
Samia Suluhu
@SuluhuSamia • 1,830,074 subscribers
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. President of the United Republic of Tanzania
Shorts
Videos

Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), Rufiji, Pwani Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutuwezesha kushuhudia tukio hili la kihistoria kwa Taifa letu. Hii ni hatua ya kujivunia katika safari yetu ya kuendelea kufanya kazi ya kujikomboa kiuchumi, ili kuiishi maana halisi ya Uhuru wetu, pamoja na malengo na ndoto za waasisi wetu. Hongera kwa kila Mtanzania.
Samia Suluhu48,274 Aufrufe • vor 7 Tagen

Ninampongeza Hawa Wanyeche, mchezaji wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, kwa kutwaa ubingwa wa Uganda Ladies Open, mashindano yaliyokutanisha wachezaji kutoka Ghana, Japan, Kenya, Nigeria, Rwanda, Tanzania na Uganda. Ushindi huu ni fahari kubwa kwa Taifa letu na unaonesha uwezo wa wachezaji wetu kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa. Serikali itaendelea kuimarisha na kuendeleza michezo nchini kwa kuweka mazingira bora kwa wanamichezo wote, pamoja na kuwawezesha kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Samia Suluhu30,036 Aufrufe • vor 14 Tagen

Leo imekuwa siku ya kihistoria kwa nchi yetu ambapo nimezindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la Mwaka 2024). Hatua hii ni utekelezaji wa maelekezo niliyotoa bungeni Aprili 2021, ambapo maboresho haya yamelenga kuiwezesha nchi yetu kuendana na mabadiliko makubwa yaliyotokea kwa miongo miwili ndani na nje ya nchi. Ninawapongeza wote mlioshiriki kuandaa sera hii, hasa wananchi mliotoa maoni, kwani mmeshiriki katika kujenga hatma ya nchi yenu na mmeweka alama isiyofutika. Aidha, nimeielekeza Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukuwa hatua za haraka, ikiwemo kutoa ufafanuzi, pindi kauli au matamko yanapotolewa kuhusu nchi yetu ili kudhibiti upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu. Nchi yetu itaendelea kubaki salama, yenye amani, umoja na utulivu, na hakuna mtu yeyote atakayetuondolea nguzo hizi muhimu.
Samia Suluhu599,445 Aufrufe • vor 1 Jahr

Nimekuwa na wasaa mzuri wa kuzungumza na kushiriki burudani na michezo pamoja na wananchi mjini Zanzibar leo jioni, mara tu baada ya kuwasili kutokea Dodoma. Ahsanteni sana kwa mapokezi mazuri na kwa upendo wenu. Pamoja na mambo mengine, nikiwa Zanzibar nitaungana na wananchi katika Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival), jukwaa muhimu linaloendelea kuwakutanisha wananchi na wadau mbalimbali katika kuenzi utamaduni, michezo, sanaa na kuimarisha mshikamano wetu.
Samia Suluhu26,833 Aufrufe • vor 19 Tagen

Leo alasiri nimetangaza uteuzi wa Baraza la Mawaziri pamoja na Naibu Mawaziri. Kwa pamoja, tutafanya kazi ya kutekeleza jukumu la msingi la kuwatumikia wananchi. Dhamana hii ni wajibu na pia deni ambalo tunapaswa kuwalipa wananchi kwa kuwatumikia kwa ari, bidii na uaminifu mkubwa. Ninawatakia kila la kheri. Mwenyezi Mungu awasimamie na kuwaongoza.
Samia Suluhu207,765 Aufrufe • vor 9 Monaten

Hotuba yangu kwa Taifa hii leo kuelekea Miaka 61 ya Muungano.
Samia Suluhu258,499 Aufrufe • vor 1 Jahr

Sambamba na mambo mengine, katika hotuba yangu ya kulifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nimevielekeza vyombo vya sheria hasa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwafutia makosa vijana na watoto wetu ambao kwa kutokujua, walifanya makosa kwa kufuata mkumbo Oktoba 29 mwaka huu. Nikiwa Mama na Mlezi, ninawasihi vijana wote kuendelea kulinda amani na mshikamano wa nchi yetu, na hata siku moja msikubali kushawishiwa kuichoma nchi yenu wenyewe.
Samia Suluhu102,200 Aufrufe • vor 9 Monaten

