Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

Lyricist while writing *Dola re Dola re *

11,578 views • 28 days ago •via X (Twitter)

0 Comments

No comments available

Comments from the original post will appear here

Related Videos

😲😳😳😳 900 dola
1:01

Sensitive content

😲😳😳😳 900 dola

Woubi Tout Kote

21,993 views • 1 year ago

Huu ujumbe wa Zitto MwamiRuyagwa Kabwe tufanye tuwezavyo umfikie Samia Suluhu hata kwa njia ya WhatsApp. Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba kwa sasa vyombo vya dola ndivyo vinavyoongoza siasa na sio siasa kuongoza vyombo vya dola. Huko nyuma vyama vya siasa ikiwemo ccm yenyewe vilikuwa na nguvu kuliko vyombo vya dola lakini kwa sasa vyombo vya dola ndio vina nguvu kuliko vyama vya siasa. Kwa sasa vyombo vya dola ndio vinapanga nani awe kiongozi ccm na 80% ya vyama vya upinzani. Vyombo vya dola vinaweza kumuondoa kiongozi yoyote kwenye vyama vya siasa wanavyoviendesha ikiwemo chama tawala na vingine kama walivyowaondoa akina Chongolo, Polepole, Kinana, Mbatia na wengine. Vyombo vya dola wanaweza kufanya hivyo kwa sababu wanamumdu Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala . Sasa vyombo vya dola ndivyo vinavyoamua nani awe mbunge au diwani wala sio wananchi tena wanaoamua. Yani kwa sasa kura za wananchi haziamui tena nani awe mbunge bali dola ndiyo inayoamua. Zamani ulikuwa ukisikia ccm wakijitapa kwamba ccm imeshika dola lakini kwa sasa dola ndiyo iliyoishika ccm. Kwamba kwa sasa ccm imebakia kama rubber stamp tu ya dola. Viongozi wa ccm hawana uhuru wa kutoa maoni na fikra zao kama zamani na wote wanalazimishwa kusifia tu serikali hata kama wakulima huko wamedhulumiwa na serikali. Muasisi wa hali hii ya kuifanya vyombo vya dola kuwa na nguvu kuliko siasa ni Magufuli na Samia amefanya kuiendeleza. Zitto amezungumza kitu cha kweli kama hali itaendelea kuwa hivi basi siku sio nyingi ccm wataondolewa na dola. Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

Mdude Nyagali

52,990 views • 1 year ago

BAJETI YA SINGAPORE 2025/26 1. Kila familia Singapore itapewa dola 800$ kupunguza gharama za maisha. 2. Kila familia yenye kipato cha chini itapewa dola 760$ ili kusaidia kulipa gharama za umeme na maji. 3. Kila kijana wa Singapore mwenye umri kati ya miaka 13-20 atapewa dola 500$ kusaidia mahitaji ya shule. 4. Kila raia yenye kipato cha chini atapewa dola 760$ kumsaidia kuendesha maisha. 5. Kila mzee Singapore mwenye kiinua mgongo kidogo atapewa dola 360$-1,390$ kwa mwezi ili kumsaidia kuendesha maisha. 6. Kila kampuni inayoajiri Msingapore angalau mmoja kwa mwaka itapewa benefit kati ya dola 2,000$ mpaka 40,000$. 7. Kila kampuni Singapore itakayoongezea wafanyakazi wake mshahara, serikali ya Singapore itachangia asilimia 40% ya hilo ongezeko. 8. Serikali imeongeza dola billioni 3$ katika mfuko wa taifa wa productivity ili kusaidia kampuni kuwa na ushindani zaidi. 9. Serikali imewekeza asilimia moja (1%) ya pato la taifa kugharamia tafiti (R&D). 10. Serikali imetenga dola millioni 150$ kwa ajili ya kuzisaidia kampuni ku-integrate Artificial Intelligence, hii pesa itagharamia AI consultancy. 11. Kila raia wa Singapore mwenye miaka 40 na kuendelea atapewa dola 4,000$ kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na kuongeza ujuzi, haswa katika kipindi hiki cha Artificial Intelligence. 12. Kila mfanyakazi wa Singapore anayeamua kusimama kazi ili aende kusoma full time atakuwa analipwa na serikali dola 3,000$ kwa mwezi kwa miezi 24 atakayokuwa anasoma. 13. Kila raia wa Singapore anayeamua kusoma akiwa kazini part time atapewa dola 300$ kwa mwezi. 14. Kila kampuni Singapore itatengewa dola 10,000$ ili kusaidia wafanyakazi wake kuongeza ujuzi. 15. Kila raia wa Singapore anayepoteza kazi atapewa dola 6,000$ kila mwezi kwa miezi sita ili kumsaidia kujiongezea ujuzi na kupata kazi nyingine. 16. Familia zenye kipato kidogo zitapewa washauri mbali mbali kuwawezesha kuwa na mipango, kuweka malengo, na kutafuta ujuzi. Kila mwanafamilia atakayejiongezea ujuzi na kupata ajira ya kudumu, serikali itampatia motisha ya dola 30,000$. 17. Kila raia atakayezaa watoto watatu na kuendelea, kila mtoto atapata dola 5,000$, mama atapata dola 5,000$, na familia itapata dola 1,000$ kwa mwaka. 18. Kila raia mzee Singapore anayejiwekea akiba voluntary kwa ajili ya bima ya afya, serikali itamwongezea dola moja kwa kila dola moja anayojiwekea. 19. Kila raia wa Singapore anayemtunza mzee nyumbani atapewa dola 600$ kwa mwezi kupunguza gharama za maisha. 20. Kila raia wa Singapore mwenye miaka 21 na kuendelea atapewa dola 600$ kutambua mchango wao katika ujenzi wa taifa. 21. Kila raia wa mwenye miaka 18 kuendelea atapewa dola 100$ kama motisha ya kushiriki shughuli za kitamaduni. 22. Kila familia itapewa dola 100$ ili kufurahia michezo kwa pamoja na wanafamilia. Bajeti kuu ya Singapore 2025 ni dola bilioni 143$ (S$), sawa na Trillion 279 za Tanzania. Hii ni bajeti ya Tanzania ya miaka 20 kama sikosei😎. Kwenye page 98 za hotuba ya bajeti, hakuna mstari hata mmoja unaoishukuru Serikali wala kiongozi yeyote. Kwenye lisaa limoja na dakika 43 za kusoma speech ya budget bungeni, sina hakika kama nimewasikia wabunge wakipiga makofi na wakishangalia, muda wote walikuwa kimya wakisikiliza. Hapakuwa na mbwembwe zozote za kuingiza hotuba ya bajeti bungeni, kiongozi ameingia tu kazi ikaanza. Nasubiri kusoma na kusikiliza hotuba ya bajeti ya Tanzania soon.

(---) Onesmo Mushi

28,462 views • 1 year ago