Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

36,206 views • 8 days ago •via X (Twitter)

2 Comments

sokomoko's profile picture
sokomoko8 days ago

Ndo maana mvua zinanyesha kdg maana

t. alulu's profile picture
t. alulu8 days ago

Sasa camera man akiondokea matako ana takaje

Related Videos

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche amekosoa namna ambavyo serikali imekuwa ikitoa tenda mbalimbali kwa Raia wa nje ya nchi na kuwaacha watanzania bila ajira, akikosoa pia usafirishaji mkubwa wa malighafi kilimo ikiwemo Korosho zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi badala ya kuongezewa thamani ndani ya nchi ili kuongeza fursa za ajira na mzunguko wa fedha nchini. Wakati wa Mkutano wake wa hadhara Mtwara Mjini leo Aprili 05, 2025, Heche ameeleza kuwa vijana wengi kwasasa wamejiingiza kwenye michezi ya kamari kutokana na kukosekana kwa siasa safi na utawala bora nchini, akiwataka wananchi wa Mtwara kujihurumia na kuchukua hatua za kukiondoa Chama Cha Mapinduzi madarakani. "Hata tukiwapa miaka 10,000 hawawezi kubadilisha nchi hii, wataendelea tu kuturudisha nyuma. Tunapita kwenye barabara za Mtwara utafikiria tunaenda kwenye maandaki ya vita." Ameeleza John Heche. Akiilingalisha Tanzania na Dubai, Heche amesema mwaka 1961 Dubai ilikuwa na watu 70,000 na ilipofika mwaka 1969 wakati Tanzania ikiwa tayari imekwishapata uhuru, Dubai ndipo ilipogundua pipa lake la kwanza la mafuta na leo hii Dubai ina watu milioni tatu huku Tanzania ikiwa na watu Milioni 63, lakini ameshangaa namna ambavyo mpaka leo Tanzania imeshindwa kujiendesha kufikia hatua ya kuikabidhi Dubai Bandari zake waiendeshe. Heche pia amekosoa namna ambavyo serikali imeshindwa kuwa na Mpango wa ujenzi wa viwanda vya Kimkakati ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha kubangua Korosho Mkoani Mtwara, akisema Kiwanda hicho kingesaidia kuongeza fursa za ajira, kusisimua uchumi wa Mtwara pamoja na kustawisha uchumi wa Wakulima kwa kuongeza thamani kwenye mazao yao ya korosho.

Jambo TV

10,563 views • 1 year ago