na kuvikarabati upya.Walipanga kung'oa jukwaa pia lakini walidhibitiwa. Vijana wa Green Guard walikuwa wanazunguka usiku kucha wakiwa na Mapanga na Virungu na vyuma vingine vyenye ncha kali. Taarifa tulizokuwa nazo ni kwamba walipanga kuua na kujeruhi watu ili Mkutano usifanyike. Kwa waliokuwa uwanjani usiku kulinda jukwaa tuliwasihi sana wasije kujaribu kujibizana nao. Ninaandika haya ili watanzania mjue nchi yetu ilipofika, na tuone namna tunavyoweza kukomesha hii hali. CCM wanayataka madaraka kwa nguvu kubwa sana, wako tayari kuua, kuteka na kumpoteza mtu yeyote kwa ajili ya madaraka. Je tuendelee hivi? Jibu ni hapana. Tufanyeje basi? Ni Lugha ngumu tu hawa viumbe wanaweza kuelewa.
Rose Mayemba11,045 次观看 • 1 个月前

Pamoja na kutokukubaliana maamuzi ya kuondoka kwako, pamoja na ukweli mwingine pia kwamba mimi ni mmoja wa watu walioumizwa sana na maamuzi uliyowahi kuyachukua. Mimi pia ni mmoja wa wachache waliochagua kukuelewa. Labda kwasababu wewe ukiwa darini unaungua mimi nilikuwa ndani ya viatu vyako. Karibu nyumbani. #Lettingthebygonesbebygones
Rose Mayemba15,513 次观看 • 2 个月前

HIDE MY ID!. Mwigulu Nchemba alipokuwa iringa akiendelea na maigizo yake ya kutengeneza matukio na kuyapa majibu kama vile ni shida za wananchi wanyonge kumbe nyingi ni za kutengeneza ili kupata umaarufu wa kujijenga kuwa ni sehemu ya wanyonge. Tukio la hivi karibuni lillitokea Iringa. Ambapo Nchemba alionekana akighazibika na kuita watumishi na baraza la madiwani kuwa ni wajinga na kuwa wamemnyang’anya baba wa kijana mlalamikaji ardhi mkoani dodoma aliyonunua mil 32 na kuwapa taasisi ya umma kwa mil 338. Ukweli ni nini ? Ukweli ni kuwa huyu kijana anaitwa PAYA, Mjomba wake na Jah People, Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Makambako na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe. Hii ni Cinema, imepangwa kabisa. Kwamba nchi hii imefika mahali mwenyekiti wa CCM wa mkoa anaeleza shida zake kwenye mikutano ya wanachi ya malalamiko. Aidha, kiwanja hicho kiwanja namba 24 kitalu AY eneo la Nzuguni ni kati ya viwanja vilivyokuwa vinauzwa kwa mnada na jiji la Dodoma mwaka 2021. Baada ya kuwa hakijauzwa, kwa njia za udanganyifu kiwanja kikauzwa shs mil 32 kwa jah people, imagine kiwanja mjini dodoma nzuguni cha ukubwa wa mita za mraba 8,700 kwa mil 32. Ofisi ya Jiji bila kujua kuwa kuna wale watumishi wahuni wameiba doc, wakaendelea na mnada wa kiwanja, kiwanja kikanunuliwa na Jkt kwa shs 337,177,685. Mzee akaitwa kuambiwa umetapeli na utapewa kiwanja kingine cha gharama ya kweli ya ulicholipa. Akakubali. Baada ya kuonana na Pm akabadili mawazo, akaondoka dodoma . Ikapangwa ziara ya iringa, sehemu ambayo baraza la madiwani halipo na haliwezi kujitetea , akaibuka Mjomba wa mwenyekiti wa chama wa mkoa kama mwanachi mnyonge kumbe ni genge la wanaotaka kuiba nchi... Haya mambo yanatia hasira sana.
Rose Mayemba19,338 次观看 • 2 个月前

Mzigo ukifika Sokoni utakuta TRA wamejazana Ofisini kwako wanataka Kodi yao, Halmashauri wanataka Ushuru wao, Sokoni wameshakuandalia risiti ya kibali cha kuingiza mzigo Sokoni. Mwenye Gari amekupandishia nauli maana gari yake imekaa porini siku tatu kwa kukwama. Watu wa Benki nao wamechachamaa umechelewesha rejesho la mwezi. Hii ni barabara ya kijiji Mfriga, Jimbo la Lupembe Mkoani Njombe. Miaka yote tangu Uhuru hizi ndo adha wanazokutana nazo wakulima na wafanyabiashara huku vijijini. Wenye wajibu wa kukomesha hali hii wako busy kumuimbia Mtukufu Malkia nyimbo za kusifu na kuabudu. Kazi yao ni kuvuna mahali ambapo hawakuwahi kuweka mbegu... Iko siku.
Rose Mayemba18,873 次观看 • 4 个月前

Hizi ndo siasa za ULAGHAI za CCM. Wananchi hawana Maji, hawana Barabara, Dawa hakuna Hospitali, watoto wanasoma kwenye shule ambazo hazina Vitabu wala Waalimu, kupata mlo mmoja kwa siku ni tabu, anakuja Mbunge anawagawia Kanga za elf tano tano kisa uchaguzi umekaribia. Dah!.
Rose Mayemba19,554 次观看 • 1 年前