
Royal Media
@royalmediatz • 320,293 subscribers
Uhakika wa Habari, Hadhi ya Kifalme.
Videos

"Nampenda mwanasiasa ambaye anasoma, tatizo wanasiasa wetu wengi sio wasomaji. Niliona jana Clip ya waziri anashindwa kueleza namna ya kuongeza thamani kwenye mazao ya uvuvi, sasa hii value edition ya uvuvi ni so basic! Kwasababu uvuvi unaanzia nchi kavu, watu wana vyombo gani? Ukienda feri pale unakuta watu 30 wanatoka na chombo kimoja wanakwenda baharini watakuja kesho asubuhi wakiwa na jodari watatu, vibua kadhaa na labda watauza laki na ishirini, watu 30 wanagawana shilingi ngapi? Kwahiyo ukitaka kuongeza thamani wawezeshe vifaa wapate boti kubwa nzuri na ziwe na uwezo wa kukaa baharini wiki nzima wawe na chakula, barafu ya kutosha ya kuhifadhi samaki na wakirudi wapate soko." ... Sasa unamuona mtu anapata shida kuzungumza mambo haya wakati mandate yako ni masuala ya uvuvi, inakuaje unashindwa kuzungumza? Kwahiyo unaona kwamba technical alitakiwa aweze kusema lakini unachokiona ni ama alipaniki au hana skills za kulisema jambo hilo, sasa tatizo linakuwa hapo. Mimi sifa yangu kwa mwanasiasa ni uwezo wa kusoma na kuwa mpana katika mtazamo wake." Amesema aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Prof. Mussa Juma Assad wakati akihojiwa na M/S Podcast kupitia Mtandao wa Youtube leo Jumatano Juni 24, 2026.
Royal Media73,568 görüntüleme • 3 gün önce

"Kuondolewa kwangu kama mnavyojua zilianza shida ndogo ndogo zile za Trilioni moja na nusu, halafu Spika Ndugai akaleta mazungumzo yale mpaka mwisho nikahisi tu mimi mwenyewe na unajua Tanzania hii ni Nchi ndogo sana, unapewa taarifa mapema kwahiyo kuna mtu akaniambia sasa hivi wameanza mchakato aa kumtafuta CAG mwingine. "Ukisoma katiba inasema kustaafu ni miaka 60 au umri wowote utakaoelekezwa na sheria. Sheria ya ukaguzi inasema miaka 65 kwahiyo ukiisoma katiba moja kwa moja unaona kuwa haiwezekani kustaafu. Na hili halikuwa jambo la hisia bali ni jambo la tafsiri ya katiba. Nikasema kwamba hapa kuna tatizo." "Nakumbuka nilikuwa Mwanza kwenye shughuli, akanipigia yuleyule Bwana aliyeniambia kuwa wameanza kutafuta CAG mpya, akaniambia unaenda kuondolewa kesho asubuhi na nina taarifa za ukweli kabisa kutoka kwenye Mamlaka. Nikashukuru tu na kusema hatukuzaliwa kukaa kwenye nafasi hizi, ikitokea mwenyenzi Mungu amejalia tuondoke tutaondoka tu. Imefika asubuhi Jumapili, kijana mmoja wa idara akanipigia kuniambia nimeona tangazo la Katibu Kiongozi kuwa saa moja baadae utaondolewa." "Nilikuwa na gari la serikali Mwanza, palepale kabla taarifa ya mimi kuondolewa haijatangazwa nikwambia dereva rudisha gari Dodoma mimi nitarudi Dar Es Salaam mwenyewe kwa ndege. Baada ya saa moja nikamsikia Kijazi kweli anatangaza." .... Jumatatu nikaenda Ofisini nikapaki gari yangu binafsi chini (IST nyekundu) nikaingia mapokezi, Kijana wa mapokezi ananiambia kuna watu juu Ofisini kwako nahisi hutoruhusiwa kuingia, nikwambia no, kwasababu leo ni tarehe nne na niliajiriwa tarehe tano basi bado mimi ni CAG technical, nikapanda juu ghorofa ya tatu, natokea tu pale nakutana na vijana wawili wanasema wameagizwa kukaa pale kulinda ofisi hivyo ni vigumu sana mimi kuingia, nilipowauliza maagizo yametoka wapi wakasema yametoka Ikulu. .... Kwakweli nilitoka pale nimekasirika kidogo kuhusu utaratibu wa kunifukuza Ofisini wakati sijamaliza muda wangu na sijapewa barua rasmi." Amesema Prof. Mussa Juma Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu wakati akizungumza na Runinga mtandao ya M/s Podcast.
Royal Media36,411 görüntüleme • 4 gün önce

