
The Chanzo
@TheChanzo • 80,838 subscribers
We Are Bilingual Multimedia Storytellers Looking At The World From Ground Up. Una habari? WhatsApp/Telegram 0753815105
Videos

Waandishi wambana kwa maswali Kamanda Muliro nje ya Mahakama
The Chanzo49,703 просмотров • 7 дней назад

Mtoto aliyepigwa risasi Oktoba 29 Manzese atamani kurudi tena shule, mama awaangukia Watanzania. Unaweza kuwasiliana na mama yake kupitia 0763747599 (Happyness Julius Melea). Mama mzazi anasema kwa kipindi chote amekuwa akimuuguza binti yake mwenyewe, na hivi karibuni aliitikia wito wa kufika mbele ya Tume ya Jaji Lila baada ya Mwenyekiti wa Mtaa anaoishi kumtaka aende. Ambapo ameeleza baada ya kutoa maelezo mbele ya Tume, alifika Ofisi za Wilaya kushughulikia taratibu za kupata msamaha wa matibabu kutokana na ugumu wa maisha anaoupitia hivi sasa.
The Chanzo87,274 просмотров • 14 дней назад

Rais Samia: Kuna uhaba wa fedha Tunguu, Zanzibar- Akizungumza leo Septemba 02, 2026, Rais Samia Suluhu, ameeleza kuwa kuna uhaba wa fedha jambo linalosababisha fedha zinazo-ombwa na halmashauri mbalimbali kutokufika kama zinavyotarajiwa. Rais Samia amewaasa viongozi wa ngazi za chini kujifunga mikanda na kukata bajeti ya matumizi ya kawaida ili kufanya shughuli za maendeleo.
The Chanzo174,519 просмотров • 2 месяцев назад

'Mimi ni CCM ya Nyerere, hii sasa hivi inanipa shida kidogo' - Alute Lissu Mahojiano kamili>
The Chanzo38,743 просмотров • 17 дней назад

Wakili Jebra Kambole ameeleza sababu zilizofanya Rais wa Chama cha Mawakili kuitwa Polisi leo Oktoba 15, 2026, ambapo amefafanua kuwa Mwabukusi alihojiwa kama shahidi huku akihojiwa kuhusu kufanya harakati, na kuibuliwa madai kuwa fedha zimeingizwa kwenye akaunti ya TLS kwa ajili ya kufadhili maandamano, jambo ambalo mawakili wameeleza kushangazwa nalo.
The Chanzo54,616 просмотров • 29 дней назад

Mama awasihi ‘watekaji wa Landcruiser nyeupe’ kumrudisha mwanaye. Watekaji walivaa jezi za Simba: ‘Mrudisheni mwanangu, mpelekeni Mahakamani’ Mama wa Juma Kijazi (30), mfanyabiashara wa chips amewasihi watekaji waliomchukua mwanaye toka Oktoba 21, 2026, na kutokomea naye kumrudisha kijana wake, ambaye ndiye mtoto wake wa kwanza. "Toka tarehe 21 Oktoba mpaka leo, sijaweka hata maji mdomoni. Siwezi kujua mwanangu yupo kwenye hali gani: anakula, analala, au amekufa. Nyinyi wakina baba mliomchukua mwanangu, mrudisheni; mpelekeni hata polisi. Naombeni mnirudishie mwanangu, popote pale alipo. Mimi ndiye mama yake. Nawaombeni sana mnirudishie mwanangu," Mama huyo amewasihi watekaji. Watekaji hao ambao hawakujitambulisha walifika katika eneo lake la kazi Kinondoni Manyanya na kupaki gari lao Landcruiser nyeupe, baada ya muda walishuka na kumkamata kijana huyo akiwa anafanya usafi, pamoja na kijana mwingine waliyemuachia. Tukio hilo limeripotiwa Polisi na kusajiliwa kwa OYB|RB|7259|2026
The Chanzo25,880 просмотров • 21 дней назад

Jussa: Rais Katoka Zanzibar imekuwa nongwa "Alivyokuwa Rais wa kwao hawakuona Tanganyika imeuliwa, leo Rais katoka Zanzibar imekuwa nongwa," Ismail Jussa, Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo. Jussa alikuwa akizungumza leo Agosti 29, 2026, katika ziara ya chama hicho, katika ukumbi wa Majid Hall, Mjini Magharibi, Unguja.
The Chanzo70,867 просмотров • 2 месяцев назад

Mikoa 10 Yenye Watu Maskini Zaidi Kwa kuangalia kipato cha mtu mmoja mmoja kwa mwaka 2025: 1. Simiyu - Milioni 1.74. 2. Kagera - Milioni 1.85 3. Singida - Milioni 1.99 4. Dodoma - Milioni 2.11 5. Pwani - Milioni 2.16 6. Tabora - Milioni 2.30 7. Kigoma - Milioni 2.30 8. Katavi - Milioni 2.46 9. Rukwa - Milioni 2.88 10. Songwe - Milioni 2.94
The Chanzo20,313 просмотров • 21 дней назад

