正在加载视频...

视频加载失败

16,682 次观看 • 29 天前 •via X (Twitter)

0 条评论

暂无评论

原始帖子的评论将显示在这里

相关视频

Tupiganie Katiba Mpya kivipi Wakati Lissu alipigania Katiba Mpya mkamfungulia kesi ya Uhaini? Tukomae na Katiba Mpya kivipi wakati Vijana walipokomaa na Katiba Mpya mwaka jana mliwapiga risasi za moto na kuwaua? Tupiganie Katiba Mpya gani ambayo vijana wa CHASO Mbeya, Mwanza, Iringa na mikoa mingine wakifanya hivyo wanafunguliwa kesi za Ugaidi na Uhaini? Tupiganiaje Katiba Mpya wakati Dr. Melkisedeki Kaijage wa UDOM amewaambia wanafunzi wake Darasani kuwa kuandamana ni Haki ya Kikatiba leo amefunguliwa kesi ya Ugaidi? Unasemaje kama unataka Amani lazima Utende Haki na usione aibu kutamka haki katika mazingira ya nchi ambayo Vijana wanatekwa, wanapotezwa, wanafunguliwa kesi za uongo za ugaidi na uhaini ? Wanaoruhusu haya yafanyike ni akina nani Bwana Nchimbi atueleze tumuelewe. BAVICHA tumesema huu ni wakati tunaohitaji VITENDO dhidi ya MANENO. Hatuhitaji kauli tamu za kutufurahisha. Wanaokula kodi zetu watanzania tunahitaji watuambie: Katiba Mpya itapatikanaje kabla ya 2029 na 2030 wakati hadi sasa hakuna Bajeti ya Mchakato huo? Hakuna Calendar ya matukio ya namna mchakato huo utakavyofanyika na kukamilika. Tutaaminije? Msimamo wa BAVICHA na Chama chetu ni No Reforms: No Election kwa Uchaguzi wa 2029 na ule wa 2030. Ni muhimu wanaotumia kodi za Watanzania wakawekeza kwenye kuhakikisha mazingira ya kupatikana Katiba Mpya ya Wananchi inapatikana kweli na sio mbwembwe na propaganda. Deogratias Mahinyila Deogratias Mahinyila Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa. 24/07/2026.

Hilda Newton

27,232 次观看 • 1 个月前