
Yericko Nyerere
@YerickoNyerereT • 256,016 subscribers
9 Awards-Winning Back to Back Best AUTHOR of the Year AFRICA 2023/2024/2025/2026 | Intelligence and Security Analyst |MNA CHAUMMA Party| CEO YECCO GROUP LTD
Shorts
Videos

Leo nimesikiliza hotuba ya Rais yenye Mamlaka kamili, Hotuba ya Rais wa Nchi Huru, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama. Pamoja na mapungufu kwenye maeneo kadhaa hasa mfano kushambulia kwa nguvu kubwa wale wanatajwa ni wachochezi wa ndani, badala yake kwa maoni yangu ilitakiwa wahubiriwe kwa lugha ya Mfariji Mkuu (Comforter in Chief), lugha ambayo Yesu na Mtume Mohamed waliitumia dhidi ya watu wema na wahalifu wa enzi hizo waliopinga kazi yao dunia, nimemuona rais kachukia sana, yes lazima achukie mbele ya washenzi wa taifa letu, ndivyo inavyotakiwa kwa taifa lenye nguvu ya kulinda uhuru wake! Lakini kwa kiasi kikubwa imekuwa hotuba thabit ya mkuu wa nchi halisi, Binafsi kwa miaka mingi nilikuwa sijaliona taifa langu likitetea ukuu wake kwamtindo wa hotuba ya Mkuu wa Nchi yenye ladha njema kama leo. Imenikumbusha hotuba ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 23 Januari 1967. Akizionya Ureno, Uingereza na Marekani. Pia imenikumbusha Rais Nyerere alipovunja uhusiano wake na Uingereza kwakumfukuza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania. Imenikubusha Rais Nyerere alipopinga ubaguzi wa Raingi kwasusia shughuli zote za kimataifa zilizoihusisha Afrika Kusini ya Makaburu hadi kufika kuzuia timu zetu za taifa kutoshiriki michuano ya Olimpiki. Na mwisho imenikumbusha hotuba ya Rais Mkapa mwaka 2001 alipopinga kwa nguvu zote shinikizo la mabeberu waliotaka kuingilia mgogoro wa ndani uliotokana na mauaji ya zanzibar na mwembechai yaliyotokana na CUF kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2000. Rais Samia amegusa vitu vingi muhimu sana ambavyo nimekuwa nikivisema tangu mwanzo, Na vingine tulivisema huko nyuma kabisa ndani ya vyama vya siasa, ikatafsirika kuwa ni propaganda. Vitu hivyo ni: 1. Amesema kuwa tukio la 29 oktoba lilikuwa jaribio la mapinduzi. Hili nilishalisema tangu siku moja baada ya jaribio lile na ndio msimamo wangu leo na kesho na historia itaandikwa hivyo! Hakukuwa na maandamano! 2. Amesema waandaaji wa uhalifu huu ni mabeberu wanaopigana vita vya kiuchumi kuzisaka raslimali zetu na ustawi wetu. Hili nilishalisema tangu siku moja baada ya jaribio lile na ndio msimamo wangu leo na kesho na historia itaandikwa hivyo! 3. Amesema vijana wengi walilipwa kuhamasisha na kufanya uhalifu huu. Hili nilishasema na kuweka ushahidi wa taasisi zilizowalipa ikiwemo taasisi ya Ford Foundation ya Marekani ambayo imemlipa Maria Sarungi kupitia taasisi yake inayoitwa Change Tanzania iliyopokea zaidi ya bilioni 10 katika kipindi kifupi cha miezi 10 tu hivi, Zingatia taasi ya Maria imesajiliwa Tanzania inatakiwa kufanya kazi zake Tanzania, lakini kwa miaka zaidi ya mitano Maria hayupo Tanzania, na taasisi haifanyi kazi zake lakini inapokea mabilioni, nakuwalipa vijana makumi kwa mamia nchini na wengine amewatoroshea Nairobi huko sasahivi. 4. Rais ameweka ukweli rasmi na kufuta propaganda ya muda mrefu iliyoenezwa na Tundu Lissu kipindi cha uchaguzi wa Chademw kwamba Mbowe amelambishwa asali. Rais amesema kuwa Lissu ndie alimpatia pesa alipokwenda kumuona Ubelgiji tena Rais alitoa pesa yake ya safari, Rais hajaishia hapo, amesema Lissu na Wenzake waliporudi Tanzania kwaamana ya Gobless Lema nk aliwapa pesa ya kujikimu. Na mwisho wakaanza kumtukana Rais huyuhuyu! Si mimi nasema, bali Rais Samia kasema yeye kwa kinywa chake! Hili jambo la Lissu kulambishwa asali mimi binafsi nilisema kipindi cha kampeni kwamba ninazo taarifa sahihi Lissu amepewa pesa, na kama nimsafi kweli mbona hajatangaza hadharani hiyo pesa aliyopewa pale Ubelgiji? Bahati mbaya tayari wanaharakati uchwara walikuwa washavamia na kuteka chama hivyo hawakusikia wala kuelewa sauti yoyote nje ya Lissu ambae alijimilikisha usafi wa moyo na mwili na akajimilikisha ukweli na haki ya nchi hii. Lakini sisi tunaomjua kuwa ni muongo na mlamba asali mkubwa, wala hatukuwashangaa, tuliacha ungo upande lifti, na sasa tunafurahi kuona ukweli umefika kwa njia ya ngazi. Rais wa nchi kafunga mjadala wa Uzushi ulioenezwa na Lissu na
Yericko Nyerere64,213 views • 6 months ago

