Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

39,942 views • 1 year ago •via X (Twitter)

0 Comments

No comments available

Comments from the original post will appear here

Related Videos

Jana nimemsikiliza SIMBA CHAWENE anavyoiongelea CHUKI ya watanzania kwa Jeshi la polisi ni kama imeletwa na MABEBERU. ACHA KUJITOA AKILI WE MZEE, haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea ndani ya miezi 8 tu, sasa fikiria matukio ya miaka zaidi ya mitano nyuma na yanayoendelea gizani huko kwenye vituo vya polisi. Leo nimeamka nikujaze akili na najua utapata ujumbe wangu tuu. Nataka ujue kuwa Chuki hii tuliyonayo kwa jeshi la polisi ilipandwa na wao polisi sasa ni muda wa MAVUNO watulie. Watanzania wamekuwa wakipigwa na kuzuiliwa kuenda mahakamani kinyume kabisa na sheria. Licha ya mahakama kusema mara kadhaa wananchi wasizuiwe Jeshi la polisi liligeuza MAHAKAMA KAMA UWANJA WA VITA DHIDI YA WANANCHI KWA KUKIUKA HATA AMRI YA MAHAKAMA. Mwezi wa 4 mwaka huu jeshi la polisi lilikusanya watu wote walioenda mahakamani kusikiliza kesi ya Tundu Lissu na kuenda kuwatesa na kuwavunja Miguu na migongo wananchi na kuwatupa kwenye fukwe za bahari na wengine kwenye misitu huko pande. Murilo alipoulizwa alisema jeshi lake la polisi halihusiki na huku tuliona kabisa wao na magari yao na sare zao wakipiga watu nje ya mahakama na kuondoka nao-majibu ya JEURI kama kawaida yake. Mkuu wa mkoa HARAMU CHALAMILA alijibu nae kwa jeuri kwa kusema Dar hakuna MAPORI hayo mapori yapo wapi, kwahiyo waliopigwa na kuvunjwa wanaleta Sanaa. Oktoba 29 jeshi la polisi walikuwa wakifuata vijana majumbani na kuwapiga risasi za vichwa na kupotea nao, miili mingi imepotezwa ndugu wameshindwa kuzika wapendwa wao. Badhi waliobahatika kuishi waliteswa na kuvunjwa miguuu bila sababu na kupewa kesi za uhaini. Kwa haya machache unataka POLISI AKIFA AU AKIPATA AJALI TUUMIE? NA UNATAKA TUSHIRIKANE NA HAWA WATU MAGAIDI HIVI WAKINA MAFWELE ,MURILO NA GEORGE AMBAO NDIO WANATOA AMRI YA YOTE HAYA. WATU SIO WAPUMBAVU JIHESHIMU. TUTAKUWEPO🫵😎

