Video wird geladen...

Video konnte nicht geladen werden

Zur Startseite

Amenunua simu lakini hawezi access Google back up ju verification code ya Gmail inatumwa kwa number ya Telkom na ilipotea

175,363 Aufrufe • vor 1 Jahr •via X (Twitter)

11 Kommentare

Profilbild von Just Kui ♏
Just Kui ♏vor 1 Jahr

How long will this go on 😂😂😂😂

Profilbild von mokorino
mokorinovor 1 Jahr

😂😂

Profilbild von Travala.com 🏨 ✈️
Travala.com 🏨 ✈️vor 4 Jahren

This one's for the Crypto Whales ⬇️ NEW exclusive & luxurious experiences have been added to Apply today & #TravelUnlikeAnyOther with your favorite cryptocurrency.

Profilbild von Arap K95
Arap K95vor 1 Jahr

Unapigia carrier wanakwambia hio line tushauza the only way ni we kuongea na owner Kupiga ni cucu ako transmara, uko za "line ilkua yngu kitambo na kuna code inatumwa si unitumie" Bckgrnd unaskia mjukuu akimwambia "Til simoit, swapaeg chomi Mulot" Woooii binance yangu wee🙆🏿‍♂️

Profilbild von OK_evin!
OK_evin!vor 1 Jahr

Siku moja ataingia twitter async contacts akujoin kwa hii sherehe. 💀😂

Profilbild von Hillary Odinga
Hillary Odingavor 1 Jahr

Multibet ya shetani kila corner,😂😂

Profilbild von Sajid abu Sajid
Sajid abu Sajidvor 1 Jahr

Ii inafaa ikuwe mini-sode pale kwa njoro wa uber 😂😂

Profilbild von 𝐖𝐞𝐬𝐥𝐞𝐲 𝐊𝐢𝐛𝐚𝐧𝐝𝐞
𝐖𝐞𝐬𝐥𝐞𝐲 𝐊𝐢𝐛𝐚𝐧𝐝𝐞vor 1 Jahr

😂

Profilbild von Kangwana Oyaro
Kangwana Oyarovor 1 Jahr

🤣🤣🤣🤣

Profilbild von Bi
Bivor 1 Jahr

Kumbe Mungu wa Wakorino ndiye Mungu wa ukweli

Profilbild von 𝘔𝘶𝘵𝘶𝘯𝘨𝘢
𝘔𝘶𝘵𝘶𝘯𝘨𝘢vor 1 Jahr

This has to be updated every two weeks bana 🤣

Ähnliche Videos

Makamu wa Rais wa Marekani na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Democratic, Kamala Harris, ametoa hotuba ya kukubali kushindwa uchaguzi wa Rais uliofanyika siku ya Jumanne na Donald Trump kuibuka Mshindi ambapo amempongeza Trump wa Republican kwa kuchaguliwa tena kuliongoza Taifa hilo. Akiwahutubia maelfu ya Wafuasi wake mbele ya majengo ya Chuo Kikuu cha Howard Mjini Washington, Harris amewataka Wafuasi wake kutokata tamaa, akiwataka waendelee kupigania masuala yaliyochochea shauku yao wakati wa kampeni “Mapambano ya uhuru wetu yanahitaji kazi ngumu lakini kama navyosema siku zote tunapenda kazi ngumu, kazi ngumu ni kazi nzuri, mapambano kwa ajili ya Nchi yetu yana thamani” “Kwa Vijana mnaotazama ni sawa kuhuzunika na kujisikia vibaya lakini tambueni kila kitu kitakuwa sawa, kwenye kampeni nilisema tukipambana tutashinda lakini wakati mwingine mapambano huchukua muda hii haimaanishi hatutoshinda, kitu muhimu ni kwamba usikate tamaa , usikate tamaa kamwe, usiache kujaribu kuifanya Dunia kuwa eneo zuri, una nguvu na kamwe usimsikilize Mtu yoyote anayekuambia kitu hakiwezekani kwakuwa hakijawahi kufanywa kabla” Harris ambaye kabla ya hotuba yake alimpigia simu Trump kukubali kushindwa na kumpongeza, amesema yeye na Rais Joe Biden watasaidia kufanikisha mabadilishano ya madaraka kwa njia ya amani. Katika hatua nyingine, Rais Biden pia ameongea na Rais Mteule Trump kwa njia ya simu ambapo amempongeza kwa ushindi aloupata kwenye uchaguzi wa November 5 na kumkaribisha kuitembelea Ikulu ya White House wakati akijiandaa kuchukua hatamu za uongozi. #MillardAyoUPDATES