Jela sio sehemu salama, hakuna aliyekaa jela akabaki na msimamo wake uleule, Nampongeza Lissu kwakubadili msimamo wake na kuomba sasa maridhiano ya mezani, Ukikomaa utafia jela ndugu….. Waulize wapinzani wengine Afrika kilichowakuta. Yuko mtu kwasababu ya uelewa mdogo anaamini kuwa Marekani na Ulaya watakuja kumtoa Lissu pale Ukonga au watakuja kuitoa CCM madarakani na Lissu awe Rais. Hizo ni ndoto za chizi na kuota ndoto kwa kiumbe cha Mwenyezi Mungu sio dhambi…. Ulaya na Marekani wanaangalia maslahi yao, Vyovyote ccm na samia watakachowafanyia watz ilimradi maslahi ya Ulaya na Marekani hayaguswi basi sahauni ndoto zenu, mtaishia kupokea barua za matamko ya kulaani na kusisitiza amani na demokrasia tu. Nakujueni mnavichwa vigumu mtakomaza mafuvu yenu kubisha… Tulishauri tangu mwanzo kwamba tufanye siasa za maridhiano, tukawaambia kuwa hii ni kesi ya kisiasa, Siasa ndio imemweka jela Lissu, na Siasa ndio itamtoa jela Lissu, kwa lugha rahisi ni kwamba Lissu lindie kafanya Lissu aende jela, na Lissu ndie atafanya Lissu atoke jela. Kwakibri na jeuri ya umamuma wetu mlitutusi mkatuita wasaliti. Bahati nzuri Lissu akili imemjia kalitambua hili japo kwakuchelewa sana, Tumpongeze na tumtie moyo… karibuni kwenye siasa za kistaarabu za maridhiano kwa maslahi ya Tanzania yetu. Ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba Mahakama iachwe ifanye kazi yake na haki ipatikane, Lissu atatukuta mbele tukiendelea na vikao vya maridhiano au atakuta nchi ilisharidhiana inaendelea vizuri na atafaidi matunda ya maridhiano. Na Yericko Nyerere
Yericko Nyerere21,792 views • 1 month ago

