Royal Media's banner
Royal Media's profile picture

Royal Media

@royalmediatz320,293 subscribers

Uhakika wa Habari, Hadhi ya Kifalme.

Videos

royalmediatz's profile picture

"Kuondolewa kwangu kama mnavyojua zilianza shida ndogo ndogo zile za Trilioni moja na nusu, halafu Spika Ndugai akaleta mazungumzo yale mpaka mwisho nikahisi tu mimi mwenyewe na unajua Tanzania hii ni Nchi ndogo sana, unapewa taarifa mapema kwahiyo kuna mtu akaniambia sasa hivi wameanza mchakato aa kumtafuta CAG mwingine. "Ukisoma katiba inasema kustaafu ni miaka 60 au umri wowote utakaoelekezwa na sheria. Sheria ya ukaguzi inasema miaka 65 kwahiyo ukiisoma katiba moja kwa moja unaona kuwa haiwezekani kustaafu. Na hili halikuwa jambo la hisia bali ni jambo la tafsiri ya katiba. Nikasema kwamba hapa kuna tatizo." "Nakumbuka nilikuwa Mwanza kwenye shughuli, akanipigia yuleyule Bwana aliyeniambia kuwa wameanza kutafuta CAG mpya, akaniambia unaenda kuondolewa kesho asubuhi na nina taarifa za ukweli kabisa kutoka kwenye Mamlaka. Nikashukuru tu na kusema hatukuzaliwa kukaa kwenye nafasi hizi, ikitokea mwenyenzi Mungu amejalia tuondoke tutaondoka tu. Imefika asubuhi Jumapili, kijana mmoja wa idara akanipigia kuniambia nimeona tangazo la Katibu Kiongozi kuwa saa moja baadae utaondolewa." "Nilikuwa na gari la serikali Mwanza, palepale kabla taarifa ya mimi kuondolewa haijatangazwa nikwambia dereva rudisha gari Dodoma mimi nitarudi Dar Es Salaam mwenyewe kwa ndege. Baada ya saa moja nikamsikia Kijazi kweli anatangaza." .... Jumatatu nikaenda Ofisini nikapaki gari yangu binafsi chini (IST nyekundu) nikaingia mapokezi, Kijana wa mapokezi ananiambia kuna watu juu Ofisini kwako nahisi hutoruhusiwa kuingia, nikwambia no, kwasababu leo ni tarehe nne na niliajiriwa tarehe tano basi bado mimi ni CAG technical, nikapanda juu ghorofa ya tatu, natokea tu pale nakutana na vijana wawili wanasema wameagizwa kukaa pale kulinda ofisi hivyo ni vigumu sana mimi kuingia, nilipowauliza maagizo yametoka wapi wakasema yametoka Ikulu. .... Kwakweli nilitoka pale nimekasirika kidogo kuhusu utaratibu wa kunifukuza Ofisini wakati sijamaliza muda wangu na sijapewa barua rasmi." Amesema Prof. Mussa Juma Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu wakati akizungumza na Runinga mtandao ya M/s Podcast.