CCM Yatangaza Kumfukuza uanachama Makamu wa Rais Mstaafu, Emmanuel Nchimbi.
The Chanzo61,612 просмотров • 2 месяцев назад

'Mkipata nafasi msaidieni mke wangu',Mhadhiri UDOM anayeshitakiwa kesi ya ugaidi
The Chanzo62,662 просмотров • 3 месяцев назад

Kamwaga: ACT Wazalendo Ichukue Uongozi Kututoa Kwenye Mkwamo wa Kisiasa Dar es Salaam. Mwandishi wa habari mkongwe nchini Ezekiel Kamwaga ametoa wito kwa chama cha ACT Wazalendo kuchukua uongozi kuelekea kukwamua mkwamo wa kisiasa nchini kwani chama hiko kina wanasiasa wenye uzoefu na masuala hayo. Akizungumza kwenye mkutano wa kitaifa ulioandaliwa na chama cha ACT Wazalendo juu ya mkwamo wa kijamii na kisiasa uliopo Tanzania kufuatia matukio ya Oktoba 29, Kamwaga amesema kwa sasa ni kama kila upande upo kifungoni hivyo unahitajika utayari wa kisiasa kutoka mahali ambapo Tanzania imefikia sasa.
The Chanzo98,171 просмотров • 6 месяцев назад

Mikoa 10 Tajiri Tanzania Bara 1. Dar es Salaam - Tsh. Trilioni 39.8 2. Mwanza - Tsh. Trilioni 16.7 3. Mbeya - Tsh. Trilioni 12.9 4. Morogoro - Tsh. Trilioni 11.4 5. Arusha - Tsh. Trilioni 11.1 6. Tanga - Tsh. Trilioni 10.9 7. Geita - Trilioni 10.5 8. Kilimanjaro - Tsh. Trilioni 10.5 9. Tabora - Tsh. Trilioni 8.7 10. Mara - Tsh. Trilioni 8.6 Hii ndio mikoa 10 inayoongoza kwa utajiri hadi kufikia mwaka 2025 kwa kuangalia pato la mkoa husika kwa mujibu wa Ripoti ya BoT ya Utendaji wa Kiuchumi ya Juni 2026 (Consolidated Zonal Economic Perfomance Report for the Quarter Ending June 2026).
The Chanzo17,086 просмотров • 24 дней назад

Mzee Warioba aonesha wasiwasi kutompata Nchimbi kwenye simu, asema sio kawaida yake.
The Chanzo43,230 просмотров • 2 месяцев назад

Katambi: Madereva, Polisi wote tunahitajiana Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobasi Katambi akizungumza na madereva eneo la Kituo cha Mabasi cha Magufuli amesema kuwa kada ya madereva na askari Polisi wanahitajiana. Katambi ameyasema haya kufuatia malalamiko yaliyotolewa na madereva dhidi ya askari Polisi wa usalama barabarani ambayo ni moja ya madai katika mgomo wao waliouanza asubuhi ya leo Jumanne. Amewataka madereva walionyang'anywa leseni zao kufika ofisini kwake kwa ajili ya kushughulikia suala lao ili waweze kuendelea na kazi. Katika hatua nyingine Katambi amesitisha suala la pointi za leseni na kusisitiza kuwa mfumo wa point za leseni haujaanza kutumia bali ulikuwa kwenye hatua ya majaribio, hivy
The Chanzo26,942 просмотров • 1 месяц назад

Salum Mwalimu: Serikali ipo, CCM ina dhamira ya maridhiano, tupunguze kelele mtandaoni Akizungumza katika mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) leo Septemba 08, 2026, mwanachama wa chama cha CHAUMMA na Katibu wa zamani wa chama hicho, Salum Mwalimu ametoa wito kwa wadau Tanzania bara kufuata mfano wa maridhiano yanayoendelea Zanzibar, akisisitiza CCM na serikali ina utashi. "Kuna fursa adhimu ipo, ambao pengine ndio hatua inayotakiwa kwenda sasa, ya watu kukaa na kuzungumza na kutengeneza framework, ambayo tayari Zanzibar tumeoneshwa mfano wake. Kwa hiyo kama ile hatua ambayo wamekwenda nayo Zanzibar, na sisi tukapunguza kelele, hasa za mitandaoni, tukajikita kwenda kutafuta tiba, inawezekana," amesisitiza Mwalimu. "Utashi upo, mimi ninaamini yanayoendelea Zanzibar yanakihusisha Chama cha Mapinduzi. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ni mmoja, na leo tunaona uwakilishi mpana wa Chama Cha Mapinduzi ukidhihirisha nia na dhamira aliyonayo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Serikali ni hiyo hiyo moja, ipo, na ukweli ipo na inatambulika, inaendelea kufanya kazi. Tutaendelea kuvutana, mambo yanakwenda."
The Chanzo36,541 просмотров • 2 месяцев назад