Mtumishi wa Mungu Nabii Boniface Mwamposa ameelekea jijini Dodoma kwa ajili ya kongamano la injili la "Malango Yako Kufunguka", linaloanza leo na linatarajiwa kuendelea kwa siku tatu. Msafara wake ulisafiri kwa treni ya SGR Tanzania kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, wakiwa wamechukua behewa zima la treni kuonesha ukubwa wa kongamano lenyewe. Kongamano hilo limeanza leo saa 8:00 mchana na kuendelea hadi tarehe 20, likijumuisha vipindi vya maombi, ibada na mafundisho.
Royal Media43,048 görüntüleme • 10 gün önce

Ombi la mchango wa maendeleo limegeuka shubiri kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge, baada ya kuwasha moto wa hasira na kuzomewa na mamia ya madereva bodaboda na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika kikao cha majumuisho kilichofanyika leo Juni 20, 2026. Zomeazomea hiyo imezuka kufuatia kauli ya mbunge huyo iliyotafsiriwa na wengi kama kejeli kwa hali ngumu ya kiuchumi,.pale alipowataka wadau hao kuanza kuchangia shilingi 1,000 kila mmoja kila siku kwa ajili ya kufadhili ujenzi wa miundombinu ya barabara mkoani humo. Mwalunenge, akijitetea jukwaani kuhusu mchango wa sekta isiyo rasmi, alishikilia hoja kuwa kipato cha makundi hayo kimeshakua na hakipaswi kuchukuliwa kama cha kimaskini, jambo lililoamsha zogo ukumbini.
Royal Media32,548 görüntüleme • 7 gün önce

"Nishukuru sana kwa heshima hii mliyotupa, ujue nilikua naangalia umbali wa kutoka kule Mpemba mpaka hapa ni zaidi ya Kilomita 15 na nimeangalia umbali wa kutoka Mjini kufika hapa ni zaidi ya Kilomita 6-7. Hapa mimi nimekaa hata network hakuna, sasa CCM kwa ujinga wao waliamini tukiwapeleka watu mbali (Km15) hawataenda kwahiyo, tutaenda tupige picha Heche akiwa na watu wawili tuseme Tunduma haijaitika. Sasa aibu yao, mmetoka Km14, mmekodi bajaji kwa hela zenu, mmekuja umbali huu, wengine mmetembea kwa mguu mbali na tonetone mtatoa." .... Tunduma We love you (tunawapenda) unajua nyie bhana ni ngome ya Chadema, sisi pale Tarime huwa tunawaigaiga hivi lakini ninyi nawavulia kofia, ninyi ni shida. Nyie, watu wa Karatu na watu wa Mbeya kila tukitaka kuwazidi mnatushinda tu. Ahsanteni sana." Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw. John Heche leo Jumatano Juni 24, 2026 akihutubiwa wananchi wa Tunduma Mkoani Songwe.
Royal Media16,778 görüntüleme • 4 gün önce

"Kwa taarifa yenu, leo nimesoma hapa kesi ya ICC (Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu) zimeingizwa kurasa 82 zinazoeleza kutoka mauaji ya watu zaidi ya 3,000 nchini, sasa wanasema hayo ni mambo ya ndani, niwaambie hakuna mambo ya ndani, ukizaa mtoto wewe Mama wa kwako mwenyewe, ukitaka kumuua majirani watakushughulikia, mauaji si mambo ya ndani dunia haitanyamaza." "Jana Mke wa Tundu Lissu na mdogo wake Polepole wamezungumza kwenye Bunge la Ulaya na Mke wake Lissu ametema kizungu kubwa, dunia haitanyamaza kwahiyo sisi tutapiga ndani na wengine kule nje. Ukisimama nchale, ukikaa nchale, ukichuchumaa nchale." ... Tunataka wamuachie Tundu Lissu, la pili tunataka katiba mpya na tunafanya mikutano hii kuzunguka nchi nzima wasipotusikiliza tutaitisha maandamano nchi nzima hakuna mtoto atakaa ndani."- John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania akizungumza na wananchi wa Mbeya Mjini leo Jumanne Juni 23, 2026.
Royal Media17,819 görüntüleme • 5 gün önce

