正在加载视频...

视频加载失败

“HATUKAMATANI KWA UTANI WA MPIRA”

68,393 次观看 • 1 年前 •via X (Twitter)

11 条评论

ndissajr 的头像
ndissajr1 年前

Linapo kuja swala la hizi timu hata wenye akili huwa wanakuja kuonekana hawana akili yani badala ya kuwambia vijana wajifunze kuongea mbele za watu pindi unapo jibizana na kiongozi wa serikali hawana ukubwa huo na mbaya alimwingiza Rais kwenye maongezi ili kujipa uhalali

Kijukuu Cha Mtume 的头像
Kijukuu Cha Mtume1 年前

Sio ni kheri, marufuku kushadadia mpira kama unajijua una patience level ya sisimizi! Mbona Msigwa anatanikika na anaenda vizuri tu, Rais mwenyewe anataniwa kwenye mada za mpira yeye papasi mmoja anayeshabikia Simba halafu anajifanya mfia damu wa Tabora asitaniwe nani na kautaka?

Mghoshiwandima 的头像
Mghoshiwandima1 年前

Huyu mkuu wa mkoa ni mshamba mmoja tu. Shida ya kuwa Kolowizard, hasira za kufungwa Tabora na Makolo anazihamishia kwa Aly Kamwe. Yeye na huyo aliyemkamata tutadeal nao tu.

Omary Sadiki 的头像
Omary Sadiki1 年前

Sasa iv kwenye mpira utekaji utaanza

SecBriefs | Making Cybersecurity Simple 的头像
SecBriefs | Making Cybersecurity Simple1 年前

🇺🇸 The Future of America is Digital—And So Are the Threats! 🔐 It’s time for a bold, national cybersecurity strategy. The new government must act fast. So must you. 🦅 🎯 Be part of the solution! Get the CYBERSECURITY DICTIONARY for Everyone, on Amazon:

BakhResa 的头像
BakhResa1 年前

Sema wewe job kichwan Amna kitu kwhy coz mnabishana mambo ya mpira upo tayari mtu akutusi kisa mpo kwenye Agenda za mpira,Andazi kwel ww kila kitu kina mipaka yake unapobishana na kiongozi hata kama Kweny mpira basi kuna lugha haupaswi kuzitumia🙏🏿

Cpt. joe 的头像
Cpt. joe1 年前

Alikamwe alikosea ila pia mkuu ajitathmini why anajibiwa vibaya sana , yule jamaa wa manunuzi si ndio alimjibu pia mshikaji vibaya?ni nyota au nini hapa hakipo sawa

M G A L E 的头像
M G A L E1 年前

Watu wanatetea mambo aliyofanyiwa Ally Kamwe na Mkuu wa Mkoa, kwa kushikiliwa kinyume na Sheria. Hakika hili taifa bado linawatu wajinga sana, Elimu ya Uraia waliikimbia. Ally Kamwe hana kosa kesheria, Aachiwe bila masharti.

BakhResa 的头像
BakhResa1 年前

Ndio umwambie kiongozi kavaa shati la ubatizo kwel 😆😆

Nkhosi 的头像
Nkhosi1 年前

Hv ww nani kakuambia kuwa mpira unatenganishwa na shughuli za maendeleo? Duniani soka sehemu ya mpira ni moja ya kiwanda kikuu cha mapato ya nchi. Na viongozi kama RC hawezi akakaa pembeni kutosimamia,kuratibu au kuhamasisha mpira mkoani mwake,nje ya hapo ni ukilaza katika DS

💰👑 的头像
💰👑1 年前

Kabisa, kaingia kwenye ulimwengu wa soka, na soka ndivyo lilivyo

相关视频

VIDEO: Viongozi wa matawi ya Young Africans SC na Wazee wa klabu hiyo mkoani Dodoma wametoa tamko kali wakimtaka Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), TFF TANZANIA Wallace Karia, kuomba radhi hadharani kwa kauli alizozitoa kufuatia kuahirishwa kwa mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga. Wakizungumza na wanahabari Jijini Dodoma leo Machi 18, 2025, viongozi na wazee hao wameeleza kutoridhishwa kwao na maamuzi yaliyofanywa, wakidai kuwa wamepoteza imani na Karia na uongozi wake. Mzee Abdalah Mtosa Ally kutoka Tawi la Chang’ombe amesema hakuna sababu ya kurudia mechi hiyo kwani tarehe 8 ilikuwa sahihi kwa mchezo huo kufanyika. "Mimi kama mzee wa Yanga Dodoma, kwa masikitiko makubwa, hatuna imani na Karia kwani tunajua wazi hana mapenzi ya dhati na Yanga. Niwaombe viongozi wa juu kutoruhusu mechi hiyo kufanyika tena. Kama ni faini tuko tayari kulipa, lakini siyo kurudia mechi na Simba," amesema Bernard Mtengwa, mmoja wa wazee wa Yanga. Naye Bodar Awadhi Ahmed, mzee mwingine wa Yanga, amesema kuwa uamuzi wa kuahirisha mechi hiyo umeleta mkanganyiko na sintofahamu kwa mashabiki wa soka, huku wengi wao wakipinga kufanyika upya kwa mchezo huo. Aidha, viongozi hao wamesisitiza kuwa hawana tena imani na Karia kutokana na kauli zake walizodai kuwa zimewadhalilisha Wanayanga. "Sisi msimamo wetu ni kutokurudia mechi. Kwanza Rais wa TFF ametudhalilisha Wanayanga, na kama ameshindwa mpira, arudi kwenye taaluma yake, kwani tunaijua," wamesema kwa msisitizo. Kwa upande wake, Mratibu wa Yanga Dodoma, Elisha Ngwando, amemtaka Karia kuwaomba radhi Wanachama wa Yanga na wanamichezo kwa ujumla kwa maamuzi aliyofanya na kauli alizozitoa. "Watu wametumia gharama kubwa, wengine wamelipia matangazo kwa ajili ya mechi hiyo," amesema Ngwando. WanaYanga hao wameendelea kusisitiza kuwa hawataki mechi hiyo irudiwe, huku wakitoa wito kwa viongozi wa juu wa mpira nchini kuhakikisha haki inatendeka kwa klabu yao.

Jambo TV

29,653 次观看 • 1 年前