正在加载视频...

视频加载失败

millardayo Sababu ya kufungiwa

36,609 次观看 • 2 年前 •via X (Twitter)

11 条评论

millardayo 的头像
millardayo2 年前

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema limejiridhisha kuwa Seif Kassim Kisauji maarufu Babu wa TikTok ametenda kosa la kimaadili wakati akitekeleza kazi zake za sanaa na limefikia maamuzi kumfungia kutokujishughulisha kufanya kazi za sanaa ndani na nje ya Tanzania kwa kipindi cha miezi sita kuanzia leo July 22,2024 na kumtoza faini ya Tsh. milioni 3 ambayo anatakiwa kuilipa ndani ya siku 7 kuanzia leo. Baraza limesema limefikia uamuzi huo baada ya kumuita Kisauji kuhusiana na ukiukwaji wa maadili akiwa kama Msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa kwa usajili Na. BST-9684-2023-2154 ambapo ukiukwani huo wa maadili ni kinyume na Kanuni ya 25 (6) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2018 na Mwongozo wa Uzingatiaji wa Maadili katika Kazi za Sanaa wa Mwaka 2023. “Baraza la Sanaa la Taifa kupitia Sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 na Maboresho yake ya Mwaka 2019 ina mamlaka ya kusimamia maadili ya msingi kwenye Sekta ya Sanaa kwa Kanuni ya 25(1)-(8) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018” “Baraza limekwishatoa na kuzindua mwongozo wa maadili katika kazi za sanaa ambao unapatikana katika tovuti yetu hivyo ni jukumu la kila Msanii na Mdau wa Sanaa na jamii kuzingatia maadili katika kazi za sanaa” #MillardAyoUPDATES

BJB_MotorsLtd 的头像
BJB_MotorsLtd2 年前

@millardayo Huyu Mzee anafamilia kweli ? Mke, watoto, wajukuu? Tuianzie hapa .... Maana hii pia inaweza kuwa afya ya akili si bure, Mzee wa haya makamo haya kufanya ujinga huu na wajukuu ni hatari Sana.

Arnold Rwekaza 的头像
Arnold Rwekaza2 年前

@millardayo Hawa mabinti walikamatwa lakin?

🅱️a©️☣️Hu➕2️⃣5️⃣5️⃣ 的头像
🅱️a©️☣️Hu➕2️⃣5️⃣5️⃣2 年前

@millardayo @ZephilineEze hiyo hapo ibamnyonga😂😂😂

Kim 的头像
Kim2 年前

@millardayo Nyieee🤣🤣

Aka Chamilion 的头像
Aka Chamilion2 年前

@millardayo Mzee Kapagawa na hela ya tick tock na hela yenyewe ikamtia kitanzi🤣🤣🤣🤣Use your money wisely Babu

DeMon 的头像
DeMon2 年前

@millardayo vitoto vya 2000 vina balaa

Ado Kafro 的头像
Ado Kafro2 年前

@millardayo Daaah hiki si kitoto kabisa

Deo Kimario 的头像
Deo Kimario2 年前

@millardayo Mzee hana familia😳

P Edwin 的头像
P Edwin2 年前

@millardayo Wamfungie tu hana adabu

Jamal Mohd 的头像
Jamal Mohd2 年前

@millardayo huyu mzee nilijuaga atakuja kukiingia tu cha kumdhalilisha

相关视频