Kwamara ya kwanza kwenye jukwaa la kimataifa, Nimeiona ladha ya sauti ya ki-nchi ambayo kwahakika niliona mwaka kati ya 1994-95 ikitoka kwa Hayati Mwalimu Nyerere wakati wa Mandela akitwaa madaraka. Leo nimemuona na kumsikia tulia.ackson Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Tanzania. Yes nimefurahishwa na majibu yake, amejibu kwa kutulia na kwa tone ya mamlaka mbele ya Wahafidhina wa Magharibi ambao bado akili zao zinaamini Afrika ni Koloni lao. Kauli hii ya Dkt. Tulia Ackson, ameitoa akifungua Mkutano Mkuu wa 149 wa IPU uliofanyika Geneva, Uswisi ambapo amewasisitiza Wajumbe wa Bunge hilo kumuamini na kumpa nafasi afanye kazi yake na waache kufikiria dhana ya Ukoloni kwa wanaofikiria hivyo ikiwemo kupinga kila kitu kwakuwa anatokea Tanzania au Afrika. Dkt. Tulia ameyasema hayo baada ya baadhi ya Wajumbe kukosoa uamuzi wake wa kufanya ziara Nchini Urusi na kukutana na Rais Vladimir Putin kuhusu vita ya Ukraine badala ya kwenda Gaza, Lakini ukifatilia Wajumbe waliokosoa wengi wanaonekana wako nje ya dunia mpya hata hawajui taarifa na ratiba za IPU kwani ni wazi Dkt. Tulia alipochaguliwa tu November mwaka jana 2023 alienda Israel na Palestine na kuonana na Viongozi wa pande zote, Wajumbe wa IPU kwa sehemu kubwa wamejazwa propaganda za ubaya wa Urusi wameshindwa hata kujua ratiba za viongozi wao. Katika maelezo ya majibu ya Tulia amesema hajachagua upande kwenye migogoro yote na kwamba IPU inapambana kurejesha amani kwenye migogoro hiyo. Wajumbe wa mkutano huu ni 1,500 wakiwemo Maspika, Naibu Maspika, Wakuu wa Misafara na Wabunge. Nafikiri sasa mmejua kwanini niliamua kuupinga Ushoga na Usagaji na kuamua kuunga mkono Urusi katika oparesheni yake Ukraine nikiamini ilikuwa imechokozwa vya kutosha na Magharibi wakiongozwa na Marekani, Chaguo kuu lilikuwa ni oparesheni hiyo ambayo sasa imerejesha heshima ya mrengo wa kushoto na kulia Duniani. Dunia pamekuwa na Adabu sio kama zamani rimonti kukaa Washington. Katika tafakuri, Kuna funzo na hoja kuu mbili zinaibuka hapa, (1)Kwanza Tulia ameona kwa macho demokrasia ya kupingwa na kujibu hoja ambapo aina hii ya maongozi yeye hajaizoea, kwakuwa ni muumini wa udikteta aliyezaliwa katika mikono ya kidikteta. (2)Pili hoja ya leo kule Ulaya kwa namna ilivyojibiwa, inaibua mjadala mpya kwamba mfumo wa chama cha Mapinduzi ambacho kimantiki mimi huwa nakataa kwakusema hiki sio chama cha siasa bali ni umoja wa vyombo vya dola yaani TISS, JWTZ, Polisi, Magereza, Uhamiaji Takukuru na TRA, Kwamba mjadala muhimu ni kuwa mfumo huu ni kandamizi na hatari sana, hauruhusu watu kutumia akili yao yote isipokuwa akili kidogo sana sawa na ile ya kutenganishia mboga na ugali tu, kipimo ni Tulia leo na kisha rejea nyuma umuone tulia wa Lumumba. Na Yericko Nyerere
Yericko Nyerere92,802 views • 1 year ago

Ukimsikiliza Lema unapata jibu kuwa ccm wameingilia uchaguzi na wako na mgombea Lissu, Lema anajenga hoja na kuitangazia Dunia kuwa Tundu Lissu akishinda atamteua Dr Slaa mwanachama hai na halali wa CCM kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Lema anayatamka haya hadharani kwakuwa ndio mipango yao halisi na pia Watamrejesha Msigwa, Mwambe, Mashinji na wanaccm wengine waliotoka CDM. Jiulizeni kama Dr Slaa mtu aliyekikimbia chama katikati ya uchaguzi akajiunga ccm akapiga kampeni Chadema isishinde kisha akazawadiwa Ubalozi kwa miaka 7 wanamrudisha ndani ya Chadema tenda anaingia moja kwa moja Kamati Kuu, watashindwa kuwarudisha wabunge wa CCM wale COVID 19? Wajumbe wa Mkutano Mkuu msikubali chama chenu kiingie mikononi kwa ccm. Dola iko kazini kukiua chama kupitia hawa akina Lema, Msigwa nk
Yericko Nyerere74,949 views • 1 year ago

Lipo la kujifunza katika hili, Moyo wangu unavuja damu!😭😭😭😭 Hivi Simba hamjifunzi chochote hapa? Ok OFA MAALUMU 1. Kitabu cha UJASUSI kwa 30,000 tu badala ya bei halisi ya 80,000/=. 2. Kitabu cha “MOSCOW: Oparesheni Ukraine” kwa bei halisi ya 150,000 Contact 0755865544
Yericko Nyerere66,991 views • 1 year ago

