
The Chanzo
@TheChanzo • 79,017 subscribers
We Are Bilingual Multimedia Storytellers Looking At The World From Ground Up. Una habari? WhatsApp/Telegram 0753815105
Videos

Sheikh Mwaipopo Anakingiwa Kifua na Wenye Mamlaka? Gumzo kubwa linaendelea mtandaoni kufuatia Katibu wa Baraza la Habari la Waislamu nchini Tanzania (BAHAKITA) Sheikh Said Mwaipopo kuendelea kutangaza vikosi vyake akivipa majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama. Wengi wameonesha kushtushwa zaidi baada ya Julai 04, 2026, Mwaipopo kujitokeza pamoja na vijana waliovalia kininja, akisisitiza ni watu wenye mafunzo ya kutoa mateso, mapambano na ulinzi na kushambulia. 'Kwa mujibu wa ibara ya 147 ya Katiba yetu inaanzisha Majeshi: Jeshi la Polisi Jeshi la Wananchi, pamoja na jeshi la magereza. Ukisoma pia sheria ya Jeshi la Polisi pamoja na huduma saidizi ni dhahiri shahiri kwamba jukumu la ulinzi, la usalama wa raia na mali zao litakuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi," anaeleza Wakili Maduhu William akizungumza na The Chanzo. "Sasa kama tumeanza kuruhusu watu binafsi kuwa na majukumu ya kiulinzi ambayo kwa uwazi ni ya Jeshi la Polisi, nafikiri hiyo haijakaa sawa. Kwa sababu kila mtu akiamua nchi hii sasa atoke hadharani aseme nina kikundi cha mbwa koko, nina kikundi cha nyuki, au cha chui mimi nafikiri kama taifa hatuwezi kufika," anafafanua zaidi Wakili Maduhu. Wengi wameonesha hofu wakilinganisha kikundi cha Mwaipopo na vikundi vya kigaidi kama Boko Haram, ambavyo msingi wa kuanzishwa hudai ni kutetea wananchi. "Kumbukumbu zangu zinaniambia ni mara ya pili inaweza ikawa mara ya tatu [anajitokeza] inazua mashaka zaidi inaonyesha kwamba huyu mtu ana baraka za mamlaka kwa sababu, mamlaka ambazo zinahusika na hicho anachokisema kazi anayotaka kuifanya zipo," anaeleza Dk. Muhidini Shangwe, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu. Shangwe ambaye ni mtafiti na mtaalamu wa mifumo ya uongozi anaeleza kuwa hofu kubwa ya jambo kama la Mwaipopo ni kujenga msingi wa kutokuwa na utawala wa sheria. "Nadhani mara ya kwanza viongozi Waandamizi wa polisi namkumbuka Kamanda Muliro alisema kwamba naye amepata hizo taarifa lakini anafanya uchunguzi. Kwa hiyo wakati bado anafanya uchunguzi, huyu bwana ameibuka tena mara ya pili,sasa utakuwa uchunguzi juu ya uchunguzi. Lakini hii ni kiashiria kwamba,sijui nitaiweka vipi kuonesha kwamba hana baraka za mamlaka," aliongeza. Mwaipopo amedai kuwa kikundi chake pia kinafanya majukumu ya kufuatilia na kuchunguza maeneo mbalimbali, majukumu ambayo yanaingiliana na majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama. "Hao anaowaita Mbwakoko hawajasajiliwa kama kampuni ya ulinzi ambayo sheria zetu za nchi zinataka kampuni za ulinzi zisajiliwe kwa ajili ya kutoa huduma za kiusalama. Inashangaza kwa nini mpaka leo Jeshi la Polisi halijamchukulia hatua," anaeleza Wakili Maduhu. The Chanzo ilimuandikia Waziri wa Mambo ya Ndani juu ya suala hili, bado haijapokea majibu.
The Chanzo10,393 Aufrufe • vor 2 Tagen