Tofauti na mitazamo ya baadhi ya wanachama wa CCM na wachambuzi wa siasa waliokuwa wakidai kuwa CHADEMA imepoteza mvuto na inaelekea ukingoni mwa siasa za Tanzania, ziara ya viongozi wake wakuu katika mikoa ya Mbeya na Njombe imeonesha picha tofauti baada ya maelfu ya wananchi kujitokeza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo. Ziara hiyo inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara John Heche pamoja na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, imevutia umati mkubwa wa wananchi waliofurika katika viwanja vya mikutano tangu saa kadhaa kabla ya viongozi hao kuwasili. Katika baadhi ya maeneo, wananchi walionekana wakisongamana kandokando ya barabara na viwanja vya mikutano ili kupata nafasi ya kusikiliza ujumbe wa viongozi hao. Mbali na mahudhurio makubwa, jambo lililoibua mjadala ni mwitikio wa wananchi katika uchangishaji wa fedha za chama kupitia kampeni ya “Tone Tone”, mamia ya wananchi wakionekana kujitokeza kwa hiari kutoa michango yao, huku wengine wakisukumana kuelekea jukwaani ili kukabidhi michango yao mbele ya viongozi wa chama hicho. Baadhi ya wananchi waliozungumza baada ya mikutano hiyo walisema wamehamasishwa na ujumbe wa viongozi wa CHADEMA kuhusu demokrasia, uwajibikaji na mustakabali wa taifa, hali iliyowafanya waone umuhimu wa kuchangia shughuli za chama. Walisema michango yao, licha ya kuwa midogo kwa baadhi yao, ni ishara ya kuunga mkono harakati wanazoamini kuwa zina manufaa kwa jamii. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema mwitikio huo katika mikutano ya Mbeya na Njombe unaonesha kuwa ushindani wa kisiasa nchini unaendelea kuwa hai, huku vyama vya upinzani vikionesha uwezo wa kuhamasisha wananchi na kukusanya rasilimali kupitia michango ya wanachama na wafuasi wao.
Royal Media14,657 görüntüleme • 4 gün önce

"Kumekuwepo na utaratibu wa msafara wetu kufuatiliwa na vyombo vya dola, watu wetu wapo makini. Mimi nitumie nafasi hii kuwaambia sisi sio wahalifu, sisi ni watanzania wema, ni watu tunaoipenda Nchi hii. Vyombo vya Dola fanyeni kazi na wajibu mliopewa kwa mujibu wa Katiba sio kutishia Chadema." "Mimi John Heche uoga niliacha tangu nilipozaliwa siku ileile kwahiyo hakuna mtu wa kunitisha mimi. Maadam sivunji sheria, nyie mnalinda wahalifu halafu mnafuatilia watu wema, mnamkamata Lissu ambaye ni mtu mwema aliyepigwa risasi 38, 16 zikaingia mwilini wake na mpaka leo Jeshi la Polisi halijawahi kutuambia nani alimpiga risasi, sasa mnatufuatilia wa nini?" ....Mnakuja kwenye mikutano ya Chadema mpo kwenye gia za kivita, mmefunika nyuso, mna marungu! Huu ni mkutano wa hadhara wa kiraia, tunataka mje hapa na nyuso za undugu na furaha. Haya mambo ya kutisha tisha watu hatutayakubali labda tuwe tumekufa, kwahiyo mkome kutufuatilia na Vijana mnaotumwa, hii Nchi watu wana machungu sana, acheni kabisa kujaribu kuipiga kiberiti nchi hii, kuna siku moto mtauwasha halafu nyote mtakimbikia."- John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema akihutubia wananchi wa Mbarali Mkoani Mbeya, leo Juni 22, 2026.
Royal Media16,419 görüntüleme • 5 gün önce

