
ROYAL TELEVISION
@Royal_Tv_Tz • 782,118 subscribers
Media Coverage
Videos

Mwandishi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa Paschal Mayala ameeleza maoni yake kuhusu kuwepo kwa Tundu Lissu mahakamani pamoja na uamuzi wa chama cha CHADEMA kutoshiriki uchaguzi, hali hiyo ilichangia kutokea kwa maandamano ya Oktoba 29. Amesema hayo hii Leo kwenye mahojiano na Jambo Tv Mayala amesema kuwa kesi ya Tundu Lissu na hatua ya CHADEMA ya kujiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi iliwaibua Gen Z nakusababisaha madhara yaliyotokea siku hiyo. Video Jambo Tv
ROYAL TELEVISION15,925 Aufrufe • vor 7 Monaten

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amemuagiza Msajili wa Vyama vya Michezo kutoa mwongozo rasmi kwa Simba Sports Club kuhusu mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo, ikiwemo marekebisho ya Katiba yake. Agizo hilo limekuja wakati Simba ikiwa kwenye hatua muhimu ya mageuzi ya kiutawala, huku wadau na wanachama wakisubiri kwa hamu mwelekeo wa mabadiliko hayo. Waziri Makonda amesisitiza kuwa ni lazima taratibu zote zifuatwe kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa ili kuhakikisha uwazi, uhalali na ulinzi wa maslahi ya wanachama. “Ni muhimu Msajili akatoa mwongozo wa wazi na wa kina utakaosaidia klabu kuelewa hatua za kisheria zinazopaswa kufuatwa,” ameeleza Waziri Makonda, akisisitiza kuwa mabadiliko yoyote ndani ya Simba yanapaswa kufanyika kwa kuzingatia misingi bora ya utawala na uwajibikaji. Hatua hiyo inaonekana kulenga kuondoa sintofahamu iliyojitokeza kuhusu mchakato wa marekebisho ya Katiba na muundo wa uendeshaji wa klabu, huku ikihakikisha kuwa mabadiliko hayo yanatekelezwa kwa njia halali na yenye kuleta tija kwa klabu na wadau wake. Video kishamba media
ROYAL TELEVISION12,951 Aufrufe • vor 6 Monaten

Mchungaji maarufu nchini, Mzee wa Upako Anthony Lusekelo, ametoa pole kwa Watanzania kufuatia machungu yaliyoikumba nchi hivi karibuni, akisema hali hiyo imeacha maumivu makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa nchini hata wakati wa vita vya Idd Amini miaka ya 1977 na 1978. Akizungumza na chombo kimoja cha habari, Lusekelo amesema kilichotokea ni machungu ya ndani kwa ndani, kwa kuwa waliohusika ni raia na askari wote ni Watanzania. Amesisitiza kuwa huu si wakati wa kulaumiana bali ni kipindi cha taifa kujitafakari kwa pamoja na kujiuliza kwa nini hali hiyo imefikiwa. “Kosa hatulifuti kwa kulaumu mtu mmoja, lazima tujiulize kama taifa kwanini tulifika hapa? Malalamiko haya hayakuanza jana, yalikuwepo muda mrefu, tukayapuuza,” amesema. Ametahadharisha dhidi ya siasa za udini akibainisha kuwa Tanzania haijawahi kuwa na utamaduni wa kubaguana kwa misingi ya dini, hivyo si sahihi kusema mtu akikosoa Rais basi anakosoa dini. “Tuachane na udini. Watu wakimkosoa Rais, hawaukosoi Uislamu, wanamkosoa Rais wao. Vivyo hivyo wakimsifu Rais, si kwamba wanasifu Uislamu. Tanzania tulishavuka huko,” amesisitiza. Akinukuu maandiko kutoka katika Biblia, Mzee wa Upako amesema, “Hekima ni kutatua tatizo bila kuanzisha lingine.” Ameonya kuwa baadhi ya viongozi wa dini wanaelekea kuanzisha tatizo jipya, kubwa na hatari zaidi, ambalo linaweza kushindikana kuzimwa na kizazi cha sasa – Gen Z kutokana na namna wanavyochukulia haki, uhuru na mawasiliano.
ROYAL TELEVISION10,287 Aufrufe • vor 9 Monaten

"Mambo ambayo hayawezi kuguswa na mabadiliko ya Sheria pekee yake; 1. Hutaweza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi. 2. Mgawanyo wa majimbo. 3. Haki ya Kugombea. Kuna mambo mengi ambayo ni muhimu yakagusa Katiba, ndio maana tunasema Katiba Mpya kwanza." Mhe. Reginald Munisi. Azam TV
ROYAL TELEVISION11,605 Aufrufe • vor 3 Jahren
Keine weiteren Inhalte verfügbar