正在加载视频...

视频加载失败

37,634 次观看 • 2 年前 •via X (Twitter)

10 条评论

J.4 的头像
J.42 年前

Hii ya Pharmacy council ndo kabisaaa…more than 165k per year halafu sijui wanafanyia nini!😂😂..ilitakiwa ada iwe 50k tu.

Dr Makumba 的头像
Dr Makumba2 年前

Si ni wito!? Kwanini tulipe Ada kutumikia Wito!?

Ngoilenya,MD 的头像
Ngoilenya,MD2 年前

@NormanJonasMD hii nzr. But last week ( 6 days ago) nime-renew leseni kwa 100k pia nimelipa deni la mwaka jana 100k jumla laki 2 Au hili la 150k nimeanza kutumika lini?

Dr. Kala. MD 的头像
Dr. Kala. MD2 年前

😅😅 haya bwana 😅

Mayolwa 的头像
Mayolwa2 年前

At least hii kada kuna namna viongozi huwa wanajirudi na kuiangalia. Kuna kada ya Mwenyekiti wangu @bajabiri, hii kada ni tatizo.

Lyidia Masika 的头像
Lyidia Masika2 年前

@ummymwalimu bado pharmacy council ni laki moja na sitini na tano (165k) nimeandika nikiwa nalia adi kwikwi na hawajaweza kujenga ata ofisi 😭😭😭😭

The Iron 的头像
The Iron2 年前

MCT Income per year ~500mil+

Master Chief 的头像
Master Chief2 年前

Katika changamoto zoote alizo nazo Daktari wameona hii ndo kubwa zaidi? Unadhani kama mngewalipa vizuri hawa watumishi wa afya wangeshindwa kulipa hiyo laki moja kwa mwaka? Kudhalilishana tu.

MedKali MD 的头像
MedKali MD2 年前

Vpi kuhusu mshahara na posho nyingine 🤔

baloho 的头像
baloho2 年前

Good start lakini 150k kwa miaka miwili bado ni kubwa.

相关视频

"Siku ya maandamano ya Oktoba 29, 2025 waandamanaji walikuja mpaka kwenye kituo changu cha mafuta na mimi nilikuwa mpaka nimeshawaambia wafanyakazi wangu kwamba wakifika tu hapa acheni na milango wazi muondoke. Walipofika tu waandamanaji likatokea kundi la watu likawaambia waandamanaji hapa hamuwezi kuchoma kwani huyu ni mwenzetu kabisa anatusemea anatupambania." "Nilikuwa na mabasi mapya 30 yalikuwa na picha ya Mama Samia yote na sikubandua lakini hawakuchoma hata moja hata juzi nimewaeleza serikali kwamba leo mtu amefanya kazi ya udereva ameshaihusisha leseni yake mara sita, ana wake wawili na watoto 20, unabadilisha ghafla taratibu kwamba madereva leseni zikiisha muda wake lazima ukasome kwanza wiki mbili kabla ya kuihuisha halafu alipe 380,000 wakati huo dereva anaishi kwa posho. Akimaliza kusoma asubiri miezi miwili kupata leseni maana yake haendi kazini, watoto hawali. Kuna kufeli pia, unamwambia arudi nyumbani wakati huo ameendesha gari miaka yote hiyo na hajawahi kupata ajali. Mimi hili suala nitalipigia kelele mpaka mwisho." "Sheria ni zilezile, trafiki ni walewale na barabara ni zile zile si kwamba kuna barabara za juu sasa hivi, maana yake tunatengeneza kundi lingine la kutupiga CCM. Hivi ni vitu vidogo vidogo sana kwani serikali inashindwa nini kuingia gharama ikatoa mafunzo kikanda kwamba madereva wote njooni msome bure? Kwasababu alama za barabara ni zilezile, leo mtu ni dereva unataka kumkalishs darasani ni kama watu wa degree sasa hivi umwambie nataka turenew vyeti vyenu njooni darasani kusoma, mtafaulu?- Joseph Kasheku Musukuma, Mbunge wa Bunge la Tanzania akizungumza na M/S Podcast.

Royal Media

43,037 次观看 • 23 天前

#VIDEO Mwigizaji Joyce Mbaga (32) maarufu kama ‘Nicole Berry’ leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Jijini Dar es salaam amesomewa mashtaka matatu ikiwemo kuendesha genge la uhalifu na kupokea shilingi za Kitanzania milioni 185.5 kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mbali ya Nicole, Mshtakiwa mwingine ametajwa kuwa ni Rehema Mahanhu (31). Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,2025 na Washtakiwa hao wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na Wadhamini wawili na kuwasilisha Mahakamani fedha taslimu shilingi milioni 46.3 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Nicole na mwenzake wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Rhoda Maingu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira wakidaiwa kuyatenda makosa hayo kati ya Julai 2024 na Machi 2025 ndani ya Mkoa wa Dar es salaam. Wakili Maingu alidai kuwa katika shtaka la kwanza Washtakiwa wanatuhumiwa kuongoza genge la uhalifu ambapo wanatuhumiwa kwa miezi hiyo na miaka hiyo wakiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam waliendesha biashara ya kihalifu au jinai, kwa lengo la kujipatia faida kutoka kwa jamii na kupokea amana au miamala bila kupata leseni kutoka BoT. Katika shtaka la pili Washtakiwa wote wanatuhumiwa kati ya Julai 2024 na Machi 2025 wakiwa eneo lisilofahamika ndani ya mkoa wa Dar es salaam walipokea amana ya shilingi milioni 185,515,000 kutoka kwa jamii bila kuwa na leseni na katika shtaka la tatu Washtakiwa waliendesha mfumo wa malipo bila kuwa na leseni ya malipo inayotolewa na BoT. #MillardAyoUPDATES

millardayo

66,666 次观看 • 1 年前

VIDEO: Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema raia wa Kenya waliowasili nchini kwa lengo la kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, walikiuka sheria za Tanzania kwa kuwa hawakuwa na leseni ya kufanya kazi za uwakili nchini, akiwaita "wanafiki" wanaotaka kuivuruga Tanzania kwa kutumia kisingizio cha haki za binadamu. Akizungumza na wanahabari Jumanne Mei 20, 2025 mkoani Dodoma wakati wa maelezo kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Ndumbaro amesema watu hao walizuiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa mujibu wa sheria za nchi. Raia hao walidai wamekuja kufuatilia kesi ya Tundu Lissu kwa misingi ya haki za binadamu, jambo ambalo Dkt. Ndumbaro amesema halikubaliki kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye taasisi imara zinazoshughulikia masuala ya kisheria kwa mujibu wa sheria zake. Kauli hiyo ya Ndumbaro imekuja siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika uzinduzi wa Sera mpya ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 (Toleo la 2024) jijini Dar es Salaam, kutoa onyo kali kwa wanaharakati wa kimataifa wanaoanza “kuvamia na kuingilia” masuala ya ndani ya Tanzania. “Tusiiwe shamba la bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka… Tumeanza kuona mwenendo wa wanaharakati ndani ya kanda yetu kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu,” alisema Rais Samia Jumatatu Mei 19, 2025. Akitilia mkazo kauli hiyo, Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika kusimamia haki za binadamu na kwamba juhudi za nje za kutaka kuibua taharuki kupitia kesi ya Tundu Lissu hazina msingi wowote wa kisheria wala kiuadilifu.

Jambo TV

22,554 次观看 • 1 年前