"Mimi nina watoto kumi na katika kumi kuna Polisi mmoja Mahita Omary Mahita. Ukienda Arusha kama utapata nafasi nenda uliza Mahita yupo wapi, watakuambia Mahita Omary Mahita ni mkono wa chuma." "Ulipata kuona walivyokuwa wanalumbana kwenye kesi ya kina Mbowe? Mwanangu ni mwanasheria."- Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Mstaafu wa Tanzania akizungumza na M&S Podcast.
Royal Media31,929 görüntüleme • 15 gün önce

"Mimi nilikuwa bungeni miaka kumi, ni mchaga, si mlisikia Spika (Job Ndugai) alisema nilikopa hela kwamba nina stress ya madeni? Mimi nilienda kule nikakwarua zote kwasababu nilijua wale wasela hawachelewi kubadilisha sera halafu nikapoteza kiinua mgongo, nikawalia timing palepale nikaenda kwa Mtunza hazina, akaniambia ninaweza kukopa mpaka milioni 300 nikamwambia leta, akaniambia kuna nyingine naweza kopa Milioni 150, nikachukua, wanakuja kushtuka wale wamenikopesha ziada Milioni 200, ikawa kama Milioni 600 hivi, wanakuja kuangalia kwenye akaunti wanakuta sifuri." "Ndugai alimind sana, Ndugai akanifukuza bungeni mwaka ili wasinilipie marejesho ili vitu viuzwe na baadae benki wakaniandikia barua ya kutaka kushikilia vitu vyangu kwani Bunge limekataa kunilipia, nikawajibu nikiwataka watafute muda na saa niwatembeze kwenye mali zangu wachague wanazozitaka ili waunganishe na mkopo wao, nikishindwa kulipa wauze." "Ndugai akanitangaza kuwa nina stress, nina presha ya madeni, nikasema poa, na kwenye akaunti hawazioni maana zilipita tu. Wakanifukuza bunge mwaka, Bashiru Ally aliyekuwa Katibu Mkuu akaniambia Magufuli anataka niwe Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM na watanilipia madeni yangu yote! Nikasema sitaki, mimi sio Blueband. Wakaniambia vitu vyangu vitauzwa? Nikawaambia vitauzwaje wakati mimi mchaga? Nitaendesha hata Haice. Sasa nikatoroka kwenda Canada, nikarudi, sina deni, Ndugai kafa, Magufuli kafa na Bashiru sio Katibu Mkuu tena, huyo sio Mungu?" "Sasa ndugu zangu tukitoka hapa tunarudi Ifakara, kama watekaji wapo hapa tutaanza safari muda sio mrefu kwahiyo wanaweza kukaa katikati hapo porini ila nawaonya Mungu wangu mimi ni kiboko mtakufa! Kama umepewa dili la utekaji hilo dili likatae utakufa na aliyekutuma atakufa, hatutaki mazishi wiki hii."Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema akihutubia kwenye mkutano wa hadhara, Mlimba Mkoani Morogoro leo Juni 18, 2026.
Royal Media20,257 görüntüleme • 9 gün önce