Kama bado kuna mwanachama au kiongozi wa chadema hajastuka hii hali na kuchukua hatua kunusuru basi huyo mwanachama/kiongozi ndie tatizo kwenye chama chetu…. Naendelea kushauri viongozi wa chama taifa wachukue hatua mwenendo huu si sawa! Msilewe kwa kuona mikutano inajaa watu, Watanzania ndivyo walivyo hata Mwamposa huwa anajaza watu, Hata Gwajima huwa anajaza watu, Hata Diamond huwa anajaza watu, Hata simba na yanga huwa zinajaza watu, Chama ni mtandao wa Uongozi. Mtandao ukifa ni vigumu kuwa na chama. Hata leo Lipumba au Mbatia ukiwapa pesa ya mkutano na maandalizi yote watajaza watu hadi wakanyagane. Watanzania sio wachoyo linapokuja suala la mtu anayeisema ccm au anayefanya miujiza ya kiroho au anayewaburudisha kwa muziki au kwa soka! Sekretarieti yote iliyokuwepo kwenye uongozi uliopita imeondoka Chadema isipo kuwa watu wawili tu Mnyika na Pambalu. Viongozi wa Kanda 8 zote za Tanzania Bara wamejiondoa Uongozi Mzima wa Mkoa Kilimanjaro kuanzia matawi, Kata, Majimbo, Wilaya na Mkoa umejiondoa, Uongozi wote wa Mkoa wa Temeke wamejiondoa. Leo uongozi wa Mkoa Tabora umeondoka. Hatustuki? Bado tunafanya propaganda kwamba hao wanaoondoka kwakuwa wamekosa vyeo ndani ya chama? Tuache uongo na kukomaza mafuvu, kuna tatizo! Hebu tukubaliane na ukweli kuwa sisi ni chama cha kidemokrasia tumekoseana turudi mezani tuyajenge. Enyi viongozi wangu, nani amewewafanya kuwa na mioyo migumu kama farao? Mimi naona mbele kuna giza!!! OFA YA PAPA MPYA INAISHA LEO. Pata Kitabu cha UJASUSI kwa 25,000 tu badala ya bei halisi ya 80,000/=. Lipia kwa: Lipa Tigo 7489022 Lipa Voda 5352627 M-Pesa. 0755865544 TIGOPESA 0715865544 CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE). Kwa Dar ni free delivery Nje ya Dar nauli 8,000/=
Yericko Nyerere55,196 views • 1 year ago

Jasusi hatari nyuma ya NGO nchini Burkina Faso. Jasusi Joe Bassey kutoka Perrot Island nchini Cana ameachia nyaraka za siri zinazofichua kwamba Bi Claire Dubois, mwanamke Mfaransa katika miaka 30 iliyopita aliwasili Burkina Faso akijifanya kama mkurugenzi wa NGO ya Magharibi iitwayo Hope Forward, ambayo shughuli zake kuu ilikuwa ni kusaidia elimu ya wasichana na afya ya wanawake. Bi Claire alijionyesha kama mwanamisaada ya kiutu aliyelenga kusaidia wanawake wa Kiafrika, akitembelea vijiji, shule, na masoko, na kutumia muda mwingi kusifu uongozi wa Burkina Faso kwenye televisheni ya serikali. Walakini, nyuma ya shuguuli hii ya kibinadamu, Bi Dubois alikuwa akijishughulisha na ujasusi. Alikuwa akikusanya taarifa za kijasusi kwenye tovuti za kijeshi, ikiwa ni pamoja na vituo vya mafunzo ya kijeshi, vituo vya mafuta, na vituo vya uongozaji wa ndege zisizo na rubani, akitumia kivuli cha kazi ya kibinadamu. Katika kazi zake zilizoonekana ni za kiraia lakini alibeba simu mbili-moja ya kiraia na ya pili ni simu maalumu kwa mawasiliano kijasusu na aliitumia kutuma barua pepe zilizowekwa katika mfumo wa ulinzi imara ambazo ni ramani zilizochakatwa vizuri na picha za setilaiti za maeneo nyeti ya kijeshi, kwenda kwa watu wa NATO na majasusi wemgine wa kigeni. Shirika la ujasusi la Burkina Faso kwa msaada wa Shirika la Ujasusi la Urusi FSB tayari lilikuwa limetilia shaka shughuli Mama huyu na kufuatilia mawasiliano yake kwa ukaribu sana hasa kuingilia mawasiliano ya simu yake ambayo ilikuwa ikitumia Setelaiti. Baads ya kujiridhisha kwamba Bi Claire anafanya shughuli za kijasusi kweli, Walifanikiwa kuzuia nyaraka hizo zisiwe zinawafikia Nato na washirika kwakuwa tayari mawasiliano hayo ya Bi Claire walikuwa wameyaingilia kila akituma email zilikuwa zinaingia Moscow sio Brusels tena. Rais Ibrahim Traoré aliwaamuru majasusi wake wamwache aendelee kukusanya nyaraka za misheni yake ili wamkamate akiwa na ushahidi halisi. Na baada ya miezi kadhaa, Hatimaye, alikamatwa na kuwekwa hadharani katika Kongamano la Kitaifa la Mamlaka ya Afrika, ambapo rais aliwasilisha nyaraka zake za siri na barua pepe zote moja kwa moja jukwaani, akifichua shughuli zake za kijasusi kwa ulimwengu. Na baadaye akazuiliwa kimya kimya na serikali licha ya shinikizo la nchi za magharibi kwakutumia mgongo wa azimio la kidiplomasia, Rais Traoré alisisitiza juu ya uwazi na haki, akisisitiza usaliti wa kuaminika ni adui wa Bukinafaso. Swali la kujiuliza, ni mashirika mangapi ya kigeni yako nchini na yanafanya shughuli wazosema watafanya bila kuwa na agenda nyingine? Wanafuatliwa kwa kiwango gani? Jibu lipo Lumumba! Na Yericko Nyerere PATA OFA YA PAPA MPYA WA ROMA Pata Kitabu cha UJASUSI kwa 25,000 tu badala ya bei halisi ya 80,000/=. Lipia kwa: Lipa Tigo 7489022 Lipa Voda 5352627 M-Pesa. 0755865544 TIGOPESA 0715865544 CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE). Kwa Dar ni free delivery Nje ya Dar nauli 8,000/=
Yericko Nyerere52,293 views • 1 year ago