Utata Kiongozi wa Dini Aliyetangaza Kikosi Chake. Serikali Yaonya Juu ya Magenge Gumzo kubwa limeendelea mtandaoni kufuatia Katibu wa Baraza la Habari la Waislamu nchini Tanzania (BAHAKITA), Sheikh Said Mwaipopo kueleza kuwa ana kikosi kwa jina la Mbwa Mwitu, ambapo ameeleza kuwa kikosi hicho kimejipanga kupambana na waandamanaji, ikiwemo kuwatambua na kuwafuata majumbani kwao vinara wanaohamasisha maandamano.
The Chanzo53,416 Aufrufe • vor 15 Tagen

Serikali: Puuzeni maneno yanayosemwa, uhusiano wa Marekani na Tanzania ni imara sana
The Chanzo15,378 Aufrufe • vor 5 Tagen

Kamwaga: ACT Wazalendo Ichukue Uongozi Kututoa Kwenye Mkwamo wa Kisiasa Dar es Salaam. Mwandishi wa habari mkongwe nchini Ezekiel Kamwaga ametoa wito kwa chama cha ACT Wazalendo kuchukua uongozi kuelekea kukwamua mkwamo wa kisiasa nchini kwani chama hiko kina wanasiasa wenye uzoefu na masuala hayo. Akizungumza kwenye mkutano wa kitaifa ulioandaliwa na chama cha ACT Wazalendo juu ya mkwamo wa kijamii na kisiasa uliopo Tanzania kufuatia matukio ya Oktoba 29, Kamwaga amesema kwa sasa ni kama kila upande upo kifungoni hivyo unahitajika utayari wa kisiasa kutoka mahali ambapo Tanzania imefikia sasa.
The Chanzo96,746 Aufrufe • vor 1 Monat

Mama asimulia jinsi alivyoshuhudia kijana wake Damour Nyakairo akichukuliwa na watu saba waliofika nyumbani kwao na Landcruiser Nyeupe. Akizungumza na The Chanzo leo Mei 02, 2026, Lilian Swai ambaye ni mama mzazi wa Damour Nyakairo, ameeleza kuwa kijana wake amechukuliwa asubuhi ya leo na watu waliokataa kujitambulisha, na kumpeleka kusikofahamika. “Wameondoka naye hatujui kapelekwa wapi. Wametoka huko watu saba wakaja,mimi nashangaa watu wanakimbia mvua au wanakimbia nini? Moja kwa moja wanamfuata Damur na mimi nimekuwa hapa. Wakamshika, wawili wanamshika na mmoja akatoa pingu mfukoni akamfunga. Nikauliza kuna nini [wakasema] tutajua huko huko, nyie nani? Wakasema tutajuana huko huko,” anaeleza Lilian Swai mama wa Damour. “Kwa hiyo wakambeba watu watatu wakamshika, wakambeba wakamburuza mpaka kwenye gari. Mimi nikawa nataka kuingia na yeye huko, wananivuta wakanitoa nje.”
The Chanzo61,810 Aufrufe • vor 2 Monaten

Hofu yatanda kwa wafanyabiashara wa Coco Beach: Wadai kupewa mwezi mmoja kuondoka kumpisha mwekezaji Wakizungumza na The Chanzo leo, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kwenye fukwe za Coco wamesema baadhi ya viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni waliwaita na kuwapa taarifa ya kutakiwa kuondoka ndani ya siku 30 kupisha uwekezaji. Katika malalamiko ya wafanyabiashara hao, wameeleza pia kusikitishwa na kauli za watendaji hao kwa mfanyabiashara wa kike, kauli zenye viashiria ya kutaka rushwa ya ngono. Kufuatia malalamiko haya ya wafanyabiashara wadogo, The Chanzo inaendelea na jitihada za kuwapata halmashauri ya Manispaa ya kinondoni kutoa ufafanuzi juu ya madai ya wafanyabiashara hawa.
The Chanzo83,893 Aufrufe • vor 3 Monaten