millardayo

40,719 Aufrufe • vor 1 Jahr

Na Mwandishi Wetu Mwandishi wa habari mwandamizi na mchambuzi wa masuala ya siasa, Ezekiel ‘Top Pen’ Kamwaga, ametoa maoni yenye utata akimtaja mwanasiasa Tundu Antiphas Lissu kuwa ni “dikteta mtarajiwa” ikiwa atapewa nafasi ya kuongoza. Kamwaga ameyasema hayo katika mahojiano na Jambo TV, akielezea wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa Lissu kisiasa. Kamwaga amesema Lissu ana uwezo mkubwa wa kudhoofisha heshima ya watu kupitia maneno yake. Ametoa mifano ya namna Lissu amekuwa akiwaita wapinzani wake majina ya dhihaka, kama vile "msaliti" au "mbogamboga," hali ambayo inatoa taswira ya tabia za madikteta kama Adolf Hitler ambao walitumia lugha ya kudhalilisha kabla ya kushambulia wapinzani wao. Ameeleza kuwa Lissu mara nyingi hana woga wa kutoa matamshi mazito, hata kama hayana ushahidi wa kutosha. Amerejelea tuhuma zilizotolewa hivi karibuni kuhusu watu wanaodaiwa kumpelekea fedha, akisema hii ni dalili nyingine ya tabia za kidikteta. Kamwaga amesema viongozi wa kidikteta mara nyingi hawaoneshi heshima kwa mamlaka ya juu wala mifumo iliyopo. Jambo hilo, kwa mujibu wake, linaweza pia kuonekana katika mwenendo wa Lissu. “Tundu Lissu ni mwanasiasa ambaye, ukimpima kwa mizani ya utawala wa baadaye, anaweza kuwa dikteta mtarajiwa. Lakini kwa sasa, aina ya siasa anayoifanya inakubalika kwa kiwango kikubwa duniani,” alisema Kamwaga. Kamwaga amesisitiza kuwa, licha ya changamoto hizo, CHADEMA ina nafasi ya kuamua mustakabali wake kwa kumpa Lissu nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama. Amesema kwamba, chama hicho kinaweza kunufaika na mtazamo wa kisiasa wa Lissu, lakini akaonya kuwa Lissu hawezi kuongoza bila uongozi thabiti wa Freeman Mbowe na timu yake. “Mbowe anaweza kuweka muundo madhubuti ambao utamruhusu Lissu kuongoza kwa ufanisi. Bila muundo huu, Lissu hawezi kufikia mafanikio ambayo Mbowe ameyapata,” aliongeza Kamwaga. Amependekeza kuwa CHADEMA iangalie namna bora ya kumpatia Lissu nafasi ya kuongoza chama bila kuharibu taswira ya Mbowe. Kamwaga alihitimisha kwa kusema kuwa siasa za Tanzania kwa sasa zinahitaji aina ya uongozi wa Lissu, lakini akasisitiza kuwa hali hiyo inapaswa kudhibitiwa ili kuepuka changamoto za baadaye.