Nilipoeleza katika Makala kuu kwamba Lissu hana sifa za kuwa Mwemyekiti wa Chadema Taifa kwasababu ni MUONGO, wengi mlipinga na natusi juu, Niliorodhesha uongo wake mwingi ikiwemo Uzushi wake juu ya kinachoitwa Mabilioni ya Abdul…. Sasa Jana akiwa Maria Space alimtuhumu na kumzuishia Mwenyekiti wa @chadematzofficial Mh Freeman Mbowe kwamba ajiamulia yeye binafsi kumwalika Mh Rais Samia kwenye kongamano la BAWACHA na kutoa tuzo! Sasa ushahidi mwingine wa UONGO wa Lissu ni katika Video Sauti akisikika akimsifu Rais na uamuzi wa chama kumwalika katika kongamano hilo! Hii ikithibitisha kuwa Lissu alishiriki kumwalika Rais kwenye Kongamano hilo Kwa namna Lissu alivyokidhalilisha chama huko nyuma na jana akikituhumu chama na viongozi wake kwa mambo mbalimbali, akitoa siri za kamati kuu na kukibagaza chama vilivyo, Nadiriki kusema, Lissu anakosa sifa hata ya kuwa mwanachama tu wa Chadema, Kama kamati ya uchaguzi itafuata kanuni za uchaguzi, Basi Lissu anatakiwa kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hiki kwakuwa amevunja maadili na kanuni za uchaguzi! Kamati kuu ya chama ina kiapo cha Wajumbe kuhakikisha wanalinda siri za chama na haitatokea mjumbe wa aina yoyote kutoa au kuzungumza mambo yaliyojadiliwa katika kamati kuu. Lakini jana Lissu kayamwaga yote hadharani jambo ambalo sio utaratibu wa vyama vyote vya siasa duniani! Inashangaza kuona leo Lissu anakanusha hata yale ambayo alishiriki kuyaamua na kuyasifia kama mambo mema. Huyu ni muongo, mnafiki, mzandiki na mtu asiye na heshimu kwa wengine. Anawatungia uzushi wenzake kwa mambo ambayo nae ni sehemu ya maamuzi, bila kujali anakiumiza chama Kwa kiasi gani, ilimradi yeye aonekane wa tofauti. Kiongozi asiye mkweli, asiye heshimu wenzake katika nia moja anapoteza sifa za kuaminika kukabidhiwa Taasisi kubwa na nyeti kama CHADEMA. Kwanamna yoyote Lissu Hafai kuwa Mwenyekiti wa Chama chetu na hafai kuwa Mwanachadema! Nasisiti kushauri Kamati kuu ikutane kumjadili na kumwajibisha kiongozi huyu aliyekosa maadili ya kichama! Na Yericko Nyerere
Yericko Nyerere63,981 views • 1 year ago