Baraza la Machifu na Wazee wa Kimila Mkoani Ruvuma limelaani vikali na kulitupilia mbali tukio lililotokea Juni 20, 2026, la kusikika kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, kuvikwa uchifu wa kabila la Wangoni, likieleza kuwa mchakato huo ulikuwa wa kisanii na ukiukwaji mkubwa wa mila na desturi. Akizungumza na waandishi wa habari jana Juni 21, Chifu Songea Mbano amebainisha kuwa baraza hilo halina taarifa yoyote na halimtambui Heche kama chifu wa Wangoni, huku akilitaka Jeshi la Polisi na Serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu aliyemvisha mavazi hayo ya kimila. Uchunguzi uliofanywa na baraza hilo umebaini kuwa aliyemvisha kiongozi huyo wa kisiasa katika tukio hilo la Juni 20 anaitwa Lucius Joseph Ponera (maarufu kama Mayau), mkazi wa mtaa wa Mshangano na msanii wa kikundi cha ngoma za kitamaduni cha 'Ligi', ambacho pia kimetajwa kuwa hakijasajiliwa kisheria. "Mila na desturi zina heshima yake, sio kila mmoja anakuja tu na kufanya vitu anavyotaka yeye. Aliye mtawaza Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA sio chifu, ni msanii wa ngoma na hana mamlaka hayo. Kwa sasa John Heche hana hadhi ya kupewa uchifu wa kabila la Wangoni kamwe, ule ulikuwa ni usanii na tunaiomba serikali imkamate huyo kijana kuhoji kwanini amefanya hivi," amesisitiza Chifu Songea Mbano. Chifu Songea Mbano amefafanua kuwa kwa mujibu vya taratibu, mtu anayetakiwa kuvikwa uchifu lazima mchakato wake uridhiwe na kupitishwa na Baraza la Machifu la Mkoa wa Ruvuma kutokana na mchango wake mkubwa kwa taifa, wana-Ruvuma, au kimataifa. Viongozi pekee wenye mamlaka ya kuvikwa ngazi hiyo bila uratibu huo wa machifu ni viongozi wakuu wa nchi kama Rais. Machifu hao wamewatoa hofu wananchi na kusitisha mijadala inayoendelea mtandaoni, wakisisitiza kuwa wao hawajihusishi na itikadi za vyama vya siasa, bali wanalinda heshima na miiko ya jadi ya kabila la Wangoni isichezewe kwa ajili ya kutafuta umaarufu wa kisiasa au kijamii.
Royal Media13,332 görüntüleme • 6 gün önce

Mzee maarufu mtandaoni, Clemence Mwandambo, ameibua mjadala mkubwa leo kufuatia kauli zake zilizojaa vitisho vya 'lockdown' ya wiki tatu na lugha ya ukosoaji dhidi ya wanaharakati wanaokosoa mwenendo wa nchi. Katika video aliyochapisha Jumanne, Juni 16, 2026, kupitia mitandao ya kijamii, Mwandambo ametumia maneno makali kuwashambulia wananchi wanaofuatilia mijadala ya mtandaooni, akidai kuwa wanataka kuingiza nchi kwenye vurugu kwa kuwasikiliza watu aliowaita "wendawazimu" na "wavuta bangi." Mwandambo ametoa vitisho vya kufungwa kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo shule, hospitali, masoko na hata mtandao wa internet, huku akidai kuwa wananchi wa maeneo ya walalahoi kama Manzese ndio watakaoteseka chumbani iwapo watasikiliza sauti mbadala. "Tunataka tuingie kwenye vurugu kwa kuwasikiliza hawa wendawazimu, kwa kuwasikiliza hawa wachochezi walioko nje ya nchi na ndani ya nchi. Sasa tutaenda kwenye lockdown ya wiki tatu; hakuna kwenda sokoni, hakuna kwenda hospitali, shule wala kazini, ofisi zote zifungwe na internet ifungwe," amesisitiza Mwandambo katika video hiyo. Katika kile kinachoonekana kusisitiza zaidi, .zee huyo amewataja majina wanaharakati maarufu akiwemo Maria Sarungi, Nuru Ndali (Nuru Vazi), Hilda Newton na wengineo, akidai kuwa wanachochea vurugu wakiwa nje ya nchi huku wakazi wa kipato cha chini wakitishiwa kujifungia ndani.
Royal Media18,035 görüntüleme • 11 gün önce

"Nimemsikia mtoto mmoja wa shule hapo hajui hata wajibu wa Mbunge, anasema John Heche amesoma shule ya Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Bulima, ni kweli nimesoma shule ya Bulima lakini kipindi hicho Bulima haikuwa shule ya Wazazi, ilikuwa shule ya bodi ya Pamba, CCM ndio wameipora sasa hivi na kuwa ya wazazi. Tukishinda nchi hii vitu hivi vyote tutavirudisha serikalini siku hiyo hiyo ikiwemo Ofisi wanazozikalia. Wataenda kupanga mtaani huko. "Mimi sijasoma shule ya CCM mimi, ningeacha shule haki ya Mungu. Hii akili yangu mnavyosikia ningeweza kusoma shule ya CCM?."- Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA akizungumza na wanafunzi wa Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa leo Juni 13, 2026.
Royal Media23,190 görüntüleme • 15 gün önce

