Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

dame akiwa Kwa healing stage

93,847 views • 2 years ago •via X (Twitter)

0 Comments

No comments available

Comments from the original post will appear here

Related Videos

VIDEO: 📍MWANZA - Katika tukio lililosababisha mshangao mkubwa kwa wakazi wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Colnel Magembe (jina linahifadhiwa) amepatikana akiwa hai, wiki moja baada ya kudaiwa kushambuliwa na kubebwa na mamba katika Ziwa Viktoria. Tukio hilo linadaiwa kutokea Machi 2, 2026, katika kitongoji cha Ilondo Magharibi, kijiji cha Buzegwe, Kata ya Kagunguli, ambapo binti huyo mwenye umri wa miaka 18 alidaiwa kuvamiwa na mamba majira ya saa 11 alfajiri alipokuwa akioga ziwani akijiandaa kwenda shuleni. Hata hivyo, kwa hali iliyowastaajabisha wengi, Mwanafunzi huyo alipatikana akiwa hai alfajiri ya Jumatatu, Machi 9, 2026, majira ya saa 11 katika eneo hilo alilodaiwa kushambuliwa na mamba, huku akiwa hana majeraha wala michubuko yoyote mwilini. Kwa mujibu wa mashuhuda, wavuvi waliokuwa wakifanya shughuli zao kandokando ya Ziwa Victoria ndio waliomuona kwanza akiwa amelala karibu na maji, katika hali ya udhaifu na kushindwa kuzungumza. Baada ya kugunduliwa, Wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walimchukua na kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe (Bomani) iliyopo Nansio kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi. Akizungumza hospitalini, baba wa mwanafunzi huyo, Deonatus Salvatory, alisema familia ilishakata tamaa ya kumpata binti huyo hai, na tayari walikuwa wameshaanza taratibu za maombolezo Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe (Bomani), Dk. Bunhya Kayila, alisema mwanafunzi alipokelewa hospitalini majira ya saa 1 asubuhi akiwa dhaifu, na uchunguzi wa awali haukuonyesha uwepo wa majeraha yoyote mwilini yanayoweza kuashiria kushambuliwa na mamba. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Goodluck Mtigandi, alisema uchunguzi wa awali haukubaini uwepo wa dalili za mnyama hatarishi katika eneo alilodaiwa kushambuliwa, huku akiongeza kuwa mamlaka zinasubiri mwanafunzi apate fahamu vizuri ili kueleza kwa undani kilichotokea na mazingira halisi ya kutoweka kwake.

Jambo TV

16,288 views • 4 months ago