Sehemu ya kazi siku ya leo nilipokutana na kufanya mazungumzo na mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, Ikulu, Dar es Salaam. Tumekuwa na mjadala mzuri kuhusu kushirikiana katika masuala ya uhifadhi pamoja na utafiti. Sambamba na hayo, nimesikiliza dhamira ya Sir Jim Ratcliffe kuitumia Klabu ya Manchester United kutangaza utalii wa nchi yetu, ambapo pia nimemkaribisha kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Michezo (Sports Academy) hapa nchini. Nimepokea na kumshukuru kwa salamu za kheri toka kwa Kocha Ruben Amorim kwa niaba ya wachezaji wa Klabu ya Manchester United, na za Kocha Mstaafu, Sir Alex Ferguson.
Samia Suluhu160,391 Aufrufe • vor 1 Jahr

Dar es Salaam 08.02.2025 My Welcome and Opening remarks at the Joint Southern African Development Community (SADC) and the East African Community (EAC) Heads of State and Government Summit on the prevailing security situation in the Eastern Democratic Republic of Congo (DRC). As regional leaders, history will judge us harshly if we remain still and watch the situation worsen day by day. In line with the principle of African solutions for Africa’s problems, our countries have a collective responsibility to ensure we urgently address the existing security challenges that have heavily impacted the well-being of innocent civilians. This joint summit meeting in Dar es Salaam presents an opportunity to recommit our collective efforts in addressing the conflicts, and reaffirm our sustainable peace and stability in the entire EAC and SADC regions. It is crucial that we find a durable solution that upholds sovereignty, promotes inclusivity and ensures that the people of DRC can enjoy the durable peace and security that they have been yearning for, for decades. As a steadfast advocate for peace in Africa, Tanzania is deeply concerned about the persistent insecurity in Eastern DRC. The ongoing conflict not only destabilizes our brotherly nation, but also puts serious dents on our consistent efforts to enhance regional integration. My country remains committed to supporting ongoing diplomatic initiatives to end this conflict, and so we call on all parties involved to positively engage in negotiations, prioritize the well-being of the people, and commit to a peaceful co-existence.
Samia Suluhu162,862 Aufrufe • vor 1 Jahr

Mapema leo nchi yetu ilipoandika historia kwa uzinduzi wa Treni ya Kisasa ya Umeme (SGR) ambapo pia nimeitumia kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma. Baada ya kukamilika kwa kazi hii njema, sasa tumeanza kazi ya vipande vipya vya Tabora kwenda Isaka, Isaka hadi Mwanza, pamoja na kile cha kutoka Tabora hadi Kigoma, na kisha kuunganisha na nchi majirani zetu ili kufungua milango zaidi ya fursa za kiuchumi kwa wananchi wetu.
Samia Suluhu205,641 Aufrufe • vor 2 Jahren

Excellencies and distinguished guests, delegates, partners and friends, welcome to Tanzania for the Mission 300 Africa Energy Summit to be held in Dar es Salaam on the 27th and 28th of January 2025. This summit marks a historic moment in our collective efforts to accelerate energy access across Africa, and to take bold actions to power our continents's future. Karibuni sana.
Samia Suluhu153,664 Aufrufe • vor 1 Jahr

Hotuba yangu mapema leo Ikulu, Dodoma nilipozindua Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025. Nina imani na uwezo na weledi wa tume hii. Taarifa yao juu ya kiini cha tatizo itatuongoza kujielekeza kwenye hatua sahihi za kiutendaji na mazungumzo ya kuleta maelewano, kuimarisha usalama, amani na umoja wetu. Mwenyezi Mungu Mtukufu awasimamie na kuwaongoza.
Samia Suluhu84,686 Aufrufe • vor 9 Monaten

Salamu kwa abiria wenzangu safarini kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam.
Samia Suluhu222,147 Aufrufe • vor 2 Jahren

Ninakipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar kwa kufanya mazungumzo na kufikia maridhiano. Hii ni hatua muhimu inayozidi kuimarisha amani, umoja, utulivu na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Maridhiano si ishara ya udhaifu bali ni alama ya ukomavu wa kisiasa unaoweka mbele maslahi ya Taifa badala ya maslahi ya vyama au ya mtu binafsi. Wananchi hawahitaji vurugu wala mivutano ya kisiasa isiyoisha. Wanahitaji amani, usalama, huduma bora za kijamii, ukuaji wa fursa za kiuchumi na ajira. Ili kufanikisha hayo, serikali itaendelea kusimama imara katika kulinda usalama wa raia na mali zao, pamoja na kudumisha heshima na hadhi ya nchi yetu. Kwa pamoja, tutafakari umuhimu wa maridhiano kama yanavyohimizwa pia katika vitabu vitakatifu: Qur'ani Tukufu Sura Al-Hujurat 10: "Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu; basi patanisheni baina ya ndugu zenu na mcheni Mwenyezi Mungu, (msipuuze jambo la kupatanisha) ili mrehemewe." Biblia Takatifu – Mathayo 5:9: "Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu."
Samia Suluhu16,611 Aufrufe • vor 1 Monat