Rais wa Marekani, Donald Trump, amezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumtania Rais wa Umoja wa falme za kiarabu, Mohamed bin Zayed Al Nahyan, kuhusu utajiri wake wakati wa hafla iliyohudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali. Katika tukio hilo, Mohamed bin Zayed alikuwa akizungumza kwa sauti ya chini, jambo lililomfanya Trump kutoa utani uliowafanya waliohudhuria kucheka. Trump alisema kuwa mtu akiwa tajiri kiasi hicho anaweza kuzungumza kwa sauti ya chini na bado akasikilizwa na kila mtu. "Nimekuwa nikijiuliza kama kuna mtu amesikia alichosema," alisema Trump huku akitabasamu, kabla ya kuongeza kuwa "utajiri mkubwa huambatana na kiwango kikubwa cha kujiamini kiasi kwamba mtu hahitaji kupaza sauti ili kusikilizwa." Kauli hiyo ilizua vicheko ukumbini na baadaye kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, ambapo wengi waliitafsiri kama mzaha wa kirafiki uliolenga kuonyesha hadhi na ushawishi wa Rais wa UAE katika jukwaa la kimataifa. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameeleza kuwa kauli hiyo ilitolewa katika mazingira ya utani na haikuonekana kuwa na nia ya kumdhalilisha kiongozi huyo, bali kuonyesha namna ambavyo viongozi wenye ushawishi mkubwa mara nyingi huwasilisha ujumbe wao kwa utulivu lakini wakasikilizwa kwa umakini mkubwa.
Royal Media17,880 görüntüleme • 11 gün önce

"Suala la Tundu Lissu mimi nipo upande wake. Watazame suala hili waachane nalo, huyu bwana atoke afanye shughuli zake. Tunamuhitaji Tundu Lissu atoke arudi uraiani, amekaa muda mrefu basi kama ni hukumu itoke ieleweke na nafikiri wakati umefika sasa Mahakama ilitazame jambo hili ahukumiwe. Jambo hili linatuchafua sana kama Taifa. Ukiwa na upinzani imara inakusaidia uliopo madarakani kukufungua macho kuona kwamba hapa hufanyi vizuri na unatakiwa kutia bidii eneo hilo. Mimi ni muumini wa upinzani imara." Amesema Bw. Buluba Mabelele, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa wakati wa mahojiano yake kwenye kituo cha runinga cha StarTv.
Royal Media16,708 görüntüleme • 11 gün önce

Mwenyekiti wa CHASO katika Chuo Kikuu cha SAUTI Mwanza Silence Mwakasala, amefunguka kiundani mara baada ya kuachiwa kwa dhamana ya masharti leo, Juni 19, 2026, akibainisha kuwa Jeshi la Polisi lilienda kumkamata kwa tuhuma za kuchapisha vipeperushi vya kuhamasisha maandamano ya tarehe 7 Julai, lakini walipokosa ushahidi walihamishia tuhuma hizo kwenye mikataba ya mikopo. Mwakasala, mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa nne katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), ameiambia Royal tv kuwa upekuzi uliofanyika ofisini kwake (stationery) na nyumbani kwake haukukuta vipeperushi hivyo vya siasa, jambo lililowafanya polisi kugeukia mikataba ya kukopesha fedha na kadi za watu walioweka dhamana na kusema hawawezi kumuacha hivi hivi. Kiongozi huyo ameeleza kuwa shinikizo la kupata dhamana hiyo asubuhi ya leo limetokana na hofu ya wito wa Mahakama Kuu baada ya mawakili wake kufungua maombi ya dharura ya Habeas Corpus namba 202606172000013657, ambapo alitolewa selo ghafla saa nne asubuhi baada ya nyaraka hizo kufika kwa RCO. "Haki zangu hazikufuatwa, nimekaa siku tisa kwa kigezo cha uchunguzi. Walipokosa vipeperushi vya maandamano ya tarehe saba, walikuta mikataba ya kukopesha fedha ofisini kwangu wakasema wakikosa huku watanishika kwenye hili la mikataba. Walivyotoa dhamana leo, walikataa nisidhaminiwe na chama, wakamlazimisha Dean wa chuo anidhamini kwa sharti kuwa nikiacha siasa nitakuwa salama," amesema Mwakasala. Mwakasala anatakiwa kuripoti polisi Jumatatu asubuhi, na kuhusu kufika Mahakama Kuu Juni 23 mbele ya Jaji Emmanuel Gingwana, atasubiri mwongozo wa mawakili wake. Ametoa wito kwa serikali akieleza kuwa wasomi wanaochagua kuwa upande wa upinzani vyuoni wanapitia wakati mgumu mno chini ya jalada la uchunguzi namba 61/2026.
Royal Media11,535 görüntüleme • 8 gün önce

