
Extreme Introvert🧕💫
@Sincerelyrahma7 • 11,412 subscribers
Proud muslim | Proud mom | JUST PROUD 😚💃🤸♀️
Shorts
Videos
1:36
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Leo ni birthday ya Mama Ryan❤️ Ila kwa mara ya kwanza, naomba nisiambiwe "Happy Birthday" Sijisikii kusherehekea chochote Badala yake, niombeeni dua, dua nyingi na kwa wingi Kiukweli kuna mapambano ambayo nimeyabeba kimya kiasi kwamba hata tabasamu langu kuna muda limekuwa sehemu ya kuficha maumivu. Kuna usiku ambao nimekesha nikimwomba Mwenyezi Mungu anipe sababu ya kuendelea, na kuna siku ambazo nimecheka mbele za watu huku moyo wangu ukiwa umechoka kupita maelezo Sijui mwaka huu utaniletea nini ila ninachojua ni kwamba nimefika hapa kwa rehema za M/Mungu na si kwa sababu nilikuwa na nguvu kuliko matatizo yangu ila ni kwa kuwa alinipa ujasiri Kama umewahi kunitakia mema, leo usinipe salamu za birthday bali nipe dua na uniombee kheri M/Mungu aniondolee yale yanayoniumiza kimya kimya, anifungulie milango ya kheri, anipe utulivu wa moyo, na aniandikie maisha yenye baraka kuliko niliyowahi kuyaota. Wakati mwingine dua moja ya kweli kutoka kwa mtu usiyemtegemea inaweza kubadili maisha kuliko maneno elfu ya pongezi. Allah anijaalie umri huu mpya uwe mwanzo wa faraja baada ya maumivu, mwanga baada ya giza, na urahisi baada ya kila ugumu. Aamiin 🤲🏽
Extreme Introvert🧕💫25,875 次观看 • 1 个月前
没有更多内容可加载