Jambo TV

53,649 Aufrufe • vor 1 Jahr

Mmoja wa viongozi na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Same Andrew Mchome amelaani kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho John Heche kutangaza kwamba ataandikia barua FIFA ili wasitishe mashindano ya AFCON nchini Tanzania kwa madai ya kuwepo kwa vikundi vilivyopanga kufanya vitendo vya kigaidi. Hatua hiyo imekuja kufuatia Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuwakamata watuhumiwa kadhaa katika maeneo mbalimbali ya nchi wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi licha ya kwamba bado vitendo vyao havijathibitishwa Mahakamani Akizungumza na waandishi wa Habari Leo Julai 29, 2026 Jijini Dar es Salaam Mchome amesema kauli ya Heche ni ya kupingwa kwa sababu inachafua taswira ya nchi kimataifa, na kuongeza kuwa hakuna chama chochote cha siasa kinachopinga maendeleo ndani ya nchi yake hivyo kitendo cha Heche kujitokeza hadharani na kudai ataiandikia FIFA barua kupinga kufanyika kwa AFCON si cha kiungwana "Juzi nimemsikia akizungumza anasema kwamba tutaandika barua FiFa kuzuia mashindano ya AFCON kutokana na kuwepo kwa viashiria vya UGAIDI, kilichopo kwenye nchi yetu sasa hivi ni kwamba, Kuna watu ambao wana tuhuma ya kupanga vitendo hivyo lakini hakuna Mahakama iliyohukumu mtu kutokana na vitendo vya UGAIDI" amesema mchome Ameongeza kuwa Kauli ya Makamu mwenyekiti huyo sio ya kizalendo kwa taifa na yaweza kutia hofu wageni wanaotamani kuja kuwekeza nchini lakini pia kutembelea vivutio vya utalii. Mchome amemtaka Heche kuacha kukigombanisha chama chao na wananchi kwani anaamini kupitia mashindano hayo ya AFCON watanzania wataenda kunufaika kwa namna moja ama nyingine kupitia ugeni mkubwa utakao kuwa nchini. "Mpenda maendeleo yeyote hawezi kuwa na roho kama hiyo ya kupinga Maendeleo, ugeni utakaoingia nchini utasaidia hadi mamalishe kupata ridhiki zao, pia utafungua ukurasa mwingine kwenye sekta ya utalii" amesema mchome

ROYAL TELEVISION PLUS

20,966 Aufrufe • vor 10 Tagen

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amemtaka Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo kuwaomba msamaha hadharani watu wote aliowahi kuwaumiza,kuwachonganisha nakuharibu maisha yao Makonda ametoa kauli hiyo mbele ya Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko kwenye maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ambayo yamefanyika katika viwanja vya Kilombero Mkoani Arusha “Nampongeza kwasababu moja kubwa, juzi ameomba radhi Bungeni, amechonganisha chonganisha sana Watu hapa na leo hapa ameanza kumsifia Mkuu wangu wa Wilaya kwa sifa zilezile ambazo alinisifiaga Mimi nilipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa lakini sasa hivi hata kulitamka jina la Makonda hawezi” “Namsifu kwa sababu aliomba radhi, alikuwa anaenda kuharibu maisha ya Watu kwa kuwadanganya Wabunge na kama Bunge lisingekuwa makini na Waziri wetu Mchengerwa kuwa imara, leo hii kuna Watu wangepoteza kazi kwasababu yake” “Sasa ombi langu kwake moja awaombe radhi Watu wote aliowafitini kwa kuwaumiza, kuwachonganisha na kuharibu maisha yao, safari ya Mbinguni hata Mimi naitaka, mambo yalivyoendelea yalipelekea simu ninazopata, unamuita Waziri wetu muongo?, hii stendi inayoanza kujengwa, hii nimemuomba Mchengerwa, ilikuwa design ndogo haikidhi viwango, akaongeza bajeti bilioni 30 ni faida kwa Wanancgi wa jiji, halafu unamuita Waziri wetu muongo!?” “Kwa kuwa Bunge limemsamehe, Mimi moyoni sina shaka nae lakini sharti langu moja aliowaumiza na kuharibu maisha yao awaombe radhi ili mbele ya Mungu na mbele ya Wanadamu tupate kibali cha kuifanya kazi hii” #MillardAyoUPDATES