Siku 260 Kutekwa kwa Polepole: Baada ya Mahakama, familia yagonga milango ya kimataifa Zikiwa zimetimia siku 260 toka aliyekuwa Balozi wa Tanzania Cuba, Humphrey Polepole, kutekwa na kupotea, familia yake imegonga hodi katika majukwaa ya kimataifa ikidai uwajibikaji. Akiongea katika kamati ya haki za binadamu ya Bunge la Umoja wa Ulaya, dada yake Humphrey Polepole, Bi Agness Polepole, amelisihi Bunge hilo kuhimiza uchunguzi huru wa kimataifa juu ya sakata hilo na mengine ya watu kutekwa na kupotezwa nchini Tanzania.
The Chanzo14,971 Aufrufe • vor 14 Tagen

Asimulia Wananchi Walivyowafukuza Waliomchukua Msaidizi wa Lissu: 'Walifyatua Risasi Nyingi Sana'
The Chanzo40,950 Aufrufe • vor 1 Monat

Sheikh Alhad: Tunaitaka Serikali ya Marekani iwakemee Maseneta mara moja “Uwepo wetu ni kelelezo tosha kwamba yanayosemwa na Maseneta hao ni uzushi, na ni kitu ambacho hakikubaliki, na ni uchochezi wa waziwazi. Kwa hiyo tungeitaka Serikali ya Marekani mara moja iwakemee Maseneta hao, na ikanushe wazi wazi kwamba kauli hiyo itabaki kuwa ni kauli yao binafsi. Ambayo kwetu sisi kama Watanzania imetuumiza sana, kwa sababu umoja tuliyo nao, na mapenzi tuliyo nayo kama Watanzania ni mkubwa," amesema Sheikh Mussa Salum ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT).
The Chanzo32,164 Aufrufe • vor 1 Monat

‘Imekuaje JWTZ lilikuwemo mule na nchi haijatangaza hali ya hatari?’ Luteni Jenerali Mstaafu Paul Meela ambaye pia ni Mjumbe wa Tume iliyoundwa na Rais kuchunguza matukio ya Oktoba 29 ametoa ufafanua wa hoja zilizokuwa zikiulizwa juu ya ushiriki wa JWTZ kwenye kukabiliana na matukio ya Oktoba 29, 2025 ilihali haikutangazwa hali ya hatari. Lt. Jenerali Meela ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
The Chanzo42,982 Aufrufe • vor 2 Monaten

Mbunge Asenga apendekeza TBC waandae taarifa ya habari ya taifa, vyombo vyote virushe.
The Chanzo204,470 Aufrufe • vor 1 Jahr

Mbunge Matiko apendekeza Gen-Z wa Kenya Wakamatwe "Udhalilishaji mtandaoni unafanywa na hao watu wa nje tunasema, lakini zinasambazwa na kwenye mitandao ya Kitanzania, tuko wapi? Kwa nini tunaruhusu hii? Ni udhalilishaji na unaweza kuona kwamba ni udhalilishaji kwa sababu Mama, yaani Rais wetu ni mwanamke," alieleza Mbunge Esther Matiko. "Lazima tukatae, tukiendelea kujua kwamba sisi sote ni Watoto wa mama Afrika Mashariki, mamlaka za nchi ya Tanzania na mamlaka za nchi jirani, ambapo nimeona, sijaona nchi jirani mamlaka zake zikikemea hili. Mshirikiane, mambo ya ndani ya hapa idara ya mawasiliano na kule Kenya, tuwakamate hawa Gen-Z wa kule
The Chanzo158,299 Aufrufe • vor 1 Jahr

Serikali ya Mtaa Iyunga Mbeya Yafyeka Mahindi Ya Wananchi Kuzuia Yasifiche Vibaka
The Chanzo404,642 Aufrufe • vor 3 Jahren
