ROYAL TELEVISION's banner
ROYAL TELEVISION's profile picture

ROYAL TELEVISION

@Royal_Tv_Tz782,118 subscribers

Media Coverage

Videos

Royal_Tv_Tz's profile picture

Mchungaji maarufu nchini, Mzee wa Upako Anthony Lusekelo, ametoa pole kwa Watanzania kufuatia machungu yaliyoikumba nchi hivi karibuni, akisema hali hiyo imeacha maumivu makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa nchini hata wakati wa vita vya Idd Amini miaka ya 1977 na 1978. Akizungumza na chombo kimoja cha habari, Lusekelo amesema kilichotokea ni machungu ya ndani kwa ndani, kwa kuwa waliohusika ni raia na askari wote ni Watanzania. Amesisitiza kuwa huu si wakati wa kulaumiana bali ni kipindi cha taifa kujitafakari kwa pamoja na kujiuliza kwa nini hali hiyo imefikiwa. “Kosa hatulifuti kwa kulaumu mtu mmoja, lazima tujiulize kama taifa kwanini tulifika hapa? Malalamiko haya hayakuanza jana, yalikuwepo muda mrefu, tukayapuuza,” amesema. Ametahadharisha dhidi ya siasa za udini akibainisha kuwa Tanzania haijawahi kuwa na utamaduni wa kubaguana kwa misingi ya dini, hivyo si sahihi kusema mtu akikosoa Rais basi anakosoa dini. “Tuachane na udini. Watu wakimkosoa Rais, hawaukosoi Uislamu, wanamkosoa Rais wao. Vivyo hivyo wakimsifu Rais, si kwamba wanasifu Uislamu. Tanzania tulishavuka huko,” amesisitiza. Akinukuu maandiko kutoka katika Biblia, Mzee wa Upako amesema, “Hekima ni kutatua tatizo bila kuanzisha lingine.” Ameonya kuwa baadhi ya viongozi wa dini wanaelekea kuanzisha tatizo jipya, kubwa na hatari zaidi, ambalo linaweza kushindikana kuzimwa na kizazi cha sasa – Gen Z kutokana na namna wanavyochukulia haki, uhuru na mawasiliano.

ROYAL TELEVISION

10,287 views • 9 months ago

No more content to load