SIR TIVA

12,431 views • 7 months ago

(✍️ na mchambuzi wetu) PAULO MAKONDA anaamini sana uchawi wa mama yake kuliko Mungu anayejifanya kumuamini. Anaamini uchawi kwenye kuvutia watu kujaa kwenye "mabonanza" yake kuliko mvuto wa chama chake. Ndani ya miezi miwili tu amejijengea maadui maelfu ndani ya serikali na ndani ya chama chake. Amegeuka kuwa msemahi wa wapinzani kwa kusema madhaifu ya chama chake kuliko kazi ya kukitetea chama chake. Anajidanganya kuwa tabia yake ya hovyo kuwatukana,kuwadhakilisha viongozi wa serikali hadharani ni kumsaidia Rais kumbe ni akili za kitoto tu. Watu wote anaowadhalilisha majukwaani ni wateule wa Rais na kuwakosoa kwa kigezo cha chama kimewaagiza ni wazi anakosoa na kudhakilisha mamlaka iliyowateua. Ziara nzima ya Makonda imejaa malalamiko na anazoita kero na kwa kurahisisha ni kuwa kama hayo yote anayokutana nayo bi ya kweli basi serikali hii imefeki kuongoza nchi na CCM imeshindwa kuongoza nchi na kinachofuata ni kwa CCM kukaa pembeni kwa sababu kwa miaka 60 imeshindwa kutatua kero hizi wakati wao ndiyo wenye serikali. Inawezekanaje wananchi wanalalamika nchi nzima na CCM ndiyo wenye serikali na dola? Kushindwa kwa watendahi wa serikali ni kushindwa kwa serikali kwa hiyo kukaa hapa na kudhani kusikiliza kero mnazozisababisha wenyewe ni utoto. Bunge mimetukanwa, mawaziri wametukanwa, mahakama imetukanwa na kuambiwa kuwa aiyo sehemu ya watanzania kukimbilia kudai haki zao. Maana yake Makonda anahamasisha watanzania kudharau mahakama na kuchukua sheria mikononi kwa kuwa mahakamani kumejaa rushwa. Tunawezaje kama taifa kuangalia hili na kuona ni jambo la kawaida mahakama inachafuliwa kuwa ni sehemu ya rushwa? Haya yote yanatokea kwa kuwa Makonda kazungukwa na wahuni na watu wajinga kama washauri wake kwenye mambo haya pamoja na uchawi na uganga ambao anaamini ndiyo ngao yake. Huwezi kuwa na mtu kama lile bonge la Kariakoo wawe washauri wako na ukafanya mambo ya maana! Haiwezekani hata kidogo. Ukiwa na watu wajinga kama washauri lazima utafanya mambo ya kijinga tu na hiki ndicho tunakiona sasa. Yaani haiingii akilini serikali ni ya CCM toka tumepata uhuru halafu CCM wenyewe mnakuja kulalamika serikali haitatui kero za wananchi! Nyie watu mmechoka sana basi tu yaani hii nchi haina vyama imara vya upinzani, mlitakiwa mpumzime mkajipange upya. HILI na ajali ni mfano mwingine wa matumizi mabaya ya mali za umma! Magari ya serikali yanafuata nini kwenye maafara wa mwenezi wa CCM? CCM kama chama mnaleta maigizo ya sijui wananchi wana kero halafu msafara wa haya mabonanza ya mwenezi wenu una magari ya serikali yote hayo! Hivi mnafanya watu hawana akili au? Inawezekana alikuwa bado anavua samaki wakati Horace Kolimba aliporopoka na kusema CCM imepoteza mwelekeo na safari ikamkuta bila kuchelewa! Sasa endelea kudhani uchawi ulionao au mama yako kule Koromije kama unavyojitapa atakupa ulinzi shauri zako utaacha wanao wanateseka kwa ajili ya kukosa kwako akili na kuharisha maneno yasiyo na maana ukidhani unamsaidia Rais. Yote haya unayofanya humsaidii zaidi ya kuwasaidia wapinzani kuonyesha hinsi gani CCM imeshindwa kuongoza hii nchi, jinsi gani serikali imefeli kuongoza hii nchi na jinsi gani CCM inadharau na kudhihaki mahakama na viongozi wa serikali ambao siyo sehemu ya CCM wala siasa! Halafu yale mambo ya kutegewa sumu vyumbani yameishia wapi? Au umekunywa maziwa kujikinga? #KigogoForum #ItafahamikaTu #NapeNiTakataka