Royal Media

36,411 views • 4 days ago

royalmediatz's profile picture

Tofauti na mitazamo ya baadhi ya wanachama wa CCM na wachambuzi wa siasa waliokuwa wakidai kuwa CHADEMA imepoteza mvuto na inaelekea ukingoni mwa siasa za Tanzania, ziara ya viongozi wake wakuu katika mikoa ya Mbeya na Njombe imeonesha picha tofauti baada ya maelfu ya wananchi kujitokeza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo. Ziara hiyo inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara John Heche pamoja na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, imevutia umati mkubwa wa wananchi waliofurika katika viwanja vya mikutano tangu saa kadhaa kabla ya viongozi hao kuwasili. Katika baadhi ya maeneo, wananchi walionekana wakisongamana kandokando ya barabara na viwanja vya mikutano ili kupata nafasi ya kusikiliza ujumbe wa viongozi hao. Mbali na mahudhurio makubwa, jambo lililoibua mjadala ni mwitikio wa wananchi katika uchangishaji wa fedha za chama kupitia kampeni ya “Tone Tone”, mamia ya wananchi wakionekana kujitokeza kwa hiari kutoa michango yao, huku wengine wakisukumana kuelekea jukwaani ili kukabidhi michango yao mbele ya viongozi wa chama hicho. Baadhi ya wananchi waliozungumza baada ya mikutano hiyo walisema wamehamasishwa na ujumbe wa viongozi wa CHADEMA kuhusu demokrasia, uwajibikaji na mustakabali wa taifa, hali iliyowafanya waone umuhimu wa kuchangia shughuli za chama. Walisema michango yao, licha ya kuwa midogo kwa baadhi yao, ni ishara ya kuunga mkono harakati wanazoamini kuwa zina manufaa kwa jamii. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema mwitikio huo katika mikutano ya Mbeya na Njombe unaonesha kuwa ushindani wa kisiasa nchini unaendelea kuwa hai, huku vyama vya upinzani vikionesha uwezo wa kuhamasisha wananchi na kukusanya rasilimali kupitia michango ya wanachama na wafuasi wao.

Royal Media

14,657 views • 4 days ago

royalmediatz's profile picture

"Mimi nilikuwa bungeni miaka kumi, ni mchaga, si mlisikia Spika (Job Ndugai) alisema nilikopa hela kwamba nina stress ya madeni? Mimi nilienda kule nikakwarua zote kwasababu nilijua wale wasela hawachelewi kubadilisha sera halafu nikapoteza kiinua mgongo, nikawalia timing palepale nikaenda kwa Mtunza hazina, akaniambia ninaweza kukopa mpaka milioni 300 nikamwambia leta, akaniambia kuna nyingine naweza kopa Milioni 150, nikachukua, wanakuja kushtuka wale wamenikopesha ziada Milioni 200, ikawa kama Milioni 600 hivi, wanakuja kuangalia kwenye akaunti wanakuta sifuri." "Ndugai alimind sana, Ndugai akanifukuza bungeni mwaka ili wasinilipie marejesho ili vitu viuzwe na baadae benki wakaniandikia barua ya kutaka kushikilia vitu vyangu kwani Bunge limekataa kunilipia, nikawajibu nikiwataka watafute muda na saa niwatembeze kwenye mali zangu wachague wanazozitaka ili waunganishe na mkopo wao, nikishindwa kulipa wauze." "Ndugai akanitangaza kuwa nina stress, nina presha ya madeni, nikasema poa, na kwenye akaunti hawazioni maana zilipita tu. Wakanifukuza bunge mwaka, Bashiru Ally aliyekuwa Katibu Mkuu akaniambia Magufuli anataka niwe Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM na watanilipia madeni yangu yote! Nikasema sitaki, mimi sio Blueband. Wakaniambia vitu vyangu vitauzwa? Nikawaambia vitauzwaje wakati mimi mchaga? Nitaendesha hata Haice. Sasa nikatoroka kwenda Canada, nikarudi, sina deni, Ndugai kafa, Magufuli kafa na Bashiru sio Katibu Mkuu tena, huyo sio Mungu?" "Sasa ndugu zangu tukitoka hapa tunarudi Ifakara, kama watekaji wapo hapa tutaanza safari muda sio mrefu kwahiyo wanaweza kukaa katikati hapo porini ila nawaonya Mungu wangu mimi ni kiboko mtakufa! Kama umepewa dili la utekaji hilo dili likatae utakufa na aliyekutuma atakufa, hatutaki mazishi wiki hii."Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema akihutubia kwenye mkutano wa hadhara, Mlimba Mkoani Morogoro leo Juni 18, 2026.

