
Veriafya
@Veriafya • 15,323 subscribers
Taarifa sahihi za afya bila upotoshaji! Fanya kazi nasi: 🗨️ DM Email: [email protected]
Videos

🚨‼️SAKATA LA MADAKTARI 7 KUFUKUZWA NA KUPEWA KAZI YA KUZUNGUKA NA GARI LA KUZOA TAKA MTAANI Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kimepokea kwa masikitiko makubwa video mjongeo yenye maudhui ya udhalilishaji wa taaluma ya udaktari, uvujishaji wa taarifa za kiutendaji, matumizi mabaya ya madaraka, unyanyasaji wa watumishi na ukiukaji wa misingi ya utumishi wa umma ya wazi. Video hiyo inamhusisha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Mafinga. Aidha, taarifa zinazoonekana katika kanzi data rasmi ya usajili na leseni za madaktari zinaonyesha kuwa Mganga Mfawidhi mhusika hana leseni halali ya udaktari kwa mwaka 2026/2027 ambalo pia ni kosa kisheria. MAT inazitaka mamlaka husika kuthibitisha taarifa hizi na kuchukua hatua za haraka kwa mujibu wa sheria na taratibu. MAT tayari imewasilisha taarifa rasmi katika ngazi za juu za Wizara ya Afya, ikiomba hatua za haraka zichukuliwe , pale ambapo ukiukwaji utathibitika, hatua stahiki za kinidhamu na kisheria zichukuliwe ili kurejesha morali ya madaktari nchini. MAT itaendelea kufuatilia suala hili kwa karibu kwa lengo la kulinda heshima ya taaluma ya udaktari, utu wa watumishi na kurejesha imani ya madaktari katika mifumo ya uwajibikaji ndani ya Serikali.
Veriafya11,374 görüntüleme • 2 ay önce

Ushauri huu ulitolewa na Dkt. Edward Machage, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto kupitia TBC Online Video: TBC Online
Veriafya21,355 görüntüleme • 5 ay önce

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma aliyasema haya Mei 14, 2024 akichangia mojawapo ya Mijadala Bungeni ambapo alimshauri Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi aone namna njema ya kutoa mafunzo yake ya elimu ya afya kwani baadhi ya watu wanatoka vijijini ambapo kazi hazifanani na wale wanaokaa mijini, akitolea mfano wa Majiji ya Dar es Salaam na Arusha. Nini maoni yako?
Veriafya10,105 görüntüleme • 6 ay önce
Daha fazla içerik yok.