
Twaha Mwaipaya
@Twaha_Mwaipaya • 326,505 subscribers
.Mratibu Wa Uhamasishaji Baraza la vijana wa chadema Taifa (BAVICHA) 2019-2025 Prison graduate 133 days in jail. Human rights defender.
Shorts
Videos

*TAZAMA VIDEO HAPO CHINI UONE JINSI WAJUMBE WA CCM WA SERIKALI YA MTAA WALIVYOMUUA KINYAMA MUOKOTA MAKOPO* 😭 Kaka kuna Tukio lilitokea siku ya Jumatatu Tar *28/09/2026* asubuhi maeneo ya Goba Kontena Mtaa wa Mbuyuni kuna *Wajumbe wa CCM wa Serikali ya mtaa* husika wakishirikiana na Walinzi Shirikishi walifanya Kitendo cha kinyama sana 😭walimkamata *Muokota Makopo* katika eneo la mjumbe mmoja wapo ambae anajulikana kwa jina la *Msasa*, baada ya kumkamata ndipo wajumbe wa Mtaa hao kwa kushirikiana na *Walinzi Shirikishi* wakaanza kumpiga sana. Hapo hawakutosheka ndipo wakampeleka mtoni na kumnywesha maji ya betri. Kisha wakamuua. Baada ya hapo polisi walifika na kuuchukua mwili, kiukweli kaka tunaomba tupazie sauti yani hawa Jamaa wanajiamini mpaka wanajichukulia maamuzi ya *kuua*. Goba nzima maeneo ya Kontena watu wamesikitika sana. Haki Iko wapi kaka kama Viongozi wa CCM wa SERIKALI za Mitaa wana nguvu mpaka za kuua watanzania. Muokota Makopo ameuwawa kikatili sana video hiyo hapo juu.
Twaha Mwaipaya73,071 次观看 • 28 天前

Hapa ni Mwanza leo Maeneo ya Nata, dereva wa bajaji alizuiwa na gari akiwa njiani . Watu waliokuwa kwenye gari hilo walimshusha dereva huyo kutoka kwenye bajaji yake na kumpakia ndani ya gari lao. Wananchi walioshuhudia tukio hilo walipiga kelele, Madereva bodaboda wakawafuatilia na kulisimamisha gari hilo, kisha kumtoa dereva huyo wa Bajaji ndani ya gari. Tukiamua tunaweza kukomesha uhuni wa UTEKAJI.
Twaha Mwaipaya38,681 次观看 • 15 天前

Kaka Mwaipaya habari, Kuna maiti ya Kijana wa KIUME imeokotwa ikiwa na majelaha mgongoni na shingoni, imeokotwa leo asubuhi Wilaya ya Temeke njia ya kutoka Mbagala Randi 3 kuelekea Kisemvule, Kama mtu atamtambua afike mochwari za TMK. Sasa hatuokoti pesa tunaokota maiti.
Twaha Mwaipaya70,856 次观看 • 1 个月前

TAARIFA YA KUTEKWA KWA KIJANA RAMA AU RAMSO MANZESE, ATAPELIWA KWA KISINGIZIO CHA KUFANYA MATANGAZO Kijana anayetambulika kwa jina la Rama au Ramso anadaiwa kutekwa siku ya Ijumaa jioni katika eneo la Manzese, Dar es Salaam, baada ya kuitwa kwa kisingizio cha kufanya matangazo ya duka la nguo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, kijana huyo alipigiwa simu na mtu aliyemweleza kuwa amefungua duka la nguo eneo la Manzese na alihitaji amfanyie matangazo matatu, kwa malipo ya shilingi 100,000. Inadaiwa kuwa majira ya mchana, mtu huyo alifika kwa kutumia pikipiki na kumchukua kijana huyo. Hata hivyo, Rama au Ramso hakuwa peke yake, kwani aliambatana na rafiki yake. Walipofika eneo la Manzese, inadaiwa walikuta gari lililokuwa limeegeshwa katika kichochoro. Watu kadhaa waliteremka kutoka kwenye gari hilo na kuanza kumpiga kijana huyo kabla ya kuondoka naye kwa nguvu. Rafiki yake aliachwa eneo la tukio na hakuchukuliwa pamoja naye. Baadaye, rafiki huyo alirudi walikokuwa wakifanyia kazi na kutoa taarifa kuhusu tukio hilo. HADI SASA, HAKUNA TAARIFA ZAIDI ZILIZOTHIBITISHWA KUHUSU ALIKO KIJANA HUYO. Tukio hili linaibua maswali kuhusu usalama wa raia na linahitaji uchunguzi wa kina ili kubaini kilichotokea, waliohusika na mahali alipo kijana huyo. TUSAIDIANE KUPAZA SAUTI. RAMA AU RAMSO YUKO WAPI?
Twaha Mwaipaya22,001 次观看 • 16 天前

MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISSU *LISSU:* Sasa naomba nimalizie. *JAJI NDUNGURU:* Je, ni sehemu ya submission? *LISSU:* Ni sehemu ya submission, wala si maneno mabaya. Ni hivi, Waheshimiwa Majaji, kesi ya uhaini ni kesi ngumu sana. Ukiachilia mbali siasa zake, ambazo pressure zake ndizo zinafanya kesi kuwa ngumu. Pamoja na kesi kuwa ngumu, nyinyi Majaji mmefanya kazi nzuri sana. Mmetusikiliza, mmetupa nafasi ya kujitetea. Hamjanikwaza. Mmekuwa wavumilivu sana. Mmefanya kazi kubwa sana na mmefanya kazi nzuri sana. Nilitaka nisimalize bila kusema haya, pengine hatutakutana tena. Nilitaka mjue kuwa moyoni mwangu mmefanya kazi nzuri. Hawa mawakili wangu wa Serikali na wao wamefanya kazi nzuri. Wamepambana sana mpaka kufika hapa. Pamoja wamekuwa na kesi ya ovyo sana. Ila wamepambana sana bila kujali nini kitatokea, wamepambana sana. Nafikiri nawatakieni heri sana. Asanteni sana. Haya ndiyo nilitaka yaingie katika rekodi. Nafikiri msipoyaingiza katika rekodi, mtanikwaza.
Twaha Mwaipaya33,697 次观看 • 1 个月前

HAPA NI NJE YA KITUO CHA AFYA CHA KIAGARA MUDA HUU ASKARI WAMEUA WATU WANNE MPAKA SASA. Muda huu, Wilaya ya Mleba, Mkoa wa Kagera, polisi wa maliasili wanadaiwa kuwaua vijana wanne wa bodaboda kwa kuwapiga risasi. Vijana hao walikuwa wamebeba mkaa. Hali imekuwa mbaya, wananchi wamepasua gari la maliasili na kuwafukuza maafisa hao. Kwa sasa, miili ya marehemu ipo katika Kituo cha Afya Kaigara. Nipo sehemu ya tukio, lakini maaskari hawaturuhusu kurekodi. Tukio hili limetokea Mleba Mjini.
Twaha Mwaipaya13,412 次观看 • 11 天前

MADEREVA WAMEWAZUIA WATALII KUENDELEA NA SAFARI ILI WAJUE TANZANIA KUNA UKANDAMIZAJI WA HAKI ZA NINADAMU. Madereva wa Malori na MABASI wanapinga mfumo wa “points”, wakitaka suala hilo kufanyiwa marekebisho kabla ya kurejea kazini. Mabasi mengi yamesimama, huku abiria waliokuwa wakitarajia kusafiri kwenda mikoa mbalimbali wakilazimika kusubiri.
Twaha Mwaipaya24,617 次观看 • 29 天前

HAPA NI MSWISWI NJIA YA MBEYA POLISI AMETAKA KUPIGWA VIBAO. Madereva wa Malori na MABASI wanapinga mfumo wa “points”, wakitaka suala hilo kufanyiwa marekebisho kabla ya kurejea kazini. Mabasi mengi yamesimama, huku abiria waliokuwa wakitarajia kusafiri kwenda mikoa mbalimbali wakilazimika kusubiri.
Twaha Mwaipaya24,383 次观看 • 29 天前

TUNDUMA KIMEWAKA MBAYA MADEREVA WAMEKATAA UNYONGE. Madereva wa Malori na MABASI wanapinga mfumo wa “points”, wakitaka suala hilo kufanyiwa marekebisho kabla ya kurejea kazini. Mabasi mengi yamesimama, huku abiria waliokuwa wakitarajia kusafiri kwenda mikoa mbalimbali wakilazimika kusubiri.
Twaha Mwaipaya17,341 次观看 • 29 天前