Загрузка видео...

Не удалось загрузить видео

На главную

12,023 просмотров • 1 год назад •via X (Twitter)

Комментарии: 2

Фото профиля Pratilac svih dešavanja
Pratilac svih dešavanja1 год назад

Ovo zerina?😂

Фото профиля Solar Heavy
Solar Heavy1 год назад

take the journey

Похожие видео

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limepiga marufuku mikusanyiko isiyokuwa halali inayodaiwa kuandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Akitoa taarifa hiyo leo Aprili 23, 2025 mbele ya waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wibroad Mutafungwa amesema watakao thubutu kushiriki katika mikusanyiko hiyo watachukuliwa hatua kali za kisheria. "Kuanzia Aprili 22, 2025 tumeanza kupokea taarifa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali zinazoonyesha kuwa baadhi ya wafuasi wa chama cha Chadema katika Mkoa wa Mwanza wanapanga kukutana na kufanya mikusanyiko isiyokuwa halali kwa lengo la kushinikiza kuachiliwa huru Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Tundu Lissu ambaye anatarajiwa kufikishwa mahakamani Aprili 24 mwaka huu," amesema. "Taarifa zinazopokelewa na Jeshi la Polisi ni kuwa wanawake na watoto wanashawishiwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kushiriki kwa wingi katika mikusanyiko hiyo isiyokuwa halali," amesema Kamanda Mutafungwa Kamanda Mutafungwa amesema kutokana na taarifa hizo jeshi hilo linawatahadharisha wananchi kutojihusisha wala kushiriki katika mikutano hiyo. "Wale ambao watajihusisha katika mikusanyiko hiyo isiyokuwa halali au kufanya vurugu, kufanya uvunjifu wowote wa amani Jeshi la Polisi halitasika kuchukua hatua kali za kisheria kama hatua mojawapo muhimu ya kulinda amani na usalama wa Mkoa wa Mwanza," amesema Ameongeza kuwa "Pia,Jeshi la polisi linawakumbusha wananchi wa mkoa wa Mwanza, kutoa tarifa za mikusanyiko hiyo isiyokuwa halali au uvunjifu wowote wa amani mara moja itakapojitokeza katika maeneo yao ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa na Jeshi la polisi,".

Jambo TV

33,357 просмотров • 1 год назад