Royal Media

20,257 views • 9 days ago

royalmediatz's profile picture

Baraza la Machifu na Wazee wa Kimila Mkoani Ruvuma limelaani vikali na kulitupilia mbali tukio lililotokea Juni 20, 2026, la kusikika kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, kuvikwa uchifu wa kabila la Wangoni, likieleza kuwa mchakato huo ulikuwa wa kisanii na ukiukwaji mkubwa wa mila na desturi. ​Akizungumza na waandishi wa habari jana Juni 21, Chifu Songea Mbano amebainisha kuwa baraza hilo halina taarifa yoyote na halimtambui Heche kama chifu wa Wangoni, huku akilitaka Jeshi la Polisi na Serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu aliyemvisha mavazi hayo ya kimila. ​Uchunguzi uliofanywa na baraza hilo umebaini kuwa aliyemvisha kiongozi huyo wa kisiasa katika tukio hilo la Juni 20 anaitwa Lucius Joseph Ponera (maarufu kama Mayau), mkazi wa mtaa wa Mshangano na msanii wa kikundi cha ngoma za kitamaduni cha 'Ligi', ambacho pia kimetajwa kuwa hakijasajiliwa kisheria. ​"Mila na desturi zina heshima yake, sio kila mmoja anakuja tu na kufanya vitu anavyotaka yeye. Aliye mtawaza Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA sio chifu, ni msanii wa ngoma na hana mamlaka hayo. Kwa sasa John Heche hana hadhi ya kupewa uchifu wa kabila la Wangoni kamwe, ule ulikuwa ni usanii na tunaiomba serikali imkamate huyo kijana kuhoji kwanini amefanya hivi," amesisitiza Chifu Songea Mbano. ​Chifu Songea Mbano amefafanua kuwa kwa mujibu vya taratibu, mtu anayetakiwa kuvikwa uchifu lazima mchakato wake uridhiwe na kupitishwa na Baraza la Machifu la Mkoa wa Ruvuma kutokana na mchango wake mkubwa kwa taifa, wana-Ruvuma, au kimataifa. Viongozi pekee wenye mamlaka ya kuvikwa ngazi hiyo bila uratibu huo wa machifu ni viongozi wakuu wa nchi kama Rais. ​Machifu hao wamewatoa hofu wananchi na kusitisha mijadala inayoendelea mtandaoni, wakisisitiza kuwa wao hawajihusishi na itikadi za vyama vya siasa, bali wanalinda heshima na miiko ya jadi ya kabila la Wangoni isichezewe kwa ajili ya kutafuta umaarufu wa kisiasa au kijamii.

Royal Media

13,332 views • 6 days ago

royalmediatz's profile picture

Mwenyekiti wa CHASO katika Chuo Kikuu cha SAUTI Mwanza Silence Mwakasala, amefunguka kiundani mara baada ya kuachiwa kwa dhamana ya masharti leo, Juni 19, 2026, akibainisha kuwa Jeshi la Polisi lilienda kumkamata kwa tuhuma za kuchapisha vipeperushi vya kuhamasisha maandamano ya tarehe 7 Julai, lakini walipokosa ushahidi walihamishia tuhuma hizo kwenye mikataba ya mikopo. ​Mwakasala, mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa nne katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), ameiambia Royal tv kuwa upekuzi uliofanyika ofisini kwake (stationery) na nyumbani kwake haukukuta vipeperushi hivyo vya siasa, jambo lililowafanya polisi kugeukia mikataba ya kukopesha fedha na kadi za watu walioweka dhamana na kusema hawawezi kumuacha hivi hivi. ​Kiongozi huyo ameeleza kuwa shinikizo la kupata dhamana hiyo asubuhi ya leo limetokana na hofu ya wito wa Mahakama Kuu baada ya mawakili wake kufungua maombi ya dharura ya Habeas Corpus namba 202606172000013657, ambapo alitolewa selo ghafla saa nne asubuhi baada ya nyaraka hizo kufika kwa RCO. "Haki zangu hazikufuatwa, nimekaa siku tisa kwa kigezo cha uchunguzi. Walipokosa vipeperushi vya maandamano ya tarehe saba, walikuta mikataba ya kukopesha fedha ofisini kwangu wakasema wakikosa huku watanishika kwenye hili la mikataba. Walivyotoa dhamana leo, walikataa nisidhaminiwe na chama, wakamlazimisha Dean wa chuo anidhamini kwa sharti kuwa nikiacha siasa nitakuwa salama," amesema Mwakasala. ​Mwakasala anatakiwa kuripoti polisi Jumatatu asubuhi, na kuhusu kufika Mahakama Kuu Juni 23 mbele ya Jaji Emmanuel Gingwana, atasubiri mwongozo wa mawakili wake. Ametoa wito kwa serikali akieleza kuwa wasomi wanaochagua kuwa upande wa upinzani vyuoni wanapitia wakati mgumu mno chini ya jalada la uchunguzi namba 61/2026.