millardayo

47,634 Aufrufe • vor 1 Jahr

VIDEO: Kufuatia video fupi iliyokuwa ikisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikimuonyesha mwanamke mmoja akiwa nje ya nyumba pamoja na watoto wake huku akiomba msaada, anayetambulika kwa jina la Josephine Mosha, mkazi wa Mtumba jijini Dodoma aliyetolewa mali zake nje ya nyumba na watu waliokuwa na silaha wanaodaiwa kuwa madalali wa mahakama, ambao walimuambia anapaswa kuondoka hapo kwani nyumba hiyo ipo katika mgogoro wa talaka. Akizungumza na Jambo TV Oktoba 13 kufuatia tukio hilo, Josephine amesema kuwa nyumba hiyo waliinunua yeye na mume wake mnamo mwaka 2023 kutoka kwa mtu aliyemtaja kwa jina la Vallence Laswai, kwa kufuata taratibu zote za kisheria ikiwemo upatikanaji wa hati miliki ya kiwanja. Ambapo katika mauziano hayo walimuuliza Laswai kama ana mke au familia ambayo inaweza kuwa na haki katika mali hiyo, ambapo Laswai alijibu kuwa ana mke aliyewahi kuzaa naye, lakini hahusiki katika mali hiyo. Aidha Josephine ameeleza kuwa wiki chache zilizopita walipokea taarifa ya kuondoka ndani ya siku 14 kutoka kwa madalali wa mahakama, na kutokana na hilo walienda katika Mahakama ya Mwanzo kuomba zuio la muda na Walishauriwa kufuata utaratibu wa kupata zuio (stop order) kutoka Baraza la Ardhi. Hata hivyo, amesema siku chache baadaye ndipo watu hao walifika nyumbani hapo na kuanza kutoa mali zao nje wakidai kuwa nyumba hiyo ipo kwenye mgogoro wa talaka kati ya aliyekuwa mmiliki wa awali, Bw. Laswai, na mwanamke anayedaiwa kuwa mke wake ambapo Josephine Mpaka sasa amerudisha vitu ndani ya Fensi ya nyumba akiwa hajui nini hatama ya Haki yake. Akizungumza na JAMBO TV kwa njia ya Simu Bw. Vallence Laswai, ambaye alikuwa mmiliki wa awali wa nyumba hiyo, amekiri kuwa aliwauzia nyumba Josephine na mume wake, kwani ndiye alikuwa mmliki halali huku akieleza kuwa mwanamke anayedai kuwa mke wake alikuwa ni mzazi mwenza na kwamba hawakuwa wakiishi pamoja tangu alipohamishiwa Dodoma kikazi mwaka mnamo mwaka 2023. Jambo TV ilimpata kwa njia ya simu mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa Laswai, lakini alikataa kuzungumzia suala hilo, akisema kuwa mipaka ya kazi yake hairuhusu kutoa maoni juu ya mgogoro huo unaoendelea.

Jambo TV

10,857 Aufrufe • vor 9 Monaten

VIDEO: Siku chache tangu mjadala wa watu waliojiita 'Wakatoliki' kuandamana hadi Ubalozi wa Vatican Nchini Tanzania uchukue sura mpya kufuatia wadau mbalimbali kulaani na kuhoji uhalali wa tukio hilo na 'Ukatoliki' wao, mapya zaidi yameendelea kuibuka kuhusiana na sakata hilo Naomi Davis Matola, Mkazi wa Kurasini, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam ameeleza masikitiko yake kutokana na kile alichoeleza kuwa baadhi ya watu wamemfananisha na mmoja wa 'Wakatoliki' hao, na kwamba baada ya taarifa zinazomuhusu kuwekwa mtandaoni amekuwa akipokea simu na kutumiwa sms nyingi za kashfa, matusi na hata wengine kumtishia maisha Akizungumza na Jambo TV, Naomi amesema kumekuwa na picha ya dada mmoja aliyekuwa mmoja wa 'Wakatoliki waandamanaji' (ambaye hamfahamu) inayosambazwa mitandaoni lakini jina, maelezo na namba iliyoambatanishwa kwenye picha hiyo ni yake, jambo ambalo limemuingiza kwenye sintofahamu kubwa kwake binafsi na familia yake kwa ujumla Neema anasema kwa muda mrefu amekuwa mgonjwa, na kwenye mazingira ya kawaida kwa muda wote huo safari zake zimekuwa za Hospitali na nyumbani tena hawezi kutembea mwenyewe, hivyo amestushwa sana na uwepo wa taarifa zinazomuhusu kuwekwa mtandaoni kuwa alikuwa mmoja wao Kufuatia sintofahamu hiyo, Neema sasa amefikisha malalamiko yake kwenye Kituo cha Polisi Kilwa Road na kupewa RB No. KLR/RB/99/2026 yenye kosa la Matumizi Mabaya ya Mtandao, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wote waliohusika kusambaza taarifa hiyo kwa namna moja au nyingine wajitokeze kufuta, na kukanusha.

Jambo TV

26,493 Aufrufe • vor 7 Monaten