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Mhe. Petro Magoti amesema vikosi vya ulinzi na usalama Wilayani humo vimejipanga kudhibiti maandamano yanayotajwa, kuratibiwa na kuhamasishwa kufanyika Julai 07, 2026. Dc Magoti amwsema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge katika baraza maalumu la Madiwani wa Halmashauri hiyo, wakijadili kuhusu ripoti ya mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka 2024/25. "Nikuhakikishie Mkuu wa Mkoa, hakuna hata mmbu atakayeandamana hiyo tarehe saba." Amesema Dc Magoti.
Royal Media10,606 görüntüleme • 8 gün önce

#VIDEO: Mwandishi wa habari mkongwe Pascal Mayalla amesema dhana ya usaliti ndani ya vyama vya siasa inatokana na kutokuaminiana miongoni mwa Wanachama na Viongozi wa Vyama husika, huku pia akisema dhana hiyo hiyo serikalini hutokana na mmoja wa Viongozi kuonesha kutopenda mazuri ama mabaya yanayopangwa ndani ya serikali. "Mtu wa kwanza nitolee mfano ni Makamu wa Rais, tangu akiwa katibu Mkuu wa CCM alikuwa akiwakataza wanachama wenzake kutowasema vibaya Vyama pinzani kwa hoja kuwa Upinzani umeruhusiwa kisheria ndani ya Katiba, akisema hakuna sababu ya chuki na kutukanana kwasababu za kisiasa. Hili Dkt. Nchimbi alilisema wazi. Dkt. Nchimbi akawa anakemea wanachama wake waliokuwa wanatoa maneno makali. Wale wana CCM wanaokemewa na Dkt. Nchimbi kwa kutoa maneno makali, wao wanamuona ni msaliti, sio mwenzao, hawatakii mema, kumbe nia ya Dkt. Nchimbi ni njema kwamba sote ni watanzania hata kama tuna tofauti za kisiasa." Amesema Mayalla. Mayalla amebainisha hayo wakati wa mahojiano yake maalumu na Mwandishi wetu wa habari leo Jumamosi Juni 06, 2026 Jijini Dar Es Salaam, siku chache mara baada ya kuzuka kwa mjadala mkali, ulioanzia kwenye Bunge la Tanzania baada ya Mbunge wa Tunguu Mhe. Simai Mohamed Said, kueleza kuwa ndani ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan yupo msaliti aliyeaminiwa na Rais Samia na baadae kuanza kwenda ndivyo sivyo, mtu huyo akihusishwa na Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi. "Ikaja siku ya sheria duniani, Dkt. Nchimbi akaalikwa kumuwakilisha Rais Samia, Rais wa TLS Bw. Mwabukusi akasema yaliyotokea Oktoba 29 ni mambo ya kuumiza tusiendelee kuyasema tunatonesha vidonda na maadam Rais ameshaunda Tume, tuipe nafasi tume itoe matokeo. Baada ya Mwabukusi kusema haya, alipokuja kuhutubia Makamu wa Rais, akasema amekubaliana na ya Mwabukusi kwamba tuache kuzungumza na tuiachie tume imalize kazi yake na akasema si tu viongozi wa CCM wasiseme bali Viongozi wote hadi wa upinzani. Hii ikafanya pia baadhi ya watu waliokuwa wakitaka mambo hayo yaendelee kusemwa kumuona kama si mwenzao." Ameongeza kusema Mayalla.
Royal Media16,391 görüntüleme • 22 gün önce
Daha fazla içerik yok.