Royal Media

11,535 views • 8 days ago

royalmediatz's profile picture

#VIDEO: Mwandishi wa habari mkongwe Pascal Mayalla amesema dhana ya usaliti ndani ya vyama vya siasa inatokana na kutokuaminiana miongoni mwa Wanachama na Viongozi wa Vyama husika, huku pia akisema dhana hiyo hiyo serikalini hutokana na mmoja wa Viongozi kuonesha kutopenda mazuri ama mabaya yanayopangwa ndani ya serikali. "Mtu wa kwanza nitolee mfano ni Makamu wa Rais, tangu akiwa katibu Mkuu wa CCM alikuwa akiwakataza wanachama wenzake kutowasema vibaya Vyama pinzani kwa hoja kuwa Upinzani umeruhusiwa kisheria ndani ya Katiba, akisema hakuna sababu ya chuki na kutukanana kwasababu za kisiasa. Hili Dkt. Nchimbi alilisema wazi. Dkt. Nchimbi akawa anakemea wanachama wake waliokuwa wanatoa maneno makali. Wale wana CCM wanaokemewa na Dkt. Nchimbi kwa kutoa maneno makali, wao wanamuona ni msaliti, sio mwenzao, hawatakii mema, kumbe nia ya Dkt. Nchimbi ni njema kwamba sote ni watanzania hata kama tuna tofauti za kisiasa." Amesema Mayalla. Mayalla amebainisha hayo wakati wa mahojiano yake maalumu na Mwandishi wetu wa habari leo Jumamosi Juni 06, 2026 Jijini Dar Es Salaam, siku chache mara baada ya kuzuka kwa mjadala mkali, ulioanzia kwenye Bunge la Tanzania baada ya Mbunge wa Tunguu Mhe. Simai Mohamed Said, kueleza kuwa ndani ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan yupo msaliti aliyeaminiwa na Rais Samia na baadae kuanza kwenda ndivyo sivyo, mtu huyo akihusishwa na Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi. "Ikaja siku ya sheria duniani, Dkt. Nchimbi akaalikwa kumuwakilisha Rais Samia, Rais wa TLS Bw. Mwabukusi akasema yaliyotokea Oktoba 29 ni mambo ya kuumiza tusiendelee kuyasema tunatonesha vidonda na maadam Rais ameshaunda Tume, tuipe nafasi tume itoe matokeo. Baada ya Mwabukusi kusema haya, alipokuja kuhutubia Makamu wa Rais, akasema amekubaliana na ya Mwabukusi kwamba tuache kuzungumza na tuiachie tume imalize kazi yake na akasema si tu viongozi wa CCM wasiseme bali Viongozi wote hadi wa upinzani. Hii ikafanya pia baadhi ya watu waliokuwa wakitaka mambo hayo yaendelee kusemwa kumuona kama si mwenzao." Ameongeza kusema Mayalla.

Royal Media

16,391 views • 22 days ago

No more content to load