KigogoForum

20,277 views • 2 years ago

Mtaka ni mbegu nzuri iliyoanguka kwenye udongo mbaya. Kuna mambo hauwezi kufake, ni ama unayo au hauna. Ameuliza swali muhimu sana ambalo Mwal. Richard Mabala amekuwa akisisitiza kila mara anaposema “Mungu pekee ndio mwenye uwezo wa kusema iwe ikawa.” Huu “uchumi wa dola trillion moja” by 2050 unatengenezwa na human resource ipi? Mtoto anayezaliwa leo hii ana mazingira yoyote ya kumwandaa kushiriki kikamilifu kwenye uchumi, tofauti na mama yake aliyezaliwa miaka 15 - 20 iliyopita? Ni kipi haswa kilichobadilika kwenye elimu ya Tanzania ambacho unaweza kusema “hawa wa jana hakika hawakuandaliwa lakini hawa wa leo wana uhakika wa kuwa rasilimali watu?” JIBU LA MSINGI NI HAKUNA. Mazingira ni yale yale, miundombinu duni ni ile ile, tatizo la walimu ni lile lile, vifaa vya TEHAMA ni changamoto vile vile, na bajeti ni kiduchu vile vile. Tena kama haitoshi ndio kwanza tumeongeza idadi ya wanafunzi mara dufu halafu juu yake tukakopi sehemu ya sera ya elimu ya Finland na kuitumbukiza Tanzania. Mwanafunzi mzuri wa policy borrowing anaweza kutabiri with certainty kuwa tulichofanya ni mbili jumlisha mbili toa nne, haswa kwa kuzingatia uhalisia wetu wa kimiundombinu. Hoja nyingine nyeti ni hii ya KUSUBIRI KUSAIDIWA KILA KITU. Yani hata kutumia wataalam wetu kama wakina Kipanya na Mabala kututengenezea makala za kufundishia imekuwa changamoto, mpaka tusubiri “WAHISANI.” Pata picha hadithi za ucheshi wa kufundishia za Mabala, ambaye ni mtaalam wa literacy, zimekutana na katuni za Kipanya, vyote kwenye program moja. Ameuliza Mtaka, ni kipi haswa kwenye katuni ya Akili and Me kinachohitaji mtu kutoka nje?? Mwisho Mtaka akagusa panapouma. Katuni za HakiElimu kuhusu uhalisia wa mazingira ya kufundishia zilikuwa na shida gani?? Hatutaki kuambiwa ukweli kuhusu hali ya madawati mashuleni, vyoo, changamoto kubwa ya walimu na uwezo wao, pepo la lugha ya kufundishia n.k. Kila mara jamaa wakidepict uhalisia, mnasema “oohhhh wanashusha moral ya walimu; ooohhh wanamdharaulisha mwalimu; ooohhh wanaondoa utu wa wanafunzi; ooohhhh blah blah blah.” Tunapenda political correctness kiasi kwamba tupo tayari kuficha ukweli na kuacha watoto waendelee kusomea kwenye mazingira ya tabu na mateso kuliko kukabiliana na ukweli.

(---) Onesmo Mushi

26,287 views • 6 days ago

Ndugu wa Mzee Wasira wamesaidie atafute namna ya kumpumzika akili yako imechoka sana -- Ugaidi ni kufanya siasa kwa kutumia bunduki au mabomu, haya ndio mambo ambayo CCM wanafanya -- Kupinga suala lolote hata kama ni kuhasi sheria zio ugaidi, ugaidi unajulikana na unatafsiri yake kisheria -- Wananchi kupitia nguvu ya umma au chama chochote kupitia nguvu ya umma wana haku kushawishi kupinga sheria zinazovunja haki za wananchi, au zinazotumika kukandamiza haki, huo sio ugaidi ni uzalendo MWISHO -- Samia anapotumia jeshi na polisi kwenye siasa hayo ni mambo gani kwenye katiba ? -- KUTEKA NA kuuwa Watanganyika hiyo ni sehemu gani ya katiba -- Kusheresha kesi hiyo ni sehemu gani ya katiba ? -- Rais kugawa mafedha kwenye mkutano hiyo ni sehemu gani ya katiba, hizo fedha zinatoka wapi? -- CCM kutumia magari ya jeshi ni sehemu gani ya katiba ? -- CCM kukiuka taratibu za usafirishaji nchini, kwa kusafirisha watu kama ng'ombe hiyo ni sehemu gani ya katiba ? sheria za usafirishaji zinajulikana , kuna waliokufa kwenye hiyo michakato -- Mwana CCM , Ramadhani Mapuli kuwa sehemu ya TUME ya uchaguzi ni katiba gani au sheria inayotaka hayo -- Kusema kuna sheria mpya ya TUME ya UCHAGUZI, lakini tume inayokwenda kusimamia uchaguzi ni ya ZAMANI hakuna TUME kuvunjwa limebadilisha tu jina kila kitu kimebaki vile vile, sheria inasemaje pale inapobadilika kwa nini hakuna heshima kwa hizo sheria ? CCM wanaongelea katiba gani Wana CHADEMA wametekwa na kupigwa vibaya kisha kutupwa maporini mchana kweupe

Think Different

13,355 views • 1 year ago