正在加载视频...

视频加载失败

51,547 次观看 • 2 个月前 •via X (Twitter)

1 条评论

harutoo 的头像
harutoo2 个月前

salah satu video favorit💦🥵

相关视频

VIDEO: Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa kuvurugwa na kuondolewa kwa dhana ya ushindani wa haki wa kisiasa ndicho chanzo kikuu kilichoharibu mfumo wa uchaguzi na misingi ya demokrasia nchini. Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati Padre Kitima akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Akirejea msingi wa kihistoria wa taifa, Padre Kitima ameeleza kuwa Mwalimu Julius Nyerere aliweka msingi thabiti baada ya uhuru kwamba uhalali wa kiongozi kuongoza lazima utokane na ushindani wa haki na wa wazi kutoka kwa wananchi, kulingana na misingi ya Katiba inayoeleza kuwa uongozi ni dhamana na wananchi ndio wenye mamlaka ya utawala "Mwaka 1962 Nyerere alisema siwezi kuwa rais wa nchi bila kuchaguliwa na wananchi baada ya kuwa tumepata uhuru tarehe 9 Disemba 1961, akasema lazima nichaguliwe nipate kile kitu kinaitwa legitimacy... ule uhalali wa kuongoza upatikane kwa ushindani ulio halali unaotoka kwa wapiga kura wananchi wenyewe. Kwa sababu tunaamini na Nyerere alijaribu kujitahidi sana kuaminisha Watanzania kwamba uongozi ni dhamana", ameeleza Padre Kitima. Akifafanua kuhusu sababu zilizofanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwa na idadi kubwa ya wagombea urais waliofikia 17 ukilinganisha na chaguzi za nyuma, Padre Kitima amefafanua kuwa hali hiyo haikutokana na kukua kwa demokrasia, bali ilitokana na mbinu za makusudi za kuondoa ushindani halisi wa kisiasa ulioanza kubomolewa tangu mwaka 2019 na 2020. Ameongeza kuwa michakato hiyo ya kisiasa ilianza kuvurugwa kuanzia ndani ya vyama vya siasa kabla hata ya kufika kwenye uchaguzi mkuu.

Jambo TV

16,282 次观看 • 2 个月前