
Ummy Mwalimu
@ummymwalimu • 951,835 subscribers
Public Health, Governance & Child Rights Advocate | Former Minister of Health, Tanzania Jan 2022 to Aug 2024 & 2015 to 2020; PO-RALG 2021 | 🇹🇿MP 2010 - 2025
Videos

Tunamshukuru sana mdau huyu! Ni kweli wapo madaktari wengi na wataalam wengine wa afya wazuri, wanaojituma na kuwajibika mno katika Hospitali zetu za umma. Tunapaswa kuwatia moyo. Hakika ujumbe huu unatia moyo na kujenga ari ya kujituma kwa madaktari wetu. Tunakushukuru sana. Hii ndio sekta ya Afya tunayopambana kuijenga awamu hii ya Rais mwenye maono Dkt Samia Suluhu ambapo kipaumbele chetu ni #UboraWaHuduma tukiweka mkazo kwenye 1. Weledi, Maadili na Kujituma kwa Wataalam 2. Upatikanaji wa Huduma kwa wakati 3. Urahisi wa Rufaa inapolazimika 4. Gharama Zinazohimilika 5. Huduma bora kwa wateja ikiwemo lugha nzuri na ya upendo kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa. Kipekee, ninawapongeza wataalamu wote waliohusika kuhudumia wagonjwa siku hii ktk Hospitali ya Mwananyamala na Taasisi ya Mifupa MOI hadi kuvutia mrejesho chanya kutoka kwa jamii. Asanteni sana sana sana. Mungu awabariki taasisiyamifupa_MOI #MwananyamalaRRH #HRMMwananyamala
Ummy Mwalimu72,513 просмотров • 2 лет назад

Kazi ni moja tu kutafuta ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika mitaa yote 181 ya Jimbo la #TangaMjini
Ummy Mwalimu31,417 просмотров • 1 год назад

Alhamdulillah, Alhamdullilah Alhamdullilah. Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehma. Nashukuru sana Mh Rais kwa kutambua kamchango kangu ktk ujenzi wa Hospitali hii na uboreshaji wa huduma za afya nchini Katika utendaji wangu Serikalini, niliongozwa na maono yako, utashi na nia yako njema ya kuleta mageuzi kwenye nchi yetu, bila kusahau chachu inayokusukuma kila uchwao ya kutaka Huduma bora kwa watanzania ndivyo vimefanya haya yote kutokea hata kwa sisi tuliokuwa wasaidizi wako. Asante sana Mkuu. Nakuombea kwa Allah akupe afya njema na uzima ili kuendeleza kazi yako nzuri na kubwa kwa watanzania.
Ummy Mwalimu23,972 просмотров • 1 год назад

Sheria, Kanuni, Maadili na Viapo vya Watoa huduma za Afya ziheshimiwe. #MaishaYaWatuKwanza
Ummy Mwalimu32,977 просмотров • 2 лет назад

#NasahaZaOdoUmmy #AfyaNiUtajiri - Yatupasa kila mmoja wetu katika kupigania maisha yetu ya kila siku tuweke kipaumbele cha juu katika kulinda Afya zetu kwani AFYA NI MTAJI; AFYA NI UTAJIRI. Pigania utajiri wa Afya then ndio upiganie utajiri wa mali. Hivi sasa, nchi yetu inakabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wenye MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA (MYA) kwa kizungu "Non Communicable Diseases (NCDs)". Magonjwa haya sasa yameongezeka kwa mara 5 hadi 9 zaidi kati ya miaka ya 80 na sasa. Miaka ya 80 ni asilimia moja (1%) tu ya Watanzania walikua na tatizo la Kisukari na asilimia 5 (5%) tu ndio walikua na tatizo la Shinikizo la Juu la Damu. Hivi sasa watu wenye kisukari nchini ni asilimia 9 (9%) na Shinikizo la Damu ni asilimia 25 (25%)! Magonjwa haya yanatumia gharama kubwa kuyatibu sambamba pia na kusababisha ulemavu wa kudumu na vifo. Katika kila vifo 3 nchini, kifo kimoja kinasababishwa na magonjwa yasiyo ya kuambikiza. Magonjwa haya ni pamoja na:- 1. Shinikizo la Juu la Damu 2. Kisukari Shinikizo la juu la Damu na Kisukari ndio kwa zaidi ya asilimia 70 husababisha mtu kupata magonjwa mengine yasiyoambukiza ambayo ni;- 3. Ugonjwa wa Moyo 4. Ugonjwa sugu ya figo (chronic kidney disease) na 5. Kiharusi (stroke) Magonjwa mengine yasiyoambukiza ni;- 6. Saratani 7. Sikoseli 8. Magonjwa ya Afya ya akili Unaweza kuzuia kupata magonjwa yasiyoambukiza. Vilevile endapo umeshapata magonjwa haya unaweza kuyadhibiti na kuishi maisha bora. Mambo makubwa ya kuzingatia ili Kuzuia na Kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na;- 1. Kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa ikiwemo kula mbogamboga na matunda kwa wingi; kupunguza matumizi ya sukari, chumvi na mafuta mengi. 2. Kufanya mazoezi ya mwili au kuushughulisha mwili angalau mara 3 kwa wiki kwa muda usiopungua dakika 30. Hata hivyo wataalam wanashauri ili kupata matokeo mazuri zaidi muda ya mazoezi uwe angalau dakika 150 kwa wiki yaani dakika 30 mara 5 kwa wiki; au dakika 40 mara 4 kwa wiki au dakika 50 mara 3 kwa wiki. 3. Punguza unywaji wa Pombe kupita kiasi. Mwisho, nisisitize wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara hasa kupima Shinikizo la Damu, Sukari pamoja na Uzito. Aidha ninawahimiza wananchi kupima saratani ikiwemo saratani ya matiti, saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya tezi dume. Ugonjwa ukigundulika mapema ni rahisi kuutibu. #MtuNiAfya #JuaNambaZako #KingaNiBorakulikoTiba #NasahaZaOdoUmmy
Ummy Mwalimu13,311 просмотров • 2 лет назад
Больше нет контента для загрузки