TBT: 2023: Niliandika hivi: “Tusipo mheshimu Prof wa Siasa Mh Freeman Mbowe katika matokeo yaliyotokea leo kwa Rais wa Tanzania Mh @samia_suluhu_hassan kutengua katazo haramu la mikutano ya vyama vya siasa, Basi tutakuwa na mapungufu makubwa vichwani mwetu. Wale waliomshambulia Mh Freeman Mbowe kwa hatua yake ya kuongoza maridhiano wanajisikiaje? Basi tuwasamehe na Tujifunze kuwa watulivu na wavumilivu katika siasa, Prof wa siasa Mh Mbowe anaiona kesho yetu kuliko sisi tufikiriavyo. Hongera Rais Samia Suluhu kwakutengua katazo kharamu la mikutano Wako watu ndani mwetu na nje yetu ambao walipinga hatua ya Mbowe kuongoza maridhiano, Leo wote tunafurahia matunda ya Maridhiano haya hatua ya awali kuelekea hatua kubwa ya kupata Katiba Mpya”. ——————- NB: Leo 2026 Mimi Yericko Nyerere, naunga mkono hatua ya Rais Samia kufungua tena milango ya maridhiano baada ya kilio chetu cha muda mrefu kuitaka serikali ifungue milango ya mazungumzo kutafuta utengamano wa kitaifa uliovurugika kwa miaka miwili iliyopita na hadi kufikia jaribio la mapinduzi la 29/12/2025 lililopelekea maafa makubwa ya mauaji.
Yericko Nyerere21,527 views • 5 months ago

Mh @tunduantiphaslissu shikilia hapohapo, huku Maccm wanaanza kuweweseka na kuzungumza mambo ambayo hayapo kivitendo😂…. Komaaaa hapo hapo hatushiriki na hautakuwepo uchaguzi bila mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na katiba mpya! Tuko tayari kuzuia uchaguzi, Tuongoze Baba Lissu!
Yericko Nyerere48,534 views • 1 year ago

Huyu alikuwa Katibu wa Mkoa Kilimanjaro, moja ya makamanda wa piganaji sana tumepoteza katika chama…. Inauma sana Binafsi nilishamaliza maonyo yangu kwa viongozi! Sasa nabaki kuwa mtazamaji tu Ok, PATA OFA YA PAPA MPYA WA ROMA Pata Kitabu cha UJASUSI kwa 25,000 tu badala ya bei halisi ya 80,000/=. Lipia kwa: Lipa Tigo 7489022 Lipa Voda 5352627 M-Pesa. 0755865544 TIGOPESA 0715865544 CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE). Kwa Dar ni free delivery Nje ya Dar nauli 8,000/=
Yericko Nyerere42,879 views • 1 year ago

Baada ya hotuba hii muhimu kwa taifa, muhimu kwa vyama vya upinzani (Chadema, Chauma, Act nk) na muhimu zaidi kwa serikali na muhimu zaidi kwa Chama cha mapinduzi. Tuweke silaha chini twende mezani tukayazungumze…. Serikali fungueni milango kwa moyo wa majuto na kukili makosa, Chadema fungueni milango kwa kukiri makosa, Chaumma fungueni milango kwa kukiri makosa, Act fungueni milango kwakukiri makosa….. na kwa pamoja twendeni tukayazungumze mezani (Maridhiano). Mwasisi wa Chadema aliyesalia sasa Mzee wetu Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema, Mlezi wa Wanasiasa wote waliopo Chadema, ACT na Chaumma amemaliza yote nasi tutekeleze! Na Yericko Nyerere
Yericko Nyerere18,830 views • 4 months ago

Haki itendeke pande zote za waovu, Walioua wawajibishwe, na Waliosababisha mauaji haya wawajibishwe: Kama tume ya uchunguzi ikithibitisha pasina shaka yoyote kwamba Chama chenu kilihusika katika “jaribio la mapinduzi la tarehe 29 oktoba 2025 lililopelekea mauaji makubwa” ambalo wewe na Lissu mliliratibu na kuliongoza vema basi hakuna namna inayoweza kuzuia chama chenu kisifutwe na wewe na wenzio mtakabiliwa na mkono wa sheria kwa kesi ya uhaini. Msijifiche kwenye msamaha wa wahanga
Yericko Nyerere14,562 views • 4 months ago